Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Haha haha haha

Hiyo mbona tayari nimepeleka swali bungeni. Nilidhani unasemea Kamati ya Bomani. Hizi nyingine ni kazi za kila siku na wala hazizuii kufanya kazi nyingine. Tumetumwa Bungeni kufanya kazi hizi. Na JF inasaidia sana kupata taarifa.

Point ya msingi katika mambo makubwa kama haya ya KAGODA ni rahisi sana kupoteza watu maboya. Ninarudia, Lowasa hahusiki moja kwa moja na KAGODA. Labda wanaofloat jina lake hapa wana ajenda fulani ambayo ninaamini ni kutuzuga.

Ninadhani what i have ni kamili. Ninaamini ni 100%!

Tatizo unasema nafuatilia, unatuacha wengine tukisubiri majibu hadi baadae. Baadae huwa haifiki.
 
Politics as usual..Nimeuliza swali uka ignore...Kuhani amekulima swali lile lile na bado unakwepa kisiasa.
Mfano niliotowa kuhusiana na kauli ya usalama wa Taifa ni similar in terms of ambiguity.
Unaposema state allowed the deal na huku ukisema Lowassa hakuwakilisha state bali chama ndipo naposhindwa kuelewa.
Kwenye execution ya hiyo deal si ni lazima kuna procedures za ku approve?
Unapothubutu kusema EL hakuhusika hata kidogo yeye binafsi una maana gani?
Kuna ubinafsi na u state hapo na sielewi vigezo vyako vya kumetetea EL na kumpakazia huyo state peke yake.

Wakati mwingine tunakuwa kama sinema ya bure na hivyo kuwapa nafasi wabaya wetu waendelee kutanua. Twende sabamba na mteremko wa mambo kwa kunyumbulisha matukio na wakati - tunaweza kukuta tanayajibu maswali yetu sisi wenyewe bila kumtegemea Mh. Zito atuandalie chakula, atuwekee mezani, atushikishe vijiko n.k. - no, no, no. We have brains - lets use them. Tuna"deal" with people who once thought they were untouchable. Mnamkumbuka first lady wa Romania alivyong'aka siku mmewe anatiwa pingu. Swali lake lilikuwa moja tu - how dare you touch HIM. Well soon the untouchables will be touched and all you need is to be patient. A luta continua !!!
 
you bring doubts and despair.

Doubts should be there. But i am honest. I am saying what i believe is the truth. I dont choose words.

Shivji once told me 'doubt everything' So i cant doubt you to doubt
 
Ha ha ha ha! Does it sound so?

Oh yes, very cogent case in behalf of Lowassa there.

Yani hujasema kwamba hakuna ufisadi wa Kagoda, wala hujasema Serikali haijahusika.

Halafu hujasema Lowassa msafi, na hujasema tumuache Lowassa apumzike.

Umesema tu nyeti zako zinakuonyesha hii ni "state-sponsored corruption." Such an impenetrable defense of him.

Tatizo ni kwamba sisi tunataka kujua who is the state, Katibu Tarafa ?
 
During that time Mkapa was the Head of State, it was not a transition period. In real sense we do not have transition period as you have in the US. Hii ni Afrika nzima karibia. Uliona Kenya au Zambia au Zimbabwe? Tanzania ni hivyo hivyo

KAGODA took money from BOT between August 1st and December 14th 2005. EL became PM December 30 2005.

Ndugu Zitto wanasiasa huwa mnatuchanganya sana.
Kwasababu hapa bado sijaelewa kabisa..Ila kama ulivyosema hapo juu kuwa hutajibu tena unaishia pale...Nayaheshimu maamuzi yako lakini kuna utata sana na tunaendelea kufuatilia kwa karibu tu.
Umesema hakuna transition period lakini kuna period ambayo umesema hakukuwa na waziri mkuu..Ndio nikauliza kuwa ni nani yuko responsible kwenye kipindi hicho ie august 1st na december 14th?
Nani anahesabika kama mtendaji mkuu wa serikali? Hiyo mifano ya Kenya na Zimbabwe siko aware nayo..Ila tuna mfano hai tu hapo bongo...Mfano ambao ninge appreciate kama tukiutumia.
 
