Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
Wanabodi,

Kwanza kabisa napenda kuwaonya wale wote wanaojaribu kwa nguvu zote kukiua chama cha Chadema kwamba hawatafanikiwa na kama watafanikiwa ni kwa sababu viongozi wa Chadema wenyewe wamepuuzia haya nitakayo andika.

Kutoka reliable sources ambayo ziwezi kuzietaja hapa ni kwamba Chadema kaa chama kinapigwa vita kubwa sana na CCM na vyombo vya usalama vinatumika sana ktk kuendesha zoezi kali na kubwa la kukiua chama. Kuna watu wawili ambao ni tishio kubwa la uongozi wa CCM nao ni Mbowe na Zitto ambao kwa imani yao ndio nguzo ya chama na wanatakiwa kushughulikiwa haraka na mapema..

Kazi hii haikuanza jana imeanza toka mwaka 2003 au 2004 kwa kutengenezwa nyaraka za siri ambazo aidha zinamhusisha Zitto au Mbowe ktk kuleta Upinzani baina yao wenyewe. Hawa wote wawili kama wapo hapa nawaomba wanisome vizuri na kama nasema uongo wanirudi na kupinga maelezo yangu. Kwa nyuakati Tofauti Mbowe au Zitto wamekuwa wakiletewa habari zingine zenye uthibitisho wa kimaandishi jinsi mmoja wao anavyompiga vita mwenzake na kwa bahati mbaya kila mmoja wao amefikia kuamini yale aloyaona na kufikia kweli kuamini na kujenga uhasama baina yao...

Navyoandika hapa Zitto ana ushahidi dhidi ya Mbowe vile vile Mbowe ana ushahidi dhidi ya Zitto na wote hawajawahi kukaa na kuzungumzia maswala haya isipokuwa kila mmoja anamtazama mwenzake kama mchawi bila kufahamu ya kwamba uchawi huu umetengenezwa kisayansi na utakubalika kwa kila hali na kuponza mahusiano ya viongozi hawa. Binafsi naamini kabisa Zitto na washabiki wake waligombea Uenyekiti wa chama kwa sababu walitaka tu kugombea kiti hicho kidemokrasia isipokuwa kwa dhana ya kwamba Chadema inatakiwa kuokolewa toka mikononi mwa Mbowe vile vile Mbowe na washabiki wake walikataa Upinzani wa Zitto kwa imani kwamba Zitto alikuwa analengo la kukiua chama..

Hivi zote ni habari walizolishwa pande zote mbili, namwona OmarIlyas akizungumza kwa machungu na jazba kubwa dhidi ya Mbowe lakini sintomlaumu kwa sababu kawa feeded information ambazo anaamini sawa na kina Mnyika ambao wanayajua mengi ya Zitto kulingana na walicholishwa toka zamani na sasa hivi wanafanya wao wenyewe. Makundi yote haya mawili hawaaminiani kwa sababu Usalama wa Taifa wameisha ifanya kazi yao na kinachosubiriwa tu ni kifo cha Chadema kupitia hawa watu wawili..

Dr.Slaa alikuwa tishio lakini sii tena kwa sababu naye walimjengea Udini na kundi la watu kumpa nafasi kubwa ya kuwa katikati ya mzozo huu mkubwa wa viongozi. Kama mnakumbuka nilipotoa pendekezo la Dr.Slaa kugombea kiti cha Urais ilikuwa na sababu na kusema kweli CCM walikuwa hawakujiandaa kwa hilo..Nilitegemea kabisa Dr.Slaa atashinda uchaguzi huo lakini wakatafuta mbinu ya Udini na ikaweza kufanya kazi japokuwa lengo kubwa la CCM lilikuwa kuleta mgogoro ndani ya Chadema kwa kupitia Mbowe na Zitto..

