Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Kagoda Agriculture Ltd: Another BOT scandal

Mkuu Zitto umesema vyema sana .Lakini sasa if that is the case kwamba the State was behind and is behind Kagoda leo watu wakimtaja Lowasa then JK hapatakuwa na kosa maana wao ndiyo walikuwa wakubwa ndani ya State ama hapa ni mimi sijaelewa ?

hujaelewa sana tu hapa ni hivi pesa ya kagoda ilichukuliwa mwezi wa kumi na kumi na kumi na moja mwaka 2005.wanasema wenzako kuwa zilichukuliwa na uongozi wa awamu iliopita kusaidia uchaguzi....Hivyo basi wakati huo serikali ilikuwa chini ya BWM ali kadhalika na chama.sasa basi hapo Lowasa hakuwepo wala jk kwenye maamuzi hayo
 
Fisadi Mkapa bado tunakula naye sahani moja mpaka kieleweke kuhusu kujimilikisha Kiwira na kuwashinikiza TANESCO kusaini na mkataba na 'kampuni' yake wa shilingi 326 billioni ambao unamlipa 146 millioni kwa siku. Ule mradi wake wa kuwaleta makaburu wa Net Group ambao uliiacha TANESCO katika hali mbaya zaidi. Ushiriki wake katika ununuzi wa rada ya kifisadi, magari na helicopters za jeshi, ndege ya Rais na pia kuuza nyumba za serikali kwa bei ya kutupa si ajabu hata kwenye Kagoda kuna mkono wake. Ameshaanza kuwa na wasiwasi hata anazikacha dhifa za kitaifa kama sherehe za uhuru na muungano sijui kama mwaka huu atahudhuria sherehe za kutimiza miaka 47 ya uhuru wa Tanganyika. Bado tunaye huyu mpaka kieleweke.

Kauli ni nyingi sana zimeshatolewa kuhusiana na hili sakata...IGP Mwema alishasema kuwa mafisadi hao wana nguvu sana na ni kama magaidi na hivyo hana nguvu ya kuwashughulikia pasipo kupoteza amani ya nchi....Kuna hawa waliokamatwa na kufunfuliwa mashtaka..Kuna ambao afya zao zinazorota...Kelele kuhusu Balali tulipiga sana lakini siasa zika take over....Hapa JF nadhani ndio mahali pekee mijadala inaendelea bila woga wa kuuliza na kutaja majina ya wahusika.

Wangwe naye RIP hakuwa mwoga na nafikiri hilo likam cost...Tunaweza kuona dhahiri kwamba mambo si mazuri huko Tanzania kwa wanasiasa wenye kufuatilia mambo ya mafisadi...Inasikitisha sana...Hata hivyo pia nashangazwa sana na wanasiasa.

Style inayotumika ku deal na issue hii ni ya namna ambayo lazima kuwindana kunaendelea na laiti tungekuwa na uwezo wa kuona chini ya mapaa basi tungeona mengi sana..Achilia mbali uchawi wa bungeni...Vitisho hadi kwa mahakimu sasa vinaendelea.

Hakuna amani yoyote itakayopotea kama haki ikichukuwa mkondo wake...Kuna wale wenye kulazimishia amani kupotea...Kwani nchi inaongozwa na jeshi?

Mimi huwa najiuliza maswali mengi sana....Siasa zikiwekwa kando basi haki itatendeka kinyume na hapo basi nchi itabaki mikononi mwa mafisadi milele.

Hao wanaodaiwa kuwa mashahidi muhimu wanafuatiliwa kwa utaratibu na huku wengine wakizorota afya zao na kupotea moja kwa moja.
Huku nasikia Mwakosya kule nasikia Mgonja.
 
