Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Hili la KAGODA sisi tumeshamaliza uchunguzi na ukweli tunaujua. Kesi hisi zitaweka yote wazi. Hakuna kitakachobaki kwani lengo letu ni kuhakikisha kuwa hali kama hii haitokei tena siku za usoni. Eti chama cha siasa kutumia fedha za umma kwa wizi ili kugharimia uchaguzi wake.QUOTE]

Mheshimiwa mbona unajikanganya sasa - Ni 'State Sponsored Corruption' au Ni 'Party Sponsored Corruption'? Au pengine ni 'Party State Sponsored Corruption'?

Kama ni State Sponsored ina maana Mkapa na Sumaye wanawajibika?

Ikiwa ni Party Sponsored ina maana wajumbe wa CC walihusika?

Na kama ni 'Party State Sponsored' ina maana Cabinet na CC zilikubaliana?

Naomba orodha ya wajumbe wa CC wakati wa Maandalizi ya Uchaguzi 2005!
 
Wacha nimsaidie mheshimiwa huyu maana ukweli kwa nafasi yake na jukumu lake kiuongozi haviruhusu yeye kusema zaidi ya hapa.

STATE + WATU = MKAPA > LUMBANGA>APSON MWANG'ONDA > BALALI +ROSTAM AZIZ

MKAPA= GODFATHER
LUMBANGA= KIRANJA
MWANGO'NDA=MSIMAMIZI
BALALI=EXECUTIONER
ROSTAM=ZE BRAIN

Wenye kujua zaidi ama tofauti naomba mnisaidie..

Tanzanianjema

Hii formula imebalance kweli? Hela ilitumika kwa kampeni ya chama au ya mtu/watu? Mtu/Watu wa Godfaza walipata fungu la kampeni?Walishinda?
 
STATE + WATU = MKAPA > LUMBANGA>APSON MWANG'ONDA > BALALI +ROSTAM AZIZ

MKAPA= GODFATHER
LUMBANGA= KIRANJA
MWANGO'NDA=MSIMAMIZI
BALALI=EXECUTIONER
ROSTAM=ZE BRAIN


Let us get this correct,Tanzania Njema. Kwa sababu huyu Apson ni Mkuu wa Usalama wa Taifa,au alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wakati wa Mkapa.
Kwa hiyo, if that is so,unasema,wahusika hapa ni;
Rais,Principal Secretary,Mkuu wa Usalama wa Taifa,Gavana wa Benki Kuu,na mfanya bishara,siyo mfanya biashara,nadhani Rostam Aziz alikuwa mweka hazina wa CCM.
This is mind boggling. Naona kuna mtu mmoja hapa ameiita The Syndicate which might delete a few lives very soon.
Na kama zilichukuliwa miezi miwili kabla ya Uchaguzi,ina maana kwamba probably zilitumika katika Uchaguzi.
Lakini kwa mfanao tukisema kwamba hakuna kosa kwa CCM kuchukua fedha Benki Kuu,kwa sabau Upinzani Tanzania hauna nguvu sana,kwamba CCM wakichukua fedha Benki Kuu kufadhili Uchaguzi,hiyo itakuwa sawa tu na CCP,Chinese Communist Party inachukua fedha katika Benki Kuu ya China,kwa sababu Upinzani wa Tanzania wapo tu watu kama Zitto Kabwe,ambao maneno mengi,lakini hawana ushawishi mkubwa kwa wananchi,ushahidi ni viti kidogo walivyopata Bungeni. Still,fedha zilizochukuliwa ni nyingi sana,na zilizotumika ni kidogo sana. It was stated kwamba 15 billion zilitumika aktika Uchaguzi,lakini 40 billion zilichotwa. Zile fedha zingine ziko wapi? In brief,zile fedha zingine ziko wapi?
 
Nadhani kuna watu wangependa sana kusikia Zitto akikubaliana nao kuwa "Yes Lowassa ni mmiliki wa Kagoda".Nadhani Mheshimiwa Mbunge ameweka wazi kile anachokijua yeye.Sasa kama kuna mwenzetu hapa anajua tofauti na anachosema Zitto,ni vema basi akakiweka hapa bayana.Kuanza kuhoji uanasiasa wa Zitto ni kukwepa mjadala wa maana,maana mara nyingi watu wanapoishiwa hoja hukimbilia kujadili personalities badala ya issues.

Kama kuna anayemwona Zitto ni m-babaishaji,sio mkweli,anatafuta umaarufu,na chochote kile negative,hiyo ni haki yake ya kikatiba na ki-JF kuwa huru katika mtazamo huo.Lakini kama tunataka kujadili hoja kwa hoja,basi nadhani Mh Zitto amekuwa consistent na anachokijua.Kuwa Mbunge wa upinzani haimaanishi kuafiki taarifa potofu dhidi ya CCM au viongozi wake.Mwanasiasa makini ni yule anayeweka mbele maslahi ya nchi/watu badala ya chama.

Tukubaliane tusikubaliane,kwa desturi za viongozi wetu ni nadra sana kumkuta angalau mmoja anapoteza "muda wake muhimu" kujadiliana na wananchi wenzake katika mahala kama JF.Siku ukimsikia Makamba au Mkuchika kaja JF basi ni kutangaza vita dhidi ya mtandao huu muhimu.Tumpongeza Mh Zitto kwa hilo,hata kama kuna wasioafikiana nae katika anachochangia hapa.Viongozi wa aina hii ni adimu,sio kwa Tanzania tu,bali hata Afrika kwa ujumla,ambapo UONGOZI MAANA YAKE NI KUWA MBALI NA WANANCHI WA KAWAIDA.

