Kama unaamini uwepo wa Mungu, usiipite hii!

Brother kila kitu hapa Duniani unachokiona kimetengenezwa au kuundwa na muhusika Gari, pikipiki, nyumba, n.k hivyo hata Dunia, Jua , mwezi yupo aliyeviumba

Ata kama ndio umeviumba hivi vitu uje utunyanyase kwamba tusipo sifu na kuabudu utatuchoma moto. Ukiamua kumsaidia mtu msaidie bila masharti. Huko mbinguni yenyewe malaika wanasifu na kuabudu bila kuchoka na huku duniani anataka kusifiwa na usiposifu na kuabudu anakuwa mkali na mwenye wivu.
 
Ndugu acha sisi washika dini tushike dini zetu sababu kuwepo kwetu katika hii dunia si kwa bahati mbaya kuna aliyetufanya kuwepo naye ni huyo ambaye wewe humuani.

Kumuamini Mungu kunahitaji utulivu wa akili kidogo si jambo ambalo kila mtu amebarikiwa nalo. Mtu akihoji kuhusu kuamini kisichoonekana unashangazwa na mtu huyu mwenye imani kuwa ana AKILI na ana ROHO vilivyo ndani ya mwili wake lakini hajatuambia hata siku moja ameviona vitu hivyo japo kwa mitambo ya kiteknolojia za hali ya juu ya kisasa.

Sisi katika Uislamu baada ya Mw/Mungu kujitangaza uwepo wake kupitia viumbe vyake vikubwa kwa vidogo kama kunyanyuka kwa mbingu, kutandazwa kwa ardhi, jua kutoka mashariki kwenda magharib mabadiliko ya usiku na mchana, mwisho wa siku akapigia mfano hata wa kwa wataalamu wa kibinadamu nankijini wanaoweza kuumba japo nzi kama wanaweza basi wafanye hivyo.

Pia akapiga mfano hata kwetu sisi wenyewe kwa namna tulivyoumba hivi hatuoni uwepo wake?
Mwisho dunia ni sehemu tu ya mapito ya mwanadamu, lolote linalompata mwanadamu huyu liwe zuri au baya ni sehemu ya mtihani kwake.

Kifo kipo, kufufuliwa kupo, kuhesabiwa kupo, pepo na moto pia vipo.
Muwe na siku njema

Hata kama hiyo qurani isinge kuwepo jua na mwezi vingekuwepo na angetokea mtu mwingine akaleta story za hivo ili kuwapa watu kazi za kufanya. Imagine dini zingekuwa hakuna unafikizir vatikani na Saudi Arabia wangekuwa matajiri wakubwa duniani. Unajua idadi ya watu watalii wanaoemda pale maka saudia kwa mwaka na mbuzi kondoo zinazo uzwa na kuchinjwa pale unajua maji ya zam zam yanauzwa pale shilingi ngapi mpaka kuyafikisha hapa Tanzania hapo bado italia kwa papa huu ni upigaji
 
Zikikaribia nyakati za mwisho, watu watakua wajuaji sana.

Hapana zama za zamani kulikuwa hakuna elimu na maarifa ila sasa hivi ni information age ukiwa mjinga umechagua mwenyewe elimu zote zinapatikana kwa lugha unayo ifahamu
 
Kiburi cha uzima.
Ukiwa na access ya kupata chakula huwezi amini kama kuna kitu kinaitwa njaa.

Lkn km huna access ya kupata chakula ndo utajua kweli kuna njaa.

Kiburi cha uzima
Unaweza ongea lolote wakati wowote hata kumtukana Mungu.
Siku uzima wako ukibanwa kwenye kona ndo utafahamu unamuhitaji mwenye nguvu zaidi ili akunasue ulipo banwa akupe nafuu au akurudishie uzima.

Acha uoga mkuu sio kwasababu eti mimi sio mslam au mkristo basi hakuna nguvu inayo nilinda na kunitetea hapa duniani hiyo nguvu ipo lakini sio kama ya watu wa dini
 
Ugumu wa maisha na kuchanganyikiwa inakusumbua kichwa pamoja na kutomjua hufanye nini ,na ukiwa mbali na Mungu pia atakuwa mbali na uso wako,

Acha kumkufuru Mungu,mwenye nguvu kuliko chochote hapa dunianiani.Mungu ni mkuu na ndiye anapaswa kuabudiwa peke yake,

Umejaa dhambi na makasiriko Bure hujui hufanye nini,

Sasa tafuta kanisa lolote wawe wanamuomba Mungu kwa njia ya kweli ,tubu dhambi fanya yale yanayompendeza Mungu ,ongea na Mungu kwa kusoma bibblia na umaanishe kutoka kwenye moyo wako na kuamini maneno yake, Huyu Mungu ninayemjua kupitia neno lake kwenye biblia utaona uwepo wake.na utalia sana kwa maneno yako ya mwanzo,na yeye atakurehemu

Ayubu alifanya hayo unayosema ona kilicho mkuta. Mungu na shetani walipanga kumtesha ayubu wa watu hadi mke akamkimbia.
 