Kwa hiyo tuwe makini sana na jitihada za CCM ktk kukibomoa chama. Zitto kayafanya makosa aloyafanya ni kutokana na jinsi alivyolishwa na Mbowe pia amekuwa akilishwa habari mbaya dhidi ya Zitto lakini nawahakikishia hakuna lolote kubwa la ukweli isipokuwa chuki imeundwa. Zipo Nyaraka za Udini na zina mihuri ya Chadema, zipo nyaraka, sms, e-mails za Chadema, Zitto na Mbowe ambazo zimetengenezwa kwa utaalam mkubwa kuonyesha aidha chuki baina yao au agenda za chama na Udini ili mradi CCM na wana IT wake wanaifanya kazi kubwa ya kukibomoa chama kutoka ndani... kazi hii haikuanza jana na sasa hivi tunaona matunda ya kazi kubwa ilitangulia. Mbowe ataendelea kuwa kiongozi bora wa chama kisiasa na Zitto ataendelea kuwa kiongozi bora wa kisera na utekelezaji.

Jihadharini sana na nguvu ya kiza!.. Masalaam.

Kumbe unasema Zitto na Mbowe wote ni UWT na wanapokea taarifa zao huko na si kwenye vikao halali vya chama??

Duh! wananchi tunadanganywa na wanasiasa ile mbaya..nafikiri kutoshiriki siasa tena..
 
Kumbe unasema Zitto na Mbowe wote ni UWT na wanapokea taarifa zao huko na si kwenye vikao halali vya chama??

Duh! wananchi tunadanganywa na wanasiasa ile mbaya..nafikiri kutoshiriki siasa tena..
Hapana mkuu Zitto na Mbowe sii wana Usalama lakini wanatumiwa sana kukiangusha chama kwa kufitinishwa, hivyo ni swala la wao kufahamu lengo la hawa watu wanaowapa hizi info.. na nyingine zinapitia kwa watu wao wenyewe wa karibu bila hata wao kujua pia kama wametumiwa kufikisha habari hizo.

Tatizo la Watanzania huamini kila wanachoambiwa hata wakiambiwa mama yako mchawi basi kesho harudi nyumbani bila kufikiria kama kweli Mama mchawi mbona kalea mimba miezi tisa, kanipekea shule kanilea hadi nimefikia hapa leo kuwa na cheo ndio uchawi wa mama unitafute miye?..

Nachowaomba tu hawa viongozi wetu (sii wako) wajichunge sana na chuki wanayoijenga baina yao kwa sababu lengo lake ni kukigharimu chama na kwa bahati mbaya kama Udini ulivyojengwa, watu wamefikia kuamini na sasa tunaufanya Udini sisi wenyewe..
 
Mkandara
Nakuunga mkono kwa maneno yako mazito, yenye busara na yaliyonyambulisha suala zima la mvutano kati ya Zitto na Mbowe.

Naomba Mkandara atueleze jambo moja muhimu hapa alilosemea; nalo ni kushindwa kwa Dr. Slaa.

Wiki tumeona waraka mwingine wa UWT, uliosanifiwa kwa malengo maalum. Unadai katika mengi kuwa, Kikwete hakushinda uchaguzi ule. Mkandara anasema, " Nilitegemea kabisa Dr.Slaa atashinda uchaguzi huo lakini wakatafuta mbinu ya Udini na ikaweza kufanya kazi..".

Nani alishinda?
 
Vipi hali yako ndugu yangu Zitto, nakutakia upone haraka urudi Tz kuwatumikia watanzanina. Habari ya Mwanahalisi imekuumiza sana hata unafikia kumshambulia mmiliki wa gazeti hili kwa kiwango kidogo cha elimu yake japo ni kiongozi mwenzako ndani ya CDM.

Sipendi kuongelea shutuma za kukosoa kiwango cha chini cha elimu ya mmiliki wa gazeti hili walichonacho watanzania wengi kwani naelewa bado unaumwa. Tatizo la adui zako walioko CDM ni kuendelea kwako kumkubatia Kafulila mwanasiasa ambaye siku zote anaendelea kuishambulia CDM. Kama Kafulila angeacha siasa za kuongelea Chadema na kufanya kazi zake za kuwatumikia wananchi wake zingepunguza chuki za wana CDM kwako.

