#COVID19 Kama Taifa limekubali chanjo ndio maslahi ya Taifa, Viongozi wote wanakuwa Bind na A Collective Responsibility Clause. Must support, Shut up or quit!

Tuwe wakweli kwenye hili. Polisi au chombo cha dola chenye mamlaka kilipaswa IMMEDIATELY kumkamata na kumhoji huyu FAKE PASTOR Gwajima. Ametoa tuhuma nzito kuhusu watu walioruhusu chanjo ziingie Tanzania kuwa wanahongwa au na Bill Gates au na wazakishaji wa chanjo wa Marekani.

Kwa uelewa wangu aliyeruhusu chanjo zije ni Rais Samia baada ya kushauriwa na timu yake ya wataalamu. Kwa hiyo tuhuma ya Gwajima inamlenga Rais SSH moja kwa moja.

TISS na POLISI kamata huyu Fake Pastor Gwajima
Mpaka leo bado anazidi kuleta damage, bado hajakamatwa
 
Sikubaliani na msimamo wa Gwajima uliotokana na kukosa elimu, lakini Gwajima hawajibiki kuendana na msimamo wa serikali. Gwajima siyo kiongozi, yeye ni muwakilishi tu wananchi. Hawajibiki kuunga mkono matendo ya serikali.
 
Waziri wa Afya, Dorothy Gwajima karudi na rungu.

Ametoa rai kuwa viongozi ambao mpaka sasa hawajachanjwa, watatakiwa waachie ngazi kwani hawawezi kusimamia kampeni ya kusimamia uchanjwaji dhidi ya corona.

Waziri wa Afya amesema kama Rais kachanja ili iwe mfano, sasa hao viongozi hawatetei msimamo wa Serikali

Tulisha liona hili huko nyuma: #COVID19 - Kuchanja sasa kuwe lazima, hasa wafanyakazi serikalini. Chanja au achia ngazi

View attachment 2028866
Naunga mkono hoja, hiki alichokisema Waziri Gwajima, ni kitu cha kweli, kama serikali yako imekubali chanjo na rais wako kachanja, wewe kiongozi wa umma, lazima uonyeshe uongozi kwa vitendo na kwa mfano, kwa viongozi wote wakuu wa umma lazima wachanje hadharani, ule uhiari, hauwahusu viongozi wa umma, kwa viongozi wa umma kuchanja ni lazima, asiyechanja aachie ngazi!.

Niliwahi kusema mahali, chanjo ya Korona japo inasemwa kuwa ni hiyari, hii ni hiyari ya lazima, kuna nchi mtu huruhusiwi kuingia bila cheti cha chanjo ya Corona. Hivyo sasa tunaanza mdogo mdogo kwa viongozi wa umma, chanjo sio hiyari ni lazima,
kama wewe ni kiongozi wa umma na huamini chanjo, achia ngazi!.
P.
 
Nawewe Pascali pungunza mihemko bwwana, hii ngoma ya corona inaitaji akili sana kukabiliana nayo, siyo ya kukurupuka nayo... Mpaka sasa tunasikia habari ya wimbi la NNE ambalo wataalam wanakuambia ni kirusi hatari zaidi ya yule wa awali, kiasi kwamba uchanjwe usichanjwe hathari ziko pale pale....
Cheki kwa sasa Taifa la Afrika ya kusini limeanza kunyanyapaliwa kisa Corona...na wakati kirusi kipo hadi ulaya wanako tunyanyapa....tutulie na kauli zetu hii vita ni yakirohoo bro, siyo ya kimwili.
 
Wanabodi,

Nimemsikia Mbunge wangu Mhe. Askofu Gwajima akipinga chanjo ya Covid na sio tu kuhamasisha watu waikatae bali hadi kutishia kwa kuwahukumu kifo, wote watakao wachanja watu!

Askofu wetu anahitaji kuelimishwa, kwanza yeye, kama Mbunge, ni mtumishi wa umma wa Watanzania wote, kisha ndio kiongozi wa kiroho kwa waumini na wafuasi wake. Hawezi kuhubiri jambo lolote mimbarini kwake, ambalo ni kinyume cha maslahi ya taifa.

Kwenye vita yoyote ya kitaifa, kama ilivyo vita ya Corona, ili kushinda vita, viongozi wote, must stand as one, Tanzania kama Taifa likiisha kubali Chanjo ya Covid Ndio Maslahi ya Taifa, Viongozi wote wa umma, wanakuwa bind na a collective responsibility clause, they must support, msimamo wa serikali.

Na kama hukubaliani na msimamo huo wa serikali, then unapaswa kunyamaza kimya yaani, "Shut Up" or kama huwezi kunyamaza, then you just Quit!

Kitendo cha kupingana na msimamo wa serikali wazi wazi kama alivyofanya Gwajima, huo ni usaliti, anatakiwa kushughulikiwa kama wasaliti wengine wote, na hatua ya kwanza ni kuachia ngazi kama mtumishi wa umma na kubaki na kazi moja tuu ya kuwachunga kondoo wake. Kitendo cha kuitumia mimbari kuhubiri siasa ni kuchanganya dini na siasa!

Je, Askofu Gwajima afanywejwe?

Pasco.
Wito huu ni muhimu sana, kilichobaki ni CCM kuonyesha uwezo wa kuwashikisha adabu.