Anyway,HAPA kuna habari zaidi kuhusu Kagoda
 
1. Hakuna mtu hapa anaweza kuprove kuwa Zito wa JF ndiye yule Zito Kabwe,Mb. Nasema hata kama hakinijibu humu kuwa ndiye yeye bado hiyo si proof.

kama ni hivyo, ni vigumu sana kuprove mengi yanayosemwa humu kwa sababu ya kiwingu kama ulichobainisha.
Lakini, wka nini asiwepo anayeweza kuprove kama kweli Zito anayelonga humu ndiye Zioto Mhe. Mbunge?
 
Hotuba ya msemaji mkuu wa kambi ya Upinzani Dr. Willibrod Peter Slaa (Mb)

Kuhusu makadirio ya matumizi ya fedha ya ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa kwa mwaka wa fedha 2008/2009


Kwa Taarifa tuliyonayo, Ripoti ya Ukaguzi wa EPA katika kifungu cha 3.20, 3.23, na 3.24, kinatamka wazi uwepo wa "fraudulent supporting documents submitted in to support claims" Yaani ufisadi uliotumika ni pamoja na kutumia hati za kugushi katika kutoa fedha kutoka BOT; malipo ya viwango visivyo sahihi au kutumia viwango visivyo sahihi vya kubadilisha fedha (yaani incorrect amounts and incorrect exchange rate). Ukaguzi ulionyesha kuwa kati ya Tshs 133 Billioni malipo ya zaidi ya 90.3 Billioni yalifanyika kwa kutumia Hati za kugushi (invalid and fraudulent supporting documents), nyaraka hizi zimeonyeshwa katika kiambatanisho C ikionyesha na majina ya Makampuni husika.

Katika kifungu cha 3.25 Ukaguzi huo ulishauri kuwa kwa malipo ya zaidi ya 42.6 Billioni uchunguzi wa kina unahitaji kufanyika. Taarifa hii haikutolewa wazi kwa Bunge wala kwa Watanzania ambao ndio wenye mali hiyo na Serikali ni mdhamini kwa niaba yao tu.

Ufisadi unaotisha zaidi ni ule uliofanyika kupitia Kampuni ya Kagoda Agriculture Ltd iliyosajiliwa nchini chini ya Sheria ya Makampuni Sura ya 212 tarehe 29 September, 2005 na kupata Hati na 54040. Wakurugenzi waliosajiliwa wa Kagoda ni watu wawili wenye anuani za Kipawa Industrial area, Plot no 87 Temeke Dar-Es-Salaam, na P.O.Box 80154 Dar-Es-Salaam, kinyume na utaratibu wa usajili Brella ambao unahitaji wakurugenzi wa Makampuni kujisajili kwa kuonyesha anuani ya mahali anapoishi na siyo Sanduku la Posta.

Isitoshe, kwenye Fomu za usajili, ambapo John Kyomuhendo amejionyesha kuwa "Promoter" hawakuonyesha kama ni wakurugenzi mahali pengine kwenye kampuni nyingine yeyote. Cha kushangaza ni kuwa Kampuni hiyo ambayo wakurugenzi wake dhahiri wanaonekana wapya kabisa katika uwanja wa biashara ndani ya wiki 8 walikuwa wamekwisha kuchotewa zaidi ya Dolla za Marekani 30.8 Millioni yaani karibu zaidi ya shs Billioni 40 kwa kinachoelezwa na ukaguzi wa EPA kuwa hati bandia ambazo dalili za wazi ni kuwa Hati hizo karibu zote zimesainiwa na watu wasiohusika na Makampuni zinazodhaniwa zimefanya biashara na Kampuni ya Kagoda (Kif.cha 3.27); baadhi ya Makampuni yaliyodhaniwa kufanya Biashara na Kagoda au hayako kabisa au yamekwisha kubadilisha majina yao (Kif.3.27), Makampuni hayo ambayo yako Marekani, Japan, Ujerumani, Italia, Ufaransa mengine hata anuani zake hazikujulikana kabisa.


Katika hali hii inayoonyesha wazi kuwa kulikuwa na kugushi. Mhe. Waziri Mkullo alipokuwa akijibu alitetea kuwa fedha za EPA si za za Serikali. Kinachotisha zaidi, Mhe. Spika, hata Kampuni ya Ukaguzi ya Deloitte kwa Barua yao kwa Gavana wa Benki Kuu ya tarehe 6 September 2006 na kwa Wakurugenzi wote wa BOT ya tarehe 10 October, 2006 walipomjulisha Gavana, pamoja na wajumbe wote wa Bodi, kati yao akiwemo Katibu Mkuu wa Hazina Bwana Gray Mgonja, kuwa kuna utata kuhusu Kampuni ya Kagoda, ambayo japo ilisajiliwa 29 September,2005 tarehe 10 September 2005 ilikuwa tayari na Mkataba wa kiasi cha fedha za Japan (Japan Yen) JPY 956,110.986 na Kampuni ya Nishizawa Ltd na Mkataba mwingine wa Dola za Marekani 9,057,463.90 wa Tarehe 12 September, 2005 na Kampuni ya Textima Ltd na mikataba hii yote inatamka kuwa "Kampuni hii imesajiliwa Tanzania kwa mujibu wa Sheria" jambo ambalo dhahiri ni udanganyifu na ni uvunjifu wa Sheria.


Isitoshe Mheshimiwa Spika,
Kampuni ya Deloitte ilionyesha katika Barua walizomwandikia Gavana na Wajumbe wa Bodi dosari zifuatazo kuwa Mikataba (Deeds of Assignments) yana maneno na mfumo unaofanana jambo linaloashiria kuna kugushi, kwani makampuni kwa kawaida yanapenda kuwa na vipengele visivyofanana.

Kati ya hati zote hizo hakuna hata moja iliyowekwa kwenye "Letter Head" ya Kampuni zao, mikataba yote imesainiwa ukurasa wa mwisho tu tofauti na kawaida ya kusaini mikataba, Makampuni 12 yana muhuri (seal) unaofanana na ule wa Kampuni ya Kagoda, Mikataba ya Makampuni ya Fiat Veicoli Industriali ya Italia, Valmet (USA) Adriano Gardella S.P.A (Italy) yote haikuwa na mihuri japo Mkataba unaonyesha kuwa muhuri umewekwa, Kampuni ya Valmet yenye Mkataba wa Dolla za Marekani 2,398,439.96 umewekewa saini na mtu anayeitwa Patrick Kevin, Mhasibu (accountant) jambo ambalo si kawaida kwa mkataba wa kiwango kikubwa kiasi hicho.

Mambo haya yote yalipaswa kutoa ishara kwa Benki Kuu kuwa mikataba yote imegushiwa lakini wala siyo Benki Kuu wala Wakurugenzi waliostuka na kuchukua hatua pamoja na barua hiyo ya Deloitte.
 
Source: bongo5 Dot com

Wenye kampuni zilizolipwa EPA hawa hapa MAJINA ya wamiliki na wakurugenzi wa makampuni matano kati ya 20 yanayodaiwa kujipatia mabilioni ya fedha isivyohalali kupitia Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA), yamejulikana.

na Tamali Vullu na Irene Mark

MAJINA ya wamiliki na wakurugenzi wa makampuni matano kati ya 20 yanayodaiwa kujipatia mabilioni ya fedha isivyohalali kupitia Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA), yamejulikana.

Akizungumza na Tanzania Daima, ofisini kwake Dar es Salaam jana, Naibu Msajili wa Makampuni na Majina ya Biashara wa BRELA, Andrew Mkapa, alisema mengi ya makampuni hayo yalisajiliwa mwaka 2005. “Kati ya majina ya wamiliki nitakayotaja, wanne wanamiliki firm (kampuni ndogo) ambazo zinaonyesha zimesajiliwamwaka 2005. “Firm ni tofauti na kampuni, kwani kunapotokea tatizo katika firm, mmiliki ndiye anayeshitakiwa na si firm, tofauti na katikamakampuni ambako huwa yanashitakiwa makampuni na si wamiliki,” alisema.

Aliwataja wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture, kuwa ni John Kyomuhendo mwenye hisa 40 na Francis Williamanayemiliki hisa 60 katika kampuni hiyo. “Kampuni ya Kagoda ilisajiliwa kwa namba 54040 kwa anuani ya Posta 80154 Dar es Salaam na waliandikisha kuwa ofisizake zipo Kipawa kitalu namba 87 Wilaya ya Temeke. “Makazi ya wamiliki hao ni Kinondoni Hananasif, kitalu namba 51 anakoishi Kyomuhendo wakati William anaishiKinondoni, Mtaa wa Lowa kitalu namba 31b 13,” alisema Mkapa.

Aidha, aliwataja wamiliki wa firm iitwayo Mibale Farm iliyosajiliwa Septemba 2, 2005 na kupewa namba 154039 kuwa niKizza Selemani na Farijala Hussein. Msajili huyo alitaja mmiliki mwingine kuwa ni Beredy Malegesi ambaye anamiliki firm ya Malegesi Law Chambers iliyosajiliwa Septemba 24, 2001 kwa namba za usajili 130278. “Mmiliki mwingine ni Paul Nyingo na Fundi Kitungi, wanaomiliki firm ya Money Planners & Consultants iliyosajiliwa Machi22 mwaka 2005 kwa namba 150731.

“Firm nyingine ni Kiloloma & Bros Enterprises inayomilikiwa na Charies Kissa, ambayo ilisajiliwa Aprili 8 mwaka 2005,”alisema. Makampuni hayo na mengine ambayo Tanzania Daima bado haijafanikiwa kufahamu wamiliki wake, yalibainika kuwayalilipwa zaidi ya sh bilioni 133 isivyo halali kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) iliyopo Benki Kuu (BoT). Hayo yamebainika baada ya Kampuni ya Ernst & Young kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo kwa niaba ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuuwasilisha ripoti ya ukaguzi wake serikalini. Baada ya kuisoma ripoti hiyo, Rais Jakaya Kikwete alimfukuza kazi aliyekuwa Gavana wa BoT, Daud Ballali kutokana nakasoro zilizobainishwa
 
Kama kweli Kagoda ilikuwa 100% state sponsored kama anavyosema Zitto, then ilikuwaje Zakia Meghji akadiliki kusema kuwa marehemu Gavana Balali alikuwa amemuongopea juu ya matumizi ya hela walizokwapua? Pili. kama hivyo ni kweli mbona wahusika wakuu wanaotajwa hawakuwa wafanyakazi serikalini? Usalama wa Taifa walikuwa na makampuni yao yaliyotajwa katika kashfa hii lakini sio Kagoda!!
 
Source: bongo5 Dot com

Wenye kampuni zilizolipwa EPA hawa hapa MAJINA ya wamiliki na wakurugenzi wa makampuni matano kati ya 20 yanayodaiwa kujipatia mabilioni ya fedha isivyohalali kupitia Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA), yamejulikana.

na Tamali Vullu na Irene Mark

MAJINA ya wamiliki na wakurugenzi wa makampuni matano kati ya 20 yanayodaiwa kujipatia mabilioni ya fedha isivyohalali kupitia Akaunti ya Madeni ya Malipo ya Nje (EPA), yamejulikana.