Ulimsaidia Kafulila kupata ubunge na kumsusa mgombea CDM jimbo la KGM KAS hii yote imejenga chuki kwako. Achana na falsafa ya kuwa wapinzani wote ni wamoja. Umekuwa ni rafiki wa CDM waliofukuzwa. Nionavyo CDM imekuwa kama familia moja hii ina maana kuwa ukiachana na mme au mkeo, rafiki yako atakayeendelea kuongea naye lazima awe adui yako. Huu ni ukweli kuwa chuki ya wana CDM kwako ni kuendelea kuwashikilia waliotoswa na chama.

Binafsi lengo lako la kuwaunganisha wapinzani nzuri lakini naona ugumu wa kufanikiwa kwani wanasiasa wetu kila mmoja ana malengo yake binafsi na huwezi kuyajua ya mioyoni mwao. Pole sana ndugu yangu Zitto.
 
Ndugu wanaJF na Chadema naomba ufafanuzi wenu zaidi kuhusu hili.

Kwa upande wangu na nilishasema tena huko nyuma wakati Zitto anataka uenyekiti Chadema. Zitto anatumiwa bila kujua, kiukweli Zitto hana uwezo wa kuongoza chama kama M/Kiti sembuse Urais ila anajidanganya kwa kupata sifa kupitia Chadema nje ya chadema hana lolote na atoke aone.

Mimi binafsi ninaona kuwa kwa Zitto ni za mwizi arobaini kwani ni kati ya walioihujumu Chadema 2010 kwa kuvujisha siri za chama.Chadema shirikianeni na wote wenye ukweli juu ya nyendo za gamba hili ndani ya chadema ili liondoke kwa aibu.

Naomba maoni yenu nitasema mengine.
 
kwa hili nakupa hongera 100%
naikubali sana kamati yako.
Unafaa kuwa waziri mkuu ila sio rais
Acha ujinga wako wewe..hata kama anataka kugombea urais anaweza na anafaa tu...kama vipi zitto we gombea tu mkuu inavyoonyesha unaweza sana ndo maana wanakupinga pinga..
 
Jiulize kwanini wasisubiri hadi muda wa uchaguzi kama wanahoja wamchague wanayemtaka.Ngoja tu ukweli utakuwa wazi.
 
Ndugu wanaJF na Chadema naomba ufafanuzi wenu zaidi kuhusu hili.

Kwa upande wangu na nilishasema tena huko nyuma wakati Zitto anataka uenyekiti Chadema. Zitto anatumiwa bila kujua, kiukweli Zitto hana uwezo wa kuongoza chama kama M/Kiti sembuse Urais ila anajidanganya kwa kupata sifa kupitia Chadema nje ya chadema hana lolote na atoke aone.

Mimi binafsi ninaona kuwa kwa Zitto ni za mwizi arobaini kwani ni kati ya walioihujumu Chadema 2010 kwa kuvujisha siri za chama.Chadema shirikianeni na wote wenye ukweli juu ya nyendo za gamba hili ndani ya chadema ili liondoke kwa aibu.

Naomba maoni yenu nitasema mengine.

Na wewe acha uwongo wako wewe, unaweza kusema ni kivipi zito anatumiwa?...hivi kati ya mbowe aliyeshawishi wenzake waandamane kisha akawakimbia na slaa aliyejificha kwenye gari na bastola na zitto nani wanatumiwa?..kipi ni bora kati ya kuwa mtumwa wa nchi yako ama kuwatumia watanzaia wenzako?...zitto kama anatumiwa basi atakuwa anatumiwa na watanzania na si vinginevyo..na ukitaka kujua hlo basi kazungumze na watanzania wa chini kabisa watakwambia zitto ni nani?..
 
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana. Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu.

Nimechukia sana, nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.

Zitto tatizo ni wewe mwenyewe na tatizo lenyewe haliko kwenye siasa bali liko kwenye mitazamo yako kuhusu maisha. Mimi mwenyewe umeniudhi, Umenikera na kunihuzunisha sana pale ulipochanganya "kutokumaliza darasa la saba" kwa mmiliki wa Gazeti la Mwanahalisi na Hoja ya Machali. Inaonyesha huwa ukifika kijijini kwako unawaona wapiga kura wako hawastahili kuwa na mbunge "Msomi" kama wewe kwani najua wengi wao hawajamaliza darasa la saba!!
 
