Madogo mnatudharua Mabroo zenu kisa tumeshindwa karibu Kila kitu

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,341
51,907
Mpo Pouwa.

Haya bhana! Yote Kheri. Mungu ndio anajua. Dharau mlizonionyeshea hakika kama kungekuwa na uchawi ningewaloga wote Mbuzi nyie, watoto niliowaona mkizaliwa, tukawakuza wenyewe, leo ninyi ndio wakuturushia mavi usoni? Kweli! kweli?

Kisa mmeshaanza kuzivua Sketi za Wadada sio? Au nini? Au niaje? Ni kwa vile vipesa vyenu mshenzi vya Udalali na kubeti ndio vinawapa kiburi? Afu dogo Mcheza amapiano unajua maneno yako bado hayajapotea akilini mwangu. Ni hiko kisabufa cha laki unusu ndio kilikufanya uropoke kwa jeuri kama tajiri anayedhamini wapiganaji wa Alshabab.

Kujua kuoga na kuvaa ndio sababu ya kutudharau siye kaka zenu tunaovaa marapurapu. Majukumu yetu ni makubwa madogo na mengi ajabu. Fikiri na fikiria familia zetu zatutegemea, waza na wazua jinsi ambavyo tunatakiwa tuwajengee ninyi ramani ili ninyi mpite kirahisi. Lakini kwa vile macho yenu machoni hayaoni mnatuona kama majinga na mbumbumbu!

Imefikia hatua mpaka mnatongoza Shemeji zenu ambao ni Wake Wetu. Hivi mnaakili ninyi watoto? Nitaua mtu Walahi! Nitapasua mtu mimi!
Kosa letu ni kuwakaribisha kwenye makazi yetu? Kosa letu ni lipi?

Vipafyumu vyenu vya elfu tano ndio vinawatia uchakaramu haramu kujitongozesha na kuwarubuni Wake zetu? Acheni dharau madogo. Jiheshiimuni tuwaheshimu.

Ni kweli kaka zenu maisha bado yanawezakuwa yanatusumbua. Huenda hata makazi kwetu ni shida. Huenda hata kula yetu bado niyakurushiana manati. Huenda bado tunapiga Wangwasuma kama Suma Jeikeitii mbele tembea nyuma geuka. Maisha yanatupeleka mperampera kama Gwaride la Hamas.

Lakini eleweni, Yote Mungu ndiye Muweza yote, na jitihada haizidi Kudura. Kufanikiwa kwenu msituone sisi mazombi na wazembe.

Nami nawaambia lililozama Magharibi ndilo hilohilo lilichomozea Mashariki. Na kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Kuweni na akiba ya maneno. Msitudharau sisi wala kumdharau yeyote kwa hali aliyonayo.

Jana mmenitukana mno. Labda mlisema mlikuwa mnanichana Ukweli. Kwa ukweli upi? Ninyi mnaujua ukweli ninyi? Si ninawauliza! Kama mngeujua ukweli basi msingenidharau.

Kisa mmefika Chuo kikuu? Au kisa nini? Au niaje?
Hamkuujua ukweli ndio maana mnatuona tuliowatangulia Wapuuzi na Watu tuliofeli. Hamtaki kutusalimia. Na tukiwasalimia mnasema tunataka kuwapiga kibomu, kuwakwara Pesa. Mnatuona kaka zenu washidashida.

Maneno yangu ni yaleyale, kuweni wapole na wanyenyekevu kabla maisha hayajawafundisha kwa njia ngumu.

Haya ngoja tuone mwisho wa mambo haya ni upi. Kama mlidhani tutashindwa kama mtuonavyo subirini mtaona. Siku zote mshindi hutokea mwishoni. Na mshindi ndiye atakayeandika historian.
Na mshindi ni yule atakayekuwa mkweli, muadilifu na mwenye haki na upendo.

Hasa wewe dogo mvaa vipensi na uliyepaka Bleach, kuwa Makini.

Alafu na wewe dogo mlokole, sijui msabato, sijui dini yako gani. Kuniona nimefeli maisha kwa sababu labda unadhani nilikuwa mhuni, au mjinga, au kuona kama nilimuasi Mungu basi nakuambia unakosea sana dogo.
Kutuona Kaka zenu tulioshindwa maisha kama waasi mbele za Mungu ni kutudharau. Mtajionea wenyewe, subirini Mkue mtayaona wenyewe.

