Ukweli mchungu: Asilimia kubwa ya Wakristu na Waislamu duniani wanafanya ibada ya sanamu bila kujua kama wanafanya ibada ya sanamu

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
15,118
27,107
Hata wewe msabato unae waponda wakatoliki, kwa mantiki ya uzi huu, wewe pia unafanya ibada ya sanamu.

Kwani ibada ya sanamu nini?

Umewahi kusikia mashabiki wa mpira wanasema " kwenye timu hii golini kuna sanamu?" Je unadhani maana yake huwaga ni nini?

Maana yake ni kwamba kwenye timu hiyo golini kuna kipa ambae hatimizi majukumu yake kama kipa. Kipa kazi yake ni kuokoa mipira yote inayo elekezwa golini kwake. Ila kama kipa huyu hadaki magoli yanafungwa tu haokoi wala nini basi watu watasema golini kuna sanamu.

Ni sawa na wanapo sema "Huyu jamaa ni baba au sanamu la baba?" Wana maanisha ni baba ambae hatimizi majukumu yake.

Vivyo hivyo kwa habari ya ibada ya sanamu.

Ibada ya sanamu ni nini sasa?

Ibada ya sanamu ni ibada yoyote ile ambayo Mungu/muungu anae ombwa hatoi majibu.

Ibrahimu alivyo yaharibu masanamu ya mababu zake alifanya hivyo sio kwa sababu yale walikuwa ni masanamu la hasha ila alifanya hivyo kwa sababu masanamu yale yalikuwa hayatoi majibu ya maombi ndio maana akaenda kuyacharaza mapanga kwa Hasira.

Kama masanamu yale ya miungu ya mababu zake yangekuwa yanatoa majibu basi Ibrahim asinge thubutu hata kunyoosha mkono wake kuyakata. Yani asinge thubutu hata kujifanya kama anajikuna.

Wakristu na waislamu na ibada ya sanamu.

Ukweli ni kwamba Asilimia kubwa ya wakristu na waislamu wengi duniani hufanya ibada za sanamu. Kwa sababu hufanya ibada zisizo na majibu. Sanamu lina masikio lakini halijibu na lina macho lakini halioni. Vivyo hivyo Mungu (wa Wakristu na Waislamu) anasikia maombi yote wanayo muomba watu wake lakini huwaga hajibu na ana ona mambo yote mabaya wanayo tendewa watu wake lakini haintervene. Anayaacha yaendelee kutokea hivyo hivyo licha ya yeye kuwa na uwezo wa kuyazuia yasitokee.

Ndio maana kwa wakristu na waislamu mtu akifanya maombi halafu yakajibiwa majibu hayo huitwa muujiza. Muujiza ni jambo ambalo sio la kawaida. Yesu alipo tembea juu ya maji uliitwa muujiza kwa sababu sio kawaida kwa mtu kutembea juu ya maji.

So maombi yanayo jibiwa na Mungu wa wakristu na waislamu huwaga yanaitwa muujiza kwa sababu sio kawaida Mungu kujibu maombi..

Hata wakristu na waislamu ndani ya nafsi zao huwaga wanajua kabisa kwamba Mungu huwaga hajibu maombi yao. Ndio maana wengi wao huenda kwa waganga kutafuta majibu ya maombi yao.

Wakristu na Waislamu wana amini Mungu anayaona zaidi madhambi yao kuliko maombi yao. Ndio maana mkristu au muislamu akitenda dhambi anakuwa na uhakika kabisa Mungu kamuona na anakuwa na ile kitu inaitwa Guilty conscious kwa sababu anajua Mungu kamuona . Lakini akifanya maombi yake anakuwa hana imani kama Mungu kayasikia na kwamba atamjibu.

Ndio maana hata kwenye Uzi wangu huu wakristu na waislamu watakuja ku comment hapa kwamba Mungu ataniadhibu kwa kuwa ninakufuru ila ningeandika Uzi nikisema nataka nifunge nimuombe Mungu awafanye watu wote duniani waache dhambi basi wakristu na waislamu hao watakuja kunidhihaki hapa kwa sababu wanajua Mungu hatonijibu kwa maana wanajua Mungu huwa hajibu maombi ya watu.

Bahati nzuri vitabu vya dini zote mbili vimeshaweka wazi kabisa kwamba Mungu huwa hajibu maombi ya watu..

