Kama Tundu Lissu hakufa kwa risasi zote zile basi jambo zito sana Mungu atafanya katika siasa za Taifa hili

TumainiEl

JF-Expert Member
Jan 13, 2010
6,257
11,424
Mh. Lissu kwa risasi alimiminiwa alipaswa kufa ila katika hali ya giza nene na mtikisiko katika siasa za Tz msg ikarudi marehem amefufuka. Wengi wetu tunaweza kusema mengi sana ila kiza kinene kimefunika hili tukio ambalo naamini limeandikwa kwa pen ya moto.

Uwenda kikawa moja ya kisa kinathibitis ha Mungu yupo na wema wapo na bado wana ishi.

Lissu kwa mshituko alipata na risasi alipigwa kuwepo leo ni muujiza mkubwa ambao huko mbele utaleta mabadiliko makubwa kwenye siasa za hili Taifa.

Uwenda wale walipanga naku hakikisha anakufa uwenda nao hawapo maana Karima ndio kitu kina tisha kuliko vyote.

Ikumbukwe hawa viongozi na washabiki wa vyama wana dini zao na hakuna dini inaruhusu mambo ya dhuluma iwe ya mali au uhai wa mtu. Maana unapogusa dam ya mtu unagusa moyo wa Mungu na usishangae kitakacho kutokea.

Mh. Lissu anasiri moja ambayo uwenda ndio uzima wake leo. Lisu ni mmoja wa wana sheria walisaidia sana watu waliodhulumiwa kesi ngumu za kiserikali huyu jamaa ndie alisimamia kama umewahi sikia dhuluma ya North Mara basi huyu mwamba alisimama na alisimama kwa kutolipwa na mtu.

Mh. Lissu aweza kuwa kama Keneth Sarawiwa japo uwenda kazi ya Mh. Lissu imekuwa yakutukuka sana kiasi risasi zilimshindwa.

Ndugu zangu watanzania wa vyama na serikali. Tuogope Karima ya Mungu ambayo naona ipo karibu sana na uwenda hakuna kiongozi au mtu yeyote ana waza au kufikiri ipo siku mambo yatabadilika maana muundo huu wa sasa ni hatari na kitisho kwa hata walio madarakani wakitoka muundo huu ipo siku utageuka kuwa jini nakuumiza watu na Mungu ameachia tukaona wenyewe.

Nimalizie kwa maneno ya Mzee Kikwete wakati fulani bungeni akiwa Rais. Namnukuu
"Tufanye mambo ambayo kesho vizazi vijavyo wasije kuchapa makaburi yetu nakuuliza hawa wazee walikuwa na akili kweli?" Mwisho akasema "Siku moja atakuja kiongozi sio mpole kama mimi akitumia nguvu ya Uraisi itakuwaje?" Ni kiongozi alicheka ila alikuwa na nia njema kutupa taifa lenye haki japo nabii akubaliki nyumbani kwake.
 
Na jambo hilo ni Katiba Mpya kupatikana na kifo cha ccm na CHADEMA na kuzaliwa KWA vyama vipya ambavyo vitashika hatamu KWA kupokezana kama Marekani ilivyo!

Na vyama Hivyo vipya vitakuwa vichache sidhani kama vitazidi vitatu;

Wenye hekima Wanaimba WIMBO huu Hapa;

"Rasimu ya warioba irudi mezani SASA iwe KATIBA MPYA"
 
Yani TZ wapumbavu ni wengi sana kuliko uhalisia wa Wananchi wenyewe walivyo.

Walionusurika kuuwawa kwa risasi ni wengi tu mitaani kuliko hata hizo alizopigwa huyo Jamaa, ila sasa CHAWA wanavyomuhusudu utadhani ni mungu Mtu

Huo ni ushamba
 
Hebu tutajie wewe mtanzania mmoja tu unayemjua wewe huko mitaani aliyewahi kupigwa risasi 16 zikamuingia mwilini na bado akanusurika...
 
Yani TZ wapumbavu ni wengi sana kuliko uhalisia wa Wananchi wenyewe walivyo.

Walionusurika kuuwawa kwa risasi ni wengi tu mitaani kuliko hata hizo alizopigwa huyo Jamaa, ila sasa CHAWA wanavyomuhusudu utadhani ni mungu Mtu

Huo ni ushamba
Wewe ndiye ulitumwa kumuua?
Alaaniwe shetani aliyewatuma.
 
Ujinga mtupu. Mwl Nyerere aliwahi kusema mtu mjinga akielimishwa ujinga unamtoka na kuwa mtu wa kawaida. Ujinga ni kukosa uelewa/elimu.
 
Lisu kwa mshituko alipata na risasi alipigwa kuwepo leo ni muujiza mkubwa ambao huko mbele utaleta mabadiliko makubwa kwenye siasa za hili Taifa.
Tuliwambia toka zamani lakini mkashupaza shingo.

Nadhani mliona kilichofata.
Hata hivyo nakupongeza kwa kukubali Ukuu wa Mungu. Siku za hapo nyuma mlichukua nafasi ya Mungu mkajifanya miungu.
 
Yani TZ wapumbavu ni wengi sana kuliko uhalisia wa Wananchi wenyewe walivyo.

Walionusurika kuuwawa kwa risasi ni wengi tu mitaani kuliko hata hizo alizopigwa huyo Jamaa, ila sasa CHAWA wanavyomuhusudu utadhani ni mungu Mtu

Huo ni ushamba
Mkuu TumainEl ni chawa maarufu wa ccm. Acha kushupaza shingo msikilize kwa makini
 
Ikumbukwe hawa viongozi na washabiki wa vyama wana dini zao na hakuna dini inaruhusu mambo ya dhuluma iwe ya mali au uhai wa mtu. Maana unapogusa dam ya mtu unagusa moyo wa Mungu na usishangae kitakacho kutokea.
Jamaa umeokokea kwa Mwamposa nini🤣🤣
 
Back
Top Bottom