Kama haufanyi hivi Biblia bado haikusaidii kiroho kushinda wachawi na majini.

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,587
15,371
Kuna makosa mengi watu wanafanya.
1: Kutumia kitabu cha biblia kama ulinzi dhidi ya wachawi au majini ni kuifanya kama irizi.

2: Kukariri mafungu alafu uyatumie kutetea dini, kubishania au kuonyeshq umwamba wako wa kukariri haisaidii.

UFANYE NINI SASA
Soma biblia, weka kwenye kumbukumbu ubongoni vifungu vya kutosha hasahasa ahadi za Mungu.

Kisha uyatamke kinywani mwako katika maisha ya kila siku. Unachokitamka ndio imani yako.

Wachawi na waganga wanatumia matamko kukuumiza, wanakutamkia lugha hasi na vinakupata kama huna ulinzi, ukikaa kimya utaumia sana. Chukua vifungu ujitamkie na kutamkia unayopitia ili neno hilo lifanyike mwili (uhalisia).

Majini na mashetani yanafanyia kazi lugha hasi kutoka kinywani mwako au mganga na wachawi, Na sisi malaika wa Mungu wanasubiri utamke neno la Mungu ili walilifanyie kazi. Ukikaa kimya unazuia wasifanye kazi.


Chukua hii
Itakusaidia.
 
Back
Top Bottom