Oh yeah, very cogent case in behalf of Lowassa there.

Yani hujasema kwamba hakuna ufisadi wa Kagoda, wala hujasema Serikali haijahusika.

Halafu hujasema Lowassa msafi, na hujasema tumuache Lowassa apumzike.

Umesema tu nyeti zako zinakuonyesha hii ni "state-sponsored corruption." Such an impenetrable defense of him.

Tatizo ni kwamba sisi tunataka kujua who is the state, Katibu Tarafa ?


Kuhani sijibu tena. Nimefikia kikomo cha kile ninachoweza kusema kwa sasa. Nimekutafunia sana.
 
During that time Mkapa was the Head of State, it was not a transition period. In real sense we do not have transition period as you have in the US. Hii ni Afrika nzima karibia. Uliona Kenya au Zambia au Zimbabwe? Tanzania ni hivyo hivyo
Wacha nimsaidie mheshimiwa huyu maana ukweli kwa nafasi yake na jukumu lake kiuongozi haviruhusu yeye kusema zaidi ya hapa.

STATE + WATU = MKAPA > LUMBANGA>APSON MWANG'ONDA > BALALI +ROSTAM AZIZ

MKAPA= GODFATHER
LUMBANGA= KIRANJA
MWANGO'NDA=MSIMAMIZI
BALALI=EXECUTIONER
ROSTAM=ZE BRAIN

Wenye kujua zaidi ama tofauti naomba mnisaidie..

Tanzanianjema
 


Ndugu Zitto wanasiasa huwa mnatuchanganya sana.
Kwasababu hapa bado sijaelewa kabisa..Ila kama ulivyosema hapo juu kuwa hutajibu tena unaishia pale...Nayaheshimu maamuzi yako lakini kuna utata sana na tunaendelea kufuatilia kwa karibu tu.
Umesema hakuna transition period lakini kuna period ambayo umesema hakukuwa na waziri mkuu..Ndio nikauliza kuwa ni nani yuko responsible kwenye kipindi hicho ie august 1st na december 14th?
Nani anahesabika kama mtendaji mkuu wa serikali? Hiyo mifano ya Kenya na Zimbabwe siko aware nayo..Ila tuna mfano hai tu hapo bongo...Mfano ambao ninge appreciate kama tukiutumia.

The Head of State in Tanzania is the Head of the Government. Rejea nimesema Sumaye hakuwa 'substantive PM'

Umeelewa?
 
Doubts should be there. But i am honest. I am saying what i believe is the truth. I dont choose words.

Shivji once told me 'doubt everything' So i cant doubt you to doubt


I doubt your honesty, and what you believe as the truth. You are not straight at any point, au ndio kureflect uanasiasa wa kitanzania?!
 
Wacha nimsaidie mheshimiwa huyu maana ukweli kwa nafasi yake na jukumu lake kiuongozi haviruhusu yeye kusema zaidi ya hapa.

STATE + WATU = MKAPA > LUMBANGA>APSON MWANG'ONDA > BALALI +ROSTAM AZIZ

MKAPA= GODFATHER
LUMBANGA= KIRANJA
MWANGO'NDA=MSIMAMIZI
BALALI=EXECUTIONER
ROSTAM=ZE BRAIN

Wenye kujua zaidi ama tofauti naomba mnisaidie..

Tanzanianjema

Umevua gloves?

Mimi simo, sijataja.
 
Mh. Zitto... mimi nakuombea usifungiwe tu tena Bungeni. Wenye meno wataweza kusaga na kumeza ulichowalisha baada ya kukichuma na kukibondabonda..... zaidi ya hapo utakuwa unaingiza vidole vinywani too much na kuishiwa kung'atwa!!
 
Wacha nimsaidie mheshimiwa huyu maana ukweli kwa nafasi yake na jukumu lake kiuongozi haviruhusu yeye kusema zaidi ya hapa.

STATE..

MKAPA= GODFATHER
LUMBANGA= KIRANJA
MWANGO'NDA=MSIMAMIZI
BALALI=EXECUTIONER
ROSTAM=ZE BRAIN

Hiyo ni "the State" ya Mkapa crime syndicate.

