Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,517
Nimechukua muda wa kutosha kuisoma Sheria ya Kanuni ya Adhabu (Sura Na. 16 iyofanyiwa mapitio mwaka 2019) na kujiridhisha pasi na shaka kuwa, kama nchi-Tanzania, ushoga umekatazwa na kuadhibiwa vikali kwenye sheria hiyo. Ni vifungu vya 154 na 155 vya Kanuni ya Adhabu.
Wahusika wote wa ushoga (anayeingilia na yule anayeingiliwa) wote wamewekewa adhabu zao pale ambapo mashtaka yao yatathibitishwa mahakamani.
Kama hiyo haitoshi, hata kujaribu kutenda ushoga/kuingilia kinyume na maumbile ni kosa chini ya Kanuni ya Adhabu. Ndiyo kusema kufanya ushoga au kujaribu kufanya ushoga kote kunahesabika kosa chini ya Kanuni ya Adhabu.
Kwakuwa sheria, inayobeba kauli na msimamo thabiti ya nchi yetu juu ya masuala ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile, kinachobakia ni mamlaka husika kuendelea kuisimamia sheria hiyo na kutokomeza tatizo hili. Ni utashi tu wa kimamlaka ndio uliobakia katika kuishinda vita hii.
Tuache porojo na tusimamie sheria. Wapo wanaojihusisha na mapenzi kinyume na maumbile wanaojulikana na wale wasiojulikana lakini wanaoweza kujulikana. Waanikwe; wakamatwe; washtakiwe na kuadhibiwa kadiri ya matakwa na taratibu za kisheria. Nchi imesema kupitia sheria, nchi iendelee kutekeleza kupitia sheria!
Vifungu husika ni hivi:
154.-(1) Mtu yeyote ambaye-
(a) anamuingilia mtu yeyote kinyume cha maumbile au,
(b) anamuingilia mnyama kimwili au
(c) anamruhusu mwanaume kumuingilia yeye mwanaume au mwanamke kinyume cha maumbile, atakuwa ametenda kosa, na atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha na wakati mwingine kifungo kisichopungua miaka thelathini .
(2) Ikiwa kosa limetendwa chini ya kifungu kidogo cha (1) cha kifungu hiki dhidi ya mtoto wa chini ya miaka kumi, mkosaji atawajibika kwa adhabu ya kifungo cha maisha.
155. Mtu yeyote ambaye atajaribu kutenda kosa mojawapo katika makosa yaliyotajwa katika kifungu cha 154 atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kwa adhabu ya kifungo kisichopungua miaka ishirini .