Kakobe awarukia wabunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kakobe awarukia wabunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hollo, Jun 18, 2008.

 1. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #1
  Jun 18, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  2008-06-18 09:19:52
  Na Simon Mhina

  Askofu Mkuu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gosple Bible Fellowship amesema wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muuungano wa Tanzania, wamelidhalilisha Taifa na kuiaibisha dunia nzima, kufuatia madai ya kuhofu kuendelea na vikao kwa sababu ya uchawi.

  Akizungumza na Nipashe jijini Dar es Salaam jana, alisema ni ajabu na aibu kubwa kuona wabunge wanazungumzia uchawi, wakati mabunge ya nchi zilizoendelea, yanajadili
  bajeti za kuwawezesha watu wao kupaa na vyombo maalum kwenda kujenga nyumba kwenye sayari ya Mars.

  Askofu Kakobe alisema dhana ya uchawi ni ujinga na upuuzi, ambayo haipaswi kupewa nafasi kwa mtu yeyote anayefahamu wajibu wake.

  Alisema hofu ya uchawi iliyowaingia wabunge, hadi Spika Bw. Samweli Sitta akatoa ufafanuzi sio tu imewapandisha chati wachawi na ndumba zao, bali pia imewarudisha Watanzania enzi za ujima.

  ``Yaani Watanzania wanawakilishwa na wabunge wanaoogopa uchawi na wanatumia muda mwingi kujadili ndumba? Mimi nimeshangaa kusikia wamehofu kukalia viti vyao kwa kudhani eti vina ndumba, hatua hii imewapandisha chati wachawi nchini. Hivi sasa wachawi nchini wanaonekana kitu muhimu hadi wanajadiliwa bungeni? Ni aibu,`` alisema.

  Alisema wabunge wamempa ushindi mkubwa shetani, kwa vile siku zote huanza kuwatia watu hofu, ili atekeleza mambo yake.

  Kufuatia tukio hilo, Askofu Kakobe alisema haoni sababu ya wabunge kufungua vikao vyao kwa sala.

  Alisema haelewi ni vipi wanafungua vikao kwa sala, halafu wanahofu ndumba.

  `1Ina maana yule Mungu wanayemuomba asubuhi, hawamuamini, wanataka kutuambia ndumba zina nguvu kuliko Mwenyezi Mungu wanayemtaja hata wakila kiapo?`` Alihoji.

  Wakati huo huo, Askofu Msaidizi wa Kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Methodist Kilaini, amesema madai ya uchawi bungeni yamemshangaza.

  Alisema ameshangaa kuona watu wakubwa kama wabunge wanaishi kwa hofu ya uchawi.

  ``Kabla Spika hajatoa ufafanuzi nilisema moyoni kwamba sasa tumefika mbali, kwamba watu wanatishiana na uchawi bungeni?`` Alisema.

  * SOURCE: Nipashe
   
 2. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #2
  Jun 18, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kweli kabisa dhana ya uchawi imepitwa na wakati kabisa!Ni aibu kujadili uchawi
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jun 18, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wandugu,
  Huyu bwana nilikuwa namsikia tu. Nilipokuwa mjini Tabora nikapata bahati ya kumuona kwenye TV. Mhhh, jamaa ni mbabe kweli. Siku hiyo alikuwa akiombea akina mama wenye watoto ila hawana maziwa yaani maziwa hayatoki. Basi baada ya kuombea kwa muda akaanza kusema waje hapa. Akina mama wakaja na yeye akawa anawashika matiti na kuonyesha maziwa yakitoka. Ana bahati kuwa hakuwepo binti wa Kichaga maana ANGELIMLABUA. Ahhh, wewe washika Matiti ya akina mama wazima? Umekuwa Justin Timberlake?? Askofu mzimana joho lake na msalaba? Sijui kuna siku atakuja aombea akina mama wasio na hamu ya kutoa vitu? Ataproove vipi kuwa sasa wanatoa? Tena mbele ya watu? Au akina baba wasio-simama? Mhhh wee Kakobe? Na eti akisafiri basi watu wanasali kwa kutumia mikanda yake ya video?????
  Kwangu mie huyu na wengine wengi ni MATAPELI wanautumia dini kuishi. Kwa maana nyingine ni WALA VYA BURE. Ana gari, nyumba, TOTOZ kama sikosei, fedha na nasikia pia hutumia VIJIUNGA kama vya ANDEREYA katika kufanikisha hili. Hebu mwenye MADATAZ anielezee zaidi maana wengi huyu jamaa wanamuogopa kama Andereya.
   
 4. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #4
  Jun 18, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  aende akawaombee ..... si kwamba yamepitwa na wakati mbona kanisani kwake kila kukicha ana tibu watu maradhi yanayotokana na uchawi ... anajiita nabii kwa kuondoa uchawi na mapepo mabaya yaliyowakumba watu ... na kuonyesha miujiza kedekede kwenye tiviiiii ... kwani naigeria huenda kufanya nini ... sasa anavyosema kinyume namshangaa keli keli ...

  kila mmoja anahofia maisha yake ... angejitolea kwenda kuwaombea au kuomba kwenye huo ukumbi hapa ningemuelewa
   
 5. G

  Gulwa JF-Expert Member

  #5
  Jun 18, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 2,784
  Likes Received: 1,963
  Trophy Points: 280
  Kakobe naye ni muumini mzuri wa imani za kishirikina, anawatia watu hofu kwa mahubiri yake kisha anawafanyia ufisadi kwa kutumia jina la Yesu, ataitwaje askofu mkuu wakati kanisa lake ni kama ofisi za mfukoni, kwani hana maaskofu wengine chini yake!
   
 6. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #6
  Jun 18, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  sasa kama nayeye anaombea wenye mambo ya kichawi kanisani kwake wanatoka kwanini asifunge safari kwenda dodoma kuombea huo uchawi tuwajua haswaa wachawi na watoke?!!!asitake kutuzingua na sera zake hapa huyu si ndo wakati flani alijiunga kupigia kampeni chama flani hadi kanisani mwake akawa anawaambia washarika wamchague huyo bosi wake???
   
 7. hollo

  hollo JF-Expert Member

  #7
  Jun 18, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 781
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  kakobe kasema kila siku wabunge wanasali kwa nini waogope uchawi?sio lazima kakobe aende bungeni akaombee!wakati kila asubuhi kuna sala bungeni
   
 8. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #8
  Jun 18, 2008
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  kakobe nae amekuwa chadema siku hizi ? anapaswa aache tabia zake hizi za kuingilia mambo ya siasa yeye na watu wengine wote wa dini , kwani wameshaona wanasiasa wakiingilia imani za watu ? nao wafanye hivyo hivyo watunze na kulisha roho zilizopotea na sio kujiingiza katika masuala ya siasa
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Jun 18, 2008
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  yeye kama haamini mambo ya kichawi kule kanisani kwake wale pepo anaowatoa wafuasi wake inakuwa ni uongo au? mbona anajichanganya kiasi hiki huyu?
   
 10. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #10
  Jun 18, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Gaijin, nasikia nyingine deal zile zinapangwa, Kwi! kwi! kwi!
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  Jun 18, 2008
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ....hahahaha kubadilisha mada si kazi kubwa sana.... haha...
   
 12. Mtaalam

  Mtaalam JF-Expert Member

  #12
  Jun 18, 2008
  Joined: Oct 1, 2007
  Messages: 1,278
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  mei pia nimeshawahi sikia mambo hayo wanapanga dili n stuffs ili kuvutia watu wengi waende kanisani mwake!!if its so ehh ni kweli sasa twaelekea mwisho wa dunia maana iliandikwa ikikaribia tutaona mambo mengi ikiwemo manabii wa uongo!!
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Msanii,
  Sikuandika ili kubadilisha mada. Hawa watu wa dini kweli wanatisha na ULAFI wao. Heri ya FISADI maana yeye anajulikana anataka nini ila watu wa DINI hujui anataka kuhubiri au anataka POWER, SEX and MONEY.
  Nasikia tu kuwa wanawake wa kichaga ukamshika matiti anakulabua na kusema "hee unashika hotel ya mtoto..." Anyway this is OLD JOKE.
   
 14. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #14
  Jun 19, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Kakobe ni kada wa CCM na mnafiki mkubwa hana huruma hata maisha ya waumini wake anawakamua nashangaa wanao mwendea sijui kufanya maombi .Jambazi in kind
   
Loading...