Kama unaamini uwepo wa Mungu, usiipite hii!

Pist_Sr

Member
Mar 6, 2020
31
60
Hello!

Kuna jibu huwa najibiwa sana na washika-dini kila ninapowauliza kwanini wao wanaamini uwepo wa Mungu. They are like, "Unaamini uchawi upo?" Nikimjibu, anakuja na hii, "Kama unaamini uchawi upo, kwanini huamini Mungu yupo?".

Yaani hapo huwa wana nadharia yao kuwa, everything is two sided, akiwa na maana kwamba kuwepo kwa nguvu za giza ni kigezo tosha kabisa cha uwepo wa Mungu. Mimi sio suala la naamini au siamini, la hasha! ni kwamba uchawi nishawahi kuushuhudia kabisa mara kadhaa. Kwangu, sio kitu cha kifikirika kabisa, ila kitu cha kufikirika ni nadharia juu ya huyo Mungu wenu.

Nikimuuliza mfia-dini, "Ushawahi kumshuhudia huyo Mungu?".. jibu lao maarufu ni hili hapa, "ndio! nishawahi kumtoa mtu mapepo kwa jina lake au kushuhudia mtu akiponywa kwa jina lake".

Well! Hivi ni kwa nini watu wanaoponywa matatizo yao kwa njia ya maombezi huwa ni watu ambao wana matatizo ambayo hayadhihiriki kwa macho ya kawaida?

Mara zote utasikia ushuhuda wa kuponywa mapepo, mara maumivu sugu ya tumbo, uti wa mgongo, n.k.. yaani ni matatizo ambayo anayajua mgonjwa mwenyewe tu! Sijawahi kusikia kuna mtu ana liuvimbe, likidonda, au tatizo lolote ambalo linaonekana wazi na kila mtu ameponywa kwa nguvu za huyo Mungu, yeye si muweza wa kila kitu! ama kuna vitu vinamshinda?

Kama yupo shuhuda wa hayo tatizo dhahiri aseme hapa. Kwanini mnakimbiliaga kwenye mapepo tu? Au ndio dawa ya moto ni moto!? Mimi hadi kuna wakati huwa nawaza kuwa hawa wachungaji, masheikh na mapadri huwa nao pia ni wachawi tu.

Kwanza, nyie wafia-dini kwanini mnaabudu kitu hakionekani? Jitu limejificha mnateseka na matatizo ya maisha, mnaliomba na hakuna kitu linawasaidia..! Una akili wewe? Hapo wewe mwenyewe ukijiuliza huyo Mungu kakusaidia nini, hauna cha kujibu zaidi ya kuanza kututajia mambo uliyoyafanya ukafanikiwa.

Tukikuuliza mambo ambayo yamekuendea kombo na ulimuomba huyo Mungu wako, utakuja na jibu la, "ni majiribu ya Mungu".. hapo ndio napoonaga wafia-dini ni wajinga kuliko hata wanyama tunaowafuga.

Kwanza nyie washika-dini ndio watu wenye matatizo mengi kuliko hata watu wanaosali. Umasikini, magonjwa, mapepo sijui majini na matakataka mengi ya ulimwengu mnayo ninyi.. lakini huwa hamshtuki kabisa. Huwa nakasirika sana pale nipo kwenye mazungumzo ya maana halafu jitu linaingiza habari za Mungu, huwa natamani hata nilizabue makofi.
 
Brother kila kitu hapa Duniani unachokiona kimetengenezwa au kuundwa na muhusika Gari, pikipiki, nyumba, n.k hivyo hata Dunia, Jua , mwezi yupo aliyeviumba
Mnaanzaga na logic lakini mkiulizwa logic mnaleta porojo.

Huyo muhusika nikikukuuliza kaundwa na nani utajibu Mungu, na nikikuuliza huyo Mungu kaundwa na nani.. utaniletea ngonjera za biblia sijui Quran.
 
Ww huna akil kama unazo Tuoneshe
 
Mungu akayafute machizi ya wanna JF wote.
Mungu akawaondoleeni vilio vyenu, iwe njaa, dhiki, umasikini, magonjwa, stress, madeni, kuukkata tamaa ya maisha nk.

Mungu yupo na atakuvusha salama

Godwin Ombeni- Kwa Mji we Mwangaza.
 
Attachments

  • Godwin-Ombeni-Kwa-Mji-Wa-Mwangaza.mp3
    4.4 MB
Hello!

Kuna jibu huwa najibiwa sana na washika-dini kila ninapowauliza kwanini wao wanaamini uwepo wa Mungu. They are like, "Unaamini uchawi upo?" Nikimjibu, anakuja na hii, "Kama unaamini uchawi upo, kwanini huamini Mungu yupo?". Yaani hapo huwa wana nadharia yao kuwa, everything is two sided, akiwa na maana kwamba kuwepo kwa nguvu za giza ni kigezo tosha kabisa cha uwepo wa Mungu. Mimi sio suala la naamini au siamini, la hasha! ni kwamba uchawi nishawahi kuushuhudia kabisa mara kadhaa. Kwangu, sio kitu cha kifikirika kabisa, ila kitu cha kufikirika ni nadharia juu ya huyo Mungu wenu.

Nikimuuliza mfia-dini, "Ushawahi kumshuhudia huyo Mungu?".. jibu lao maarufu ni hili hapa, "ndio! nishawahi kumtoa mtu mapepo kwa jina lake au kushuhudia mtu akiponywa kwa jina lake".

Well! Hivi ni kwa nini watu wanaoponywa matatizo yao kwa njia ya maombezi huwa ni watu ambao wana matatizo ambayo hayadhihiriki kwa macho ya kawaida? Mara zote utasikia ushuhuda wa kuponywa mapepo, mara maumivu sugu ya tumbo, uti wa mgongo, n.k.. yaani ni matatizo ambayo anayajua mgonjwa mwenyewe tu! Sijawahi kusikia kuna mtu ana liuvimbe, likidonda, au tatizo lolote ambalo linaonekana wazi na kila mtu ameponywa kwa nguvu za huyo Mungu, yeye si muweza wa kila kitu! ama kuna vitu vinamshinda? Kama yupo shuhuda wa hayo tatizo dhahiri aseme hapa. Kwanini mnakimbiliaga kwenye mapepo tu? Au ndio dawa ya moto ni moto!? Mimi hadi kuna wakati huwa nawaza kuwa hawa wachungaji, masheikh na mapadri huwa nao pia ni wachawi tu.

Kwanza, nyie wafia-dini kwanini mnaabudu kitu hakionekani? Jitu limejificha mnateseka na matatizo ya maisha, mnaliomba na hakuna kitu linawasaidia..! Una akili wewe? Hapo wewe mwenyewe ukijiuliza huyo Mungu kakusaidia nini, hauna cha kujibu zaidi ya kuanza kututajia mambo uliyoyafanya ukafanikiwa. Tukikuuliza mambo ambayo yamekuendea kombo na ulimuomba huyo Mungu wako, utakuja na jibu la, "ni majiribu ya Mungu".. hapo ndio napoonaga wafia-dini ni wajinga kuliko hata wanyama tunaowafuga.

Kwanza nyie washika-dini ndio watu wenye matatizo mengi kuliko hata watu wanaosali. Umasikini, magonjwa, mapepo sijui majini na matakataka mengi ya ulimwengu mnayo ninyi.. lakini huwa hamshtuki kabisa. Huwa nakasirika sana pale nipo kwenye mazungumzo ya maana halafu jitu linaingiza habari za Mungu, huwa natamani hata nilizabue makofi.
Ndugu acha sisi washika dini tushike dini zetu sababu kuwepo kwetu katika hii dunia si kwa bahati mbaya kuna aliyetufanya kuwepo naye ni huyo ambaye wewe humuani.

Kumuamini Mungu kunahitaji utulivu wa akili kidogo si jambo ambalo kila mtu amebarikiwa nalo. Mtu akihoji kuhusu kuamini kisichoonekana unashangazwa na mtu huyu mwenye imani kuwa ana AKILI na ana ROHO vilivyo ndani ya mwili wake lakini hajatuambia hata siku moja ameviona vitu hivyo japo kwa mitambo ya kiteknolojia za hali ya juu ya kisasa.

Sisi katika Uislamu baada ya Mw/Mungu kujitangaza uwepo wake kupitia viumbe vyake vikubwa kwa vidogo kama kunyanyuka kwa mbingu, kutandazwa kwa ardhi, jua kutoka mashariki kwenda magharib mabadiliko ya usiku na mchana, mwisho wa siku akapigia mfano hata wa kwa wataalamu wa kibinadamu nankijini wanaoweza kuumba japo nzi kama wanaweza basi wafanye hivyo.

Pia akapiga mfano hata kwetu sisi wenyewe kwa namna tulivyoumba hivi hatuoni uwepo wake?
Mwisho dunia ni sehemu tu ya mapito ya mwanadamu, lolote linalompata mwanadamu huyu liwe zuri au baya ni sehemu ya mtihani kwake.

Kifo kipo, kufufuliwa kupo, kuhesabiwa kupo, pepo na moto pia vipo.
Muwe na siku njema
 
Mnaanzaga na logic lakini mkiulizwa logic mnaleta porojo.

Huyo muhusika nikikukuuliza kaundwa na nani utajibu Mungu, na nikikuuliza huyo Mungu kaundwa na nani.. utaniletea ngonjera za biblia sijui Quran.
Hili swali lako la kaundwa na nani achana nalo. Halina maana kwa sababu hakuna mwenye uwezo wa kukujibu pia kama kungekua na namna ya kukupa jibu ubongo wako ni dhaifu sana kuweza kuelewa Uundwaji wa MUNGU.

Wewe hata mechanism ya nguvu ya pumzi ya uhai unayoiita ya kwako huijui utafaham vipi nguvu iliyoifanya uwe nayo? Asubuhi unaamka kama mbuzi au nguruwe huna control ya mwili wako kuwa sasa najiamsha halafu unataka maelezo ya kina ya uumbaji wa nguvu iliyosababisha kuamka kwako

Ni sawa na mende wawili wanaokula nyaya ndani ya gari waulizane kuhusu mfumo wa rejeta unavyofanya kazi.
 
Hello!

Kuna jibu huwa najibiwa sana na washika-dini kila ninapowauliza kwanini wao wanaamini uwepo wa Mungu. They are like, "Unaamini uchawi upo?" Nikimjibu, anakuja na hii, "Kama unaamini uchawi upo, kwanini huamini Mungu yupo?". Yaani hapo huwa wana nadharia yao kuwa, everything is two sided, akiwa na maana kwamba kuwepo kwa nguvu za giza ni kigezo tosha kabisa cha uwepo wa Mungu. Mimi sio suala la naamini au siamini, la hasha! ni kwamba uchawi nishawahi kuushuhudia kabisa mara kadhaa. Kwangu, sio kitu cha kifikirika kabisa, ila kitu cha kufikirika ni nadharia juu ya huyo Mungu wenu.

Nikimuuliza mfia-dini, "Ushawahi kumshuhudia huyo Mungu?".. jibu lao maarufu ni hili hapa, "ndio! nishawahi kumtoa mtu mapepo kwa jina lake au kushuhudia mtu akiponywa kwa jina lake".

Well! Hivi ni kwa nini watu wanaoponywa matatizo yao kwa njia ya maombezi huwa ni watu ambao wana matatizo ambayo hayadhihiriki kwa macho ya kawaida? Mara zote utasikia ushuhuda wa kuponywa mapepo, mara maumivu sugu ya tumbo, uti wa mgongo, n.k.. yaani ni matatizo ambayo anayajua mgonjwa mwenyewe tu! Sijawahi kusikia kuna mtu ana liuvimbe, likidonda, au tatizo lolote ambalo linaonekana wazi na kila mtu ameponywa kwa nguvu za huyo Mungu, yeye si muweza wa kila kitu! ama kuna vitu vinamshinda? Kama yupo shuhuda wa hayo tatizo dhahiri aseme hapa. Kwanini mnakimbiliaga kwenye mapepo tu? Au ndio dawa ya moto ni moto!? Mimi hadi kuna wakati huwa nawaza kuwa hawa wachungaji, masheikh na mapadri huwa nao pia ni wachawi tu.