Niambie "the State" ya Kikwete regime wakati wa Richmonduli, EPA, Kagoda.
 
The Head of State in Tanzania is the Head of the Government. Rejea nimesema Sumaye hakuwa 'substantive PM'

Umeelewa?

Kuna head of state ofcourse ni raisi na kuna mtendaji mkuu na nafikiri ni waziri mkuu..Na ukisema state sponsored hakuna kiongozi wa serikali iliyokuwepo madarakani ambaye atakuwa hausiki.

Umeelewa?
 
I doubt your honesty, and what you believe as the truth. You are not straight at any point, au ndio kureflect uanasiasa wa kitanzania?!

Mama, naamini kuna limit ya yale anayoweza kuongea kwenye mihadhara kama hii hali kesi yenyewe bado iko jikoni kisheria na kila pande. Na pale Mh. Mbunge anapoamua kushirikiana nasi waziwazi, basi tusi question sana integrity yake pale anaposema yuko 100% sure na anachokisema au kukiamini. Ahsante.

SteveD.
 
Mimi simo, sijataja.

You see, hicho ndio anachoogopa Zitto hicho.

That's what I'm talking about nikisema Zitto anataka kujijengea gravitas. Ile image ya back bencher truth teller na kukemewa kemewa na Spika haitaki tena. Ameshaingizwa kwenye wanaoaminiwa na Tume za Rais.

You see, this is why Dr. Slaa is the most ballsy leader in modern history of Tanzania.
 
Hiyo ni "the State" ya Mkapa crime syndicate.

Niambie "the State" ya Kikwete regime.

Kasema hajibu tena, Steve kamwambia asiendelee kuongea atafungiwa kule bungeni. Mwacheni aendelee kufuatilia to know the truth, believe in it then, he is honest.
 
Kasema hajibu tena...

Kwani tulitegemea majibu ?

Toka lini Mtanzania akapata majibu bana ?

Tuna formulate maswali na ku brainstorm majibu wenyewe kila siku hapa, na the Zitto's of the world couldn't give a hoot kutafuta majibu.

Ukishabweteshwa na privileges za Tume za Rais na kuweza kutembea kwenye corridors na sebule za Magogoni bila kuulizwa we nani utakumbuka kutafutia wananchi majibu ?
 
Slaa aapa kufa na Kagoda

2008-11-22 10:52:04
Na Waandishi Wetu

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa, amesema atatoboa siri ya majina ya wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited, katika ziara ya operesheni Sangara inayotarajiwa kuendelea hivi karibuni kama wahusika wakuu hawatafikishwa mahakamani.

Kagoda ni miongoni mwa kampuni zilizotajwa kuhusika katika ufisadi wa fedha za Akaunti ya Malipo ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambapo msemaji wa Wizara ya Katiba na Mambo ya Sheria, Omega Ngolle, alisema kamwe Mkurugenzi wa Mashitaka ya Jinai (DPP), Elieza Feleshi, hawezi kutaja majina ya wamiliki hao, licha ya kukagua mafaili ya watuhumiwa wa EPA.

Badala yake, Ngolle alisema jukumu la kutaja majina hayo linaweza kufanywa na Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela).

Hata hivyo, taarifa kutoka Brela ambazo zilichapishwa kwenye gazeti hili jana, zilieleza kuwa timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kuchunguza wizi wa EPA ndani ya BoT chini ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Johnson Mwanyika, ndiyo inayojua majina ya wamiliki wa kampuni hiyo.

Umiliki wa kampuni hiyo inayodaiwa kuchota asilimia 45 ya Sh. bilioni 90 zilizoibwa na kampuni 13 kati ya 22 ambayo yaliiba jumla ya Sh bilioni 133 ndani ya EPA, umezidi kuzua utata na maswali mengi kwa jamii.

Brela ilisema Kamati ya Mwanyika ndiyo inashikilia jalada hilo kwa sasa na yale ya makampuni mengine 21 yanayotuhumiwa kuchota fedha za EPA.

Akizungumza na Nipashe kwa njia ya simu jana, Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Karatu (Chadema), alidai kuwa inashangaza kuona mamlaka zinazohusika, 'zinatupiana mpira' kuhusu umiliki wa Kagoda na suala zima la EPA, licha ya ukweli wake kujulikana wazi.

