Kamishna wa Uhamiaji Manyara amejibu hoja Kisomi; ni kweli katika macho ya sheria gari na bendera siyo mali ya CCM; CHADEMA kuweni makini na hii move

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
879
4,112
Kilichojibiwa na Idara ya Uhamiaji ndicho kinachoitwa majibu katika macho ya sheria. Si kila bendera ya kijani ni bendera ya CCM na siyo kila bendera ya kijani yenye nembo ya CCM siyo mali ya CCM.

Kamishna wa Uhamiaji Manyara amepewa nguvu ya kufanya uchunguzi kwa mijubu wa sheria ya Uhamiaji. Kwa kweli mimi nimependa majibu yake kwa sababu amejibu kwa ufupi ila akizingatia sheria inayosimamia. Awali niliunga mkono kile kinachoshabikiwa katika mtandao wa X lakini nimelazimika kwenda kusoma sheria ya Uhamiaji.

Kifungu cha 46 cha sheria ya Uhamiaji ya mwaka 2016 kinasema ni kosa kusafirisha au kufanya ulanguzi wa binadamu. Faini yake ni kifungo kisichopungua miaka ishirini au faini isiyopungua milioni tano. Kifungu hicho kinasema pia kifaa kinachotumika kwenye magendo kutaifishwa.

Nakubaliana na Kamishna huyu kwamba lile gari siyo mali ya chama cha mapinduzi. Lakini pia hata wale waliotoa taarifa za umiliki wanakiri kwamba lile gari siyo mali ya chama cha mapinduzi bali ni la mwanachama na kiongozi wa chama cha mapinduzi. Kwa tafsiri nyingine mali za kiongozi wa chama siyo mali za chama na uhalifu wa kiongozi wa chama siyo uhalifu wa chama cha siasa.

Kuhusu Bendera; nakubaliana naye pia kwamba bendera ile siyo mali ya chama cha mapinduzi ila inafanana na bendera ya chama cha mapinduzi.

Kuhusu wito wa kutohusisha uhalifu ule na chama cha mapinduzi; nakubaliana naye kwamb uhalifu wa kijana yule siyo uhalifu wa chama na hakuna sheria inayoweza kuthibitisha chama kuhusika.

Pamoja na kukubaliana naye napenda kuwatahadharisha sana viongozi wa kisiasa kusoma kifungu hiki cha 46 cha sheria ya Uhamiaji.
Viongozi wa kisiasa wengi mnamiliki magari na hayo magari mnawapa madereva ambao nafsi zao zimeficha siri kubwa. Kumbukeni kesi ya kubumba ya Mbowe.

Kifungu hiki cha sheria ambacho Uhamiaji wanakwenda kukitumia kutaifisha ile gari kinatoa adhabu ya faini kwa Dreva aliyekamatwa na kwa aina ya kesi hii naamini yule kijana atalipa faini kwa kukiri makosa na gari itaitishwa.

Swali lakujiuliza, hakuna uwezekano wakawepo vijana kama huyu watakaotumika kutumia magari ya viongozi wa upinzani kisha wakikamatwa hayo magari yataifishwe? Siku likikamatwa gari lenye bendera ya chadema tutafurahia kusikia vyombo vya dola vikisema gari husika ni mali ya chadema? Tutafurahia kuona mali binafsi za kiongozi wa chadema zikiitwa mali za chadema?

Tukubali kujifunza yafuatayo

1. Mali ya mtu binafsi inapotumika kutenda uhalifu isihusishwe na taasisi

2. Viongozi wa vyama vya upinzani chukueni sana taadhari mnapowapa watu magari yenu kwani binadamu mwenye nia ovu hana alama

3. Wenye nyumba za kupanga na vyombo vya usafiri someni sheria hiyo ya uhamiaji msijejutia mtakapoambiwa mali zenu zimetumika kuhifadhi wahamiaji haramu.

