Kagera: Kimondo chadaiwa kudondoka Bukoba

Muda sio mrefu kimedondoka kimondo kikubwa saaana hapa Bukoba.

Taarifa zaidi zinafuatia

______________________________________________
Updates

TAHARUKI kubwa imewakumba wakazi wa mkoa wa Kagera baada ya kuonekana kwa mwanga mkali na ngurumo katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo usiku wa kuamkia leo.

Baada ya kusambaa taarifa hizo, Daily News Digital imezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio.

"Ni kweli kumekuwa na mwanga unaofanana na nyota kubwa katika anga la Bukoba kushuka uelekeo wa Magharibi wa Ziwa Victoria uliofuatiwa na ngurumo wa wastani wa mfanano wa radi," amesema Brigedia Jenerali Gaguti.

SOURCE:HABARI LEO
Lakin sababu kubwa ya hicho kimondo ni IPI!?
 
wahayaa wana taabu sana, yaani wao kuona miale angani tuu wakasema kimondo kimeanguka? hivi wanajua shughuli ya kimondo kuanguka ardhini?
 
Ila sisi tuna matatizo sana. Unaongeleaje rambirambi kwenye swala kama hili? Baadala ya kuulizia kuhusu composition ya hicho kimondo kwa wataalamu wa geology, watu mnaanza kuongelea rambirambi. Unaweza kukuta ni chanzo kizuri cha umeme lakini akili zetu sisi zitakifanya kua janga au kivutio baadae. Kwanini swala hili liwe janga?
 
Ulitamani kiangukie kwenye ardhi kavu kuliko ziwani ili wafe watu au? Ina maana wewe unajua kuliko wanasayansi na Mkuu wa mkoa aliyetangaza kuhusu hicho kimondo na alikishuhudia mwenyewe?
 
habari za kimondo kuanguka ardhin sijui ziwani waachie ma scientist, porojo porojo zingine peleka kwenye vijiwe vya kahawa vya huko kamuchumu, mkuu wa mkoa na kimondo wapi na wapi
 
kimondo hakiwezi kuanguka ziwani bila kuacha traces kama ashes & fragments ardhini, wahayaa inabidi waelimishwe vimondo ni nini na vinatoka wapi? kabla ya kutafuta kiki za kikatereroo!
 
habari za kimondo kuanguka ardhin sijui ziwani waachie ma scientist, porojo porojo zingine peleka kwenye vijiwe vya kahawa vya huko kamuchumu, mkuu wa mkoa na kimondo wapi na wapi
cc: Nipashe, Mwananchi, U-tube.
 
Picha sio rahis kupatikana ila tukio lilitokea make wengi waliingiwa na hofu wakidhania ni tetemeko

Sasa nani akumbuke kupiga picha
mnasema kimeanguka Bukoba, si mpige picha hicho kilichoanguka? mona pale mbozi kinaonekana na maliasili wapiga piga hela kwa watalii?
 
Wanadaii ni mshana jr alikosea njia kwa maelekezo ya Kiranga
 
Ulitamani kiangukie kwenye ardhi kavu kuliko ziwani ili wafe watu au? Ina maana wewe unajua kuliko wanasayansi na Mkuu wa mkoa aliyetangaza kuhusu hicho kimondo na alikishuhudia mwenyewe?
Mmeanza story ya kimeangukia ziwani...[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji23][emoji23][emoji23]Itakuwa kimepiga katerero ziwa victoriaa...!!
 
Ni kitu mfano jiwe jeusi kilichopo huko Mbozi vwawa songwe
Kumbe hujaenda shule ndio maana shabiki yake yule Mkuu Wa Mkoa kilaza mwenzako... Kimondo hukujui nenda mbozi ukakione kipo kilishaanguka kule bado kipo
 
Ni kitu mfano jiwe jeusi kilichopo huko Mbozi vwawa songwe
Kamuelezee aliyeuliza bwege we Mimi nimeshakiona Mbeya ni kwetu... Afu usirudie tena kuniquote bila sababu za msingi au unataka Basha?
 
Ila sisi tuna matatizo sana. Unaongeleaje rambirambi kwenye swala kama hili? Baadala ya kuulizia kuhusu composition ya hicho kimondo kwa wataalamu wa geology, watu mnaanza kuongelea rambirambi. Unaweza kukuta ni chanzo kizuri cha umeme lakini akili zetu sisi zitakifanya kua janga au kivutio baadae. Kwanini swala hili liwe janga?
Hao wanaoongelea rambirambi , hata haijajulikana ni nini , wameathirika kisaikolojia na mfumo wa ufipa st.
 
Back
Top Bottom