Mtu huwezi kumdharau rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM. Najua wote watapiga magoti kuomba msamaha, nashauri kwa Polepole na Gwajima, msamaha wao iwe ni kuchanja hadharani, kisha wawahamasishe wafuasi wao kuchanja. Jerry Slaa asamehewe tuu bila masharti.
P
 
Wito huu ni muhimu sana, kilichobaki ni CCM kuonyesha uwezo wa kuwashikisha adabu.

Mtu huwezi kumdharau rais wa JMT na Mwenyekiti wa CCM. Najua wote watapiga magoti kuomba msamaha, nashauri kwa Polepole na Gwajima, msamaha wao iwe ni kuchanja hadharani, kisha wawahamasishe wafuasi wao kuchanja. Jerry Slaa asamehewe tuu bila masharti.
P
Msimamo ni ule ule hakuna kuchanjwa sisi wa ufufuo na uzima.
Nyie wengine chanjeni, hata mkichanja mara 100.

Kwani ubunge kitu gani au kuwa CCM ndo ufunguo wa kuingia mbinguni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Gwajima ni mpumbavu tu na wanayemuunga mkononi wapuuzi vilevile.Hoja ni chanjo au chanjo ya Mmarekani? Kama hoja ni chanjo ya mmarekani kwanini iwe ya corona pekeyake na si chanjo zingine ambazo watoaji ni wale wale.

Chanjo za watoto chini ya miaka 5 zinatolewa na hao hao bure, kwanini nazo tusizikate, maana kama lengo ni kutuuua
watatumia hata hizo za watoto za surua, ndui, kifua kikuu, tetekuwanga, polio, pepopunda (tetenus) za wajawazito.

Hakuna dawa hospitalini zilizotengenezwa na waafrica, zote zinatoka kwa hao hao.Dawa za Ukimwi, kifua kikuu, presha, kisukali, madawa ya operation, Cancer kwa Ujumla dawa zote zinatoka kwa hao watu weupe, hivyo awaambie sereikali wapige marufuku dawa zote za wazungu zisitumike nchini, vinginevyo kama nia ni kutuuua watatumia haya madawa na chanjo kutekeleza azma yao.

Kama issue ni mmarekani tuagize chanjo ya Urusi au China au Cuba au Iran maana naye nasikia anatengeneza yake.

Ni Mpumbavu pekee anayetaka Tanzania ijitenge na dunia kwenye chanjo wakati hatuna uwezo wa kutengeneza kidonge
.Mtu yeyote humu ataje kidonge kilichowahi kutengenezwa Tanzania na kutumika humu nchini. Ni wendawazimu kudhani nchi
ambazo haina urafiki wowote kama Marekani na Urusi au na China au na Cuba au na Irani eti ziungane kwenye suala la chanjo ili kuwaua Watanzania.

Huyu bwege Gwajima anachanganya tu habari mara analeta mambo ya dini eti chapa 666 sijui chanjo ni mpinga kristo, kama ni hivyo basi tulishapigwa chapa ya ndui mara bado ipo kwenye majaribio, mara zimetengenezwa kwa muda mfupi, anajaribu kulinganisha
chanjo zilizotengenezwa miaka ya 1950s wakati teknoloji ikiwa duni na miaka hii ambapo dunia ipo mbali kiteknolojia.

Anataka kutuambia hizo nchi ambazo zimetengeneza chanjo ambazo ambazo kwanza zina sera na mitazamo tofauti, zote zina lengo la kuwaua watanzania? Kwa kipi kilichopoTanzania hadi wapange njama za kuua watanzania? na kwa faida ipi kwao? Bongo kweli vilaza wanazidi kuongezeka
Yani wewe mpumbavu bado unauliza ilo swali ambalo lina majibu siku nyingi ,kwani ujui chanjo zote tunazo tumia zimepayikana kwa utaratibu tofauti wa hii ya covidi ??? ,je kunaugonjwa gani wenye chanjo nyingi kama kovidi?, mbona magonjwa yote yanachanjo aina moja au mbili tu sasa covidi inachanjo za tofauti zaidi ya aina 10 tena zikiwa tatanishi wala hazina ufanisi kama chanjo za magonjwa mengine nje ya kovidi ,,,,sasa acha nikujibu swali lako la wapinga chanjo...kwanza atupingi chanjo bali tunapinga hizi chanjo feki za kovidi hadi itakapo patikana chanjo ya uhakika kama chanjo ya ndui na zinginezo . Pia kwanini Rais Samia kachanja mara moja wakati wazungu wana chanja mara hadi 4 kubust ,kama kweli yeye bado anayo imani na chanjo kwanini achachanja mara nyingi ili kubusti
 
Kitendo cha kupingana na msimamo wa serikali wazi wazi kama alivyofanya, huo ni usaliti, anatakiwa kushughulikiwa kama wasaliti wengine wote, na hatua ya kwanza ni kuachia ngazi kama mtumishi wa umma
Pasco.
Spika JYN ameonyesha njia, kama taifa limekubali mkopo, kupinga mkopo hadharani ni usaliti na Spika ameachia ngazi, vipi hawa viongozi wa umma wapinga chanjo?.
P
 
Back
Top Bottom