Politics as usual..Nimeuliza swali uka ignore...Kuhani amekulima swali lile lile na bado unakwepa kisiasa.
Mfano niliotowa kuhusiana na kauli ya usalama wa Taifa ni similar in terms of ambiguity.
Unaposema state allowed the deal na huku ukisema Lowassa hakuwakilisha state bali chama ndipo naposhindwa kuelewa.
Kwenye execution ya hiyo deal si ni lazima kuna procedures za ku approve?
Unapothubutu kusema EL hakuhusika hata kidogo yeye binafsi una maana gani?
Kuna ubinafsi na u state hapo na sielewi vigezo vyako vya kumetetea EL na kumpakazia huyo state peke yake.
Kwenye masuala ya kuruhusu wizi wa fedha BOT kwa kufoji nyaraka ni hatua ipi inamwingiza waziri mkuu katika kuweka sahihi, kuandika dokezo au kutoa amri ya kimadaraka kuamuru malipo yapitishwe bila mizengwe.
Kwamba alijua fedha inaibiwa ili kusaidia CCM ishinde hilo sina ubishi.
Ukisikia taarifa kwamba " serikali imetoa uamuzi fulani" haina maana vyombo vyote vya serikali Polisi Jeshi,Bunge,Mahakama na Ofisi ya Rais vimefikia uamuzi na kutoa tamko la pamoja.
Vingunge wachache wasiofika 10 wana uwezo wa kukaa na kutoa uamuzi kama chama na kuamuru waziri muhusika atoe tamko kupitia redio ya taifa kuhusu maamuzi mapya ya serikali.
Vivyo hivyo wizi huu ulipikwa ndani ya chama na kubarikiwa kisha kondoo wa kafara wakapigwa shinikizo kuufanikisha. Wale wenye dhambi sasa wanarudi na kujaribu kumchinja kondoo aliyekufa ili kuondoa dhambi ile ile. Kafara siku haiendeshwi hivyo.
Richmond kondoo wake.
EPA kondoo wake, kama kondoo hawapatikani wahusika jiandaeni kufa kifo cha dhambi ni halali yenu.
State sponsered, State house, State ni maneno tata kama unatafuta utata.
Fedha tunajua kwa kiwango kikubwa ziliishia kugharimia uchaguzi wa CCM kwa kuingizwa kwenye mifuko binafsi ya viongozi wa CCM na siyo account za CCM kama chama, na nyingine ziliishia kwenye UFUKSA.
Tukisema State sponsered katika nchi ambayo chama tawala ni dola pia kiwingu cha watu kinapungua na kuacha kundi lisilozidi watu 12 kujibu maswali kuhusu Kagoda.
Naomba wana CCM, wapenzi wa CCM mashabiki na waganga wao wa jadi wasituvuruge, watulie kama wananyolewa kwa wembe.
Hii issue bado mbichi kabisa, tena kwa taarifa yenu mwakani ni lazima iingie rasmi mezani kwa Obama, hapo mtajua kama Mharage ni mboga au mlo kamili.
Jiandaeni kuva vilemba vya manyasi na mabua ya mpunga. Nahii zenu nyie(kumradhi).