Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Mkuu umekurupuka toka wapi?Ulikuwa wapi kipindi miaka 6 inapita bila kuongezwa hata mia. Kama hukujitokeza kudai kwa woga wako tuliza kiherehere.
We hujui?Kwa nini wafanyakaz huongezewa au huwa wanastahili kuongezewa mshahara?
Ndio maana nimeulizaWe hujui?
Kasome ibara ya 23(2) ya katiba ya JMT.Ndio maana nimeuliza
iweke hapa mkuu niisome.Kasome ibara ya 23(2) ya katiba ya JMT.
Hoja hapa ni kuongeza mishahara kwa mujibu wa katiba ya JMT. Hivyo iwe ni mshahara mdogo au mkubwa lakini lazima uwe just renumeration. Hakuna nchi isiyokuwa na sekta ya umma au binafsi. Kama ndio hivyo hata huko Usa watu wote wangefanya kazi sekta binafsi.Piganeni uzalishji wenye ufanisi na uchumi upande, mpaka watu wawe na uwezo wa kuacha kazi zenye mishahara midogo serikalini, waende kufanya kazi zenye mishahara mikubwa au biashara sekta binafsi.
Karibu dunia nzima kazi za serikali ni kazi zenye mishahara midogo.Kuna siku nilikuwa naangalia kitu kinahusiana na kazi za Wafanyakazi wa Ikulu ya Marekani. Uzuri wa Marekani vitu vingi vinawekwa wazi mitandaoni, hususan vitu vya serikali vinavyoenda kwa kodi za wananchi.
Nilivyoona mishahara yao (wafanyakazi wa White House) wengi sana ilikuwa kama wanafanya kazi za kujitolea, wengine mishahara yao niliwazidi kwa mara mbili, karibia tatu.Hawa ni watu waliosoma mpaka graduate school wengi wao,wana masters au zaidi.
Lakini mishahara yao ukiiangalia unaona kabisa hawa hawakwenda kufanya kazi kwa sababu ya mshahara. Ama wana nia ya kusaidia watu, ama wanataka kutengeneza connections na experience wazifanyie kazi baada ya kufanya kazi serikalini.
Kuna gavana mmoja wa state maarufu Marekani aliamua kutogombea tena u gavana, huku watu wanampenda bado. Aliulizwa na mtu wangu wa karibu kwa nini hagombei?Akajibu kwamba kazi za serikali zina maslahi madogo, anataka kwenda kufanya kazi kwenye private sector kwenye maslahi makubwa, kwani anaona kashachangia uongozi wa serikali, ni zamu ya watu wengine kuchangia.
Sisi tatizo letu hatuna private sector ya kueleweka ku absorb watu, watu wanahemea kazi za serikali na wanataka ziwatoe. Granted, mishahara ikiwa chini sana inakuwa kama utumwa, hata kazi ya wito lazima iangalie basic needs.Lakini, bila kujenga private sector yenye ufanisi na uchumi mzuri, kutegemea mishahara ya serikali ipande ni mbio za sakafuni. Kwa sababu serikali yenyewe inaendeshwa kwa kodi za private sector.
Ukianza kupanga mshahara mkubwa na kuulazimisha serikalini, kama nchi ina uchumi mdogo, walipa kodi wachache, hata huo mshahara serikali ikipandisha itakuwa na matatizo kulipa watu.
Hizi ni kanuni za uchumi tu.
Nyongeza ya namna gani unayoizungumzia? Mimi nazungumzia nyongeza inayokidhi mahitaji ya mfanyakazi. Nakushauri wewe acha kukariri kuwa Paye ndogo ndio kupata mshahara mkubwa.Tumia akili kdg, unaweza kupewa hiyo nyongeza ya kila mwaka ila PAYE ikawa kubwa sana. Hata hiyo nyongeza ikaoneka si kitu chochote
Acha usumbufu.iweke hapa mkuu niisome.
Wewe ndiyo msumbufu kuja kulalamikia nyongeza ya mshahara.Acha usumbufu.
Hao wa sekta binafsi unaowazungumzia ni wa aina gani? 80% ya sekta binafsi wanafanya kazi kwa wachina na wahindi na mishahara yao ni midogo sana.Wafanyakazi wa serikalini mnapenda sana kulialia,wenzenu wa binafsi hawajui mambo hayo mnayodai na wanaishi.Hawana mikopo wala nyongeza wanaishi tu na wamejipanga vizuri hadi ni wenye nyumba wenu.Nyie mnafeli wapi?
Mimi nazungumzia haki ya kikatiba ya kila mtanzania.Wewe ndiyo msumbufu kuja kulalamikia nyongeza ya mshahara.
Kwa hiyo hawastahili nyongeza?Mbona wanakatwa kodi inaenda Serikalini kama ni kwa wahindi na wachina wasiachwe tu?Watu walipe kodi wanaofanya kazi kwa wachina wewe upewe nyongezza ya mshahara?Sasa sikiliza Chagu,Ili nyongeza iwepo lazima uchumi ukue.Hao wa sekta binafsi unaowazungumzia ni wa aina gani? 80% ya sekta binafsi wanafanya kazi kwa wachina na wahindi na mishahara yao ni midogo sana.
Kwa wafanyakazi wa Serikalini tu?Mimi nazungumzia haki ya kikatiba ya kila mtanzania.
Mkuu kwani rais akitangaza nyongeza kima cha chini huwa anabagua sekta binafsi?Kwa hiyo hawastahili nyongeza?Mbona wanakatwa kodi inaenda Serikalini kama ni kwa wahindi na wachina wasiachwe tu?Watu walipe kodi wanaofanya kazi kwa wachina wewe upewe nyongezza ya mshahara?Sasa sikiliza Chagu,Ili nyongeza iwepo lazima uchumi ukue.