Vipi hali yako ndugu yangu Zitto, nakutakia upone haraka urudi Tz kuwatumikia watanzanina. Habari ya Mwanahalisi imekuumiza sana hata unafikia kumshambulia mmiliki wa gazeti hili kwa kiwango kidogo cha elimu yake japo ni kiongozi mwenzako ndani ya CDM.

Sipendi kuongelea shutuma za kukosoa kiwango cha chini cha elimu ya mmiliki wa gazeti hili walichonacho watanzania wengi kwani naelewa bado unaumwa. Tatizo la adui zako walioko CDM ni kuendelea kwako kumkubatia Kafulila mwanasiasa ambaye siku zote anaendelea kuishambulia CDM. Kama Kafulila angeacha siasa za kuongelea Chadema na kufanya kazi zake za kuwatumikia wananchi wake zingepunguza chuki za wana CDM kwako.

Ulimsaidia Kafulila kupata ubunge na kumsusa mgombea CDM jimbo la KGM KAS hii yote imejenga chuki kwako. Achana na falsafa ya kuwa wapinzani wote ni wamoja. Umekuwa ni rafiki wa CDM waliofukuzwa. Nionavyo CDM imekuwa kama familia moja hii ina maana kuwa ukiachana na mme au mkeo, rafiki yako atakayeendelea kuongea naye lazima awe adui yako. Huu ni ukweli kuwa chuki ya wana CDM kwako ni kuendelea kuwashikilia waliotoswa na chama.

Binafsi lengo lako la kuwaunganisha wapinzani nzuri lakini naona ugumu wa kufanikiwa kwani wanasiasa wetu kila mmoja ana malengo yake binafsi na huwezi kuyajua ya mioyoni mwao. Pole sana ndugu yangu Zitto.
Mkuu! Hata kama kubenea ni standard 4, mchango wake ni mhimu hata zaidi ya hao ma-prof.
 
Pole sana . Maelezo uliyotoa yanatosha na umeshawahi kutoa maelezo zaidi ya haya.Tafadhali concentrate kwenye afya yako tu ili urejee salama.Pumzika vya kutosha,najua unavyo-feel

Anyone decent will, by now, have seen enough to note that this scenario will be a disaster. We are going backwards with do-or-die kinda of politician s ambition and it is a shame some people cannot see that.

Kwanza pole kwa kuugua, siasa bwana ni kuumana wala usipate presha, mbona bado! lakini mambo haya yanapomfika mtu ndio mitihani ya kijamii ambayo hututambulisha busara za mhusika. Zito suala kama hili liliwahi kukufika ukiwa Sudani kusini katika msafara wa Rais, leo yamekufika ukiwa mgonjwa hospitalini umelazwa. Katika nyakati zote your reaction has failed me and very disappointing.

Zito wewe ni kiongozi, umejaliwa akili nyingi sana, umejaliwa kipaji cha kuwasiliana na umma na hicho kipaji cha kusimamia kwa dhati shida za umma, lakini hiyo haitoshi sisi kukuamini mpaka pale utakapo faulu mitihani ya majaribu mabaya kama haya ya kuzushiwa au mipango yako inaposhindwa kufika mwisho kwa kadiri unavyotegemea.

Mimi nakupenda, nakushabikia na napenda uwe kiongozi wangu, lakini uanadamu wako unauonyeshja sana unapokuwa umekabiliwa na matatizo ya kisiasa. Vua hicho kiatu cha udhaifu wa kibinadamu ambao unakupelekea kuharakisha kutoa majibu rahisi na maoni ya mambo yanayokuhusu na kukugusa vinginevyo hali hii kila wakati inakuongezea au kuimarisha tofauti na watu unaowadhania na mimi sijui lakini katika hali ya kawaida inaongeza tofauti zenu na pengine inakutafuna wewe zaidi kuliko maadui zako kisiasa. Natafuta siku kuongea na wewe tukiwa wawili ili tuone katika hali hii ufanyaje, wewe nyota yako inang'ara unaowatu wanaokutakia mabaya nje ya CDM na ndani ya CDM.

