ypointer4
JF-Expert Member
- Feb 17, 2010
- 633
- 523
Fafanua hapa
Fafanua hapa
Bila kufikishwa mahakamani? Au ya gwajima inatosha?huyu akamatwe na apelekwe gerezani
Nani kafungwa kwa kutuhumiwa? Hama Dar ukaishi TandahimbaKichwa cha habari kinajieleza, Makonda tayari anatuhumiwa, kwanini mamlaka haziwajibiki juu ya tuhuma za huyu bwana mkubwa, wapo watumishi wengi wa serikali saivi baadhi yao, wamefungwa wengine wamefukuzwa kazi, lakini walituhumiwa kama huyu bwana mkubwa, mamlaka zilichukua hatua yakawakuta yalowakuta, why Makonda
Kichwa cha habari kinajieleza, Makonda tayari anatuhumiwa, kwanini mamlaka haziwajibiki juu ya tuhuma za huyu bwana mkubwa, wapo watumishi wengi wa serikali saivi baadhi yao, wamefungwa wengine wamefukuzwa kazi, lakini walituhumiwa kama huyu bwana mkubwa, mamlaka zilichukua hatua yakawakuta yalowakuta, why Makonda
Rubi hujambo
Mkuu Nyani Ngabu,mfumo wa kisheria wa nchi yetu ya Tanzania hauruhusu mtu binafsi kumfungulia mwingine,na kuendesha kesi mahakamani,kesi ya jinai. Kinachotakiwa ni kwa mtu mwenye ushahidi dhidi ya jinai ya mwingine kuuwasilisha ushahidi huo kwa mamlaka zinazohusika,mfano polisi au TAKUKURU,ili hatua stahiki zichukukiwe. Mamlaka hizo na nyinginezo,kama Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ndizo zitakazomshtaki mhusika. Ndiyo kusema,wenye kuamua kushtaki au la ni watawala waliopo kwenye mamlaka hizo iwe ushahidi umekabidhiwa au ule walionao wenyewe.
GSM wapo tayari kuwanunua majaji wote na mashahidi wote, mfano sasa kuna Madalali wametumwa kwenda kijijini kolomije na shule zote alizosoma Daudi Albert makonda wakawanunue watu ( Rushwa) waache kutoa ushirikiano kwa Gwajma na wengineo, kesi ili iweze kuendeshwa inabidi ifunguliwe nje ya Nchi lakini hapa Tanzania lazima Mkulu ataingilia maamuzi kama alivyokuwa akimfanyia Lema.Nianze kwa kusema tu kuwa mimi ni mbeba maboksi nisiyejua mengi hususan kwenye hiyo fani ya 'wasomi' wabobezi [wanasheria] ambao ndiyo majiniasi wetu wenye kuongea Viingereza hatari lakini salama. Nimeishia kidato cha nne tu. Kwa hiyo msinihoji sana kuhusu elimu yangu. Ni ndogo sana.
Sasa hapa nilipo na ujinga wangu huu najiuliza maswali kadha wa kadha na sipati majibu.
Hivi kinachodaiwa dhidi ya Makonda ni kosa la jinai?
Kama ni kosa la jinai na kama kweli ushahidi upo, tena ambao ni wa kutosha na kuridhisha kabisa, kwa nini hao watu waolizitoa hizo tuhuma hawaendi kumfungulia kesi mahakamani?
Au haiwezekani kwa raia kwenda kufungua kesi mahakamani kwa manufaa ya umma dhidi ya kiongozi?
Manake mpaka sasa kilichopo au niseme ambacho nakijua mimi kupitia hii mitandao ya kijamii ni maneno tu kuwa Paul Makonda si jina lake halisi.
Jina lake halisi ni Daudi Bashite. Lakini sijaona ushahidi wowote ule uliotolewa na hao watuhumu unaothibitisha hizo tuhuma zao.
Sasa maneno tu peke yake si ushahidi wa lolote maana mtu yeyote yule anaweza kuzua lolote lile dhidi ya yeyote yule kwa sababu yoyote ile.
Nyie 'wasomi', hivi kweli haiwezekani kwenda kumfungulia mashitaka huyo Paul Makonda kama kweli ushahidi wa yanayosemwa dhidi yake upo?
Si mumburute tu mahakamani huko akaaibike rasmi. Au ni majungu tu?
Necta ya Tanzania au Necta ya wapi? Kama ni ya Tanzania sahau milele kwani huko mpaka waziri wa Elimu wamepewa amri toka juu wamlinde makonda kwa gharama yeyote ile.NECTA NDIYO YENYE UWEZO WA KUTHIBITISHA UHALALI WA CHETI CHA MAKONDA PEKEE.
Kupeleka kesi ya makonda mahakama ya Tanzania ni kupoteza mda kwani huko GSM wamejipanga kutumia pesa zao zote kuhujumu kesi mpaka makonda apate ushindi.
Ki-msingi hakuna mwenye ushahidi wa vyeti kwa sababu Daud Bashite alipata '0'kidato cha 4. Hapo cheti hakuna! Cheti cha Darasa la 7 nacho kilifutwa tangu miaka 90. Mimi nimemaliza primary 1992 na sikupata cheti cha darasa la 7 vilikuwa vimeshafutwa. Hapa ushahidi ni wa shule alikosoma makonda. Km alisoma koromoje alikuwa anaitwa nani!!? Hata km atanunua watu lkn kwenye madafutari ya mahudhurio jina la Paul makonda halitaonekana.Sasa kama hivyo ndivyo basi Gwajima atuonyeshe hivyo vyeti alonavyo ofisini kwake.
doooh!! ñyuzi SITA, tena kwa siku moja?hauna kazi nyingine za kufanya? ama mods wanakulipaga ukianzisha uzi? na huo nao ni ubaguzi na double std kwa upande wao. iweje wewe ulipwe ukianzisha wakati sie hatulipwi? au mods sie wengine wanatuona how come tu??Leo nyuzi zangu sita zimeunganishwa tena mbaya zaidi zina maudhui tofauti
Hana huduma ya mkopo!?.Nashukuru sana ndugu. Nilikuuliza kwa kuwa ulianza kutoa elimu humu nikadhani ninaweza kupata elimu zaidi toka kwako na wangine wakafaidika pia kupitia jukwaa hili. Samahani sikuelewa kuwa ulikuwa "unaitangaza huduma unayoiuza".
Asante kwa uliyonijuza ndugu lakini kwa sasa sina hicho kiasi nitakapokipata sitachelewa kuja kupata elimu zaidi.
Bahati mbaya nchi yetu kwa sasa hakuna serikali ila kuna "siri Kali"Kesi ya jinai inaendeshwa na serikali na sio mtu binafsi.
Mwenye wajibu wa kuchunguza na kumpeleka huyo jamaa mahakamani ni serikali.