GwaB
JF-Expert Member
- Mar 19, 2014
- 5,185
- 6,990
Kimondo ni neno la kiswahili linalomaanisha jabali au mwamba unaopatikana katika mzunguko wa sayari zingine zilizoko katika anga za juu. Miamba hiyo ambayo inaendelea kuzunguka kwenye mzunguko wa sayari zake, huwezeshwa kubaki kwenye huo mzunguko kwa msaada wa nguvu ya mvutano wa sayari mama. Mvutano ukipungua au kuongezeka huo mwamba utaelea au kuanguka kwenye sayari yake au kuiacha sayari hiyo hadi utakapo karibia sayari nyingine na hivyo kuvutwa kuelekea sayari mpya.
Kilichotokea Kagera inawezekana ikawa ni kimondo kilichodondoka katika anga yetu kutoka anga za juu sawa sawa na kile kilichododoka huko Mbozi-Mbeya na kwa kuwa hadi leo siku ya tatu hatujasikia mlipuko, basi uwezekano wa kuwa silaha za kijeshi ni mdogo na hivyo kukazia nadharia ya kudondoka kwa Kimondo. Tanzania haijaendelea kiasi cha kuwa na radar za kuweza kuangazia anga yetu yote kuona kitu kinachoikaribia anga yetu zaidi ya ndege tu na ni kwa baadhi ya maeneo . Ni nchi kubwa tu zenye uwezo wa kufuatilia mwenenendo wa vimondo na wakati mwingine kukokotoa mwelekeo, mwendo wa kimondo hadi sehemu kitakapoangukia. Sayansi hizi za "Astronomy", "Astrology" au "Astrophysics" zinafundishwa juu juu tu kwenye nyuo vyetu kama mada katika la somo la msingi.
Mara ya mwisho kusikia habari za kudondoka kwa Kimondo ilikuwa miaka mitano iliyopita wakati Kimondo kilidondoka katika mji
wa Chelyabinki tarehe 15 February, 2013 na kililipuka mita chache kabla ya kuanguka ardhini. Tukio la Kimondo kwa siku za hivi karibuni ni lile lililotokea tarehe 26 June, 2018 ambapo miji kadhaa inchini urusi ilishuhudia Kimondo kikilipuka angani. Tembelea hii tovuti kwa nia ya kujifunza zaidi.. https://www.sciencealert.com/an-asteroid-exploded-over-Russia-this-week....
Mara nyingi vimondo vingi huungua angani mara tu vinapoingia katika anga za juu kabisa za sayari yetu, msuguano kati ya hewa na mwamba wa Kimondo hutoa sauti kali na miale ya moto inayofanana na ile ya radi, haijapata kutokea kwa kimondo kuanguka katika makazi ya watu, mara nyingi vinaangukia baharini.Ukubwa wa vimondo unaweza kufikia gari dogo la aina yoyote ile, kwa hiyo kama ni kuleta madhara kama hakikulipuka, athali zake zinaweza kuharibu miundombinu na watu wachache kuumia au hata kufariki dunia.