Kwa mujibu wa Dk Slaa anayeaminika kuwa ndiye mtu wa kwanza kuibua sakata la ufisadi wa EPA na BoT kwa ujumla, wamiliki wa kampuni hiyo wanaojulikana, aliwataja kwa majina (tunayahifadhi).

Hawa wamiliki wa Kagoda wanajulikana, lakini hata kama wanatoa visingizio, basi wangewakamata watu wawili na kuwafikisha mahakamani, huko ndipo siri za wamiliki wengine zingejulikana,`` alisema.
Dk. Slaa alisema sakata la ufisadi uliofanywa na Kagoda haliwezi \'kufumbiwa macho` kwa kuwa linahusu na kuathiri maisha ya wananchi.


Alidai kuwa miongoni mwa matukio yanayotia shaka ni kampuni hiyo kufanikiwa kuchota kiasi cha Sh bilioni 40, ikiwa ni ndani ya wiki nane tu tangu ipate usajili.

Alidai kuwa tukio hilo lilifanyika mwaka 2005, ikiwa ni muda mfupi kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na Madiwani, hali inayozua hoja ya kutaka kujua mahali zilipoelekezwa fedha hizo.

Nacho Chama cha Wananchi (CUF), kimemtaka Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) kuacha ``kigugumizi`` juu ya Kagoda na badala yake awafikishe mahakamani watuhumiwa wa Kampuni ya Kagoda kwa kuwa wamiliki wake wanafahamika.

Akizungumza na Nipashe jana, Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, alisema kampuni hiyo ndiyo ya kwanza kugundulika kuchota fedha za EPA.

Alisema inashangaza kuona kuwa licha ya kampuni hiyo kuwa ya kwanza kugundulika kuiba fedha hizo mpaka sasa wahusika hawajafikishwa mahakamani.

Alisema wakaguzi wa ndani wa BoT walibainisha kuwa Kagoda ilichota zaidi ya Sh. bilioni 40.

Lazima hawa watu wajulikane na washtakiwe, hata kama wamerejesha fedha, lazima washtakiwe maana walighushi nyaraka na kama mtu amerejesha fedha zitumike kama kidhibiti kuwa kweli aliiba,� alisema Lipumba.

Alimshauri DPP kuwafikisha mahakamani haraka ili kujibu maswali ya wananchi ambayo wamekuwa wakijiuliza kuhusu nani hasa wamiliki wa kampuni hiyo.

Inawezekana kuna watu waliwekwa mbele tu, lakini waliokula fedha wengine, lakini hao vigogo ni rahisi kupatikana watafutwe wakasimame mahakamani kama wenzao,`` alisema.

Naye Mwenyekiti wa chama cha PPT Maendeleo, Peter Mziray, alisema watu wanashauku ya kuwaona vigogo wa Kagoda kwa kuwa ndiyo ya kwanza kushutumiwa katika wizi huo.

Alisema kama kuna watu walibambikizwa, lakini fedha zikaliwa na watu wengine ni vyema DPP akawasaka watu hao na kuwaunganisha na washtakiwa wengine.

Kagoda sio mzimu ni watu na lazima wajulikane hata kama kule Brela hawapo, ile akaunti iliyotumika lazima kuna picha ya waliokuwa wakiitumia,� alisema.

Katika hatua nyingine, mshtakiwa Rajabu Maranda, anayekabiliwa na kesi ya wizi wa fedha za EPA ameachiwa kwa dhamana baada ya kutoa hati ya mali yenye thamani ya Sh. milioni 450.

Maranda alidhaminiwa mbele ya Hakimu Mkazi, Hadija Msongo, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jana.

Mshitakiwa huyo anakuwa wa 18 kuwa nje kwa dhamana kati ya 20 ambao walifikishwa mahakamani hapo kwa siku tofauti kuanzia Novemba 5, mwaka huu.

Mshitakiwa huyo alipata dhamana baada ya kukaa gerezani kwa muda wa wiki mbili akikabiliwa na kesi nne tofauti za kuibia BoT.

