Kama tumeshindwa si aibu

Sijali

JF-Expert Member
Sep 30, 2010
2,589
1,679
Leo hii watu wengi washangazwa na namna nchi za Ghuba ya Uajemi, kama Emirati, Kuweit, Oman na Qatar zilivyopiga hatua kubwa, ambapo miaka ya sitini hadi sabini nchi hizi zilikuwa nyuma na maskini hata kuliko Tanzania.
Ujanja walioufanya ni kuwa: kwanza walitambua na kukubali kuwa wao wako nyuma. Pili walitambua kuwa itawachukua miaka mingi sana wakitaka wao wenyewe wajiendeleze bila ya msaada wa wengine, kuanzia kusoma, kuhitimu, kupata uzoefu nk. Walichokifanya: waliwaalika wahamiaji kwa wingi, hasa wale wenye fani zilizohitajia uzoefu. Wakawa wanawachukua 'wastaafu' katika fani mbali mbali kutoka Ulaya na Marekani kuwaendeshea mathalan miundombinu ya barabara, mipango miji, vyuo na mashule na hata majeshi. Wakati huo wote wakiwatuma raia wao nje kusoma, na wale waliopo ndani kupata uzoefu kwa wageni hawa. Ndipo hii leo twawaona wameendelea kwa muda mfupi, na sasa watu wao wamerudi kuendesha yale waliyokuwa wakiendesha wageni.
Waarabu hawakuwa wachoyo au wajinga wa kutaka 'to re-invent the wheel' (kuvumbua upya gurudumu) kama wasemavyo Waingereza. Bali walikubali kuwa wapole, wasikizi na hata wanyonge hadi mradi wao ulipotimia. Hii leo hata Wazungu wanahamia Dubai ili waajiriwe chini yao!
Fananisha hao na akili ya kichoyo na kiburi ya Mwafrika. Ni dhahiri kuna mambo mengi hatuyajui wala hatuyawezi, lakini kwa akili zetu za 'kizalendo' afadhali tuharibu kuliko kuongozwa na 'mgeni'. Unaona mambo yanaenda kombo kila kona: bandari, elimu, kilimo, usimamizi wa madini, mipango miji, elimu ya kodi, mabenki, mifuko ya ustaafu....mengi ni kwa sababu ya ukosefu wa taaluma na experience. Lakini tumeshikilia pale pale 'uzalendo' na akiliza 'Kibanga ampiga mkoloni'!
Sehemu pekee tunapo 'meza' kiburi chetu ni mpira wa miguu. Katika mpira tu tunaruhusu 'wageni' waje kutusaidia! Kana kwamba mpira ndiyo kipa umbele cha maisha ya Watanzania!
Pumbaaaaaaaaf!
 
If you look at their mode of life and their lifestyle in general you can observe that BLACKS are born with the situation like an half-mad mentality and mindsets."
Jan Smuts, the First Prime Minister of Union of South Africa
 
Leo hii watu wengi washangazwa na namna nchi za Ghuba ya Uajemi, kama Emirati, Kuweit, Oman na Qatar zilivyopiga hatua kubwa, ambapo miaka ya sitini hadi sabini nchi hizi zilikuwa nyuma na maskini hata kuliko Tanzania.
Ujanja walioufanya ni kuwa: kwanza walitambua na kukubali kuwa wao wako nyuma. Pili walitambua kuwa itawachukua miaka mingi sana wakitaka wao wenyewe wajiendeleze bila ya msaada wa wengine, kuanzia kusoma, kuhitimu, kupata uzoefu nk. Walichokifanya: waliwaalika wahamiaji kwa wingi, hasa wale wenye fani zilizohitajia uzoefu. Wakawa wanawachukua 'wastaafu' katika fani mbali mbali kutoka Ulaya na Marekani kuwaendeshea mathalan miundombinu ya barabara, mipango miji, vyuo na mashule na hata majeshi. Wakati huo wote wakiwatuma raia wao nje kusoma, na wale waliopo ndani kupata uzoefu kwa wageni hawa. Ndipo hii leo twawaona wameendelea kwa muda mfupi, na sasa watu wao wamerudi kuendesha yale waliyokuwa wakiendesha wageni.
Waarabu hawakuwa wachoyo au wajinga wa kutaka 'to re-invent the wheel' (kuvumbua upya gurudumu) kama wasemavyo Waingereza. Bali walikubali kuwa wapole, wasikizi na hata wanyonge hadi mradi wao ulipotimia. Hii leo hata Wazungu wanahamia Dubai ili waajiriwe chini yao!
Fananisha hao na akili ya kichoyo na kiburi ya Mwafrika. Ni dhahiri kuna mambo mengi hatuyajui wala hatuyawezi, lakini kwa akili zetu za 'kizalendo' afadhali tuharibu kuliko kuongozwa na 'mgeni'. Unaona mambo yanaenda kombo kila kona: bandari, elimu, kilimo, usimamizi wa madini, mipango miji, elimu ya kodi, mabenki, mifuko ya ustaafu....mengi ni kwa sababu ya ukosefu wa taaluma na experience. Lakini tumeshikilia pale pale 'uzalendo' na akiliza 'Kibanga ampiga mkoloni'!
Sehemu pekee tunapo 'meza' kiburi chetu ni mpira. Katika mpira tu tunaruhusu 'wageni' waje kutusaidia! Kana kwamba mpira ndiyo kipa umbele cha maisha ya Watanzania!
Pumbaaaaaaaaf!
Ni muda wa kuanza kukubaliana na matatizo yetu na kuruhusu wenye uwezo wa kuyatatua kushiriki kuyatatua.

Tuachane na fikra za kijinga tulizo nazo sasa.
 
Kuukalia uchumi ndio chaguo kuliko kuleta wenye rasilimali na ujuzi kuanzisha miradi na kushare matunda.
Nasikia mazungumzo ya ubia wa mradi wa gesi mtwara uko hatarini kuvunjika sababu wawekezaji wanaona hakuna tija.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom