Mathias Byabato
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,049
- 773
AUGUST 15:KONGAMANO LA UWEKEZAJI LINAFANYIKA MUDA HUU
-------------------------------------------
AUGUST 14: WAZIRI MKUU AKIFUNGUA WIKI YA KAGERA
AUGUST13:
AUGUST 12:Wiki ya uwekezaji Kagera imeanza rasmi na ratiba ya leo.
Wiki ya uwekezaji Kagera imeanza kwa kufanya mkutano wa wafanyabiashara kutoka nchi za Tanzania, Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo, Burundi, Rwanda, Uganda na Kenya pamoja na mabalozi. Picha Mkuu Wa Mkoa Kagera Brigedia Jeneral Marco Gaguti akitoa salamu za ufunguzi katika ukumbi wa ELCT BUKOBA HOTEL
picha hapo chini
www.mwananchi.co.tz
By Phinias Bashaya, Mwananchi pbashaya@mwananchi.co.tz
Bukoba. Mkuu wa Mkoa wa Kagera (RC) nchini Tanzania, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amefungua wiki ya Kagera kwa kuwaita wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo.
Katika hotuba aliyoitoa leo Jumatatu Agosti 12,2019 amesema Kagera ni eneo la kimkakati kiuchumi na kuwa fursa zilizopo zinakidhi uwekezaji wa kitaifa.
Wiki ya uwekezaji Kagera inahudhuriwa na mabalozi wote wanaowakilisha Tanzania katika nchi za Afrika Mashariki na kati ambao pia wameambatana na makundi ya wafanyabiashara kutoka katika nchi hizo.
Kwa mujibu wa ratiba mabalozi hao wataeleza fursa za masoko, huduma na bidhaa zilizopo katika nchi hizo na jinsi ya kuzifikia huku wakielezwa fursa za uwekezaji zilizopo mkoani Kagera.
Kwa mujibu wa RC Gaguti keshokutwa Jumatano Agosti 14,2019, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atafika kuzindua mwongozo wa uwekezaji wa Mkoa wa Kagera.
Endelea kufuatilia Mwananchi kwa habari zaidi
---------------------------------------------------
Updates:Maadalizi yako tayari.
------------------------------------
Wanabodi.
Mkoa wa Kagera umebuni na utatekeleza wiki ya uwekezaji Kagera ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Tz Kasim Majaliwa.
Kuna mambo mengi ambayo nataka uyajue na kufahamu kujua Kagera kabla ya wiki hiyo,wakati na baada ya kumalizika kwa hiyo wiki. Nitakupatia dondoo kadhaa kupitia thread hii ambayo itakuwa inakujuza yanayojiri katika maelezo,picha na video na hatimaye uweze KUWEKEZA Kagera.
Binafsi sitaweza kujibu maswali ya kiundani maana mimi nawajuza tu yanayojiri hapa Bukoba maana kutakuwepo ugeni mkubwa sana kutoka mataifa tofauti tofauti wakiongozana na mabalozi wa nchi hizo.
Wiki hiyo itahusisha maonesho ya fursa zilizopo,maonesho ya tamaduni za Kagera,kongamano,kutembelea mbuga mpya za Burigi,Ibanda na Rumanyika,burudani za kila aina,
Kumbuka Bukoba ni mji pekee Tanzania unaofikika kwa chini ya saa 7 kutoka majiji manne ambayo ni Mwanza,Kigali,Bujumbura na Kampala.
Kumbuka Kagera ni mkoa pekee Tanzania ulio lango kuu la nchi jirani ambazo ni Uganda,Burundi,Rwanda,Kenya,DRC Congo.
==============================================================================================

Wiki ya uwekezaji Kagera yaanza, wawekezaji waitwa kuwekeza
Mkuu wa Mkoa wa Kagera (RC) nchini Tanzania, Brigedia Jenerali Marco Gaguti amefungua wiki ya Kagera kwa kuwaita wawekezaji kuchangamkia fursa zilizopo.