Watu kama kina Zitto ni wapinzani njaa waliojawa na tamaa tu ya kuwa na madaraka hawana chochote na wala msikubali kudanganyika. Hawa siku zote wanailaumu serikali iliyoko madarakani kwa vitendo vyake kadhaa vya kuwanyima wananchi taarifa za msingi zinazohusu uendeshwaji wa nchi, leo hii Zitto anakuja hapa na kuwalingishia wanaJF kuwa ana taarifa za msingi ambazo wanatamani kuzijua lakini hatawapa!!! Sasa kama hauko tayari kusema unayoyajua ni nani alikwambia uanze kutoa fununu humu, watu wazima hawataki fununu wanataka taarifa kamili, na kama huwezi kutoa hiyo taarifa tutakuchukulia kuwa taarifa hiyo hauna. Huu upinzani njaa njaa ndio unaosababisha ukiritimba wote ulioko Tanzania. Sasa wewe Zitto hutoi hizo taarifa hapa in full kwa kumuogopa nani???anhaa kumbe na wewe huwa unaogopa kutoa taarifa za mambo muhimu kwa wananchi! Je siku ukiwa waziri unaweza kutoa siri za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa nchi??? kwa ujumla, wewe na the other so called wapinzani mnakera na kuchefua kwa unafiki wenu.

Na hawa ndio watanzania wanaotaka uongozi bora. Kaka uongozi ni dhamana na wajibu. Kama unataka kila kiongozi aseme bila ya kuwa na mstari basi ni wazi uongozi tulionao unakutosha....

Tanzanianjema
 
Yawezekana kwamba Haya ni mashambulizi sahihi lakini yasiyo ya lazima.

Zitto kakanusha kwamba Lowassa hahusiki kama mtu binafsi.
Ugomvi wote umeanzia hapo.
Ili kesi inoge wengine tungependa kusikia Lowassa yumo.
Hajamlazimisha mtu kukubali kwamba Lowassa kama Lowassa hayumo kwenye list ya umilikiwa Kagoda.
Mtuhumiwa mwingine katika mada hii Rostamu Bin Azizi yeye bado anabakia kwenye list na anang'aa kweli kweli. Kitendo cha Zitto kumbakiza Rostamu peke yake kwenye utuhumiwa kinaelekea kupata upinzani hapa.

Sasa upinzani njaa wa kisiasa unazaliwa vipi?
Kujawa na tamaa kunaingiaje hapa?

Inawezekana Zitto ni mwoga sana, nakubali, kwa sababu ameshindwa kusema kila kitu anachokijua.
Lakini Mimi Madela Wa Madilu na wewe ni waoga kuliko Zitto kwa sababu tunaogopa kutumia majina yetu halisi kwenye mtandao, lakini mafundi wa kudhani kuna waoga kuliko sisi tufichao ID zetu.

Kweli Nyani kamwe hataona sehemu anayotumia kukalia. Hii hii hii hii!
 
Yawezekana kwamba Haya ni mashambulizi sahihi lakini yasiyo ya lazima.

Zitto kakanusha kwamba Lowassa hahusi kama mtu binafsi.
Ugomvi wote umeanzia hapo.
Ili kesi inoge wengine tungependa kusikia Lowassa yumo.
Hajamlazimisha mtu kukubali kwamba Lowassa kama Lowassa hayumo kwenye list ya umilikiwa Kagoda.
Mtuhumiwa mwingine katika mada hii Rostamu Bin Azizi yeye bado anabakia kwenye list na anang'aa kweli kweli. Kitendo cha Zitto kumbakiza Rostamu peke yake kwenye utuhumiwa kinaleta kinaelekea kupata upinzani hapa.

Sasa upinzani njaa wa kisiasa unazaliwa vipi?
Kujawa na tamaa kunaingiaje hapa?

Inawezekana Zitto ni mwoga sana, nakubali kwa sababu ameshindwa kusema kila kitu anachokijua.
LAkini Mimi Madela Wa Madilu na wewe ni waoga kuliko Zitto kwa sababu tunaogopa kutumia majina yetu halisi kwenye mtandao, lakini mafundi wa kudhani kuna waoga kuliko sisi tufichao ID zetu.

Kweli Nyani kamwe hataona sehemu anayotumia kukalia. Hii hii hii hii!

Nakubaliana moja kwa moja...Unaweza kuta ni mbunge ama waziri huyo ama kada tu wa chama kingine..Lakini sidhani kama ni busara kwa mwananchi usiyetumia jina lako kumponda mh mbunge kama una nia nzuri na jamvi hili na mustakabali ulioko mbele yetu kama Taifa.
 
Watu kama kina Zitto ni wapinzani njaa waliojawa na tamaa tu ya kuwa na madaraka hawana chochote na wala msikubali kudanganyika. Hawa siku zote wanailaumu serikali iliyoko madarakani kwa vitendo vyake kadhaa vya kuwanyima wananchi taarifa za msingi zinazohusu uendeshwaji wa nchi, leo hii Zitto anakuja hapa na kuwalingishia wanaJF kuwa ana taarifa za msingi ambazo wanatamani kuzijua lakini hatawapa!!! Sasa kama hauko tayari kusema unayoyajua ni nani alikwambia uanze kutoa fununu humu, watu wazima hawataki fununu wanataka taarifa kamili, na kama huwezi kutoa hiyo taarifa tutakuchukulia kuwa taarifa hiyo hauna. Huu upinzani njaa njaa ndio unaosababisha ukiritimba wote ulioko Tanzania. Sasa wewe Zitto hutoi hizo taarifa hapa in full kwa kumuogopa nani???anhaa kumbe na wewe huwa unaogopa kutoa taarifa za mambo muhimu kwa wananchi! Je siku ukiwa waziri unaweza kutoa siri za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa nchi??? kwa ujumla, wewe na the other so called wapinzani mnakera na kuchefua kwa unafiki wenu.

System umerudi eeeh?! nilifikiri wewe vita vyako ni dhidi ya Mbowe tu... kumbe wote?!
 
Kipindi cha mwisho cha maisha ya Mwalimu, Prof. Haruoub Othman aliwahi kupata baraka za Mwalimu ili aandike biography ya Mwalimu. Bahati mbaya Mwalimu akafariki kabla hilo halijafanyika.

Wakati mwingine umri ni kikwazo cha wazee waliokuwa viongozi kuweza kuandika historia yao ama ya nchi yetu, lakini wakifuatwa simulizi za kusisimua na maelezo yenye manufaa yatabubujika. Wanahitajika vijana wenye nia njema ya kutaka kuwepo kumbukumbu kuhusu viongozi wa taifa letu na historia ya Taifa kwa ujumla wajitokeze kufanya kazi hiyo, tena wajitokeze mapema.

Naamini wakati ule ni Watanzania wachache sana waliowaza kwamba Mwalimu atafariki kama walikuwepo basi walikuwa ni 'wachawi'. Katika vichwa vya wananchi wengi, wazo kwamba iko siku Mwalimu atafariki halikuwepo kabisa! Tumeishapata fundisho kwamba hakuna binadamu aliye immortal. Kwa maana hiyo, ni changamoto kwa wazee wenye nguvu bado na vijana wenye ujuzi na uwezo wa kutafiti na kuandika waanze kuifanya kazi hiyo kwa manufaa ya taifa letu. Wahenga walisema linalowezekana leo lisingoje kesho!

Ahsante Bibi Ntilie, kwangu mimi itabidi tuanze na Mzee Kawawa. Ashinikizwe hata kwa ncha ya mtutu aandike biography... it would be worthy it in the long term!!! 🙂
 
Hivyo wewe una maoni gani? Mhe Zitto. sema. jieleze bwana. Una lipi la mbadala au unafurahia posho tu na wewe!!!!!!!

Tusichokielewa ni nini jamani? Amesema maoni yake kama mtu binafsi hapa. Akitaka kutamka kama kiongozi itabidi atoe tamko la chama chake au kama mbunge au kama mmoja wa wanakamati mbalimbali zilizopo.
 
Zitto na Chadema poleni sana kwa kuingia mtego wa mastermind EL na RA.

The only person who is above the law in TZ is the president and ex presidents whether we like it or not. FACT

EL na RA wanataka sakata la Kagoda limuhusishe mkapa sababu wanajua once mkimtaja Mkapa then issue ya KAGODA inakuwa dead on arrival. Sisemi Zitto ana nia mbaya lakini ameshategeka akidhani Mkapa anahusika Kagoda.