Mwanagenzi

Soma Uhamiaji: Dereva na V8 Iliyobeba wahamiaji Haramu 20 wa Ethiopia Isihusishwe na CCM
 
Sawa lakini fikiria ile ingekuwa nembo ya chama kingine, narrative ingekuwa hiyo hiyo ?
Hii wake up call kwa vyama vingine na watu binafsi ; magari yetu yanaweza kutumika kisiasa huko mbeleni kupaka chama matope.........tulishangilia na kulazimisha lile gari ni mali ya CCM basi kesho likikamatwa lenye bendera ya Chadema itatulazimu tukubali kwamba nalo ni mali ya chadema...........

Yeye ametekeleza wajibu wake kwa umakini sana, ipo siku hii kauli yake itakisaidia chama kingine kuepuka kuhusishwa na uhalifu wa mtu binafsi kwa mipango yake.
 
Hii walk up call kwa vyama vingine na watu binafsi ; magari yetu yanaweza kutumika kisiasa huko mbeleni kupaka chama matope.........tulishangilia na kulazimisha lile gari ni mali ya CCM basi kesho likikamatwa lenye bendera ya Chadema itatulazimu tukubali kwamba nalo ni mali ya chadema...........

Kwa taarifa yako, siku ikikamatwa yenye rangi na bendera ya chadema, ndio watakoleza na kukinukisha chama. Acha kujitoa ufahamu.
Gari ina jina na umiliki wa kada wa CCM, utaachaje kuihusisha? Vijana mtakufa masikini kifikra. Wenzenu huko Afrika Magharibi wameamka tayari. 20k zisiwadumaze akili.
 
Hii walk up call kwa vyama vingine na watu binafsi ; magari yetu yanaweza kutumika kisiasa huko mbeleni kupaka chama matope.........tulishangilia na kulazimisha lile gari ni mali ya CCM basi kesho likikamatwa lenye bendera ya Chadema itatulazimu tukubali kwamba nalo ni mali ya chadema...........

Yeye ametekeleza wajibu wake kwa umakini sana, ipo siku hii kauli yake itakisaidia chama kingine kuepuka kuhusishwa na uhalifu wa mtu binafsi kwa mipango yake.
Hapa lazima kitalipwa kisasi kuna gari la m4c litakamatwa tu
 
Mleta mada kuna kitu unakisahau kuhusu tukio lile, moral of that story ni kuwa, CCM huwa inatumika kama kichaka cha kuficha uovu na kufuga uhalifu. Kama hujaelewa hili, basi fuatilia haya;

1. Nyumba nyingi za kuuza gongo, juu ya paa kuna bendera ya CCM inapepea.

2. Maskani nyingi za kuuza ngada na bangi mbele yake kuna shina la wakereketwa wa CCM na ulingoti wenye bendera ya CCM inapepea.

3. Madereva wengi wakiwa barabarani ili kukwepa kukamatwa ovyo na trafiki hupeperusha bendera ya CCM kwenye magari yao au huandika maneno ya kuipromote CCM na serikali yake.

4. Wafanyabiashara wengi (hususani wabaya) ili kukwepa kufuatiliwa na mamlaka za serikali na kodi basi humiliki kadi za CCM na huwa busy kuchangia pesa zao kwenye shughuli za CCM.

5. Fremu nyingi za biashara ili kukwepa kodi na kufuatwa fuatwa na TRA au mamlaka za serikali huweka picha ya rais au bendera ya CCM.
 
Mleta mada kuna kitu unakisahau kuhusu tukio lile, moral of that story ni kuwa, CCM huwa inatumika kama kichaka cha kuficha uovu na kufuga uhalifu. Kama hujaelewa hili, basi fuatilia haya;

1. Nyumba nyingi za kuuza gongo, juu ya paa kuna bendera ya CCM inapepea.

2. Maskani nyingi za kuuza ngada na bangi mbele yake kuna shina la wakereketwa wa CCM na ulingoti wenye bendera ya CCM inapepea.

3. Madereva wengi wakiwa barabarani ili kukwepa kukamatwa ovyo na trafiki hupeperusha bendera ya CCM kwenye magari yao au huandika maneno ya kuipromote CCM na serikali yake.

4. Wafanyabiashara wengi (hususani wabaya) ili kukwepa kufuatiliwa na mamlaka za serikali na kodi basi humiliki kadi za CCM na huwa busy kuchangia pesa zao kwenye shughuli za CCM.

