Hawezi kuwa middle man wa kupokea mchango wa shule. Kwani shule haina watunza fedha? Pesa amepewa kwa sababu watu walitaka ama kununua ushawishi wake kisiasa au kama malipo kwa mchango wake kuhakikisha hiyo pesa inatoka au sababu nyingine binafsi (self-interest). Ameleta hoja ya mchango wa shule baada ya mambo haya "kuleak".Je pesa alipokea lini na shuleni alipeleka lini? Pengine swali hili si muhimu kwa sasa kwa kuwa wameshachakachua system nzima. Yaani huyu Professor anatuambia kuwa kama asingekuwa na ushawishi kisiasa angepewa tu mchango wa billion 1.6 M kisa tu Rugemalira ni kaka yake? Dada zake Rugemalira wengine amewapa kiasi gani? Au kwa kuwa si viongozi wa shule, basi hawajapata kitu? HAlafu huyu alifanya kazi UN, yaani ni mtu wa standards hizo.
Jana nimesoma BBC habari kwamba Waziri wa Afya huko Hispania (Anna Mato) amejiuzulu si kwa kufanya kosa lolote bali kwa ushiriki wa mume wake wa zamani (ex-husband) kwenye kitu wanaita Gurtel Scandal - a huge scheme involving illegal party donations or kickbacks from businesses seeking contracts. Mahakama ilijiridhisha kwamba huyu mama hakuwa anafahamu ufisadi huo na hivyo hana kosa la kujibu. Hata hivyo, bado aliamua kujiuzulu akisema, she had not herself been linked with any crime but that she was standing down for the good of the government. Hizi ndio standards za Mama Tibaijuka. Na huu ndio utawala bora. Mama Tibaijuka alipaswa kuwajibika na kueleza umma ni jinsi gani hana hatia ili kulinda heshima yake. Kuendelea kung'ang'ania tu ni mchango wa shule wakati kila kitu kiko wazi kuwa amelipwa hela ya wizi katika mazingira yanayoonesha kuwa waliomlipa wana sababu binafsi za kifisadi ni kujidhalilisha. Mambo ya kung'ang'ania awaachie kina Pinda na Werema ambao si standard yake.