Kagera: Kimondo chadaiwa kudondoka Bukoba

Kagera: Kimondo chadaiwa kudondoka Bukoba

Robot la Matope

JF-Expert Member
Joined
Apr 10, 2015
Posts
8,593
Reaction score
17,559
Muda sio mrefu kimedondoka kimondo kikubwa saaana hapa Bukoba.

Taarifa zaidi zinafuatia


______________________________________________
Updates



TAHARUKI kubwa imewakumba wakazi wa mkoa wa Kagera baada ya kuonekana kwa mwanga mkali na ngurumo katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo usiku wa kuamkia leo.

Baada ya kusambaa taarifa hizo, Daily News Digital imezungumza na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ambaye amethibitisha kutokea kwa tukio.

"Ni kweli kumekuwa na mwanga unaofanana na nyota kubwa katika anga la Bukoba kushuka uelekeo wa Magharibi wa Ziwa Victoria uliofuatiwa na ngurumo wa wastani wa mfanano wa radi," amesema Brigedia Jenerali Gaguti.

SOURCE:HABARI LEO


Habari zaidi, soma=>Serikali: Kilichoanguka Bukoba mkoani Kagera inawezekana ni Kimondo - JamiiForums
 
Back
Top Bottom