Lakini pia nadhani Ben unatoa maoni ya kishabiki na mapenzi zaidi badala ya kujenga CDM. CDM is not a holly house, it comprises ordinary people, led by ordinary people, therefore conflicts are expected, but they should not destroy the party, instead they ought to be used to leap the party forward by managing them healthly.
 
Zitto tatizo ni wewe mwenyewe na tatizo lenyewe haliko kwenye siasa bali liko kwenye mitazamo yako kuhusu maisha. Mimi mwenyewe umeniudhi, Umenikera na kunihuzunisha sana pale ulipochanganya "kutokumaliza darasa la saba" kwa mmiliki wa Gazeti la Mwanahalisi na Hoja ya Machali. Inaonyesha huwa ukifika kijijini kwako unawaona wapiga kura wako hawastahili kuwa na mbunge "Msomi" kama wewe kwani najua wengi wao hawajamaliza darasa la saba!!

Na hoja zingine umeziona? unajichoresha hater!
 
Na hoja zingine umeziona? unajichoresha hater!
Kwenye mijadala kila mtu ana uhuru wa kuchagua nini cha kujadili. Hater. WHY??

Halafu elewa kwamba mimi sikuwa nachambua bandiko zima la Zitto kama wafanyavyo wachambuzi wa vitabu!!
 
Watanzania tubadilike tuache mapenzi ya mtu kwenye siasa tuangalie sera za chama. Tujifunze KWA JK WENGI WALIMPENDA KWA STAILI KAMA HII YA ZITTO LAKINI NAAMINI LEO JK HATA UKIMPA UKUU WA SHULE YA SEKONDARI HATA FANYA VIZURI

kampeni za uchaguzi 2010, Zitto alikuwa akimpigia kampeni Kafulila

na Kafulila akiwapigia kampeni wenzake akiwepo Machali ili kukirejesha NCCR kwenye chati

ni mkakati wa muda mrefu, pamoja na kutumiwa kukisambaratisha Chadema

Zitto anauchu wa nyadhifa kubwa ktk chama na taifa(japo anadai aliingia kwenye siasa kwa bahati mbaya)
 
.......nimeipenda hii Kigarama, hoja iliyomezani ni ya Machali na wala siyo ya kumaliza au kutomaliza la saba, ndo shida yetu pia wagonga urimbo, tukifuta ujinga kidogo tu basi tunaona watu wote majuha
Zitto tatizo ni wewe mwenyewe na tatizo lenyewe haliko kwenye siasa bali liko kwenye mitazamo yako kuhusu maisha. Mimi mwenyewe umeniudhi, Umenikera na kunihuzunisha sana pale ulipochanganya "kutokumaliza darasa la saba" kwa mmiliki wa Gazeti la Mwanahalisi na Hoja ya Machali. Inaonyesha huwa ukifika kijijini kwako unawaona wapiga kura wako hawastahili kuwa na mbunge "Msomi" kama wewe kwani najua wengi wao hawajamaliza darasa la saba!!
 
tatizo watu hapa JF wamechoka na maisha magumu lakini wao wanaona njia pekee yakuondokana na hili ni kuisupport chadema... hapana sote tunataka mabadiliko lakini lazima tukubali pia kuna mapungufu makubwa ya kiuongozi ndani ya chadema na Pro-CDM wanajaribu kuuficha kwa kujifanya hawaoni na kusifia kila kitu.

Ukifatilia kwa undani comments za wengi Pro-cdm na matendo ya viongozi utagundua kuna kitu kimejificha juu ya malengo haswa ya hiki chama. lets wait and see mwisho wake
 
Ndugu wanaJF na Chadema naomba ufafanuzi wenu zaidi kuhusu hili.

