Jumatatu nilisema kwamba washtakiwa wa EPA,wote,kila mmoja wao,wasamehewe. Watu wengine wakauilza,kwa nini wasamehewe,wakaniambia,"You are a ***** for making that suggestion" Lakini sasa I am told kwamba Waziri Mkuu Mstaafu Lowassa na Mbunge Rostam Aziz ndio wamiliki wakuu wa Kagoda Agric. Co.. Sasa, siyo rahisi zaidi kuwaachia huru watu kama hawa badala ya kuwapeleka Mahakamani?
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. Kwa taarifa nilizonazo, Lowasa kama mtu binafsi hahusiki na KAGODA. Ana matatizo yake lakini katika hili mtakuwa mnamwonea tu. Sasa tusionee watu. Tuwe wakweli. KAGODA, kwa taarifa nilizo nazo mimi ni state sponsored corruption.
Halafu nimesikia Lowassa aliwahi kumfanyia wema mkubwa Ndugu Rais. Nimesikia,again,from a reliable source,kwamba siku moja Mwalimu Nyerere alimwita Nd. Jakaya Kikwete aende Msasani. Alipofika kule,Mwalimu akamwamia Ndiugu Jakaya,kwamba,"Wewe kijana,ni hodari wa kazi,ni mwanamapinduzi.....,sasa ,nenda sasa hivi,kachukue form ugombee Urais" Sasa,Ndugu Jakaya Kikwete akakatoka pale,lakini alikuwa hana fedha za kufanyia hiyo kazi. Ndipo,akaenda kwa Lowassa,na akapata hizo fedha. Nimezipata hizi habari,from a reliable source,na,nadhani,zinaeleza kwa nini hawa watu hawajapelekwa Mahakamani mpaka sasa.
Watu wamewahi kuandika kuhusu suala hili. Kikwete hakuwa mgombea wa Mwalimu Nyerere. Mwalimu hakuwahi kumwambia Kikwete agombee. Inawezekana Mwalimu alitumia wazee wengine kutuma salamu hizo lakni sio kwa ndugu Kikwete kwenda Msasani. Ndugu Kikwete aliambiwa akachukue fomu na Mzee Mwinyi Ikulu Dar es Salaam, wakati huo Kikwete ni Waziri wa Fedha - Jenerali aliwahi kuandika kuwa Kikwete alitembea kwa mguu kwenda ikulu kupata 'amri' hiyo majira ya saa moja jioni.
In conclusion,ningependa kusema,kwamba hawa watu,kama wanapelekwa Mahakamani wapelekwe,kama wanaachiwa huru,waachiwe huru,it is all the same to me. Rais ana uwezo wa kuwapeleka Mahakani,and The President can rescind the order at any time,at any time. Wale wanaosema Rais ana uwezo wa kupeleka watu Mahakamani,lakini hana uwezo wa kuwatoa watu Mahakamani,au kuwatoa jela,hao ndio wanaotaka kuzifanya kazi hizi ziwe ngumu,au zionekani kwamba ni ngumu.
Halafu nimepita Karatu,wiki chache zilizopita,nikasikia kwamba Ndugu Lowasa,anafanya matayarisho ya kugombea Urais mwaka 2010,au 2015,na anawaambia watu wote wanaotaka kugombea Ubunge katika Bunge lijalo,wawasiliane naye wapate msaada wa fedha. Hii ni chaos,kama watu watatumia ill gotten gains kutafuta Urais. Katika Mathematics,inaitwa Chaos. Kwamba ukianza vibaya,maendleeo yako ya badaye yatakuwa mabaya.
Hili laweza kuwa kweli!
Mwalimu Nyerere alitaka kuwasaidia waongoze nchi. Lakini baadaye aliingilia kati na kumsaidia Ndugu Mkapa. Sijui kwa nini Mwalimu alibadili mawazo yake.
Agenda ya Mwalimu has always been Salim Ahmed Salim. Hajawahi kuwa na ajenda ya Lowasa wala Kikwete. Na hili ndio tatizo la Tanzania, viongozi wetu hawaandiki na wasaidizi wao hawaandiki na hivyo zinabaki speculations na rumours tu.
Labda ni kwa ajili ya maneno yao ambayo walikuwa wanyazungumza,na yaliyokuwa yanazungumzwa kuhusu wao,kwamba wanataka "kuichukua nchi",ndio maneno ambayo hata sasa utayasikia ukienda kule Karatu,kwamba "Lowasa na rafiki zake wanataka kuichukua nchi" Maneno kama haya ukiyasikia kwamba watu wanataka "kuichukua nchi",ukiyasikilza yanakuwa kama ya kifisadi.
Again,I say,haya mambo hayanihusu mimi. As far as I am concerned,hili swala kwangu mmi limekwisha,kwa sababu nimeshawafahamu hawa mafisadi,ni akina nani,and that is all I wanted. Haya mambo yajadiliwe bila kujali nani atakasirika. Yajadiliwe kama timu ya mpira inavyojadili mambo wakati wa half time,bila ya kujali nani ataudhika. Muhimu ni kuwaondoa tu watu wasiohusika kabla ya kuanza kujadiliana.