Hapa kuna issue mbili.

issue no.1 State hse waliauthorize serikali itoe baadhi ya pesa kusaidia uchaguzi wa 2005. Kagoda iliundwa na wajanja wa Idara na RA (with his godfather EL on the sidelines) kwa nia ya kuchukua pesa za uchaguzi plus pesa za kwao binafsi kupitia mgongo wa uchaguzi wa 2005.

Issue no.2 Kagoda in totality waliibia BOT pesa, lakini Kagoda nayo iliibiwa pesa na RA, EL na wengine ambao siwezi kuwataja but U can read btn the lines ( trust me the syndicate will delete few lives in the comes months, no question about it).

Sasa Zitto anaporukia vitu eti Kagoda inamuhusisha Mkapa anafall kwenye target ya syndicate sababu once ukimuweka Mkapa then the issue is dead, itabaki kelele barabarani. Mkapa akupata hata senti moja ya Kagoda, na kamati ya Mwanyika ina taarifa kamili kama Zitto akiweza kuzipata.

Mirambo, Caspian, Peter Noni, 16%, 19%, 35%, RA, EL, Vodacom, DG, 12.5 billion election 2005.

Ni hayo tu.
 
Watu kama kina Zitto ni wapinzani njaa waliojawa na tamaa tu ya kuwa na madaraka hawana chochote na wala msikubali kudanganyika.

Sasa kama wakina Zitto ndio wenye tamaa ya madaraka, je hao ambao wameng'ang'ania madaraka miaka nenda rudi tuwaiteje ? Pamoja na kuvurunda kila kitu kwa nini unakubali wao wakudanganye kila kukicha.

Hawa siku zote wanailaumu serikali iliyoko madarakani kwa vitendo vyake kadhaa vya kuwanyima wananchi taarifa za msingi zinazohusu uendeshwaji wa nchi, leo hii Zitto anakuja hapa na kuwalingishia wanaJF kuwa ana taarifa za msingi ambazo wanatamani kuzijua lakini hatawapa!!! Sasa kama hauko tayari kusema unayoyajua ni nani alikwambia uanze kutoa fununu humu, watu wazima hawataki fununu wanataka taarifa kamili, na kama huwezi kutoa hiyo taarifa tutakuchukulia kuwa taarifa hiyo hauna.

Yaani huyo Zitto akupikie chakula, akuwezee mezani, akusokomezee mdomoni na akutafunie halafu ulmaumu kwa kushindwa kwako kumeza. Halafu unathubutu kulalamika ati ulikuwa unakitamani hicho chakula.

Huu upinzani njaa njaa ndio unaosababisha ukiritimba wote ulioko Tanzania. Sasa wewe Zitto hutoi hizo taarifa hapa in full kwa kumuogopa nani???anhaa kumbe na wewe huwa unaogopa kutoa taarifa za mambo muhimu kwa wananchi! Je siku ukiwa waziri unaweza kutoa siri za ufisadi unaofanywa na viongozi wa juu wa nchi???

Huo unaouita ukiritimba ni kitu gani hasa na nani mwoga kati yako wewe na Mh. Zitto. Wewe unayejiita ZeMarcopolo au Zitto anayejiita Zitto. Dont throw stones if you live in a glass house au una ukoo na huyo baharia wa karne ya 12.

kwa ujumla, wewe na the other so called wapinzani mnakera na kuchefua kwa unafiki wenu.

Anayekera humu anaonekana hata kwa aliye na chongo. Wanaochefua wote wameshikwa pabaya and this time watatafuta pa kujificha na hawatafanikiwa. Dakika zinazidi kuyoyoma na kitanzi kinazdi kubana - ole wenu na washirika wenu.
 
Na hawa ndio watanzania wanaotaka uongozi bora. Kaka uongozi ni dhamana na wajibu. Kama unataka kila kiongozi aseme bila ya kuwa na mstari basi ni wazi uongozi tulionao unakutosha....

