Kama ni kweli na ushahidi upo....

Kama ni kweli na ushahidi upo....



Aliyemteua anamlia timing tu amtumbue ,kwanza amempa muda "ajitumbue" na aondoke kwa "heshima" lakini jamaa ameubeba mzigo asiouweza. Anapata flashback ya kufunga nyuzi za viatu za watu wale ambazo zinamwogopesha.
Huyu Mr. Daudi ni wazi amezikubali tuhuma zinazoelekezwa kwake kwa sababu huu ukimwa wake juu ya vyeti halali na halisi. Kama anavyo ni suala la kulizima kwa dakika 2 tu. Ni kama hapana kazi tu na kutumbua jipu.

Mr. Daudi kama anavyo vyeti halali na halisi ambayo ni vyake, kwa kelele zinazopingwa kwamba aviweke hadharani basi naamini kwa anavyopenda kamera na tv angelikwishafanya mkutano na waandishi wa habari na kuwaonesha F,0-zake na Div. 1 zake.

Magu na Mr. Daudi wanaviziana. Ni nani kati yao anayemchelewesha mwenzake?

Tumecherewa kweli kweri, mwende kuwatumikia wadanganyika.





Nani ajuaye? Maandiko matakatifu nayo yanatisha .
"... Ambaye hajatenda dhambi (aliye msafi) na awe wa kwanza kumrushia mawe" .
 
chige naona umefuta bandiko lako fasta kabla sijakushukia.

Hahahaaa safi sana. Umejistukia kuwa umechemka ukajirudi mwenyewe.
 
You see man... your reference now is Askofu Gwajima lakini ukisoma bandiko lako umewataka wana- JF ndio wakupe ushahidi!

JF tumejaa watu wa kawaida ambao hatuwezi kuwa na access za kupata tangible evidence hata kama panaweza wakawepo wanaofahamu pasipo na shaka yoyote kwamba Makonda ni Fraud!!

Gwajima sio ordinary person na hakuna ushahidi wa uwepo wake hapa JF!! Na wala sina sababu ya kumsikiliza kwa sababu nilishamsikiliza hapo kabla!! Na endapo kumbukumbu zangu zipo sawa, kuna mahali amesema wazi ana ushahidi Makonda amefoji lakini kwa sasa anamwachia Rais! Akasisitiza atashangaa sana endapo Rais atanyamaza kimya na kwamba, akiona mamlaka zinataka kufunika kombe; kila kitu ataanika wazi!!!

Huyo ni Gwajima ambae sio ordinary person na amesema wazi wazi bila kificho!!! Na huyu ndie unapaswa kumdai ushahidi ingawaje !!!

Wana JF hatuwezi kuwa na ushahidi kwa kuzingatia sababu nilizotaja awali!! Kwavile hatuna access ya kuwa na ushahidi na hivyo kutokuwa na nguvu kisheria kuripoti mahakamani basi mahakama yetu pekee ni mahakama ya umma!!! Tungekuwa na access ya evidence, ushahidi ungepelewa kwenye court of law ambako Makonda angetakiwa akajitetee na ku-prove otherwise!!

Lakini kwavile akina sie tunatumia mahakama ya umma; basi Makonda nae anapaswa ku-prove otherwise mbele ya mahakama ya umma!! Kudai evidence ni usual tactic inayotumiwa na wahalifu wote duniani!!

Hata wezi wa Escrow wametutaka tutoe ushahidi! Hata wezi wa EPA nao walitutaka tutoe ushahidi!! Wale waliotuumiza kupitia Richmond walitumia njia ile ile ya wahalifu wenzao kwamba tutoe ushahidi!! Hata Rizmoko majuzi amesema watu watoe ushahidi kwamba anauza sembe! Hata ukimkamata Kinje leo nae atakutaka ushahdi!!!

Hivyo basi, hoja ya kudai ushahidi haijawahi kuwa na katu haitakuja kuwa hoja ya ku-prove kwamba muhusika hakutenda uhalifu kwa sababu tu watu wameshindwa kutoa ushahidi! Na inakuwa haina maana yoyote unapomtaka mtu wa kawaida ndie awe mtoa ushahidi husika!!!!!
 
Ukiona mtu haelewi hata hili nae atakuwa alibashitika katika elimu yake...
Taarifa zinapimwa. Unataka kufananisha uwepo wa magaidi watakaohatarisha usalama wa nchi na watu wake na shutuma zilizotoka kwa mtu anayejibu mapigo? Polisi wanajiridhisha na tuhuma kabla ya kuhoji au kukamata. Lkn bado gwajima ana nafasi ya kupeleka hivyo vyeti vya makonda mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake au atamsubiri makonda atoe vyake mpk lini?
 
chige naona umefuta bandiko lako fasta kabla sijakushukia.