Hata hivyo, kabla ya mshitakiwa kuachiwa kwa dhamana, mahakama hiyo iliahirisha kusoma maelezo ya awali baada ya upande wa utetezi kuomba muda wa kupitia maelezo hayo ambayo yalichelewa kuwafikia.

Mahakama ilikubaliana na ombi hilo na ikapanga Desemba 5 mwaka huu kuwa ndiyo siku ya itasikilizwa maelezo ya awali.

Aidha, mshitakiwa mwenzake katika kesi hiyo Farijala Hussein alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na hivyo alirudishwa gerezani hadi atakapotimiza masharti.

Katika kesi hiyo, Maranda na Farijala wanadaiwa kuiba Sh. 1,864,949,294.05 baada ya kudanganya kuwa kampuni ya Kiloloma Brothers ya Tanzania imehamishiwa deni na Kampuni ya B.C Cars Export Ltd ya Mumbai.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 5, mwaka huu watakaposomewa maelezo ya awali.

Maranda ambaye ni Kada wa CCM Mkoa wa Kigoma akisubiri kusikilizwa kwa maelezo ya awali ya kesi yake katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, aliyashambulia magazeti ya kampuni ya The Guardian Ltd kuwa yanamwandama .

Magazeti hayo yamekuwa yakifuatilia kwa karibu suala la EPA tangu liibuliwe mwaka jana hadi kesi zilipofunguliwa mahakamani.

Wakati huo huo, kesi ya wizi inayowakabiliwa Jayantkumar maarufu kama Jeetu Patel, Amit Nandy na Ketan Chohan iliahirishwa jana mbele ya Hakimu Mkazi, Richard Kabate wa mahakama hiyo.

Katika kesi hiyo, washitakiwa wanadaiwa kughushi na kujipatia Sh. 3,323,974,942.30, baada ya kudanganya kuwa Navy Cut Tobacco (T) Ltd imehamishiwa deni na kampuni ya Matsushita Electric Trading ya Japan.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 18, mwakani itakapotajwa tena.

Imeandaliwa na Mashaka Mgeta, Joseph Mwendapole na Hellen Mwango.

SOURCE: Nipashe
 
You see, hicho ndio anachoogopa Zitto hicho.

That's what I'm talking about nikisema Zitto anataka kujijengea gravitas. Ile image ya back bencher truth teller na kukemewa kemewa na Spika haitaki tena. Ameshaingizwa kwenye wanaoaminiwa na Tume za Rais.

You see, this is why Dr. Slaa is the most ballsy leader in modern history of Tanzania.

Kuhani, nadhani utakuwa humtendei haki Zitto katika hili. Tumeshaona hata kwa wenzetu walioendelea kwenye mahojiano yao na waandishi wa habari njinsi wanavyoweza kukwepa maswali ambayo huleta direct confrontation baina yao na waajiri. Sisi kama wananchi ni waajiri wa wabunge, lakini ili wawe wabunge ni lazima wale viapo ambavyo vitathibitisha maadili ya kazi zao kama vile ambavyo inatakiwa kuwa kulingana na miongozo tuliojiwekea sisi wananchi - Katiba.

Sasa kumlazimisha kiongozi kutamka maneno fulani ambayo yatafurahisha jamvi na kumfanya awe shujaa kwa dakika chache za JF hali zitakazo mfanya asiweze kuwakilisha wananchi wa jimbo lake kwa kipindi kisicho julikana, huko ni kutomtendea haki. Tukubali kwamba ameshataja mengi ambayo hamna kiongozi mwingine ameweza kutaja tayari kuhusiana na swala hili na kwenye thread hii.

Je, tuwe watu wa kulazimishana tu katika kila jambo, kwa kuchukulia kila neno linaloandikwa iwe kimakosa au bila makosa kwa dhati kwenye mtandao kama tamko la katiba? Hapana, huu utakuwa unyanyasaji wa kimtandao (cyber bullying). Jambo ambalo wote naamini tungependa kuepukana nalo. Tuko kwenye majadiliano ndugu yangu, basi pale mtu anapoenda mrama/mlama asihukumiwe jumlajumla. Ni mawaidha yangu, ahsante.


SteveD.
 
Back
Top Bottom