Kwanza, nyie wafia-dini kwanini mnaabudu kitu hakionekani? Jitu limejificha mnateseka na matatizo ya maisha, mnaliomba na hakuna kitu linawasaidia..! Una akili wewe? Hapo wewe mwenyewe ukijiuliza huyo Mungu kakusaidia nini, hauna cha kujibu zaidi ya kuanza kututajia mambo uliyoyafanya ukafanikiwa. Tukikuuliza mambo ambayo yamekuendea kombo na ulimuomba huyo Mungu wako, utakuja na jibu la, "ni majiribu ya Mungu".. hapo ndio napoonaga wafia-dini ni wajinga kuliko hata wanyama tunaowafuga.

Kwanza nyie washika-dini ndio watu wenye matatizo mengi kuliko hata watu wanaosali. Umasikini, magonjwa, mapepo sijui majini na matakataka mengi ya ulimwengu mnayo ninyi.. lakini huwa hamshtuki kabisa. Huwa nakasirika sana pale nipo kwenye mazungumzo ya maana halafu jitu linaingiza habari za Mungu, huwa natamani hata nilizabue makofi.
Hapana wanakuuliza hvyo sio kwasababu hyo, wanakuuliza hvyo kwasababu wachawi na majini pia wanakiri Mungu yupo.

Tena wew ulitakiwa uamin Mungu yupo kwakua umepata bahati ya kuwaona mpaka wachawi.
 
Kiburi cha uzima.
Ukiwa na access ya kupata chakula huwezi amini kama kuna kitu kinaitwa njaa.

Lkn km huna access ya kupata chakula ndo utajua kweli kuna njaa.

Kiburi cha uzima
Unaweza ongea lolote wakati wowote hata kumtukana Mungu.
Siku uzima wako ukibanwa kwenye kona ndo utafahamu unamuhitaji mwenye nguvu zaidi ili akunasue ulipo banwa akupe nafuu au akurudishie uzima.
 
Ugumu wa maisha na kuchanganyikiwa inakusumbua kichwa pamoja na kutomjua hufanye nini ,na ukiwa mbali na Mungu pia atakuwa mbali na uso wako,

Acha kumkufuru Mungu,mwenye nguvu kuliko chochote hapa dunianiani.Mungu ni mkuu na ndiye anapaswa kuabudiwa peke yake,

Umejaa dhambi na makasiriko Bure hujui hufanye nini,

Sasa tafuta kanisa lolote wawe wanamuomba Mungu kwa njia ya kweli ,tubu dhambi fanya yale yanayompendeza Mungu ,ongea na Mungu kwa kusoma bibblia na umaanishe kutoka kwenye moyo wako na kuamini maneno yake, Huyu Mungu ninayemjua kupitia neno lake kwenye biblia utaona uwepo wake.na utalia sana kwa maneno yako ya mwanzo,na yeye atakurehemu
 
Nimeishia pale uliposema kwamba uchawi umewahi kuuona.nikagundua wewe NI bogus kbs Kama kweli unaamini Kuna uchawi......

Kwa taarifa tupo watu kibao ambao tunaamini Mungu yupo na vilevile hakuna uchawi Wala nguvu za Giza
Uchawi=ujinga.
 
Kiburi cha uzima.
Ukiwa na access ya kupata chakula huwezi amini kama kuna kitu kinaitwa njaa.

Lkn km huna access ya kupata chakula ndo utajua kweli kuna njaa.

Kiburi cha uzima
Unaweza ongea lolote wakati wowote hata kumtukana Mungu.
Siku uzima wako ukibanwa kwenye kona ndo utafahamu unamuhitaji mwenye nguvu zaidi ili akunasue ulipo banwa akupe nafuu au akurudishie uzima.
Kiumbe dhaifu hakiwezi hata kuzuia haja akipata amueba tumbo likamvuruga vizuri lakini anataka ahoji kuhusu uumbaji wa MUNGU.
 
Back
Top Bottom