Akizungumza na Tanzania Daima, ofisini kwake Dar es Salaam jana, Naibu Msajili wa Makampuni na Majina ya Biashara wa BRELA, Andrew Mkapa, alisema mengi ya makampuni hayo yalisajiliwa mwaka 2005. "Kati ya majina ya wamiliki nitakayotaja, wanne wanamiliki firm (kampuni ndogo) ambazo zinaonyesha zimesajiliwamwaka 2005. "Firm ni tofauti na kampuni, kwani kunapotokea tatizo katika firm, mmiliki ndiye anayeshitakiwa na si firm, tofauti na katikamakampuni ambako huwa yanashitakiwa makampuni na si wamiliki," alisema.

Aliwataja wamiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture, kuwa ni John Kyomuhendo mwenye hisa 40 na Francis Williamanayemiliki hisa 60 katika kampuni hiyo. "Kampuni ya Kagoda ilisajiliwa kwa namba 54040 kwa anuani ya Posta 80154 Dar es Salaam na waliandikisha kuwa ofisizake zipo Kipawa kitalu namba 87 Wilaya ya Temeke. "Makazi ya wamiliki hao ni Kinondoni Hananasif, kitalu namba 51 anakoishi Kyomuhendo wakati William anaishiKinondoni, Mtaa wa Lowa kitalu namba 31b 13," alisema Mkapa.

Aidha, aliwataja wamiliki wa firm iitwayo Mibale Farm iliyosajiliwa Septemba 2, 2005 na kupewa namba 154039 kuwa niKizza Selemani na Farijala Hussein. Msajili huyo alitaja mmiliki mwingine kuwa ni Beredy Malegesi ambaye anamiliki firm ya Malegesi Law Chambers iliyosajiliwa Septemba 24, 2001 kwa namba za usajili 130278. "Mmiliki mwingine ni Paul Nyingo na Fundi Kitungi, wanaomiliki firm ya Money Planners & Consultants iliyosajiliwa Machi22 mwaka 2005 kwa namba 150731.

"Firm nyingine ni Kiloloma & Bros Enterprises inayomilikiwa na Charies Kissa, ambayo ilisajiliwa Aprili 8 mwaka 2005,"alisema. Makampuni hayo na mengine ambayo Tanzania Daima bado haijafanikiwa kufahamu wamiliki wake, yalibainika kuwayalilipwa zaidi ya sh bilioni 133 isivyo halali kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje (EPA) iliyopo Benki Kuu (BoT). Hayo yamebainika baada ya Kampuni ya Ernst & Young kufanya uchunguzi wa tuhuma hizo kwa niaba ya Mdhibiti naMkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) na kuuwasilisha ripoti ya ukaguzi wake serikalini. Baada ya kuisoma ripoti hiyo, Rais Jakaya Kikwete alimfukuza kazi aliyekuwa Gavana wa BoT, Daud Ballali kutokana nakasoro zilizobainishwa

kuna dalili ya kwamba evidence ya umiliki ilibadilishwa , sasa kama faili lilibadilishwaa , je account zilikuwaje, na movement za pesa zilikwenda wapi. pia inawezekana kuna watu wanalo original evidence kabla hazijabadilishwa, ndio maana wameweza kutamka watu fulani kuwa owner wa hiyo kagoda. na juu ya hivyo mbona huyo william na john hawajapelekwa mahakamani? na Pili kwanini kuna kuja theory nyingine kwamba aliye fanya kosa hilo ni Baba wa Mtu fulani ambaye amefariki, hivyo hakuna waku mpeleka mahakamani, baada ya watoto kurudisha hiyo hela.
 
Kagoda ni hatari

• Mtikisiko utazidi wa Lowassa, Karamagi, Msabaha

na Salehe Mohamed
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

KITENDAWILI cha kufikishwa mahakamani ama kutajwa majina ya watuhumiwa wa wizi wa fedha katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) kupitia Kampuni ya Kagoda kimeendelea kuwa kigumu baada ya kuelezwa kuwa kunaweza kusababisha kuyumba kwa utawala wa nchi, siasa na uchumi.

Habari za kuaminika ambazo Tanzania Daima Jumapili, imezipata zinadai kuwa umiliki wa kampuni hiyo hadi hivi sasa imegubikwa na utata kutokana na serikali pamoja na Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kushindwa kuweka bayana majina ya wamiliki, licha ya kuwapo kwa kelele za wananchi wakitaka watuhumiwa watajwe na kufikishwa mahakamani.

Habari hizo zinaeleza kuwa ni vigumu zaidi kwa vigogo hao wa Kagoda kupandishwa kizimbani, kwani hiyo itakuwa ni hatari na mtikisiko mkubwa zaidi kutokea hapa nchini kuliko hata ule uliotokea katika sakata la Richmond ambalo lilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na mawaziri wawili kuachia ngazi kwa kuhusishwa na kashfa hiyo.

Mtikisiko huo ulimfanya Rais Jakaya Kikwete, kuvunja baraza la mawaziri na kuunda jingine huku akiwaacha mawaziri kadhaa ambao wanadaiwa kuhusika kwa namna moja au nyingine katika vitendo vya kifisadi, ikiwemo kutoa baraka juu ya uchotaji wa fedha hizo.

