Kama Taifa tumeshindwa kweli kutoka hapa tulipo hata kwa mambo madogo?

TRABSOH

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
339
546
Wakuu habari za wakati huu,

Kama Taifa kwa miaka 60 tumeshindwa kupiga hatua katika kila nyanja hata mambo madogo yametushinda inashangaza hata mambo madogo ya wananchi kuzaa kwa mpangilio tu ili kumudu gharama za maisha haiwezekani?

Mtu ana chumba kimoja ana watoto wanne mtu huyu atapiga hatua lini? Au ndo kila mtoto anakuja na bahati yake, mambo ya ridhiki mafungu saba!

Matatizo ya Taifa husika yanaondolewa na wazawa si wageni, ni kweli hatuwezi kubadilika watu kuzaa kwa mikakati kulingana na kipato chao.

Ni kweli wazee tumeshindwa hata kupanga miji yetu yani mji kama kahama mafinga uko geita inakuwa na kesho tu wanetu wataishi pia kwenye slums ambako kikosi cha waokoaji watashindwa kuokoa watu kwasababu akupitiki ni kweli tumeshindwa kupanga hiyo miji? Vitu vidogo kama hivyo vilivyowezekana miaka 2000 nyuma huko kwa wenye akili duniani, sisi leo 2023 hatuwezi!

Boda boda wanapata ajari kila siku wanakufa wanapata vilema vya maisha amna tafiti ila piki piki zimeharibu maisha ya watu wengiii mnoo zimezalisha yatima na tegemezi, ni kweli mamlaka hazioni hilii wala hazipangi kuja kusitisha kuingiza na kusajili piki piki mpya ile kuwe na limit ya idadi ya vyombo hivii, barabara mpya zinajengwa lakini amna plans za kuwa na njia zao ndogo ili wawapunguzie hatari ya ajari na magari, hakuna hata mipango mikakati ya miaka ijayo kuwa na ajira mbadala ili vijana wasikimbilie uku kweli? Nini tutaweza sasa ! Itatuchukua miaka mingapi kutoka hapa?.

Elimu yetu ni duni hatuna uwezo wa kugharamia tafiti nzito katika Taasisi zetu za vyuo vikuu, bhas ata kusimammia project ndogo zenye tija kwa wanachi nayo hatuwezi? vyuo vikuu mwaka 2023 mtu ana miaka minne chuoni ana graduate na projects ya mashine ya kusaga karanga ambazo ni project za secondary huko Europe, unaona mwanasiasa ana gawa jembe kwa wakulima kweli 2023?

Vyuo vimeshindwa kuwaandaa wanafunzi kuwa wabunifu kusaidia Taifa lao, yan watu wanakaa miaka minne chuoni washindwe kukaa kwenye kikundi na kuja na mashine ndogo ya gharama ndogo itakayomfaa mkulima wa chini kuinunua imsadie kuandaa shamba kwa haraka kuliko jembe la mkono?

Tunashindwa kabisaa kufanya kozi za science zilete mabadilko yetu ya ndani hata kama budget aitoshi bhas mawazo yafanyike kwa udogo ila mawazo kweli yawe yanaleta solutions kwa wananchi sio kugradauate na gpa kubwa project za kindergarten, mtu akienda na wazo zito anaambiwa hili hutaweza badilisha title.

Taifa la watu wajinga hata kunawa mikono baada ya kutoka chooni ni kazi.
Taifa la vijana wasiojua wasome nini wanauliza tu kozi yenye ajira ni ipi au kozi inahusu nini kumaanisha ata details za kwenda kutoa google hawezi kuzipata!

Vizazi vijavyo watateseka sana pengine hata mito itakuwa imekauka kwasababu tunashindwa hata kutunza kwa ajili yao tunawaza tulipo tu si tuendako.

Kwelii hata mambo madogo yametushinda!?
 
Wakuu habari za wakati huu..
Kama Taifa kwa miaka 60 tumeshindwa kupiga hatua katika kila nyanja hata mambo madogo yametushinda inashangaza hata mambo madogo ya wananchi kuzaa kwa mpangilio tu ili kumudu gharama za maisha haiwezekani? Mtu ana chumba kimoja ana watoto wanne mtu huyu atapiga hatua lini? Au ndo kila mtoto anakuja na bahati yake ,mambo ya ridhiki mafungu saba!
Matatizo ya Taifa husika yanaondolewa na wazawa si wageni, ni kweli hatuwezi kubadilika watu kuzaa kwa mikakati kulingana na kipato chao.
Ni kweli wazee tumeshindwa hata kupanga miji yetu yani mji kama kahama mafinga uko geita inakuwa na kesho tu wanetu wataishi pia kwenye slums ambako kikosi cha waokoaji watashindwa kuokoa watu kwasababu akupitiki ni kweli tumeshindwa kupanga hiyo miji? Vitu vidogo kama hivyo vilivyowezekana miaka 2000 nyuma huko kwa wenye akili duniani, sisi leo 2023 hatuwezi!!
Boda boda wanapata ajari kila siku wanakufa wanapata vilema vya maisha amna tafiti ila piki piki zimeharibu maisha ya watu wengiii mnoo zimezalisha yatima na tegemezi, ni kweli mamlaka hazioni hilii wala hazipangi kuja kusitisha kuingiza na kusajili piki piki mpya ile kuwe na limit ya idadi ya vyombo hivii, barabara mpya zinajengwa lakini amna plans za kuwa na njia zao ndogo ili wawapunguzie hatari ya ajari na magari , hakuna hata mipango mikakati ya miaka ijayo kuwa na ajira mbadala ili vijana wasikimbilie uku kweli? Nini tutaweza sasa ! Itatuchukua miaka mingapi kutoka hapa?.

Elimu yetu ni duni hatuna uwezo wa kugharamia tafiti nzito katika Taasisi zetu za vyuo vikuu, bhas ata kusimammia project ndogo zenye tija kwa wanachi nayo hatuwezi? vyuo vikuu mwaka 2023 mtu ana miaka minne chuoni ana graduate na projects ya mashine ya kusaga karanga ambazo ni project za secondary huko Europe, unaona mwanasiasa ana gawa jembe kwa wakulima kweli 2023? Vyuo vimeshindwa kuwaandaa wanafunzi kuwa wabunifu kusaidia Taifa lao, yan watu wanakaa miaka minne chuoni washindwe kukaa kwenye kikundi na kuja na mashine ndogo ya gharama ndogo itakayomfaa mkulima wa chini kuinunua imsadie kuandaa shamba kwa haraka kuliko jembe la mkono?. Tunashindwa kabisaa kufanya kozi za science zilete mabadilko yetu ya ndani hata kama budget aitoshi bhas mawazo yafanyike kwa udogo ila mawazo kweli yawe yanaleta solutions kwa wananchi sio kugradauate na gpa kubwa project za kindergarten, mtu akienda na wazo zito anaambiwa hili hutaweza badilisha title.
Taifa la watu wajinga hata kunawa mikono baada ya kutoka chooni ni kazi.
Taifa la vijana wasiojua wasome nini wanauliza tu kozi yenye ajira ni ipi au kozi inahusu nini kumaanisha ata details za kwenda kutoa google hawezi kuzipata!
Vizazi vijavyo watateseka sana pengine hata mito itakuwa imekauka kwasababu tunashindwa hata kutunza kwa ajili yao tunawaza tulipo tu si tuendako.
Kwelii hata mambo madogo yametushinda!?
Kwa mfumo uliopo usitegemee mabadiliko!!
 
Kwa mfumo uliopo usitegemee mabadiliko!!
Kaka hata kuzaa kulingana na kipato cha mtu nayo ni mfumo? Watu wanaongezeka kwa kasi huku serikali yenyew ndo hii rushwa kila mahali kasi ya kinyonga 2060 maisha yatukuaje kwa wanetu na wajukuu
 
Kaka hata kuzaa kulingana na kipato cha mtu nayo ni mfumo? Watu wanaongezeka kwa kasi huku serikali yenyew ndo hii rushwa kila mahali kasi ya kinyonga 2060 maisha yatukuaje kwa wanetu na wajukuu
Kwan ku reduce uzaaji hiyo si program ya utawala wa Nchi husika? So kama viongoz wanadai kua nyie zaeni fotoeni watoto, unategemea nn hapo? That's why nimekwambia tatizo ni mfumo!!
 
Me naona serikali imefanikiwa mambo mengi japo kwa asilimia kadhaa ila nililiona limefaulu asilimia 100 ni channel ya tanzania safari channel pale nawasifu tbc mmeupiga mengine jitahidini
 
Bila kupambana na ufisadi na ubinafsi hakuna cho chote mtu mweusi anaweza kufanya. Daima atabakia kuwa msindikizaji tu hapa duniani!

IMG_20230729_084104_495.jpg
 
Bila kupambana na ufisadi na ubinafsi hakuna cho chote mtu mweusi anaweza kufanya. Daima atabakia kuwa msindikizaji tu hapa duniani!

View attachment 2764776
Sasa tumeoza maana rushwa na ubinafsi ni tabia sasa yani hata kupata tenda ya kubeba tofalii unaweza jikuta unaambiwa kwenye 15 elfu buku mbili yangu na msimamizi, tunawezaje kuondoka hapo kuweka sheria ngumu za kutekeleza kunyongwa mpaka kufa au maana uwezi sema utoe elimu kwa watoto wakat baba zao ni wezi na wachoyo wenye ubinafsi
 
Kwani mnatakaje labda? Kwanini msijikubali tu vile mlivyo? Kuna haja gani ya kuwakia tamaa maisha ambayo kiuhalisia unajua fika kamwe hutoyaweza?