Kwa upande wangu na nilishasema tena huko nyuma wakati Zitto anataka uenyekiti Chadema. Zitto anatumiwa bila kujua, kiukweli Zitto hana uwezo wa kuongoza chama kama M/Kiti sembuse Urais ila anajidanganya kwa kupata sifa kupitia Chadema nje ya chadema hana lolote na atoke aone.

Mimi binafsi ninaona kuwa kwa Zitto ni za mwizi arobaini kwani ni kati ya walioihujumu Chadema 2010 kwa kuvujisha siri za chama.Chadema shirikianeni na wote wenye ukweli juu ya nyendo za gamba hili ndani ya chadema ili liondoke kwa aibu.

Naomba maoni yenu nitasema mengine.
Wewe ni mjinga kuliko hata Kubenea unabwabwaja ujinga hapa bila hata aibu!..hivi kweli unaweza ukamlinganisha zitto na mbowe katika nyanja ya uongozi hapa tanzania?

...hivi haujui kama Mbowe amekuwa akihakikisha hakuna mtu anayechipua kumpiku ktk chadema? ...kwanini huko kutumiwa kwa zitto kuanzie pale tu alipoamua kugombea uenyekiti na si pengine popote?...hivi kweli unatumia akili kufikiri au ndo yale yale masaburi yenu watoto wa mbowe?

...hebu waulize mapacha watatu=mbowe, slaa na komu ni nini hasa kinawasumbua kwa zitto zaidi ya dhamira?...zitto amafaa sio tu kuwa raisi wa tanzania hata wa afrika kwa ujumla au umesahau kuwa kiongozi bora hapatikani kwa kabila lake wala pesa zake kama mbowe bali ni uwezo wake?
 
Kabwe pona haraka uje uwashauri vijana wenzako wala si kuanzisha vurugu maana kila mtu anavuta kwake.plz afadhali kama kuna mmoja amepotoka na hasa kafulila mu6oyeoi
 
Zitto tatizo ni wewe mwenyewe na tatizo lenyewe haliko kwenye siasa bali liko kwenye mitazamo yako kuhusu maisha. Mimi mwenyewe umeniudhi, Umenikera na kunihuzunisha sana pale ulipochanganya "kutokumaliza darasa la saba" kwa mmiliki wa Gazeti la Mwanahalisi na Hoja ya Machali. Inaonyesha huwa ukifika kijijini kwako unawaona wapiga kura wako hawastahili kuwa na mbunge "Msomi" kama wewe kwani najua wengi wao hawajamaliza darasa la saba!!
Kwani Komu kamaliza darasa la ngapi? Hivi kweli nyie hamuoni ubaya wa magazeti yanayo milikiwa na viongozi wenzako wa chama, ndio yanakuwa mbele kukuharibia jina?..Jamani tuwe wakweli kama kafanya kweli zipo njia za kumuuliza Zitto na sii kuanika ktk vyombo vya habari kabla hajaulizwa yeye.
 
Mkandara
Nakuunga mkono kwa maneno yako mazito, yenye busara na yaliyonyambulisha suala zima la mvutano kati ya Zitto na Mbowe.

Naomba Mkandara atueleze jambo moja muhimu hapa alilosemea; nalo ni kushindwa kwa Dr. Slaa.

Wiki tumeona waraka mwingine wa UWT, uliosanifiwa kwa malengo maalum. Unadai katika mengi kuwa, Kikwete hakushinda uchaguzi ule. Mkandara anasema, " Nilitegemea kabisa Dr.Slaa atashinda uchaguzi huo lakini wakatafuta mbinu ya Udini na ikaweza kufanya kazi..".

Nani alishinda?
Kikwete hakushinda. Alipata 27%. Lakini NEC kwa ushirikiano na usalama wa taifa walichakachua na kupika kura. Kwenye kituo nilichosimamia mimi kama wakala kulikuwa na wapiga kura 400 na zaidi. Waliojitokeza kupiga kura walikuwa 301. Kati ya hizo Kikwete alipata kura 31 na Slaa 258. Kuna ndugu yangu Musoma alikuwa naye wakala. Aliniambia Kikwete alipata kura 3 Musoma mjini lakini akatangazwa mshindi.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom