Mkuu
Nyani Ngabu,mfumo wa kisheria wa nchi yetu ya Tanzania hauruhusu mtu binafsi kumfungulia mwingine,na kuendesha kesi mahakamani,kesi ya jinai. Kinachotakiwa ni kwa mtu mwenye ushahidi dhidi ya jinai ya mwingine kuuwasilisha ushahidi huo kwa mamlaka zinazohusika,mfano polisi au TAKUKURU,ili hatua stahiki zichukukiwe. Mamlaka hizo na nyinginezo,kama Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ndizo zitakazomshtaki mhusika. Ndiyo kusema,wenye kuamua kushtaki au la ni watawala waliopo kwenye mamlaka hizo iwe ushahidi umekabidhiwa au ule walionao wenyewe.