Au ndiyo zile sera za kudanganyana kwa kulazimisha kwamba watu wote waishi levo moja ya maisha?

Mungu mwenyewe kaumba weupe, wengine weusi, warufu wengine wafupi, vilema ,vipofu, viziwi, wasioongea n.k

Jikubali tu vinginevyo utapasuka kichwa kwa mambo ambayo huyawezi hadi unaingia kaburini. We jikubali tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kwahiyo hapa tulipo ni sawa? Hatupaswi kutoka? kila mtu akipata nafasi aibe kwa ajili yake na familia yake na si Taifa na wananchi wanaotoa kodi, tusijali kuhusu wengine boda boda wakifa ovyo ovyo ni sawa tukubali hayo ndo maisha yetu?
 
Uafrika hasa utanzania ni Laana.

Waafrika wana upumbavu wa milele.

Waafrika hasa watanzania wamelaanika.
 
Kaka hata kuzaa kulingana na kipato cha mtu nayo ni mfumo?
Kumbe ni nini sasa ndugu yangu?

Wewe mwenyewe kwenye andiko lako umegusia ishu ya mfumo mbovu wa elimu. Kama ni hivyo, basi automatic hili la family planning nalo ni elimu. Hii kitu lazima ifundishwe kuanzia kindergarten levels hadi huko juu. Swali ni Je, ipo inafanyika? Inaleta impact Kwa kiasi gani?

Bila watu kuelimishwa umuhimu wa kupanga uzazi, hali hii usiyoitaka itaendelea kuwa
Watu wanaongezeka kwa kasi huku serikali yenyew ndo hii rushwa kila mahali kasi ya kinyonga 2060 maisha yatukuaje kwa wanetu na wajukuu
Kumbe unajua tatizo..

Hii ndiyo maana yake hasa watu wanaposema tatizo ni mfumo mbovu wa kikatiba unaozaa mfumo wa utawala mbovu, dhaifu na corrupt kuanzia chini hadi juu..

Na hii ndiyo sababu mambo hayaendi.

Yaani Kwa mfumo wetu wa kujitawala ni kwamba, taifa zima la watu karibu milioni 65 eti linategemea kichwa na akili za mtu mmoja aitwaye "Rais" kuamua Kila kitu hadi huku kijijini.

Na hili ujue au usijue, lakini kiuhakika ndilo tatizo kuu. Na daima hii haiko sawa. Na hatuwezi kamwe hatuwezi kwenda popote kwa hatua za haraka kama tukiendelea na utaratibu chini ya mfumo huu wa kujitawala na kujiamulia mambo yetu kama nchi..

Na hebu chukua mfano wa ishu ya changamoto ya umeme iliyopo sasa.

Ni tatizo lililodumu kwa zaidi ya miaka 30 sasa tangu wakati wa utawala wa Ben Mkapa na likaja kuwa very serious wakati wa utawala Kikwete. Likapungua kidogo wakati wa Magufuli na sasa liko very serious wakati huu wa huyu mama. Na story na sababu ni zilezile miaka yote and yet, no solution..!

Unadhani tatizo ni nini maana sababu zinazotajwa na watawala hawa ni zilezile miaka yote lakini hakuna utatuzi?

Ishu ni mfumo mbovu wa utawala usiojengwa ktk misingi ya uwajibikaji na kuwajibishana Kwa mujibu wa katiba na Kisha sheria nzuri.

JAWABU la kuondoa au kupunguza ukiritimba huu ni wote tuamue ku- revisit mfumo wetu wa kujitawala kupitia katiba na kisha kurekebisha au kutengeneza upya kabisa. Kutokea hapo tunaweza kuanza kupiga hatua za maana kwenda mbele kuliko ilivyo sasa..
 
Kwani mnatakaje labda? Kwanini msijikubali tu vile mlivyo? Kuna haja gani ya kuwakia tamaa maisha ambayo kiuhalisia unajua fika kamwe hutoyaweza?

Au ndiyo zile sera za kudanganyana kwa kulazimisha kwamba watu wote waishi levo moja ya maisha?

Mungu mwenyewe kaumba weupe, wengine weusi, warufu wengine wafupi, vilema ,vipofu, viziwi, wasioongea n.k

Jikubali tu vinginevyo utapasuka kichwa kwa mambo ambayo huyawezi hadi unaingia kaburini. We jikubali tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwamba unataka watu wajikubali na Umaskini wao?

Una mawazo finyu na fikra za kimaskini sana.
 
Back
Top Bottom