Tufanye nini sasa ee rabbi? Vunja masanamu (Vunja connection na Mungu asie jibu maombi yako na anza sasa kumtafuta Mungu mwenye kujibu maombi yako. Acha ibada ya sanamu sasa)
 
Najibiwa sana na Mwenyeezi Mungu sijawahi kuamka saa 8 usiku au saa 9 nisali nimlilie Mungu asinijibu sio kweli hata mchana kabla ya kufanya lolote nasali namuomba Mungu asimamie jambo langu Wallah linakuwa hapo hapo namuomba Mungu bwana ww mabwana mfalme wa mbinguni na ardhini yeye ndo tunamuabudu na kumuomba.
 
Unakuwa umemuomba jambo ambalo wewe tayari unakuwa unaweza kulifanya na lipo ndani ya uwezo wako. Kwa mfano wewe watu wanakusifu ni mpishi mzuri sana wa chakula. Mimi mwenyewe nimekupa sana biryani lako . Sasa Umepika biryani lako na maandazi yako ya kisomali na chai yako ya maziwa ya kisomali ambavyo tayari watu wanavipenda naturally. Una amka usiku kuomba dua Mungu akusaidie biashara yako itoke siku hiyo na kweli asubuhi wateja wana miminika kama kwa Mwamposa. Wewe utasema ni Mungu majibu dua yako lakini kumbe ni kwa sababu ya utaalamu wako..

Hata vitabu vya dini hizi mbili (ukristu na uislamu vimeweka wazi kabisa kwamba Mungu huwaga hajibu maombi ya watu ndio maana mnatakiwa kuwa na subra mnaambiwa kimafumbo kila mwenye subira yupo na Mungu ili msije mkahoji mbona maombi yenu hayajibiwi. Subira inayo tajwa hapo sio ile subira ya kusubiria wiki mbili hell no hiyo subira ya kusubiria wiki mbili ni kusikilizia. Subira inayo tajwa hapo ni ile ya kusubiria majibu siku ya kihama. Yani wewe tenda matendo yako mema hapa duniani omba maombi yako yote ila na lipo utalipwa siku ya kihama)
 
Mbona kama unalazimisha watu waamini unachotaka , wewe una kitu gani mpaka watu wakuamini unayosem?

Mpaka unakufa hakuna mtu anafuata upuuzi wako.

Mwenye akili hutoa elimu ,sasa wewe unapigia debe imani yako ,ukiulizwa maswali utakimbia ndip tatizo lenu bado mko wachache kw vile hamna ushawishi.
 
USiabudu sanamu mkuu. What is insanity? Insanity is doing the same thing over and over again but expecting different results.

Ndicho mnacho kifanya watu wa dini. Mnamuomba Mungu siku zote miaka yote hampati majibu ila hamuachi kuendelea kumuomba kwa sababu mnatarajia kupata matokeo tofauti. That is insanity bro..
 
Siabudu sanamu mkuu. What is insanity? Insanity is doing the same thing over and over again but expecting different results.

Ndicho mnacho kifanya watu wa dini. Mnamuomba Mungu siku zote miaka yote hampati majibu ila hamuachi kuendelea kumuomba kwa sababu mnatarajia kupata matokeo tofauti. That is insanity bro..
Wewe inakuhusu nn? Kwa mfano wewe huamini dini ila kutwa unaandika nyuzi za dini.

Kwani huwezi kujifunza kuhusu imani yako ,watu billion na kuendelea wamaanini ,sembuse wewe ambaye hata ushawishi hauna😅
 
Ndio hao hao wanao chinjana na kubaguana kwa sababu ya dini. Sitaki watu waendelee kuchinjana na kubaguana kwa sababu ya dini ambazo hata hivyo Msingi wake mkuu ni ibada za sanamu tu .
 
Ndio hao hao wanao chinjana na kubaguana kwa sababu ya dini. Sitaki watu waendelee kuchinjana na kubaguana kwa sababu ya dini ambazo hata hivyo Msingi wake mkuu ni ibada za sanamu tu .
Uwezo wako mdogo sana ,watu duniani wanabaguana kwa dini tu ...Kama unaamini mawazo hayo ni mjinga kabisa.

Watu duniani hata hapa Tanzania wanabaguana kwa ukanda ,makabila ,race mbalimbali ,maskini vs matajiri .

Kiduninia mataifa yanabaguana ,race (wazungua ,araba , Africa).

Wewe unabaguliwa kwa ngozi wako ila kweny dini hakuna ubaguzi watu wote ni wamoja.

Jaribu kuzunguka eti dini imeleta Ubaguzi.. Huoni vita yq CCM vs CHADEMA humu?
 
Hata wewe msabato unae waponda wakatoliki, kwa mantiki ya uzi huu, wewe pia unafanya ibada ya sanamu.

Kwani ibada ya sanamu nini?

Umewahi kusikia mashabiki wa mpira wanasema " kwenye timu hii golini kuna sanamu?" Je unadhani maana yake huwaga ni nini ?