Mimi acha nipumzike, kaugali kameshaiva.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Pole braza, ila ulikimbilia mwenyewe kuoa hukuishia hapo ukamzalisha mkeo kama vile mashine yafoto kopi Kila mwaka anazaa😁

Ndio Mimi nimdogo kwako lakini nimekuzidi timing broo niheshim.sio lazima nikusalimie wewe pia unaweza ukanisalimia umli ni namba tuu.

Na ukiwa na changamoto yahela usiste kusema braza.
 
pole braza.ila ulikimbilia mwenyewe kuoa hukuishia hapo ukamzalisha mkeo kama vile mashine yafoto kopi Kila mwaka anazaa😁

ndio Mimi nimdogo kwako lakini nimekuzidi timing broo niheshim.sio lazima nikusalimie wewe pia unaweza ukanisalimia umli ni namba tuu.

naukiwa nachangamoto yahela usiste kusema braza.

Nafikiri umeamua uwe sehemu yangu ya kutulizia hasira zangu za Maisha.
Nitapiga mtu. Ninyi madogo acheni dharau.
 
Taikon wa fasihi.

Labda nikukumbushe.
Ni kweli mmetufunza vyema, ni kweli mlituonesha njia sahihi ya sisi vijana wenu kuweza kupita.
Mmetulea vyema katika maadili yaliyotukuka.
Sina shaka na hilo.

Lakini nyinyi hao hao ndio leo hii mkaamua kutusaliti na kutugeuka.
Eti mnahofia mtapoteza milki zenu.

Wakati wenu ulikuwa ni ule na si sasa.
Sasa tumekuwa na tuna uelewa wa kila kitu katika ulimwengu huu.
Mapenzi mliyotuonesha kumbe yalikuwa ni yale yaliyojaa unafiki,mnayotuonesha kwenye mwanga na tuwapo gizani ni kuturushia mawe na kujinadi kwa kucheka.
"Wale hawatuoni hahahahaha"

Wakati wenu umeisha.
Pumzikeni kwa amani kabla hatujafikia uamuzi wa kuwapumzisha kwa mabavu.
Yangu ni hayo tu.
 
Taikon wa fasihi. Labda nikukumbushe. Ni kweli mmetufunza vyema, ni kweli mlituonesha njia sahihi ya sisi vijana wenu kuweza kupita. Mmetulea vyema katika maadili yaliyotukuka. Sina shaka na hilo. Lakini nyinyi hao hao ndio leo hii mkaamua kutusaliti na kutugeuka. Eti mnahofia mtapoteza milki zenu. Wakati wenu ulikuwa ni ule na si sasa. Sasa tumekuwa na tuna uelewa wa kila kitu katika ulimwengu huu. Mapenzi mliyotuonesha kumbe yalikuwa ni yale yaliyojaa unafiki,mnayotuonesha kwenye mwanga na tuwapo gizani ni kuturushia mawe na kujinadi kwa kucheka. "Wale hawatuoni hahahahaha" Wakati wenu umeisha. Pumzikeni kwa amani kabla hatujafikia uamuzi wa kuwapumzisha kwa mabavu. Yangu ni hayo tu.
Kupata majaliwa. Madogo acheni dharau
 
pole braza.ila ulikimbilia mwenyewe kuoa hukuishia hapo ukamzalisha mkeo kama vile mashine yafoto kopi Kila mwaka anazaa😁

ndio Mimi nimdogo kwako lakini nimekuzidi timing broo niheshim.sio lazima nikusalimie wewe pia unaweza ukanisalimia umli ni namba tuu.

naukiwa nachangamoto yahela usiste kusema braza.
Hahahaha 🤣🤣🤣🤣🤣 hahahaha hahaaaaaaaaaaaa....
 
Mpo Pouwa.

Haya bhana! Yote Kheri. Mungu ndio anajua. Dharau mlizonionyeshea hakika kama kungekuwa na uchawi ningewaloga wote Mbuzi nyie, watoto niliowaona mkizaliwa, tukawakuza wenyewe, leo ninyi ndio wakuturushia mavi usoni? Kweli! kweli?

Kisa mmeshaanza kuzivua Sketi za Wadada sio? Au nini? Au niaje? Ni kwa vile vipesa vyenu mshenzi vya Udalali na kubeti ndio vinawapa kiburi? Afu dogo Mcheza amapiano unajua maneno yako bado hayajapotea akilini mwangu. Ni hiko kisabufa cha laki unusu ndio kilikufanya uropoke kwa jeuri kama tajiri anayedhamini wapiganaji wa Alshabab.

