Inakera, inaudhi na inauma sana kuona katiba yetu inawafanya wananchi kuwa wanyonge. Hawana sauti, hawana maamuzi na wala hawawezi kupindua chochote kilichoamuliwa na viongozi (serikali).
Chanzo cha upuuzwaji huu wa sauti za wananchi, uvizwaji wa nguvu ya wananchi na viongozi kutoogopa/ kutoheshimu hasira/ maoni ya wananchi ni katiba mbovu tuliyo nayo.
Katiba imempa mamlaka makubwa sana rais. Hakuna kiongozi au raia yeyote anayeweza kuukwepa mkono wa adhabu wa rais endapo ataenda kinyume naye kwa katiba yetu hii. Hii ndiyo sababu watu wameamua kujikomba, kuwa machawa na kushabikia hata upuuzi unaofanywa rais ili maisha yaende.
Magufuli alifanya mambo ya hovyo yasiyopaswa hata kuelezewa ktk zama hizi, lkn kulikuwa na kundi kubwa la watu walioimba na kusifu upuuzi wa Magufuli. Sababu tu katiba yetu ni mbovu.
Kwa katiba yetu hii tutakujq kumpata rais atakayeamua kuuza baadhi ya mikoa kwa nchi jirani au mabeberu na hatutamfanya kitu. Mzee Mwinyi aliuza pori la Loliondo tumemfanya nn? Kikwete amekabidhi gesi yetu ya Mtwara (ni kama kauza tu) kwa wachina, tumemfanya nn? Samia naye atafanya chochote anachotaka kufanya, wananchi mtapiga kelele lkn hakuna mtakachomfanya. Mf. Alianzisha tozo (huku akijua tunalipa Kodi). Tumelalamika lkn mpk leo tunaitoa na kiodi tunalipa. Hatujamfanya kitu.
Suluhu ya haya yote ni kuunda katiba itakayomfanya rais kuwa mtumishi wa wananchi na siyo mtawala wa wananchi. Katiba itakayounda mihili huru na taasisi zenye nguvu. Katiba itayomfanya rais kuwa chini ya sheria, yaani akingua anawajibishwa ama anaondoshwa.
Nawasihi watanzania tuipiganie katiba mpya ili sisi na vizazi vyetu tuishi vyema katikati nchi yetu.
Nimemaliza, kama hutaki kimpango wako.