Acha uoga mkuu sio kwasababu eti mimi sio mslam au mkristo basi hakuna nguvu inayo nilinda na kunitetea hapa duniani hiyo nguvu ipo lakini sio kama ya watu wa dini
Kwa hivyo tunakubaliana kuna nguvu (Super Power)inayoweza kumlinda na kumtetea mtu duniani.
Wenzio hiyo nguvu wameiita Mungu.
Wewe unaiitaje?
 
Ukiona mtu anapinga uwepo WA mungu muweza WA yote ujue hajasoma au hajaelimika,

Kwa Sisi Wana AI tunajua elimu/ujuzi uliotumika kuumba ubongo ni WA Hali ya juu sana na sio accident, so lazima awepo muweza WA kufanya hilo na ndio maana tunamwita mungu Kwa maana anaweza kuliko yote,

Kwa wale madaktari watakwambia hivohivo, binaadamu Yuko perfect, na uumbaji huo usingewezekana bila kuwepo mwenye uwezo wa juu sana, na ndiyo yeye aitwaye mungu muweza wa vyote,

Ukisogea kwenye dunia, solar systems, viunbe wengine...... Ni the same

There must be the almighty to make everything perfect in the order you observe today. You don't need to see or touch the almighty, you just look around and you will see his creations
 
Hello!

Kuna jibu huwa najibiwa sana na washika-dini kila ninapowauliza kwanini wao wanaamini uwepo wa Mungu. They are like, "Unaamini uchawi upo?" Nikimjibu, anakuja na hii, "Kama unaamini uchawi upo, kwanini huamini Mungu yupo?".

Yaani hapo huwa wana nadharia yao kuwa, everything is two sided, akiwa na maana kwamba kuwepo kwa nguvu za giza ni kigezo tosha kabisa cha uwepo wa Mungu. Mimi sio suala la naamini au siamini, la hasha! ni kwamba uchawi nishawahi kuushuhudia kabisa mara kadhaa. Kwangu, sio kitu cha kifikirika kabisa, ila kitu cha kufikirika ni nadharia juu ya huyo Mungu wenu.

Nikimuuliza mfia-dini, "Ushawahi kumshuhudia huyo Mungu?".. jibu lao maarufu ni hili hapa, "ndio! nishawahi kumtoa mtu mapepo kwa jina lake au kushuhudia mtu akiponywa kwa jina lake".

Well! Hivi ni kwa nini watu wanaoponywa matatizo yao kwa njia ya maombezi huwa ni watu ambao wana matatizo ambayo hayadhihiriki kwa macho ya kawaida?

Mara zote utasikia ushuhuda wa kuponywa mapepo, mara maumivu sugu ya tumbo, uti wa mgongo, n.k.. yaani ni matatizo ambayo anayajua mgonjwa mwenyewe tu! Sijawahi kusikia kuna mtu ana liuvimbe, likidonda, au tatizo lolote ambalo linaonekana wazi na kila mtu ameponywa kwa nguvu za huyo Mungu, yeye si muweza wa kila kitu! ama kuna vitu vinamshinda?

Kama yupo shuhuda wa hayo tatizo dhahiri aseme hapa. Kwanini mnakimbiliaga kwenye mapepo tu? Au ndio dawa ya moto ni moto!? Mimi hadi kuna wakati huwa nawaza kuwa hawa wachungaji, masheikh na mapadri huwa nao pia ni wachawi tu.

Kwanza, nyie wafia-dini kwanini mnaabudu kitu hakionekani? Jitu limejificha mnateseka na matatizo ya maisha, mnaliomba na hakuna kitu linawasaidia..! Una akili wewe? Hapo wewe mwenyewe ukijiuliza huyo Mungu kakusaidia nini, hauna cha kujibu zaidi ya kuanza kututajia mambo uliyoyafanya ukafanikiwa.

Tukikuuliza mambo ambayo yamekuendea kombo na ulimuomba huyo Mungu wako, utakuja na jibu la, "ni majiribu ya Mungu".. hapo ndio napoonaga wafia-dini ni wajinga kuliko hata wanyama tunaowafuga.

Kwanza nyie washika-dini ndio watu wenye matatizo mengi kuliko hata watu wanaosali. Umasikini, magonjwa, mapepo sijui majini na matakataka mengi ya ulimwengu mnayo ninyi.. lakini huwa hamshtuki kabisa. Huwa nakasirika sana pale nipo kwenye mazungumzo ya maana halafu jitu linaingiza habari za Mungu, huwa natamani hata nilizabue makofi.
"Huwa nakasirika sana
1647513739407.png
pale nipo kwenye mazungumzo ya maana halafu jitu linaingiza habari za Mungu, huwa natamani hata nilizabue makofi".
Mkuu, hiyo haitakuwa njia nzuri ya kumfundisha Ustaarabu kwamba kila jambo lina wakati wake.
 
Ata kama ndio umeviumba hivi vitu uje utunyanyase kwamba tusipo sifu na kuabudu utatuchoma moto. Ukiamua kumsaidia mtu msaidie bila masharti. Huko mbinguni yenyewe malaika wanasifu na kuabudu bila kuchoka na huku duniani anataka kusifiwa na usiposifu na kuabudu anakuwa mkali na mwenye wivu.
Elezea kwa ushahidi kutoka kwenye Biblia tafadhari kama usemayo ni ya kweli.
 
Kwa hivyo tunakubaliana kuna nguvu (Super Power)inayoweza kumlinda na kumtetea mtu duniani.
Wenzio hiyo nguvu wameiita Mungu.
Wewe unaiitaje?

Hiyo super power sio mungu sisi tunaita energy na pia haitupi adhabu tukifa wala haituhukumu kwa chochote ikiwamo moto mkali wa jehanam
 
Aisee kama haujawai ona nguvu na miujiza ya Mungu bora ukae kimya kuliko kudhihaki.
Tena nakwambia siku ya hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilofaa kwani kwa maneno yako utatangazwa kama mwadilifu au utahukumiwa.
 
Ukiona mtu anapinga uwepo WA mungu muweza WA yote ujue hajasoma au hajaelimika,

Kwa Sisi Wana AI tunajua elimu/ujuzi uliotumika kuumba ubongo ni WA Hali ya juu sana na sio accident, so lazima awepo muweza WA kufanya hilo na ndio maana tunamwita mungu Kwa maana anaweza kuliko yote,

Kwa wale madaktari watakwambia hivohivo, binaadamu Yuko perfect, na uumbaji huo usingewezekana bila kuwepo mwenye uwezo wa juu sana, na ndiyo yeye aitwaye mungu muweza wa vyote,

Ukisogea kwenye dunia, solar systems, viunbe wengine...... Ni the same

There must be the almighty to make everything perfect in the order you observe today. You don't need to see or touch the almighty, you just look around and you will see his creations

Hivi wewe mkuu kungekuwa na mungu au kuna kwenda mbinguni unadhani wazungu wangegawa biblia bure au waarabu wangegawa hizo qurani bure au unadhani wanakupenda sana. Kwanini wasitafsiri vitabu vya kemia bailogia na jiographia wao wakakutafsiria biblia mpaka ya kabila lako? Hukiulizi ni mchezo huo wa kukutawala fikra zako. Wewe ndio umesoma alafu hukaelimika mzungu akupe kitu bure toka lini au mwarabu
 
Elezea kwa ushahidi kutoka kwenye Biblia tafadhari kama usemayo ni ya kweli.

Mkuu biblia nacho kitabu? Hivi unadhani mzungu anakupenda sana kukupa hiyo biblia au unadhani huku afrika kulikuwa hakuna mungu mpaka wakoloni walivyokuja na biblia ndio wakamleta mungu.

Kama huyo mungu wa biblia angekuwa mungu angekuja mwenyewe hapa afrika sio mpaka aletwe na wazungu wakoli waliokuja kuiba na kubaka wanawake wetu huku afrika.

Kama mbinguni ingekuwa kweli unadhani wazungu wangekupa biblia.? Dawa ngapi za kutibu magonjwa wanazo wanaficha ila biblia wakakupa bure. THINK
 
Shida ya kushiba hii. Hoja hazina mipangilio, unataka kuona watu wakicharuka then ujihisi mshindi kwa andiko lako. Anyway, amini unachokiamini.
 
Mkuu biblia nacho kitabu? Hivi unadhani mzungu anakupenda sana kukupa hiyo biblia au unadhani huku afrika kulikuwa hakuna mungu mpaka wakoloni walivyokuja na biblia ndio wakamleta mungu.
Kama huyo mungu wa biblia angekuwa mungu angekuja mwenyewe
Unahakika Biblia iliandikwa na hao wazungu unaowasema? na kwani hao wazungu sio binadamu kama sisi..!


Nb Haujajibu swali langu.
 
Back
Top Bottom