Hahahaaa safi sana. Umejistukia kuwa umechemka ukajirudi mwenyewe.
Hapana sio kunishitukia! Unajua nina tatizo moja... nikianza kuandika; maneno yanakuja tu kama mvua matokeo yake posts zangu zinakuwa ndefu!! So, what I did ni kujaribu kuipunguza... just editing!! Sasa niliamua kui-delete kabisa huku nikii-edit kwa sababu nilihofu huenda ungei-access mapema... na ndicho ulichofanya!
 
You see man... your reference now is Askofu Gwajima lakini ukisoma bandiko lako umewataka wana- JF ndio wakupe ushahidi!

Anhaaa umerudi, sio?

Safi sana...sasa twende hoja kwa hoja na mstari kwa mstari.

Naomba tuanzie hapo kabla hatujaendelea na mengine.

Nionyeshe mahali kwenye bandiko langu la kwanza hapa ambapo nimewataka wana-JF ndio wanipe ushahidi.

Naomba sana tuanzie hapo ili tusipoteze focus. Nipe, nionyeshe nukuu ya mimi kutaka hivo, tafadhali sana.
 
Wewe si umeshaambiwa sheria zimenajisiwa! Imebidi kutumia mob justice
 
Mkuu, Moja ya raha ya maongezi nikujiwezesha kwa wa kile anachokiongea mwenzako kukielewa, kwa mtindo wa JamiiForums kusoma na kuelewa kile kilichoandikwa.

Na ndio nakubaliana na wewe, hapa inaongelewa ni ushahidi wa jamhuri juu ya mtuhumiwa.

Na ushahidi wa muajiriwa juu ya muajiri, yaani mimi na wewe aka mwananchi, mlipa kodi Ikiwa ndani ya Dar au mikoani, au kwa msemo sahihi mimi na wewe ndio tunaolipa mishahara, kwa hio jamhuri au kwa kuanzia ofisi ya Mkuu wa Mkoa ndio atupe ushahidi, na sio vice versa.

Naelewa neno Public office au kwa maneno mepesi ofisi ya kwako, yangu na wote sisi humu, hilo neno bado naona linakutatiza.

Nakushauri google it, utapata kufunguka Mkuu , kwa hio kwa comment yako hapo mimi kutoka nje ya mada, mbona nimo at the core of it, kama Dunia na kilichomo ndani yake.

Tutazidi kufahamishana mkuu, ukielewa wewe na mimi basi, taratibu tutaelewana kwa jengine.

Na jengine kwa argument ya kusema mtendaji wa serikali aka Wakuu wa mikoa ambao si wakuchaguliwa yaani wa kuteuliwa na sio accountable kwa anao waongoza yaani sisi wananchi, haina mashiko kwa sababu hapo unaongelea jamhuri yaani serikali kwa ujumla wake, ndio sasa panakua pazuri zaidi, Kwa hio ni amri tu toka juu iende wizara ya elimu, kumlinda mtendaji kwa njia ambayo itutaarifu niyaje.

It sting both ways.. Ndio maana akiwa wazi na sisi kondoo basi tumeridhishwa na mtendaji wetu, tunaangalia mengine muhimu zaidi ya
Haya.
Mbona yuko wazi tayari? Ambaye hayuko wazi ni gwajima amekaa na ushahidi ofisini kwa nini?
 
Kwa hiyo mimi nikija hapo ulipo na kukutwanga ngumi kwenye chembe huwezi kwenda mahakamani kunifungulia mashitaka ya kukushambulia?
Hapana hawezi kwenda mahakamani kukufungulia mashtaka bali atakwenda polisi ambao watakufungilia mashitaka mahakamani na yeye atakuwa shahidi wa kwanza wa jamuhuri!
 
Hahaaa...nipo huku Ikungulyabashashi kaka.

Nasikia tu hadi wachungaji wanasema eti Paul Makonda si jina lake bali jina lake ni Daudi Bashite na ushahidi wanao lakini hawatuonyeshi huo ushahidi.

I wonder why!

Things that make you go hmm....
WALA UNGA, WAUZA UNGA, ACHENI KUMUANDAMA MAKONDA ! MBONA HAMJAMSHUTUMU KABLA HAJAANZISHA VITA YA BWIMBWII ?!
 
Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.

Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.

Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?

Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?

Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?

Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.

Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.

Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.

Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?

Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
1da7320cdcb2b2767b5e2dc56ef201b0.jpg
 
Ahahahaaa....kwa hiyo kumbe huyo Gwajima naye hakuuonyesha huo ushahidi anaodai anao.

Hivyo hatuwezi hata kujua kama kwamba [1] anao kweli na [2] ni ushahidi unaotosha na kuridhisha.

Hivyo hata yeye anaweza akawa anazusha tu ili kupoteza kabisa lengo na kuzua mparaganyiko tu.
Kama alivyozusha bajeti kuhusu orodha wa watu wa drugs!!!! Au yeye alionesha ushaidi?
 
Back
Top Bottom