Namuombea Msamaha Askofu Kakobe kwa watu wote

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,753
218,362
Baada ya kumsikia Askofu Kakobe akihubiri kanisani kwake bila uoga kuhusu umuhimu wa kurejeshwa kwa Tanganyika, natangaza rasmi kumsamehe madhambi yake yote aliyoyatenda kwa kushirikiana na Magufuli kwenye mambo mbalimbali wakati wa awamu ya 5.

Kakobe baada ya kutishwa na uongozi wa kikatili wa awamu ya 5, kwa kuulizwa kuhusu uraia wake na kusingiziwa kwamba anahifadhi pesa nyingi za sadaka kwenye majaba, aliamua kukengeuka na kujisalimisha kwa Jiwe, akajikomba na kuhudhuria hafla kadhaa za Ikulu, na kutufanyia kejeli sisi wapigania haki tuliosimama imara kwa kauli kwamba anakula bata Ikulu.

Lakini kwa kauli zake za sasa, nimeamua kujitokeza hadharani kumuombea msamaha, kwa Mungu na kwa kila binadamu.

Akizungumzia masuala ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Askofu Kakobe amesema kwamba, yapo mambo yasiyo ya Muungano, ambapo kwa Zanzibar yanashughulikiwa na Serikali ya Zanzibar, amehoji kwamba mambo hayo ambayo siyo ya muungano huku Tanganyika yanashughulikiwa na nani, maana Tanganyika haipo na ilishapotea. Kakobe ameona umuhimu wa kuirejesha Tanganyika ili nayo ishughulikie mambo yasiyo ya Muungano kama ifanyavyo Zanzibar.

Kwa kumalizia, Kakobe amewaapisha waumini wake kwa kuwaambia kwamba kurudi kwa Tanganyika ni suala la muda tu, kwa vile suala hilo lina Mungu ndani yake, na ndio maana hata wakati Nyerere akiwa hai kulikuwa na wabunge walioipigania Tanganyika, walioitwa G55.

Mungu ibariki Tanganyika.
 
Duh, nimeishia njiani.
Kumbe wewe ndo unayetangazia watu msamaha!
 
Back
Top Bottom