Hivi ni kweli waweza kuomba jambo kwa Mungu likatokea?

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
9,502
19,301
Ilinichukua muda sana kugundua yafuatayo katika maombi:

1. Yesu ametupatia mamlaka kufunga chochote hapa duniani, au kufungua chochote hapa duniani, na kitafungwa au kufunguliwa na mbinguni. maana yake ni kwamba kitatimia hivyo hivyo kama ulivyotamka. Unaweza kuamuru chochote ambacho maadui zako wamekipanga ofisini, biasharani au popote kifungwe. unaweza kuamuru kila kilichofungwa kifunguke, chochote kilichofanywa na mashetani kifungwe au kifunguke, vile utakavyotamka, inatokea hivyo hivyo kama ukitamka kwa imani na kama moyoni mwako unao uhusiano na Mungu.

MATHAYO 18:18, Amini nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani, yatakuwa yamefungwa na mbinguni, na yoyote mtakayoyafungua duniani, yatakuwa yamefunguliwa na mbinguni.

2. NGUVU YA MAPATANO. Mimi nikipatana na ndugu yangu katika imani, kuomba jambo fulani kwa Mungu, Mungu atatusikia, na atafanya. unapitia shida kazini, biashara, ugonjwa au uzushi au chochote, patana na ndugu yako katika imani (wote kama mmeokoka kwasababu Mungu huwasikia waliookoka tu wasiookoka dhambi zinamkinga nao), muombe iwe kwa kufunga au kwa kutokufunga kadiri ya imani yenu, na Mungu ameahidi atasikia na kufanya.

Tena, wawili wenu watakapopatana duniani katika jambo lolote watakaloliomba, watafanyiwa na Baba yangu aliye mbinguni. Kwa kuwa, walipo wawili watatu wamekusanyika kwa Jina langu, name nipo papo hapo katikati yao.

3. Ninaweza kuwapiga upofu maadui zangu ikatokea. mfano, makazini, biashara au maisha ya kawaida, kuna kikundi cha watu au mtu mmoja anania mabaya juu yako, amepanga mabaya, ameahidi kukuumiza au vyovyote vile, unaweza kumpiga upofu, ububu, na kupotea ili asifanikiwe. usiombe kwamba wawe kipofu wa mwili, ni kwamba unampiga upofu katika ulimwengu wa roho ili asikuone au apotee kirohoni hivyo kimwilini atasahau hata alichokuwa anataka kufanya. wengi watasema ni uchawi wa kikristo ila sio. mashetani au wachawi wa mwanza kwa mfano, wanaweza kutumwa kwako ukiwa kibaha, ukaomba wapotee au wakusahau, wao wakaruka wakajikuta wamedondoka kilimanjaro au songea badala ya kwako pale kibaha, au wakasahau. hii imetokea sana. au boss anataka kukufukuza kazi kwa hila, file lako liko mezani kwake, atasahau kabisa kama uliamuru kwa Imani, itatokea. pamoja na kwamba hata kimwili, ukiwa mtu wa Mungu unao uwezo kuamuru chochote kikatokea.

2WAFALME 6:18, Na walipomtelemkia Elisha, akamwomba Bwana akasema, uwapige nakusihi watu hawa kwa upofu. Bwana akawapiga kwa upofu sawaswa na neno la Elisha. Ukisoma MATENDO 13:11, Paulo akijaa nguvu za Roho Mtakatifu, alimwamuru Elima (Yule mchawi) aliyekuwa akizuia injili, awe kipofu kwa muda na ikatokea mara. ukisoma 1WAFALME 17:1, Basi Eliya Mtishibi, wa wageni wa Gileadi, akamwambia Ahabu; kama Bwana Mungu wa Israel aishivyo, ambaye ninasimama mbele zake, hakutakuwa na mvua wala umande miaka hii, ila kwa neno langu. i.e ilitokea hivyohivyo.

JOSHUA 10:12-13, Ndipo Yoshua akanena na jBwana siku hiyo ambayo Bwana aliwatoa Waamori mbele ya wana wa Israel, akasema mbele ya macho ya israek;- “wewe jua simama kimya juu ya Gibeoni, na wewe mwezi simama katika bonde la Aiyalon” ndipo jua likasimama, na mwezi ukatulia…basi jua
likasimama kimya katikati ya mbingu, wala halikufanyaharaka kuchwa kama muda wa siku nzima.

YAKOBO 5:17, Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana akiomba kwa bidii. /eliya alikuwa manadamu mwenye tabia moja na sisi, akaombakwa bidii mvua isinye, na mvua haikunya juu ya nchi muda wa miaka mitatu na miezi sita. Akaomba tena mbingu zikatoa mvua, nayo nchi ikazaa matunda yake.

4. unaweza kuwachafulia watesi wako usemi. Kumbuka ilivyotokea wakati wa ujenzi wa mnara wa Baabel, Mungu aliwachafulia usemi wale watu kwasababu walikuwa wanaenda kinyume na lengo lake. wakavurugikiwa lugha, hawakuelewana. HATA SASA katika ulimwengu wa Roho, kuna watu huwa wanakaa vikao dhidi yako, hao ni binadamu, ila kuna mashetani kabisa nayo huwa yanakaa vikao dhidi yako ili yakuangamize au kukudhuru kwa naman mbalimbali. UNAWEZA KUOMBA wachafuliwe lugha, na ikatokea. kwanini? kwasababu tumepewa mamlaka ya kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule Adui shetani.

MARKO 11:12, hata asubuhi alipotoka Bethania, aliona njaa, akaona kwa mbali mtini wenye majani, akauendea ili labda aone kitu juu yake, na alipoufikilia hakuona kitu ila majani, maana si wakati wa tini. Akajibu akawaambia, tangu leo hata milele mtu asile matunda kwako. Wanafunziwake wakasikia. Na asubuhi walipokuwa wakipita waliuona ule mtini umenyauka toka shinani. Petro akakumbuka habari yake, akamwambia, Rabi, tazamamtini ulioulaani umenyauka. Yesu akajibu akawaambia, mwaminini Mungu. Amini nawambia, yoyote atakayeuambia mlima huu ng’oka ukatupwe baharini, wala asione shaka moyoni mwake, ila aamini kwamba hayo asemayo yametukia, yatakuwa yake. Kwasababu hiyo, nawaambieni, yoyte myaombayo mkisali, aminini ya kwamba mnayapokea, nayo yatakuwa yenu.

kwa msiojua, kiburi chote cha mlokole kipo hapo. yeye hana uchawi, hana nguvu zingine zozote anategemea, anategemea mamlaka ya Jina la Yesu kuamuru chochote, na huwa vinatokea. kuna watu wanaishi kwenye matatizo makubwa kwasababu tu waligusa watauwa wa Mungu, waliwaonea, waliwadhurumu n.k na wao kwasababu hawana nguvu za dunia hii wakaenda chumbani, wakafunga mlango, wakaomba kwa Mungu wao au wakaamuru katika maombi, na vinatokea. wewe unamjia kimwili, yeye anaenda kiroho, na yanakuja kudhihirika kimwili, na unaweza usijue kama unateseka kwasababu yake.

Efe 6:12​

Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

NB: maombi haya simaanishi kwamba uende ukaombe watu wafe, kama wachungaji wengine wanavyofundisha, Yesu anasema mkiwa katika kusali msamehe kwanza. wewe omba Mitego yao, au shughuli zao mbaya dhidi yako, au nia yao mbaya, viharibike, wapigwe upofu wanapokuja kukudhuru, wachafuliwe usemi/lugha wasielewane wao kwa wao, nalo litatokea. Usiombe watu wafe, wasije kufa kweli, Mungu anawapenda hivyo hivyo hata kama ni waovu, hata sisi tulikuwa waovu kama tungeombewa mabaya tusingeishi leo.
 
Back
Top Bottom