#COVID19 Kufuatia Umuhimu wa Chanjo Kwa Baadhi ya Kada, Kuna Haja ya Kuanzisha Hiyari ya Lazima, Watu Wachanje Kwa Lazima au Tuendelee Kubembelezania Hiyari?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,468
113,583
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" mada ya leo ni kuhusu chanjo ya Corona.

Naomba uanze bandiko hili kwa hii clip

Kufuatia Umuhimu wa Chanjo Kwa baadhi ya kada, japo chanjo ni hiyari, na ukweli ni kwamba mwitikio wa kuchanja kwa hiyari bado ni mwitikio duni, Ili kuliokoa taifa kwa zile kada muhimu na kada hatarishi, jee kuna kuna umuhimu sasa na sisi Tanzania kuanzisha hiyari ya lazima kwa baadhi ya kada hatarishi kuambukizika kwa urahisi na zile kada muhimu, au tuendelee tuu na uhamasishaji wa kubembelezania chanjo ni hiyari?.

Baadhi ya nchi za wenzetu wamefanya chanjo ni hiyari ya lazima kwa baadhi ya kada, mfano majeshi, polisi, public workers, ni lazima wachanje, asiyetaka aachie ngazi au kufukuzwa kazi.

Hivi sisi Tanzania, kama kweli tuko serious na chanjo, kuna ubaya wowote nasi tukaanzisha hiyari ya lazima?.
Paskali.
Rejea kuhusu chanjo ya Corona



 
Kabla ya kuandika haya uliyoyaandika kuna maswali kama journalist ulipaswa kujiuliza.

1. Huko tunapoita kwa wenzetu wamefanikiwa kuondoa tatizo?,

2. Je , tangia wameanza kuchanja kwa zaidi ya asilimia 80 ya watu wao tatizo limeongezeka au limepungua ?

3. Je, tunachanja as a matter of fashion au tunachanja kukabiliana na tatizo ambalo data zote zinaonyesha chanjo zimeshindwa kulikabili?

4. Vipi kuhusu utaratibu wa boosters , tutawamambiaje watu kurudia kuchanja kwa mara ya pili wakati wenzetu waliochanja kwa lazima na boosters juu bado imeshindikana?

5. Tafiti zinaonyesha jamii ya watu weusi hataa huko US ndio wamechanjwa kwa uchache wengi wakipinga hiyo chanjo, vipi kuhusu Tz yenye majority weusi , unategemea watakubali kirahisi tu!?
 
Tuchanje kwa kulazimishana pale tu itakapopatikana chanjo moja inayoeleweka na itakayoonesha matokeo makubwa. Kuna nchi mpaka Sasa wamechanja chanjo sita! Na bado tatizo lipo, Tanzania waliotangulia wapo wenye chanjo tatu, mbili, moja na zero.

Kwakua hatujafikia hatua mbaya ya maambukizi tuendelee kubembelezana na kuombana na chanjo ibaki kuwa hiari.
 
Angalia hii video, utajua kuwa UVIKO-19, ni ya kutengeneza.
Na hatuwezi kwenda kwa akili za "ki Pasco Mayalla" tukafanikiwa.
C - Coronavirus
O - Omnicron virus
V - ?????
I - Ihu virus
D - Delta virus.

Haya chanjeni, bado hiyo "V" inakuja. Mtapiga booster!
 
Kwa nini ulazimishe watu kuchanja?
Kama wewe umechanja si hautapata madhara ya COVID-19 wewe kama wewe?
Uliyechanja baki na chanjo yako, na wasiochanja wabaki na msimamo wao.
Ni Nchi gani iliyochanja na mpaka sasa imeondoa tatizo la Covid?
 
Huna hata chanjo moja uliyozalisha kwa kufanya tafiti zako, ambayo walau imefanyiwa majaribio kwa mazingira yako ikatoa matokeo chanya. Halafu, uje uweke ulazima kwa chanjo wamezalisha wengine huko!!!

Hii ni kulazimisha kufanyia kazi mawazo wa wengine bila ku challenge.

Umeandika kwa mtindo wa swali ndiyo, lakini Corona siyo tatizo kama wakati uleeeee.
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huja na makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa" mada ya leo ni kuhusu chanjo ya Corona.
Kaka Paskali unazungumzia kuchanja kwa aina gani? Mtaani huku watu wana kadi kuwa wamechanja, tena wengine hata ile ya pili lakini hawajanja. Kwahiyo, kama kadi ndio kitambulisho cha kuchanja, kalaghabhao!!!
 
Kinga isiyokinga ni mtihani mkubwa sana kuelewesha kwa Watu.

Hoja ya kwamba ukipata chanjo hata ukipata covid huumwi sana bado ni hoja isiyoniingia sana akilini, kwani bado wapo wanaopata maambukizi na kupata madhara madogo au hata wasionyeshe dalili yoyote ili hali hawajachanjwa.
 
P umechanjwa?? Tuanze na wewe!
Au umeshakuwa kibaraka wa chanjo?!
Serikali ina michanjo hakuna wananchi wanakubali kuchanjwa,
Sasa inahofia michanjo ITAEXPAYA, ndiyo kina Paskali wanapoanza kutumika kutuletea propaganda za kuhamasisha chanjo!

Sijachanjwa, na sijaugua, siyo Delta, Alpha, Omicron wala Microphone!

HAINA maana kuchanjwa kisha kila baada ya muda unachanjwa tena tutageuka broilers!
Kila wiki chanjo!
 
Back
Top Bottom