Kafulila,Tibaijuka live Star TV

1000GB

JF-Expert Member
Oct 21, 2013
540
500
Tibaijuka anakwepa swali.. Je ni haki benk kutoa 3bilion kwa wakati mmoja kulingana na sheria za kibenki.. Hahaha mama hataki hata kusikia hilo swali..
 

Mr. Mangi

JF-Expert Member
Sep 21, 2014
1,514
2,000
Dah! Huyu mama anatia hasira na majibu yake yasio na kichwa wala miguu, mwizi mkumbwa
 

Opaque

JF-Expert Member
Oct 24, 2008
1,133
1,500
naomba kukuuliza,kwani kafulila yeye ni waziri wa nishati au waziri kivuli wa nishati
Kafulila anazo documents za sakata la ESCROW ACCOUNT kwa kuwa yeye ndiye aliyeleta hoja hiyo bungeni. Anayetakiwa kuzijibu hizo documents za Kafulila ni mtu mwenye documents kama hizo kutoka Wizara au Idara husika, mfano Wizara ya Nishati na Madini, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, hao ndio wenye uwezo wa kuzungumzia au kujibu kuhusu documents za Kafulila.
 

Honey Faith

JF-Expert Member
Aug 21, 2013
15,797
2,000
Huyu mama ana temper za ajabu yani hawezi kujenga hoja zaidi yakupanic yani alikuwa anajichanganya changanya
 

Bukwabi

JF-Expert Member
Dec 30, 2013
3,295
2,000
Hivi Rugemalira alishamaliza mgawo? Huku hata manyunyu ya mgawo hayajafika. Au mpaka uwe na sifa gani? Tujuzane please!
 

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,219
2,000
Nawaomba star tivii watuletee kubwa la maadui baba wa mafisadi na mkuu wa madili A.k.A chenge
 

Nyamgluu

JF-Expert Member
Mar 10, 2006
3,151
2,000
Huo ndo ukweli,kafulila anaenda na document za mambo ya nishati kwa waziri wa ardhi na majumba anategemea kuachieve nini?.
kafulila hanaga akili kweli,anakwenda kuweka mjadala na mtu wa ardhi mambo ya mitambo ya umeme?
Kafulila yeye ni waziri wa nini? Nishati na mitambo ya umeme?

Utetetzi mkubwa wa mama ni kwamba hakujua hela zimetokea wapi yeye kapokea kama msaada wa shule. Ukweli ni kwamba, sijui labda wenzetu hizo hela kwao ni kama elfu 10, lakini kwa hali yeyote Elungata leo hii nikikupa 1.6 billion kama mchango tu wa shughuli yako, aisee kama utapokea bila kujiuliza basi una matatizo ndugu!

Manake kesho nikija kumwomba shemeji anisindikize dubai sijui utasemaje?
 
Last edited by a moderator:

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,432
2,000
Hawezi kuwa middle man wa kupokea mchango wa shule. Kwani shule haina watunza fedha? Pesa amepewa kwa sababu watu walitaka ama kununua ushawishi wake kisiasa au kama malipo kwa mchango wake kuhakikisha hiyo pesa inatoka au sababu nyingine binafsi (self-interest). Ameleta hoja ya mchango wa shule baada ya mambo haya "kuleak".Je pesa alipokea lini na shuleni alipeleka lini? Pengine swali hili si muhimu kwa sasa kwa kuwa wameshachakachua system nzima. Yaani huyu Professor anatuambia kuwa kama asingekuwa na ushawishi kisiasa angepewa tu mchango wa billion 1.6 M kisa tu Rugemalira ni kaka yake? Dada zake Rugemalira wengine amewapa kiasi gani? Au kwa kuwa si viongozi wa shule, basi hawajapata kitu? HAlafu huyu alifanya kazi UN, yaani ni mtu wa standards hizo.

Jana nimesoma BBC habari kwamba Waziri wa Afya huko Hispania (Anna Mato) amejiuzulu si kwa kufanya kosa lolote bali kwa ushiriki wa mume wake wa zamani (ex-husband) kwenye kitu wanaita Gurtel Scandal - a huge scheme involving illegal party donations or kickbacks from businesses seeking contracts. Mahakama ilijiridhisha kwamba huyu mama hakuwa anafahamu ufisadi huo na hivyo hana kosa la kujibu. Hata hivyo, bado aliamua kujiuzulu akisema, she had not herself been linked with any crime but that she was standing down for the good of the government. Hizi ndio standards za Mama Tibaijuka. Na huu ndio utawala bora. Mama Tibaijuka alipaswa kuwajibika na kueleza umma ni jinsi gani hana hatia ili kulinda heshima yake. Kuendelea kung'ang'ania tu ni mchango wa shule wakati kila kitu kiko wazi kuwa amelipwa hela ya wizi katika mazingira yanayoonesha kuwa waliomlipa wana sababu binafsi za kifisadi ni kujidhalilisha. Mambo ya kung'ang'ania awaachie kina Pinda na Werema ambao si standard yake.
Maelezo yako marefu yanavunjwa na maneno machache sana,''fedha za escrow hazikua za umma".
 