Tanzanianjema

Unajua wanasiasa huwa wanafurahia sana tabia ya watu kusahau mapema. Hivi mara hii imeshasahaulika kuwa wapinzani walikuwa wanaisukuma serikali iwataje watuhumiwa wa EPA! Sasa hapa anakuja the so called mpinzani na madai kuwa yeye anawajua, halafu hataki kuwataja! sasa iwapo wao the so called wapinzani wanaamini kuwa ni muhimu kwa wahusika wa sakata la EPA kutajwa kwa wananchi na wao wanakili kuwafahamu ni kwanini hawawataji? Wapinzani wanawachezeeni akili na msiposhtukia sasa hivi mtajikuta kwenye dimbwi la maji machafu huku wao wakiwakejeli. Siku zote walikuwa wanapiga kelele za EPA, hivi sasa muziki wao umebadilika, umekuwa KAGODA. Hivi hamuwezi kuona usanii wa kisiasa kwenye hii legal issue. Wacheni mahakama ifanye kazi na mwenye ushahidi apeleke mahakamani.
 
Sidhani kama unahitaji kufahamu jina la mchangiaji ili uweze kujua uzito wa hoja yake.
 
Oh yeah, very cogent case in behalf of Lowassa there.

Yani hujasema kwamba hakuna ufisadi wa Kagoda, wala hujasema Serikali haijahusika.

Halafu hujasema Lowassa msafi, na hujasema tumuache Lowassa apumzike.

Umesema tu nyeti zako zinakuonyesha hii ni "state-sponsored corruption." Such an impenetrable defense of him.

Tatizo ni kwamba sisi tunataka kujua who is the state, Katibu Tarafa ?

Oooooooh kuhani kidole na jicho,mimi mtu mdogo sana ktk uongozi(joke)
 
Zitto na Chadema poleni sana kwa kuingia mtego wa mastermind EL na RA.

The only person who is above the law in TZ is the president and ex presidents whether we like it or not. FACT

EL na RA wanataka sakata la Kagoda limuhusishe mkapa sababu wanajua once mkimtaja Mkapa then issue ya KAGODA inakuwa dead on arrival. Sisemi Zitto ana nia mbaya lakini ameshategeka akidhani Mkapa anahusika Kagoda.

Hapa kuna issue mbili.

issue no.1 State hse waliauthorize serikali itoe baadhi ya pesa kusaidia uchaguzi wa 2005. Kagoda iliundwa na wajanja wa Idara na RA (with his godfather EL on the sidelines) kwa nia ya kuchukua pesa za uchaguzi plus pesa za kwao binafsi kupitia mgongo wa uchaguzi wa 2005.

Issue no.2 Kagoda in totality waliibia BOT pesa, lakini Kagoda nayo iliibiwa pesa na RA, EL na wengine ambao siwezi kuwataja but U can read btn the lines ( trust me the syndicate will delete few lives in the comes months, no question about it).

Sasa Zitto anaporukia vitu eti Kagoda inamuhusisha Mkapa anafall kwenye target ya syndicate sababu once ukimuweka Mkapa then the issue is dead, itabaki kelele barabarani. Mkapa akupata hata senti moja ya Kagoda, na kamati ya Mwanyika ina taarifa kamili kama Zitto akiweza kuzipata.

Mirambo, Caspian, Peter Noni, 16%, 19%, 35%, RA, EL, Vodacom, DG, 12.5 billion election 2005.

Ni hayo tu.

.......Mkuu Moelex23....duuhh.......naona Mh Zitto kasahau kulikuwepo na kitu kinaitwa "MTANDAO"..........nini nafasi ya EL ndani ya mtandao......ukisema mastermind ya mchezo wa EPA.......EL ni jina la juu kabisa.........

.....Nakubaliana na Mh Zitto kuwa.....kesi ikiunguruma ya Kagoda.....kwa mazingira ya mchongo ulivyokuwa......itakuwa ni vigumu sana kumtia EL hatiani............lakini ukweli utabakia kuwa EL naye alitufisadi ndani ya EPA........
 
Kuhani, nadhani utakuwa humtendei haki Zitto katika hili. Tumeshaona hata kwa wenzetu walioendelea kwenye mahojiano yao na waandishi wa habari njinsi wanavyoweza kukwepa maswali ambayo huleta direct confrontation baina yao na waajiri. Sisi kama wananchi ni waajiri wa wabunge, lakini ili wawe wabunge ni lazima wale viapo ambavyo vitathibitisha maadili ya kazi zao kama vile ambavyo inatakiwa kuwa kulingana na miongozo tuliojiwekea sisi wananchi - Katiba.

Sasa kumlazimisha kiongozi kutamka maneno fulani ambayo yatafurahisha jamvi na kumfanya awe shujaa kwa dakika chache za JF hali zitakazo mfanya asiweze kuwakilisha wananchi wa jimbo lake kwa kipindi kisicho julikana, huko ni kutomtendea haki. Tukubali kwamba ameshataja mengi ambayo hamna kiongozi mwingine ameweza kutaja tayari kuhusiana na swala hili na kwenye thread hii.

Je, tuwe watu wa kulazimishana tu katika kila jambo, kwa kuchukulia kila neno linaloandikwa iwe kimakosa au bila makosa kwa dhati kwenye mtandao kama tamko la katiba? Hapana, huu utakuwa unyanyasaji wa kimtandao (cyber bullying). Jambo ambalo wote naamini tungependa kuepukana nalo. Tuko kwenye majadiliano ndugu yangu, basi pale mtu anapoenda mrama/mlama asihukumiwe jumlajumla. Ni mawaidha yangu, ahsante.

SteveD.

Steve umesema ukweli. Tatizo sisi hapa wapiganaji wa JF tunatumia nicknames na the people who are on the front line kule Bungeni e.g Zitto na Dr. Slaa wakija hapa they use their actual names na they are not hiding their identities. Nafikiri hatuwatendendei haki. Kwa vile hili swala liko mahakamani, let the justice system take its course na baada ya verdict, then lets all raise HELL should there be any cover ups.
 
Sidhani kama unahitaji kufahamu jina la mchangiaji ili uweze kujua uzito wa hoja yake.

Nikuchekeshe.
Hii hiii hii hii hii!
Wengine humu ndani siyo watu katika maana ya binadamu.

Kujua jina la mchangiaji ni muhimu sana sana.
Wengine humu ndani ni Alien kutoka Sayari za mbali, nyuso zetu ni za kijani na hatuna maumbo ya kibinadamu. Tumejiunga hapa ili kupata joto la jamvi tu kwa vile tuna access na mtandao 24/7.
In short, we have nothing to lose because we dont carry the weight of our words in our own shoulders.

Sasa kwa wengine wasio sisi, jamvi hili ni stepping stone ya kurukia kule kuliko halisi the fact that they are still in infancy stage within the rotten system, ni muhimu kuficha ID zao. Kuficha ID zao si kuficha ukweli kuhusu uraia wao wa Galaxy nyingine, bali ni kuvuta muda ili saa itimie ya kuweka mambo wazi.
Wanakata tawi la mti walo kalia, ni upumbavu wenye akili nyingi. Wanajua wazi kabisa Tawi likikatika wao pia wanakwenda nalo chini lakini matumaini yao yapo kwenye uhai wa shina, chipukizi jipya litamea na mti wao utashamiri tena, inshallah masika ikifika.

Mbegu ikitia ngumu kuonja mauti kamwe haizai. Kifo cha mbegu kadhaa si bure ni mwendelezo wa uhai mwingi mpya na wenye nguvu kuliko ule wa awali. Read my lips

No hesitation,"The supremacy of message is synonymous to the presenter"
 
.......Mkuu Moelex23....duuhh.......naona Mh Zitto kasahau kulikuwepo na kitu kinaitwa "MTANDAO"..........nini nafasi ya EL ndani ya mtandao......ukisema mastermind ya mchezo wa EPA.......EL ni jina la juu kabisa.........

.....Nakubaliana na Mh Zitto kuwa.....kesi ikiunguruma ya Kagoda.....kwa mazingira ya mchongo ulivyokuwa......itakuwa ni vigumu sana kumtia EL hatiani............lakini ukweli utabakia kuwa EL naye alitufisadi ndani ya EPA........

Pamoja na kwamba mimi na Zitto tuko kwenye mapambano pamoja, Sangara n.k. mara zote ananikwaza likijitokeza suala lolote linalomhusu Rostam na Lowassa! Anapata taabu sana kuwakosoa watu hawa. Sitaki kuguess, lakini napata wasiwasi kuwa kiongozi wangu anashindwa kutenganisha urafiki na mapambano. Ni kiongozi wangu huyu, lakini sifurahii tabia hii. Naona kama anatumika, pengine bila kujijua! Kwa sababu, huwezi ukaja na blanket statement ya kwamba Kagoda ni "state sponsored", so what? State inajiendesha yenyewe au na watu? Suala la msingi hapa: ni watu gani hao? Mbona wafanyakazi wa BOT wako ndani wakati wote tunajua kuwa walikuwa wanatumwa tu hao, wanatumwa na watu wanaoendesha "state"? Eventually watu hao tutawajua! Ni u-mdebwedo wa hali ya juu kutaka tuwaache ili tusubiri kuifunga hiyo "state"!

Wana JF, tukirogwa kutumia argument ya Zitto ya "state sponsored", tutashindwa kujibu maswali mengi. Utaishia kusema hata Rajabu Maranda, kada wa CCM, mweka hazina wa CCM wa Mkoa, hakutakiwa kukamatwa kwa kuwa hapo kuna mazingira ya "CCM sponsored" wizi! Akina Mwakosya wa BOT hawakutakiwa kukamatwa kwa kuwa yapo mazingira ya "BOT sponsored" wizi! Naogopa kama bosi wangu kakamatishwa mshiko, maana EL na RA, hawajambo kwa hilo!

Sisi tunachokijua ni kuwa Lowassa na Rostam waliongoza jeshi la mtandao la kutafuta fedha. Kama Kagoda Co. iliundwa na "state" kuwasaidia kwenye kazi hiyo haramu, wa kuwashika mashati sisi ni hao hao EL na RA. Wao ndo watuambie huyo mdudu "state" yukoje!
 
Wana JF, tukirogwa kutumia argument ya Zitto ya "state sponsored", tutashindwa kujibu maswali mengi

Fataki hapo umegonga ikulu!

Hapa nimebidika kusema.

1. Hakuna mtu hapa anaweza kuprove kuwa Zito wa JF ndiye yule Zito Kabwe,Mb. Nasema hata kama hakinijibu humu kuwa ndiye yeye bado hiyo si proof. Yeyote anaweza kujiita Zito na akasema mimi ndimi. Hivyo mambo ya kuanza kuspeculate kuwa oh Zito anaweza kufungiwa kwa sababu ya kuchangia hapa mna maanisha kuwa Admin ametoa details na ip za Zito wa JF na uchunguzi wa kina umefanywa na kujua kuwa kweli ni yeye na kama ni hivyo kwani hata ninyi mnaojifanya kutumia nick names zenu sasa usalama wenu ni upi hapa?

Kwa wasionielewa nasema kuwa Zito mwanachama wa JF anaweza kuwa zito Mbunge kweli lakini nani anafikiri kuwa ni rahisi kuprove hivyo simply eti kwa sababu ametumia jina la kweli. Mbona wako wengi majina hayo ya kweli ndio kwao ya utani?

2. Kwa kweli niseme wazi kuwa si kwamba watu wanataka kutomtendea Zito haki. Yeye ndiye anataka kutuzuga hapa.
Logic inakuwa kwamba kama Zito anasema ana taarifa kamili anayoiamini 100% lakini hayuko tayari kusema hapa nani ni Kagoda na nani alichota nini basi angekaa kimya tu kuliko kutoa statement mbili ambazo mimi nasema zinatakiwa kuwekwa kwenye darubini kali.
a. Kujaribu kumtaja mtu kwa jina na kusema apewe haki yake kuwa hausiki kabisa 100% ina maana unawajua kwa undani wanaohusika sasa kwa nini umtaje mmoja kwa KUMUONDOA, je unamaanisha kuwa wengine USIOWAONDOA (sijui kutoka seti gani) ambao hukuwataja wote ndio wamehusika? Vinginevyo endelea kusafisha wote wasiohusika basi ili tusiendelee kuchanganya magugu na mazao tunayohitaji kwa wale sisi ambao hatuna taarifa ya nani ni Kagoda kweli na nani ni wezi wetu na ni akina nani walishirikiana na wezi.
Kwa kuwa hapa JF vichwa viko makini, niseme kuwa hata kama ni kwa kufuata maadili ya kutoingilia Mahakama (kwamba suala hili tayari linashughulikiwa), suala si tu kujizuia kutotaja wanaoshukiwa (watuhumiwa) tu pia ni kutojaribu kutaja wasiostahili kushukiwa!

b. Zito wa JF, Kuna sehemu umeonyesha kadhia ya kuhusisha fedha zilizochotwa na Chama na Uchaguzi na huyu unayejaribu kutushawishi hausiki si tu kuwa ni Mwanachama wa chama hicho alikuwa kiongozi. Ukiacha Ki- 'state', Je unaweza kutuhakikishiaje kuwa huko Chamani pia hakusiki kwa 100% maana kuhusika si lazima wewe ndio uibe hata kwa kujua kinachoendelea katika mpango wowote wa wizi na wewe ukanyamaza bado una hatia, nadhani unalijua hilo Zito.

Kwa vile vichwa viko makini hapa JF, napenda kukujulisha kuwa endapo unaamini kuwa fedha iliyoibiwa ilitumika katika uchaguzi na hatimaye Chama kilichoshinda kikaunda Serikali basi kwa hakika ungetakiwa kuona haki inatendeka ya kutengua uchaguzi huo au walioingia kwa rushwa (tena ya fedha za umma zilizoibiwa) wote wanastep down na bahati mbaya sana unayejitahidi kumsafisha hapa ndiye PM wa kwanza katika hiyo Serikali na kwa nafasi aliyopewa japo sasa hayupo ofisini bado anapata mafao fulani mpaka sasa.

Zito wa JF, mimi siamini kama Chama fulani kilitumia fedha za wizi wakati wa uchaguzi, mwenzangu je wewe unaamini hivyo? na kama unaamini hivyo bado utaendelea kumsafisha kwa asilimia100%?

c. Sasa uliposema kuwa wizi huu ulikuwa 'state sponsored' yaani hapo ndipo ulijikoroga kabisa. Ndugu yangu hata katika kesi za mauaji ya kimbari inakuwa ngumu kabisa Majaji kufikia hatua ya kusema tukio hili lilikuwa 'state sponsored'! Zito wa JF fikiri mara mbili na ndio maana watu humu wamesikitishwa sana na maadishi yako sasa. Kaka hii ni kauli nzito sana yaani State ikae na kupitisha kitu kama hicho? Tafadhali jua pia kuwa Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete Mugabe, Moi, Museveni, n.k wangeweza / wanaweza kuamua jambo fulani kama 'wao' wakawashirikisha baadhi ya watu fulani kama 'wao' na sio 'State' hupo hapo! Sasa tueleze hapa jamvini kinagaubaga jinsi State kama State tunavyoijua sisi walivyokaa wakaamua kuchota fedha na kuzitua kwa njia isiyokubalika.

Zito wa JF ndio maana watu wameanza kwa kukuuliza kuwa nini maana ya 'State' na wewe unajibu kuwa ni 'Watu' wakati na wewe ni mtu kwa hiyo na wewe umehusika na sakata la Epa au? Kwa hiyo definition yako sote humu JF ambao tunajijua kuwa ni Watu basi tunahusika na hapo ndipo namuunga mkono Fataki kuwa sasa hakuna swali litajibika!

Samahani sana Zito wa JF mimi naendelea kuthamini mchango wako hapa lakini leo katika hili pengine umejikuta umeongea yale ambayo hukutaka kuyaongea. Hivyo ni vyema uamue kuwa wazi kutueleza kile unachokijua au ufute kauli yako na usiseme lolote tusubiri tu mahakama na zaidi ya yote hukumu ya kweli itakayotolewa na Mungu wetu kuanzia hapa hapa duniani hata kama ni baada ya muda mrefu.
 
Back
Top Bottom