Hollo
JF-Expert Member
- Apr 21, 2008
- 827
- 165
2008-06-18 09:19:52
Na Simon Mhina
Askofu Mkuu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship amesema wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, wamelidhalilisha Taifa na kuiaibisha dunia nzima, kufuatia madai ya kuhofu kuendelea na vikao kwa sababu ya uchawi.
Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, alisema ni ajabu na aibu kubwa kuona wabunge wanazungumzia uchawi, wakati mabunge ya nchi zilizoendelea, yanajadili
bajeti za kuwawezesha watu wao kupaa na vyombo maalum kwenda kujenga nyumba kwenye sayari ya Mars.
Askofu Kakobe alisema dhana ya uchawi ni ujinga na upuuzi, ambayo haipaswi kupewa nafasi kwa mtu yeyote anayefahamu wajibu wake.
Alisema hofu ya uchawi iliyowaingia wabunge, hadi Spika Bw. Samweli Sitta akatoa ufafanuzi sio tu imewapandisha chati wachawi na ndumba zao, bali pia imewarudisha Watanzania enzi za ujima.
``Yaani Watanzania wanawakilishwa na wabunge wanaoogopa uchawi na wanatumia muda mwingi kujadili ndumba? Mimi nimeshangaa kusikia wamehofu kukalia viti vyao kwa kudhani eti vina ndumba, hatua hii imewapandisha chati wachawi nchini. Hivi sasa wachawi nchini wanaonekana kitu muhimu hadi wanajadiliwa bungeni? Ni aibu,`` alisema.
Alisema wabunge wamempa ushindi mkubwa shetani, kwa vile siku zote huanza kuwatia watu hofu, ili atekeleza mambo yake.
Kufuatia tukio hilo, Askofu Kakobe alisema haoni sababu ya wabunge kufungua vikao vyao kwa sala.
Alisema haelewi ni vipi wanafungua vikao kwa sala, halafu wanahofu ndumba.
`1Ina maana yule Mungu wanayemuomba asubuhi, hawamuamini, wanataka kutuambia ndumba zina nguvu kuliko Mwenyezi Mungu wanayemtaja hata wakila kiapo?`` Alihoji.
Wakati huo huo, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodist Kilaini, amesema madai ya uchawi bungeni yamemshangaza.
Alisema ameshangaa kuona watu wakubwa kama wabunge wanaishi kwa hofu ya uchawi.
``Kabla Spika hajatoa ufafanuzi nilisema moyoni kwamba sasa tumefika mbali, kwamba watu wanatishiana na uchawi bungeni?`` Alisema.
* SOURCE: Nipashe