Maana yake ni kwamba kwenye timu hiyo golini kuna kipa ambae hatimizi majukumu yake kama kipa. Kipa kazi yake ni kuokoa mipira yote inayo elekezwa golini kwake. Ila kama kipa huyu hadaki magoli yanafungwa tu haokoi wala nini basi watu watasema golini kuna sanamu.

Ni sawa na wanapo sema " Huyu jamaa ni baba au sanamu la baba?" Wana maanisha ni baba ambae hatimizi majukumu yake.

Vivyo hivyo kwa habari ya ibada ya sanamu.

Ibada ya sanamu ni nini sasa?

Ibada ya sanamu ni ibada yoyote ile ambayo Mungu/muungu anae ombwa hatoi majibu.

Ibrahimu alivyo yaharibu masanamu ya mababu zake alifanya hivyo sio kwa sababu yale walikuwa ni masanamu la hasha ila alifanya hivyo kwa sababu masanamu yale yalikuwa hayatoi majibu ya maombi ndio maana akaenda kuyacharaza mapanga kwa Hasira.

Kama masanamu yale ya
miungu ya mababu zake yangekuwa yanatoa majibu basi Ibrahim asinge thubutu hata kunyoosha mkono wake kuyakata. Yani asinge thubutu hata kujifanya kama anajikuna..

Wakristu na waislamu na ibada ya sanamu.

Ukweli ni kwamba Asilimia kubwa ya wakristu na waislamu wengi duniani hufanya ibada za sanamu. Kwa sababu hufanya ibada zisizo na majibu. Sanamu lina masikio lakini halijibu na lina macho lakini halioni. Vivyo hivyo Mungu ( wa wakristu na waislamu) anasikia maombi yote wanayo muomba watu wake lakini huwaga hajibu na ana ona mambo yote mabaya wanayo tendewa watu wake lakini haintervene. Anayaacha yaendelee kutokea hivyo hivyo licha ya yeye kuwa na uwezo wa kuyazuia yasitokee.

Ndio maana kwa wakristu na waislamu mtu akifanya maombi halafu yakajibiwa majibu hayo huitwa muujiza. Muujiza ni jambo ambalo sio la kawaida. Yesu alipo tembea juu ya maji uliitwa muujiza kwa sababu sio kawaida kwa mtu kutembea juu ya maji.

So maombi yanayo jibiwa na Mungu wa wakristu na waislamu huwaga yanaitwa muujiza kwa sababu sio kawaida Mungu kujibu maombi..

Hata wakristu na waislamu ndani ya nafsi zao huwaga wanajua kabisa kwamba Mungu huwaga hajibu maombi yao. Ndio maana wengi wao huenda kwa waganga kutafuta majibu ya maombi yao.

Wakristu na waislamu wana amini Mungu anayaona zaidi madhambi yao kuliko maombi yao. Ndio maana mkristu au muislamu akitenda dhambi anakuwa na uhakika kabisa Mungu kamuona na anakuwa na ile kitu inaitwa Guilty conscious kwa sababu anajua Mungu kamuona . Lakini akifanya maombi yake anakuwa hana imani kama Mungu kayasikia na kwamba atamjibu.

Ndio maana hata kwenye Uzi wangu huu wakristu na waislamu watakuja ku comment hapa kwamba Mungu ataniadhibu kwa kuwa ninakufuru ila ningeandika Uzi nikisema nataka nifunge nimuombe Mungu awafanye watu wote duniani waache dhambi basi wakristu na waislamu hao watakuja kunidhihaki hapa kwa sababu wanajua Mungu hatonijibu kwa maana wanajua Mungu huwa hajibu maombi ya watu...

Bahati nzuri vitabu vya dini zote mbili vimeshaweka wazi kabisa kwamba Mungu huwa hajibu maombi ya watu..

Tufanye nini sasa ee rabbi? Vunja masanamu( Vunja connection na Mungu asie jibu maombi yako na anza sasa kumtafuta Mungu mwenye kujibu maombi yako. Acha ibada ya sanamu sasa)
Wazee wetu walikuwa wakiomba mvua asubuhi...mchana yanyesha.
 
Kwa wakristo biblia inatufundisha tusiangalie vinavyoonekana bali visivyoonekana maana vinavyoonekana ni vya muda tu na visivyoonekana ni vya milele
2 kor 4: 8

Kitu kingine Mungu ana njia zake zakukufanya utoke kwenye shida au dhiki na anatuhakikishia iwe shida au dhiki au njaa katika hayo yote tutashinda na zaidi ya kushinda
Warumi 8:37
 
Back
Top Bottom