"Kuna mkakati wa hali ya juu kuhakikisha vigogo wa Kagoda hawafikishwi mahakamani na siku wakipandishwa, basi kuna kila dalili nchi kutikisika na watu wenye heshima zao kuumbuka," kilisema chanzo hicho cha habari.

Miongoni mwa waasisi wa wizi wa EPA, kupitia Kampuni ya Kagoda ni mwanasiasa mkongwe aliyewahi kupata nyadhifa mbalimbali katika vipindi vyote vya utawala wa nchi hii tangu ipate uhuru wake.

Mwanasiasa huyo ambaye alitarajiwa kuwa mfano wa kuigwa kutokana na kuishi na kufanya kazi muda mrefu na hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, hivi sasa ameonekana ndiye kinara wa kuvunja maadili.

Kampuni ya Kagoda inadaiwa kujichotea sh bilioni 40 katika kipindi cha mwezi mmoja tangu iliposajiliwa mwaka 2005 na inadaiwa kuwa uanzishwaji wake ulitokana na mawazo ya vigogo kadhaa wa kisiasa waliopo madarakani na wengine wamemaliza muda wao.

Uchotaji fedha huo mara ya kwanza ulihusishwa na matumizi ya usalama baada ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Zakhia Meghji, kuthibitisha taarifa hizo wakati akitoa ufafanuzi kwa wanasiasa machachari waliokuwa wakizihusisha fedha hizo na vitendo vya kifisadi.

Kitendo cha Meghji kushindwa kujieleza vizuri ndani ya Bunge, kilionyeshwa wazi kwamba kuna kasoro, hali iliyosababisha baadhi ya wabunge kuomba itafutwe kampuni ya kufanya ukaguzi wa hesabu dhidi ya tukio hilo (BoT).

Meghji, hakuweza kuendelea kuibeba kauli yake hiyo kwani baadaye alinukuliwa kuwa alipewa taarifa zisizo na ukweli na aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) marehemu Daud Ballali.

Kuhusika kwa vigogo wa siasa katika wizi huo ndiko kunakowafanya wahahe usiku na mchana ili kuhakikisha hakuna nyaraka zinazowahusisha moja kwa moja na umiliki wa kampuni hiyo, sambamba na kufanya kila wawezalo kuhakikisha hawapandi kizimbani.

Mazingira ya uchotaji wa fedha hizo yalifanyika wakati taifa likiwa katika mchakato wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, ndiyo maana baadhi ya wanasiasa wamekuwa wakikituhumu chama kimoja kikubwa cha siasa kuhusika katika kashfa hiyo, licha ya viongozi wake kukataa kuhusika na wizi huo.

Kagoda, iliweza kujichotea kiasi kikubwa hicho cha fedha katika muda wa mwezi mmoja tangu imesajiliwa, jambo ambalo limezua maswali mengi yasiyo na majibu miongoni mwa Watanzania na kuhoji imekuwaje kampuni ngeni kuaminiwa na kupatiwa kiasi kikubwa cha fedha bila kufanyiwa uhakiki wa kina na watendaji wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), ambao ndio waliokuwa na dhamana ya kutoa fedha hizo.

Pamoja na kampuni hiyo kuchota kiasi kikubwa cha fedha lakini hadi hivi sasa wamiliki wake hawajulikani na hawajafikishwa mahakamani, licha ya wamiliki wa kampuni nyingine zilizoiba fedha za EPA kufikishwa mahakamani, hali inayoibua maswali mengi kwa jamii.

Mmoja wa kigogo ambaye kampuni yake ilihusishwa na wizi wa EPA, hivi karibuni aliumwa ghafla na kuchanganyikiwa, baada ya kupewa taarifa kuwa yeye ni mmoja wa watu watakaoburuzwa mahakamani, licha ya kulipa fedha alizoiba.

Kigogo huyo ambaye anasifika kwa kufadhili mambo mbalimbali ya kijamii, alichanganyikiwa zaidi pale alipotaka kwenda kutibiwa nchi jirani na kukataliwa kusafiri na watu wa usalama, kwa kile kilichodaiwa ni maandalizi ya kumburuza mahakamani.


Kukataliwa huko kulimfanya awajie juu baadhi ya watendaji na kuwatishia kuanika namna wizi ulivyofanyika na watu waliohusika, bila kuangalia vyeo vyao na nafasi waliyonayo katika jamii, iwapo serikali itadhamiria kumpandisha kizimbani.

Tishio hilo lilimsaidia, kwani aliruhusiwa kwenda nchi jirani kupatiwa matibabu huku akilenga kutorejea hapa nchini kwa hofu ya kuburuzwa kortini, alirejea hapa nchini baada ya kuhakikishiwa kuwa si mmoja wa watu watakaopandishwa mahakamani kama alivyosikia awali.

Kigogo huyo inadaiwa hakuhusika katika wizi huo wa EPA, lakini alijikuta akihusishwa baada ya kununua kampuni iliyoshiriki kuchota fedha za EPA kutoka kwa rafiki yake wa karibu na mwanasiasa ambaye aliogopa kuendesha kampuni hiyo kwa kisingizio cha kuonekana ana mali nyingi ndani na nje ya chama.

Alipokuja kutambua kauziwa kampuni iliyoshiriki wizi wa EPA, alimfuata rafiki yake ambaye hakumpa ushirikiano unaotakiwa, jambo lililosababisha wawili hao kutokuelewana mpaka hivi sasa.

"Wafanyabiashara hawa uhusiano wao mpaka hivi sasa si mzuri, yule aliuza kampuni haonekani kujali tatizo linalomkabili rafiki yake aliyemuuzia kampuni," kilisema chanzo chetu cha habari.