1000GB

JF-Expert Member
Oct 21, 2013
540
500
Asante Escrow tunajifinza mengi.. Pia Tunawafahamu wengi wakiwepo ma profesor mambumbu..

Pia najivunia hata me ni laprofesa..
 

Lancanshire

JF-Expert Member
Sep 20, 2014
14,014
2,000
anasema pesa iliingia kwa akaunti yake kwa sababu anaaminika

Ha ha ha ha kwahiyo akaunti ya shule yake haiaminiki?kwa hiyo Ada ya shule yake inaingia kwenye akaunti yake binafsi. Kachemka Hawa ndio maprofesa WA ccm
 

Elungata

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
37,432
2,000
Kafulila yeye ni waziri wa nini? Nishati na mitambo ya umeme?

Utetetzi mkubwa wa mama ni kwamba hakujua hela zimetokea wapi yeye kapokea kama msaada wa shule. Ukweli ni kwamba, sijui labda wenzetu hizo hela kwao ni kama elfu 10, lakini kwa hali yeyote Elungata leo hii nikikupa 1.6 billion kama mchango tu wa shughuli yako, aisee kama utapokea bila kujiuliza basi una matatizo ndugu!

Manake kesho nikija kumwomba shemeji anisindikize dubai sijui utasemaje?
Ha ha ha,ntamruhusu waende nae akapate kusafisha macho.
 
Last edited by a moderator:

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,140
2,000
my take Prof amejimaliza kwa kweli;

shida yangu ni uwiano wa mgawo

Mheshimiwa Spika, Kamati inajiuliza ni nini mahusiano ya moja
kwa moja kati ya Viongozi hawa na malipo yaliyotokana na Akaunti
ya Tegeta ESCROW. Mfano kwa upande wa viongozi wa kisiasa
ambao waliingiziwa fedha katika akaunti zao binafsi ni; 1. Mhe. Andrew Chenge (Mb), ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali na sasa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, shilingi bilioni 1.6;
 2. Mhe. Anna Tibaijuka (Mb) na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi shilingi bilioni 1.6;
 3. Mhe. William Ngeleja (Mb) na ambaye alikuwa Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4
 4. Ndg. Daniel N. Yona ambaye alikuwa pia Waziri wa Nishati na Madini shilingi milioni 40.4;
 5. Ndg. Paul Kimiti ambaye ni Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Sumbawanga shilingi milioni 40.4
 6. Mhe. J.A.K Mujulizi aliingiziwa shilingi milioni 40.4.


Mheshimiwa Spika, pia kwa upande wa Watumishi wa umma
 1. Ndg. Philip Saliboko ambaye alikuwa mtumishi wa RITA aliingiziwa shilingi milioni 40.4,
 2. Ndg. Emmanuel Daniel Ole Naiko ambaye alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) aliingiziwa shilingi milioni 40.4
 3. Ndg. Lucy L. Appollo ambaye ni Mtumishi wa TRA aliingiziwa shilingi milioni 80.8. (twice)

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Viongozi wa Madhehebu ya Dini walioingiziwa fedha na Benki ya Mkombozi ni 1. Askofu Methodius Kilaini shilingi 80.9,
 2. Askofu Eusebius Nzigirwa shilingi milioni 40.4
 3. Mchungaji Alphonce Twimann Ye Simon shilingi milioni 40.4.
 

Mocrana

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
536
250
hahha ilikuwa vise versa mkuu
Hivi muhongo Jana alisema ameagiza Tanesco wasikate umeme siku mbili hizi kuanzia Jana.Haisee hili lijamaa ni limuhongo kweli..aisee ebu wenye number za wabunge wajulishwe walilipue aisse
 

tamimusalim

JF-Expert Member
Jun 17, 2014
1,823
1,225
ImageUploadedByJamiiForums1417154574.626954.jpg Nimefulaishwa sana na kituo cha star tv ,kufanya jitihada na kuwakutanisha profesor anna tibaijuka,na david kafulila katika mjadala kuhusu escrow uliorushwa na kituo hiko leo asubuhi katika kipindi cha habari kuu,kipindi hiko kilichoendeshwa na mtangazaji joyce mwakalinga kulisikika vijembe kutoka kwa kafulila dhidi ya tibaijuka ,na tibaijuka dhidi ya kafulila,cha kushangaza profesor anna tibaijuka alikataa kumpa mkono mh:david kafulila walipokuwa wanamaliza kipindi kama ishara ya kumaliza mjadala kwa amani
 

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,310
2,000
Manager wa bank ya stanbic Bank tawi la Dar-es salaam Raia wa Uganda amejiuzulu kufuatia kashfa ya Sakata la ESCROW kwa kuruhusu/kuachia/uzembe uliosababisha utakatishaji fedha za ESCROW katika Bank hiyo.


Source: Star tv
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom