Agenda ya Mkataba wa DP World tuipumzishe, sasa twende na Katiba Mpya

sifi leo

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
5,013
8,369
Watanzania sasa tufike hali tukubaliane na hali tu, ya kuwa tunapobweka sana tunasikika, na walio madarakani wanaelewa na kusikia vibweko vyetu.

Siamini ya kuwa tumefika hali au wakati wa kutowaamini watawala wetu kiasi hiki. Nina imani kabisa Rais Samia na Makame Mbarawa na wenzao wote wamesikia vibweko vyetu na sisi ni wakati wa kutafuta agenda nyingine ili tuendelee kuwapopoa mpaka washuke watusikie.

Binafsi natumia nafasi hii kutoa Maua kwa Freemani Aikaeli Mbowe katika suala la Mkataba wa Bandari, baba uliupiga mwingi na kwa msimamo dhabiti hakika pokea Maua yako.

Kwa kuwa ili dude wewe ndio uliliamsha kupitia vyanzo vyako pokea Maua yako baba.

Baada ya kelele nyingi, baba Freeman Mbowe tukubaliane ya kuwa, ni vigumu sana Mh. Rais na wale mabwana wa DP World kudisclose yaliyomo ndani ya mkataba, maana watakuwa wamejiacha uchi. Mara nyingi mikataba huwa ni confidencial wakuu.

Kwa kuwa tumeambiwa wamerekebisha na kwa kuwa tulikuwa hatupingi uwekezaji bali tulipinga some content of the contract na zenyewe tunaambiwa zimerekebishwa, ni vyema sasa genda hiyo ipumzishwe ndugu twende na Katiba mpya.
 
Ccm wakikuambia wamerekebisha mkataba ,uje wameharibu kbs mkuuu hawaaminiki hao wachumia tumboo..
 
Back
Top Bottom