kaka mheshimiwa machali yuko sahihi kabisa kwani toka awali zitto anakwenda kinyume na matakwa ya chama chake.huyu zitto ni mnafiki tu na kibaraka wa ccm .kuondoka kwake chadema kutakuwa bora zaidi chama kitastawi na yeye ndo utakuwa mwisho wake.viva chademakuna ukweli asilimia 95 kwenye hii habari, zitto na kafulila wanatumika!
Duuh! Kaka,Kama Zitto ni tatizo na sio uongozi wenu na siasa za kiujanjaujanja iweje kuondoka kwa Zitto Chadema kuweze kuwavuruga na sio kuwapa nafasi ya kujijenga. Lakini pia iweje Kiongozi wa CCM anapokataa kunyamazishwa eti kwa maslahi ya chama iwe haramu lakini anapotokea kiongozi wa Chadema asiyekubali kunyamazishwa ama kunyamazia mambo ya hovyohovyo iwe haramu (Double standard zisizoweza kumsaidia mtanzania kamwe)
Hivi ni vipi Zitto akataka huo urais at any cost na sio Freeman Mbowe aliyetayari kupanga na kutekeleza mikakati haramu dhidi ya washindani wake kama Dr Slaa na Zitto? Hivi ni nani aliyesikika akilalama kuwa wale watu watatu waliokufa kule Arusha hawakutosha ili kujenga chuki zaidi kwa CCM na Chadema ifaidike kisiasa? Hivi ni nani anayeendeleza siasa za majungu katiika magazeti yenu (zinazokomaza makundi ndani ya Chadema) eti katika kuhakikisha kuwa anammaliza Zitto kwa kosa la kuthubutu kushindana naye katika nafasi za uongozi za Uenyekiti na baadaye Uongozi wa Upinzani bungeni ambao kwake yeye ni "platform" ya kujijenga kwa Watanzania ili kama asemavyo" come to 2015 awe Presidential Material"? Hivi ni nani aliyekuwa mstari wa mbele kuhonga viongozi wa Chadema majimboni ili wasabotage kampeni za wagombea wenu ambao anaona wao ni tishio kwa nafasi yake ya Uenyekiti na safari yake ya Ugombea Urais 2015
Ulichokiandika hapa kinathibitisha ukilaza wako katika kupambana na hoja na vizingiti vya kisiasa vinavyokumba ndoto yenu ya siasa za madaraka...Lakini pia weweukiwa kama kiongozi wa Chadema unathibitisha hisia halisi za kundi la wahafidhina ndani ya chama chenu katika mantiki nzima ya maslahi, siasa na chuki za kidini...Hivi ni nani aliyekimbilia kwa Maaskofu akiwaahidi kuwa anenda kujiendeleza kielimu ili baadae aweze kugombea urais na hata alipotishiwa kung'olewa kidemokrasia katika nafasi yake ya uenyekiti akatumia hoja ya kuwa Maaskofu hawatakuwa tayari kuona vyama vyote vikuu vinaongozwa na Waislamu
Kweli ni kilaza. Unajifaragua kama mwanasiasa wakati unashindwa hata kujua tofauti ya itikadi na sera? Ndio maana mnambiwa muende shule na msome masuala ya siasa za dunia yetu. Siasa za kujifunzia katika magazeti ya udaku wa kijamii na kisiasa kama Mwanahalisi ni hatari kwa Tanzania ijayo.
Nijuavyo katika tafiti zote zilizofanyika umaarufu wa Zitto umekuwa ukipanda na sio vinginevyo. Chuki na hisia zenu kuwa mnafanikiwa kupunguza umaarufu wa Zitto ndio zinaendeleza kuwadumaza huku mwenzenu anazidi kujitanua sio tu nchi lakini hata katika medani za siasa za kimataifa. Ninyi bakini na pety and parochial politics mkidhani watanzania hawa walioamka na kung'amua uvundo wa CCM wataendelea kuamini katika ugoigoi wa kifikira, nia za chuki na uozo wa Chadema....
Hili dua lenu la kuku kuwa Zitto atahamia CCM kamwe haliwezi kutimia. Kamwe Zitto hatahamia CCM.
Halafu angalia fikira za "wakombozi" wanaotuuzia chai za "DEMOKRASIA" wakati bado mnashindwa kujiondoa katika na utando wa siasa za kihafidhina za kuwapa Umungu viongozi wetu. Eti hakuna mtu wa kulinganishwa na Dr Slaa (ofcourse yapo ya Dr Slaa ambayo hayawezi kulinganishwa na mtu mwengine lakini sio uwezo wa kuongoza nchi na kuleta mabadiliko ya kweli na yaliyo makini yenye tija kwa watanzania). Udaktari wa Theolojia haumtoshi sasa mnaanza kumpa Umungu. Halafu baadae mtakuja lalamika viongozi haohao mnaowapa umungu wanavyogeuka kuwa miungu watu.....
Good news..Kwa mtindo huu kuiondoa serikali ya CCM madarakani itakuwa ni ndoto!
Sasa kosa la Kubenea ni lipi? Yeye amemnukuu Machali, mbunge wa Muhambwe, wilayani Kasulu mkoani Kigoma. Huyu ndiye anayemtuhumu Zitto kuwavurugia chama chao.
Mpaka hapo sioni kosa la Kubenea. Yeye ametimiza wajibu wake wa kusikiliza kila mmoja. Amesikiliza. Ameandika. Amemtafuta Kafulila, amempata. Amejieleza.
Katika hili, mtendeeni haki mwenzenu, badala ya kumtuhumu na kumtukana eti amenunuliwa? Je, kumuandika Zitto, ndiyo kununuliwa? Kama kila mtu atakayemuandika Zitto, Samwel Sitta kanunuliwa, basi tunakoenda kubaya.
kaka mheshimiwa machali yuko sahihi kabisa kwani toka awali zitto anakwenda kinyume na matakwa ya chama chake.huyu zitto ni mnafiki tu na kibaraka wa ccm .kuondoka kwake chadema kutakuwa bora zaidi chama kitastawi na yeye ndo utakuwa mwisho wake.viva chadema
Mbona wengine hawakushinda kwa umaarufu wako? Acha kuondoka kwenye hoja. Jibu tuhuma. Wewe ni mtata, tena unatumiwa na Rostam na Zoka.
Mbomoa nchi ni Mwananchi mwenyewe na ndiye mjenga nchi, ZITTO hawezi kuibomoa NCCR katu hizi ni chuki binafsi dhidi ya ZITTO maana hapo awali walisema anampango wa kuhamia NCCR kisa, kumfuata rafiki yake Kafulila.
Hiki chama hakieleweki mara tatizo ni M/kiti leo ZITTO mara Kafulila asingekuwa Kafulila wangepata hata huo ushindi wanao uona leo wa 4mps. Tatizo ni nini ? kama hawalioni wafanye uchaguzi mpya chama kisukwe upya kuanzia juu hadi chini