MTAZAMO
JF-Expert Member
- Feb 8, 2011
- 19,643
- 33,432
Inawezekana Gwajima kawakera wengi lakini kwangu nashukuru amesema maana tunaijua nchi yetu, tatizo la umeme lilitumika tukapigwa! Hata hii issue ya Uviko ni vizuri maswali ya msingi yajibiwe kitaalam.Wanabodi,
Nimemsikia Mbunge wangu Mhe. Askofu Gwajima akipinga chanjo ya Covid na sio tu kuhamasisha watu waikatae bali hadi kutishia kwa kuwahukumu kifo, wote watakao wachanja watu!
Askofu wetu anahitaji kuelimishwa, kwanza yeye, kama Mbunge, ni mtumishi wa umma wa Watanzania wote, kisha ndio kiongozi wa kiroho kwa waumini na wafuasi wake. Hawezi kuhubiri jambo lolote mimbarini kwake, ambalo ni kinyume cha maslahi ya taifa.
Kwenye vita yoyote ya kitaifa, kama ilivyo vita ya Corona, ili kushinda vita, viongozi wote, must stand as one, Tanzania kama Taifa likiisha kubali Chanjo ya Covid Ndio Maslahi ya Taifa, Viongozi wote wa umma, wanakuwa bind na a collective responsibility clause, they must support, msimamo wa serikali.
Na kama hukubaliani na msimamo huo wa serikali, then unapaswa kunyamaza kimya yaani, "Shut Up" or kama huwezi kunyamaza, then you just Quit!
Kitendo cha kupingana na msimamo wa serikali wazi wazi kama alivyofanya Gwajima, huo ni usaliti, anatakiwa kushughulikiwa kama wasaliti wengine wote, na hatua ya kwanza ni kuachia ngazi kama mtumishi wa umma na kubaki na kazi moja tuu ya kuwachunga kondoo wake. Kitendo cha kuitumia mimbari kuhubiri siasa ni kuchanganya dini na siasa!
Je, Askofu Gwajima afanywejwe?
Pasco.
Zipo taarifa nyingi za waliochanjwa huko nje kuwa ni waathirika wa hili wimbi jipya la uviko, je kinga imesaidia nini?
What if hao wanaochanjwa ndio wanakuja kuambukiza zaidi (hapa wataalam wafafanue).
Baadhi ya chanjo zilisitishwa huko zinakotoka je tumejirithisha ni salama kwa utafiti upi? Wasiwasi isiwe tumetumia maelekezo ya hao manufacturers kuamua badala ya kufanya utafiti hadi wa components za chanjo hizo. Kamati iliyotushauri ilifanya kazi siku chache tu!
Matokeo ya matumizi ya hizi chanjo si lazima iwe ni mwezi au wiki, madhara yanaweza kutokea hata miaka 10 au zaidi ijayo!
Huu ugonjwa kuanzia kuibuka kwake hadi suluhisho lake yamejaa utata mwingi sana, tunapaswa kwenda kiutata hivyo hivyo badala ya wimbo wa twende na dunia! Hoja za hao wazungu wangetaka kutumaliza wangeshafanya hivyo ni mfu maana ni sawa usahau kufunga mlango hadi asubuhi alafu sababu hukuibiwa basi uamue kuishi daima bila kufunga mlango!
Mwisho, Mch Gwajima staili yake ya kujenga hoja Inawezekana kuleta ukakasi na kama alivyosema Mh January Makamba mjadala juu ya usalama wa chanjo ni muhimu lakini si kuhamasisha kinyume ili maoni yako tu yachukuliwe.
Hata mimi binafsi ningetamani swala ya usalama wa chanjo lijadiliwe na wataalamu kwa uwazi baada ya kufanyika utafiti wa kina ikiwemo hizo components za chanjo. Ndio maana baadhi ya mataifa wametengeneza chanjo zao kwa usalama wao.
Swala la chanjo hata kama ni hiari haiondoi wajibu wa serikali tunayoiamini kuweka mazingira ya kuaminika juu ya swala hili. Chanjo na facts zake plus conspiracy inayoizunguka inahitaji kujibu maswali ambayo ni mjadala dunia nzima.