Bunge la nchi liwe kwa ajili ya mambo makubwa ya Kitaifa na Kimataifa, sio mambo madogo madogo

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,245
45,480
Wabunge kutumia muda wa bunge la taifa kuulizia barabara ya wilaya na kituo cha afya na shule ya kata ya zitajengwa lini sio matumizi mazuri ya muda wa bunge, huenda wengine wanauliza ili wasikike tu na wao wameuliza.

Ikiwa bunge linatenga bajeti kila mwaka na kuweka mipango ya mwaka na miaka mitano kwa nini mbunge anainuka kuulizia tena mambo ya bajeti iliyotengwa na mipango ya jimboni kwake?

Bunge linapaswa kujadili bajeti kuu, sera na mipango ya kitaifa, miradi mikubwa ya kimkakati, mikataba, usalama wa nchi, sheria kuu za nchi na kuisimamia serikali. Bunge halipaswi kujadili mambo madogo madogo ya Wilaya, Halmashauri na kata.
 
Imefikia hatua Bunge linakaa kama kamati kujadili honorary PhD degrees. Kweli?
 
Wabunge kutumia muda wa bunge la taifa kuulizia barabara ya wilaya na kituo cha afya na shule ya kata ya zitajengwa lini sio matumizi mazuri ya muda wa bunge, huenda wengine wanauliza ili wasikike tu na wao wameuliza.

Ikiwa bunge linatenga bajeti kila mwaka na kuweka mipango ya mwaka na miaka mitano kwa nini mbunge anainuka kuulizia tena mambo ya bajeti iliyotengwa na mipango ya jimboni kwake?

Bunge linapaswa kujadili bajeti kuu, sera na mipango ya kitaifa, miradi mikubwa ya kimkakati, mikataba, usalama wa nchi, sheria kuu za nchi na kuisimamia serikali. Bunge halipaswi kujadili mambo madogo madogo ya Wilaya, Halmashauri na kata.
Wajifunze kwa Luhaga Mpina
 
Rudi darasani kasome kazi za Bunge kabla Somo la Civics halijafutwa!
 
Wabunge kutumia muda wa bunge la taifa kuulizia barabara ya wilaya na kituo cha afya na shule ya kata ya zitajengwa lini sio matumizi mazuri ya muda wa bunge, huenda wengine wanauliza ili wasikike tu na wao wameuliza.

Ikiwa bunge linatenga bajeti kila mwaka na kuweka mipango ya mwaka na miaka mitano kwa nini mbunge anainuka kuulizia tena mambo ya bajeti iliyotengwa na mipango ya jimboni kwake?

Bunge linapaswa kujadili bajeti kuu, sera na mipango ya kitaifa, miradi mikubwa ya kimkakati, mikataba, usalama wa nchi, sheria kuu za nchi na kuisimamia serikali. Bunge halipaswi kujadili mambo madogo madogo ya Wilaya, Halmashauri na kata.

Mkuu hata hivyo una moyo wa kusikiliza hilo bunge. Mimi nimeshalipuuza muda mrefu, hata muda wa kulisikiliza sina.
 
Bunge linajadili kuhusu usambazaji wa picha za ngono mitandaoni! Yaani wabunge wanaumizwa na picha za ngono huku mitandaoni, maana wao na familia zao wanamiliki smartphones na wana hela za bundle, hivyo kwao hilo ndio tatizo! Mambo ya ajira, maji nk kwao sio shida maana hivyo vyote wanavimudu kutokana na vipato vyao.
 
Wabunge kutumia muda wa bunge la taifa kuulizia barabara ya wilaya na kituo cha afya na shule ya kata ya zitajengwa lini sio matumizi mazuri ya muda wa bunge, huenda wengine wanauliza ili wasikike tu na wao wameuliza.

Ikiwa bunge linatenga bajeti kila mwaka na kuweka mipango ya mwaka na miaka mitano kwa nini mbunge anainuka kuulizia tena mambo ya bajeti iliyotengwa na mipango ya jimboni kwake?

Bunge linapaswa kujadili bajeti kuu, sera na mipango ya kitaifa, miradi mikubwa ya kimkakati, mikataba, usalama wa nchi, sheria kuu za nchi na kuisimamia serikali. Bunge halipaswi kujadili mambo madogo madogo ya Wilaya, Halmashauri na kata.
Bunge la 2020 linajadili uganga wa kienyeji tu.

Mwigulu Feb, 2023
 
Mambo ya kimataifa yajadiliwe vipi na bunge?

Wale wabunge ni wawakilishi wa wananchi [hata kama ikisemwa hawakuchaguliwa na wanachi] sasa iweje hawa watu wakajadili mambo ya kimataifa bungeni? nani atawasemea wananchi wa maeneo yao kero zao?

Hayo unayosema; vituo vya afya, zahnati, na barabara, ndio mambo yanayowakera wananchi kwenye maeneo yao, ndio maana wako bungeni kuwasemewa na wabunge wao.

Mambo ya kimataifa iachie wizara ya mambo ya nje, hilo ndio jukumu lake, usitake bunge liingilie majukumu yasiyo yake.
 
Kama wabunge wanajadili mradi wa mamia ya mabilioni au trillion wa maji, afya, barabara, umeme n.k kwa ujumla wake au ambao ni wa kimkatai kwa wilaya au mikoa kadhaa hiyo ni sawa lakini kama mbunge anamuulizia bungeni waziri lini umeme wa REA utafika kata, kijiji au vitongoji kadhaa tu jimboni kwake hiyo sawa kabisa.

Hivyo vitongoji, kata na kijiji kama vipo ndani ya jimbo husika bado sioni tatizo lolote kwenye hilo, bado mbunge anafanya kazi yake ya kuwakilisha wananchi wake kwenye hayo maeneo husika, ndani ya jimbo lake.
 
Zingetungwa kanuni za mambo ya kitaifa na mambo ya kansel kwa madiwani. Hata maswali mengine yalipaswa yaelekezwe kwenye halmashauri. Mambo ya barabara za vijijini, maji na umeme nk madiwani wana haki ya kuhoji serikali kuu / mawaziri na majibu yakawasilishwa na mbunge au mkurugenzi
 
Wabunge kutumia muda wa bunge la taifa kuulizia barabara ya wilaya na kituo cha afya na shule ya kata ya zitajengwa lini sio matumizi mazuri ya muda wa bunge, huenda wengine wanauliza ili wasikike tu na wao wameuliza.

Ikiwa bunge linatenga bajeti kila mwaka na kuweka mipango ya mwaka na miaka mitano kwa nini mbunge anainuka kuulizia tena mambo ya bajeti iliyotengwa na mipango ya jimboni kwake?

Bunge linapaswa kujadili bajeti kuu, sera na mipango ya kitaifa, miradi mikubwa ya kimkakati, mikataba, usalama wa nchi, sheria kuu za nchi na kuisimamia serikali. Bunge halipaswi kujadili mambo madogo madogo ya Wilaya, Halmashauri na kata.
Ni kweli unachosema. Tatizo wabunge wetu walio wengi, upeo wao ni mdogo sana.

Ili uweze kujadili mambo makubwa unahitaji uwe na uelewa mkubwa kichwani mwako. Kwa sababu wengi uelewa na upeo wao ni mdogo, inawalazimu waokoteze mambo ya mitaani ndiyo wakayapeleke bungeni wakiamini hayo yatawafanya wasikike kwa wananchi. Lakini ukweli ni kwamba kuna wananchi wachache sana wenye muda wa kuwafuatilia wanaongea nini huko Bungeni kwa sababu inajulikana hakuna chochote cha maana.

Wakati ule Bunge likiwa na akina Dr. Slaa, Tundu Lisu, Mchungaji Msigwa, Chenge, Heche, n.k; humu JF zingekuwa zimejaa mada za Bunge.

Leo wabunge wanaongelea wanaume wasiotahiriwa! Sijui kutotahiriwa kwa hao wanaume kunaathiri vipi maendeleo ya nchi.
 
Back
Top Bottom