5. Fremu nyingi za biashara ili kukwepa kodi na kufuatwa fuatwa na TRA au mamlaka za serikali huweka picha ya rais au bendera ya CCM.
 
Kilichojibiwa na Idara ya Uhamiaji ndicho kinachoitwa majibu katika macho ya sheria. Si kila bendera ya kijani ni bendera ya CCM na siyo kila bendera ya kijani yenye nembo ya CCM siyo mali ya CCM.

Kamishna wa Uhamiaji Manyara amepewa nguvu ya kufanya uchunguzi kwa mijubu wa sheria ya Uhamiaji. Kwa kweli mimi nimependa majibu yake kwa sababu amejibu kwa ufupi ila akizingatia sheria inayosimamia. Awali niliunga mkono kile kinachoshabikiwa katika mtandao wa X lakini nimelazimika kwenda kusoma sheria ya Uhamiaji.

Kifungu cha 46 cha sheria ya Uhamiaji ya mwaka 2016 kinasema ni kosa kusafirisha au kufanya ulanguzi wa binadamu. Faini yake ni kifungo kisichopungua miaka ishirini au faini isiyopungua milioni tano. Kifungu hicho kinasema pia kifaa kinachotumika kwenye magendo kutaifishwa.

Nakubaliana na Kamishna huyu kwamba lile gari siyo mali ya chama cha mapinduzi. Lakini pia hata wale waliotoa taarifa za umiliki wanakiri kwamba lile gari siyo mali ya chama cha mapinduzi bali ni la mwanachama na kiongozi wa chama cha mapinduzi. Kwa tafsiri nyingine mali za kiongozi wa chama siyo mali za chama na uhalifu wa kiongozi wa chama siyo uhalifu wa chama cha siasa.

Kuhusu Bendera; nakubaliana naye pia kwamba bendera ile siyo mali ya chama cha mapinduzi ila inafanana na bendera ya chama cha mapinduzi.

Kuhusu wito wa kutohusisha uhalifu ule na chama cha mapinduzi; nakubaliana naye kwamb uhalifu wa kijana yule siyo uhalifu wa chama na hakuna sheria inayoweza kuthibitisha chama kuhusika.

Pamoja na kukubaliana naye napenda kuwatahadharisha sana viongozi wa kisiasa kusoma kifungu hiki cha 46 cha sheria ya Uhamiaji.
Viongozi wa kisiasa wengi mnamiliki magari na hayo magari mnawapa madereva ambao nafsi zao zimeficha siri kubwa. Kumbukeni kesi ya kubumba ya Mbowe.

Kifungu hiki cha sheria ambacho Uhamiaji wanakwenda kukitumia kutaifisha ile gari kinatoa adhabu ya faini kwa Dreva aliyekamatwa na kwa aina ya kesi hii naamini yule kijana atalipa faini kwa kukiri makosa na gari itaitishwa.

Swali lakujiuliza, hakuna uwezekano wakawepo vijana kama huyu watakaotumika kutumia magari ya viongozi wa upinzani kisha wakikamatwa hayo magari yataifishwe? Siku likikamatwa gari lenye bendera ya chadema tutafurahia kusikia vyombo vya dola vikisema gari husika ni mali ya chadema? Tutafurahia kuona mali binafsi za kiongozi wa chadema zikiitwa mali za chadema?

Tukubali kujifunza yafuatayo

1. Mali ya mtu binafsi inapotumika kutenda uhalifu isihusishwe na taasisi

2. Viongozi wa vyama vya upinzani chukueni sana taadhari mnapowapa watu magari yenu kwani binadamu mwenye nia ovu hana alama

3. Wenye nyumba za kupanga na vyombo vya usafiri someni sheria hiyo ya uhamiaji msijejutia mtakapoambiwa mali zenu zimetumika kuhifadhi wahamiaji haramu.

Mwanagenzi

Soma Uhamiaji: Dereva na V8 Iliyobeba wahamiaji Haramu 20 wa Ethiopia Isihusishwe na CCM

Hayo aliyeeleza huyo Kijana wa uhamiaji, na ambayo wewe unakubaliana nayo, hata mtoto wa darasa la 4 anaweza elewa, hukutakiwa hata kutuletea sheria kutueleza hayo.
 
Back
Top Bottom