Kagoda imeendelea kuwa gumzo hapa nchini, kiasi cha kumfanya Mwenyekiti wa Shirikisho la Wenye Viwanda Tanzania (CTI), Reginald Mengi, kutamka waziwazi kwamba mafisadi wote waliohusika lazima wafikishwe mahakamani bila kujali walikuwa wana miliki kampuni gani, wana nyadhifa gani serikalini au kwenye chama tawala.

Mengi, mmoja wa wafanyabiashara wanaoheshimika nchini, alisema litakuwa jambo la ajabu kama wamiliki wa kampuni ya Kagoda hawatatajwa majina ili wajulikane na kufikishwa mbele ya sheria kujibu tuhuma zinazowakabili.

Wakati Mengi, akitoa kauli hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Dk. Edward Hoseh, kwa nyakati tofauti amenukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwakamata mafisadi hao mara moja kunaweza kuyumbisha uchumi wa taifa.

Hatua ya kiongozi huyo aliyepewa jukumu zito la kuhakikisha anaokoa haki za Watanzania, inaonyesha wazi kwamba uchumi wa taifa hili unashikiliwa na watu fulani ambao hawapaswi kuguswa.

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahimu Lipumba, katika mkutano wake na waandishi wa habari mwannzoni mwa wiki iliyopita alisisitiza kuwa fedha za EPA zinahusika na uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 uliokipa ushindi Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Alisema inawezekana fedha zote hazikwenda katika uchaguzi kutokana na waliopewa jukumu la kuiba fedha hizo kuzitumia kwa mambo yao, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa wizi huo uliratibiwa na viongozi wa CCM.

"Inawezekana CCM hawakupelekewa fedha zote lakini ukweli unabaki pale pale kuwa mazingira yanaonyesha wazi ziliibwa kipindi cha uchaguzi na zilitumika kuwapa ushindi CCM," alisema Lipumba.


Wakati Lipumba akisema hayo, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), amesema atahakikisha watuhumiwa wa Kagoda wanafikishwa mahakamani hata kama wataendelea kulindwa na serikali.

Alisema wamiliki wa Kagoda wanapaswa wafikishwe kortini, kwani wamechota kiasi kikubwa cha fedha ukilinganisha na kampuni nyingine.

Sakata la EPA linatokana na makampuni 22 kukwapua sh bilioni 133, kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jambo lililomfanya Rais Jakaya Kikwete kutengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, Daud Ballali na kuunda tume iliyoongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, kuchunguza wizi huo baada ya ripoti ya Kampuni ya Ernst & Young kuthibitisha kuwapo kwa wizi.

Timu hiyo ilifanya kazi yake na kukabidhi ripoti kwa rais, ambaye alitoa muda kwa baadhi ya kampuni kurejesha kiasi hicho kabla ya Novemba mosi na kuahidi kuwa kampuni itakayoshindwa kufanya hivyo itaburuzwa kortini.

Rais Kikwete, aliitekeleza ahadi hiyo kwa kumkabidhi Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Elieza Feleshi, majalada ya kampuni zilizokwapua fedha za EPA.

DPP hadi sasa ameshawafikisha katika Mahakama ya Kisutu, watuhumiwa 20 wa wizi huo huku 18 kati ya hao wakipata dhamana ambazo zilikuwa na masharti magumu.

Washitakiwa waliofanikiwa kutoka kwa dhamana ni pamoja na Jeetu Patel, Amit Nandy, Ketan Chohan, Vinodbhai Patel, Bahati Mahenge, Davies Mwakale, Eddah Mwakale, Japhet Lema, Ajay Somani, Jay Somani na Johnson Lukaza.

Wengine ni Mwengesi Lukaza, Godfrey Mosha, Davis Kamungu, Ester Komu na kada maarufu na mweka hazina wa CCM, Shaaban Maranda.
 
KAGODA: The secret document that ''tells all''

THIS DAY

KAGODA Agriculture Limited signed a secret document with the Bank of Tanzania (BoT) to facilitate the illegal payment of more than $30.8m (approx. 40bn/-) from the external payment arrears (EPA) account, it has been revealed.

According to latest THISDAY findings, the secret document exposes the real beneficiary of the funds embezzled from the key BoT forex account during 2005/06.

It has been widely reported that two virtually unknown individuals - John Kyomuhendo and Francis William � were used by at least two prominent local business tycoons as fronts to camouflage their (tycoons) real involvement in Kagoda.

Kyomuhendo, whose name was used for documentation purposes as 'director' of Kagoda, is understood to have given power of attorney to one of the business tycoons immediately after the central bank transferred the funds to the company's accounts.

This tycoon, believed to have actually employed Kyomuhendo in one of his well-known companies, quickly withdrew the funds from Kagoda's bank accounts and used an elaborate money-laundering scheme provided by an equally well-known business partner to hide the monies elsewhere.

Officials close to the EPA scandal investigation led by Attorney General Johnson Mwanyika now say a written contract was prepared by the then BoT governor Dr Daudi Ballali (now deceased) as an ''insurance policy'' should anything go wrong after the huge payment was made to Kagoda.

''When Ballali was given instructions from the highest levels of government to approve the dubious payment to Kagoda, he decided that there should be some sort of written understanding between the central bank and the real beneficiary of the funds paid to Kagoda,'' said a well-placed source familiar with the scandal.

The source added: ''While Ballali certainly cannot be absolved from blame, there were powerful people in government who ordered him to authorise the payments to Kagoda.''

Insiders say several other documents that are yet to be made public name senior officials in the third phase government of ex-president Benjamin Mkapa who ''forced Ballali to okay the payment of more than 40bn/- to Kagoda.''

Imani David Mwakosya, who was the Head of Bilateral and Commercial Debt (HBCD) at the BoT at the time of the 133bn/- EPA scandal, is said to be one of ''only a few people aware or in possession of the secret document between the BoT and Kagoda.''

Mwakosya, who is also one of only two suspects still being held in remand prison in the ongoing EPA scandal prosecutions, is reported to hold ''valuable secrets'' related to the scandal.

And auditors who uncovered the scandal identified Mwakosya as the person ''primarily responsible for EPA account administration.''

Prosecutors have so far filed criminal charges against a total of 20 people at the Kisutu Resident Magistrate's Court in Dar es Salaam in connection with the EPA scam.

Eighteen of the accused persons have been released on bail. They include Mwakosya's former boss at the central bank, Ms Esther Komu, who was the deputy director of the BoT Debt Department (DDDD) which falls under the directorate of economic policy.

The prosecution team has already announced that Peter Noni, who served as BoT Director of Economic Policy, is among the many witnesses it will call to the stand to testify in the upcoming trial hearings.

After serving as director of economic policy, Noni was appointed to the post of BoT Director of Strategy Planning and Performance Review.

Other senior BoT officials scheduled to appear in court as prosecution witnesses have been named as Tamali Mwakilema, who has also served as deputy director of the BoT debt management department, Emmanuel Boaz, Elisa Isanja, Rashid Mwanga, Samwel Mark, Athumani Mtengeli, and Stela Chaula.

The Assistant Registrar of the Business Registration and Licensing Authority (BRELA), Andrew Mkapa, and senior officials from the Kenya Commercial Bank (KCB) and Commercial Bank of Africa (CBA) have also been listed as prosecution witnesses in the EPA trials.
 
Lakini jamani lazima tujiulize hivi na hawa wafanyakazi wa benki kuu(BOT) hawana kabisa maadili ya kazi yao katika utoaji wa fedha za umma na upokeaji?Maana yake naona walichofanya hapa ni kama kichaa kapewa rungu;vinginevyo ndiyo na wao wabinafsi(mafisadi)!Hapa sasa ndipo nipo wakubali HakiElimu "Elimu siyo cheti bali uwezo."
Kwasababu,ninavyojua mimi unatakiwa kufanya kazi kwa mujibu sheria na taratibu tofauti na hivyo ni bora ujiuzuru kwa manufaa ya Taifa na ndipo utakapotambulika shujaa kinapotokea kimeo kama hichi cha EPA.
 
Lakini jamani lazima tujiulize hivi na hawa wafanyakazi wa benki kuu(BOT) hawana kabisa maadili ya kazi yao katika utoaji wa fedha za umma na upokeaji?Maana yake naona walichofanya hapa ni kama kichaa kapewa rungu;vinginevyo ndiyo na wao wabinafsi(mafisadi)!Hapa sasa ndipo nipo wakubali HakiElimu "Elimu siyo cheti bali uwezo."
Kwasababu,ninavyojua mimi unatakiwa kufanya kazi kwa mujibu sheria na taratibu tofauti na hivyo ni bora ujiuzuru kwa manufaa ya Taifa na ndipo utakapotambulika shujaa kinapotokea kimeo kama hichi cha EPA.


This tells you about the rise and fall of Balali "R.I.P" (or enjoy ur day)
 
Majina yanayoonekana katika kufungua kampuni ya Kagoda japo yapo but it seems walitumika tuuu na ndiyo maana inakuwa vigumu kuwabebesha mzigo mzima wa Kagoda. Tunachotaka kuona hapa ni movement ya ile fedha baada ya kuingia kwenye Kagoda Bank Account then zilitokaje??? Nani aliidhinisha zile vourcher??? Nani alisaini check book zao if at all nyingine zilikuwa zinatoka kwa check book???? Mbona tuna hit around the bush wakati ukitaka kuwakamata unawapata tu kirahisi??? After all ni sisi hapa tunajitahidi kuwafahamu, intelligence na Serikali yake inafahamu kila kitu kuhusu Kagoda. Huo ni ukweli. This Day and Kulikoni nawasifu wanatukumbusha ya Kagoda na EPA in general but ukweli unafahamika. Wanaweza pia kuwapeleka hao walioandikwa kama Wakurugenzi mahakamani kwa fidia fulani na mwisho wa siku kesi zote hizo hukumu itaangukia BOT. Ndivyo nionavyo mimi.
 
Time will never come for these people. Tusisahau, Duniani kwa sasa, Money is everything. zile nyimbo za Bob Marley kuwa ....you can sometimes fool people but you cant fool all the people all the time... hazina nafasi kwa sasa. Tuishi kwa matumaini tu. In this contemporary World, if you have maney, you can fool all the people all the time the way you like. people acheni kuota Kagoda wala richmond. Imeshatoka ile.
 
All EPA suspects to face trial, says DPP

2008-11-26 11:04:17
By Joyce Kisaka

Director of Public Prosecutions Elieza Feleshi said yesterday his office would prosecute all suspects linked to the siphoning of 133 billion/- from the Bank of Tanzania External Payment Arrears (EPA) account, including those of Kagoda Agricultural Company regardless of their status.

The DPP also revealed that those who cleared their EPA debts were not exempt from trial.

Speaking exclusively to The Guardian, Feleshi said he would not be pushed to hurry up the prosecutions for the sake of succumbing to public pressure or any other quarter.
“We are professionals. We must maintain the ethics of our profession,`` the DPP said.

Asked to comment specifically on Kagoda, and whether he had the guts to charge its owners as they were rumoured to be big fish, the DPP simply laughed and affirmed that no one would escape the dragnet as long as he was part of the EPA suspects` list.

He reminded this reporter that there was a time when members of the public believed that the trial of EPA suspects would never take place, but this is exactly what is happening.

``People will know the truth once all the suspects are also arraigned,`` Feleshi said.

He said once a case file was handed to his office for prosecution, all suspects would be treated impartially regardless of their status or colour.

Responding to a question as to whether those who would be tried are only those who did not settle their EPA debts, the DPP cited as an example defendants Jeetu Patel and Njake who fully cleared their balance but were being prosecuted.

On the other hand, the DPP cautioned against rumour-mongering.

``We do not work on hearsay. We are an authority that utilizes proven information. Whoever has concrete information should go to the Director of Criminal Investigations and hand over the details,`` he said.

When requested to comment on Prime Minister Pinda`s remarks that the DPP would soon succumb to public pressure by prosecuting suspects who were linked to Kagoda, the DPP said what the Premier actually meant was that ``we have no plans to swallow the files,`` but they had to work on them according to law.

``We would have to go through the files and that needs time. Please give us room to work on this matter ``he said.

He said his responsibility was to approve the prosecution of suspects brought before a magistrate, and he was still doing that job. ``Court cases are filed according to merit. This is what members of the public should understand,`` he said.

``We should respect each other`s profession. Give us room work rather than concentrate on distorted information,`` he said.

SOURCE: Guardian
 
Nadhani KAGODA watafikishwa mahakamani 2010 miezi ya nne nne hivi....
 
Revealed: Forged Kagoda papers were full of flaws

- At same time, Yusuf Manji said to be in Kenya for medical treatment

THIS DAY


Hard times indeed: The spectre of elderly blind citizens accompanied by their young `sons` or `daughters` on undiscriminating begging missions has become a common sight in various parts of Dar es Salaam. Even school pupils aboard commuter buses are not spared the begging hand, as pictured along Morogoro Road at Magomeni Mapipa yesterday.
THISDAY REPORTER
Dar es Salaam

WHILE investigators are still haggling over whether or not to file criminal charges against prominent individuals behind Kagoda Agriculture Limited, it has been learned that forged documents used by the company to siphon over 40bn/- from the Bank of Tanzania had obvious flaws, thus presenting a clear-cut case to prosecute.

As already well-established by both auditors and investigators, the glaring errors evident in the documents include the use of obsolete names of creditor companies, incompatible dates, and poorly-forged signatures.

A total of 12 forged legal documents known as deeds of assignment were used to make illegal payments from the BoT’s external payment arrears (EPA) account to Kagoda, to the tune of $30,732,658.82 (approx. 40bn/-) in total.

All the documents were signed between September 10 and November 5, 2005 - a timespan obviously too short for Kagoda to have negotiated and signed assignments of debts with 12 different foreign creditors from across the globe.

Sources close to the investigations have also noted that the forger(s) of the documents used the same contractual terms and wording for all the different foreign creditors, which is also considered unrealistic since different companies are likely to insist on different clauses.

Investigations by THISDAY have further revealed that none of the deeds of assignment are on company letterheads or include contact details for representatives of the creditor companies.

In one of the forged documents that supposedly formalized the assignment of a debt of $2,398,439.96 to Valmet USA, the forger used a fictitious name - Patrick Kevin - to sign the document purportedly as the company’s accountant, although it is against standard practice for an accountant to sign such a large contract on behalf of a company.

The forger(s) of the documents also fumbled in the fabrication of seals for the 12 different foreign creditor companies, and ended up using fake seals all identical to that of the local Kagoda company.

In the forged Kagoda papers seen by THISDAY, the deed of assignment for Daimler Benz AG, a German company, was purportedly signed by a fictitious director named Christopher Williams, but the signature appeared as W Christopher.

All the Kagoda documents were signed in Dar es Salaam before the same B.M. Sanze, an Advocate and Notary Public and Commissioner of Oaths. Some documents were dated even before the Kagoda company was officially registered at the Business Registration and Licensing Authority (BRELA).

’’Even an amateur could tell you that these documents are fake. You don’t even need forensic experts from the police CID (criminal investigations department) to inspect these deeds of assignment,’’ a source close to the Kagoda investigation told THISDAY.

Samuel Sithole, lead audit and engagement director of Deloitte & Touche of South Africa which is the international auditing firm that first discovered the massive Kagoda fraud, raised serious questions regarding the use of old names for companies and the speed with which the Kagoda transactions were approved by BoT.

However, following these queries on the Kagoda forgeries, the then BoT governor Dr Daudi Ballali (now deceased) opted to sack Deloitte & Touche as the central bank’s auditor.

So far, the government has not filed any criminal charges against prominent individuals behind the Kagoda company as pressure continues to mount on both the EPA scandal probe team led by Attorney General Johnson Mwanyika and the Director of Public Prosecutions, Eliezer Feleshi, to act.

Meanwhile, Dar es Salaam-based business tycoon Yusuf Manji was yesterday reported to have been flown to Kenya for ’’emergency medical treatment’’ again, after making a similar trip recently.

Manji, chief executive officer of Quality Group Limited, has previously been linked to the Kagoda company, but denied any involvement in the EPA scandal.

It is understood that he was initially treated at the Aga Khan Hospital in Dar es Salaam before being flown to the Kenyan capital, Nairobi.
 
Back
Top Bottom