Kujua kuoga na kuvaa ndio sababu ya kutudharau siye kaka zenu tunaovaa marapurapu. Majukumu yetu ni makubwa madogo na mengi ajabu. Fikiri na fikiria familia zetu zatutegemea, waza na wazua jinsi ambavyo tunatakiwa tuwajengee ninyi ramani ili ninyi mpite kirahisi. Lakini kwa vile macho yenu machoni hayaoni mnatuona kama majinga na mbumbumbu!

Imefikia hatua mpaka mnatongoza Shemeji zenu ambao ni Wake Wetu. Hivi mnaakili ninyi watoto? Nitaua mtu Walahi! Nitapasua mtu mimi!
Kosa letu ni kuwakaribisha kwenye makazi yetu? Kosa letu ni lipi?

Vipafyumu vyenu vya elfu tano ndio vinawatia uchakaramu haramu kujitongozesha na kuwarubuni Wake zetu? Acheni dharau madogo. Jiheshiimuni tuwaheshimu.

Ni kweli kaka zenu maisha bado yanawezakuwa yanatusumbua. Huenda hata makazi kwetu ni shida. Huenda hata kula yetu bado niyakurushiana manati. Huenda bado tunapiga Wangwasuma kama Suma Jeikeitii mbele tembea nyuma geuka. Maisha yanatupeleka mperampera kama Gwaride la Hamas.

Lakini eleweni, Yote Mungu ndiye Muweza yote, na jitihada haizidi Kudura. Kufanikiwa kwenu msituone sisi mazombi na wazembe.

Nami nawaambia lililozama Magharibi ndilo hilohilo lilichomozea Mashariki. Na kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho. Kuweni na akiba ya maneno. Msitudharau sisi wala kumdharau yeyote kwa hali aliyonayo.

Jana mmenitukana mno. Labda mlisema mlikuwa mnanichana Ukweli. Kwa ukweli upi? Ninyi mnaujua ukweli ninyi? Si ninawauliza! Kama mngeujua ukweli basi msingenidharau.

Kisa mmefika Chuo kikuu? Au kisa nini? Au niaje?
Hamkuujua ukweli ndio maana mnatuona tuliowatangulia Wapuuzi na Watu tuliofeli. Hamtaki kutusalimia. Na tukiwasalimia mnasema tunataka kuwapiga kibomu, kuwakwara Pesa. Mnatuona kaka zenu washidashida.

Maneno yangu ni yaleyale, kuweni wapole na wanyenyekevu kabla maisha hayajawafundisha kwa njia ngumu.

Haya ngoja tuone mwisho wa mambo haya ni upi. Kama mlidhani tutashindwa kama mtuonavyo subirini mtaona. Siku zote mshindi hutokea mwishoni. Na mshindi ndiye atakayeandika historian.
Na mshindi ni yule atakayekuwa mkweli, muadilifu na mwenye haki na upendo.

Hasa wewe dogo mvaa vipensi na uliyepaka Bleach, kuwa Makini.

Alafu na wewe dogo mlokole, sijui msabato, sijui dini yako gani. Kuniona nimefeli maisha kwa sababu labda unadhani nilikuwa mhuni, au mjinga, au kuona kama nilimuasi Mungu basi nakuambia unakosea sana dogo.
Kutuona Kaka zenu tulioshindwa maisha kama waasi mbele za Mungu ni kutudharau. Mtajionea wenyewe, subirini Mkue mtayaona wenyewe.

Mimi acha nipumzike, kaugali kameshaiva.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Umevurugwani?
 
Taikon wa fasihi.

Labda nikukumbushe.
Ni kweli mmetufunza vyema, ni kweli mlituonesha njia sahihi ya sisi vijana wenu kuweza kupita.
Mmetulea vyema katika maadili yaliyotukuka.
Sina shaka na hilo.

Lakini nyinyi hao hao ndio leo hii mkaamua kutusaliti na kutugeuka.
Eti mnahofia mtapoteza milki zenu.

Wakati wenu ulikuwa ni ule na si sasa.
Sasa tumekuwa na tuna uelewa wa kila kitu katika ulimwengu huu.
Mapenzi mliyotuonesha kumbe yalikuwa ni yale yaliyojaa unafiki,mnayotuonesha kwenye mwanga na tuwapo gizani ni kuturushia mawe na kujinadi kwa kucheka.
"Wale hawatuoni hahahahaha"

Wakati wenu umeisha.
Pumzikeni kwa amani kabla hatujafikia uamuzi wa kuwapumzisha kwa mabavu.
Yangu ni hayo tu.

Ninyi ndio mtapumzika kwa amani.
Nishasema Linalozama magharibi ndio hilohilo lilichomozea Mashariki.
Ninyi si wajiajiri. Tutaona
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom