Chagu wa Malunde
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 8,708
- 5,711
Kwanza kabisa watanzania wanatakiwa kutambua kuwa kila mtanzania anayo haki ya kupata mshahara unaostahili kukidhi mahitaji ya msingi. Ibara ya 23(2) imetamka wazi kuwa watanzania wanaofanya kazi wanatakiwa wapate just remuneration. Hivyo kupata mshahara unaostahili ni takwa la kikatiba na ni haki ya msingi.
Inapotokea mkuu wa nchi haongezi mshahara watumishi wa umma au sekta binafsi kwa muda wa miaka sita hili ni tatizo kubwa. Mbaya zaidi ni sababu zinazokuwa zinatolewa kuwa ni kuwekeza kwanza kwenye maendeleo ya taifa ili baadae wafanyakazi waongezwe mishahara.
Mbaya zaidi wakati mnajikita kuwekeza kwenye maendeleo gharama za maisha pia zinapanda juu hivyo ni wazi kuwa hata kama taifa linajenga miundo mbinu, shule na mahospital kwa miaka sita gharama za maisha pia zitakuwa zimepanda juu, maana miaka sita sio haba.
Achana na kujikita katika kuwekeza kwenye maendeleo. Mkuu wa nchi anaposema kuwa hawezi kuongeza mshahara sababu ya ugonjwa ambao haijulikani lini utaisha hili nalo ni tatizo. Kama Covid 19 ndio sababu ya kushusha uchumi na pato la taifa letu. Tunafahamu lini huu ugonjwa utaisha ili uchumi wetu upande na kupandisha mishahara?
Hivyo ni wazi kuwa kama Katiba ya JMT inatamka kuwa wafanyakazi wanatakiwa kulipwa mshahara unaokidhi mahitaji yao, basi serikali hainabudi kuwaongeza. Maana sababu zinazotolewa kutoongeza mishahara hazina mashiko. Gharama za maisha zimepanda na katiba inapaswa kuzingatiwa.
Hivyo kama ikitokea kuna namna serikali inakuwa inatoa sababu hazina mashiko juu ya kuongeza mishahara watumishi wafanyakazi wawe wanaenda mahakamani kudai haki hiyo ya kikatiba.