Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Kafulila na Zitto wanaivuruga NCCR - Moses Machali

Status
Not open for further replies.
Zitto imemuuma ndio maana anaropoka. Lakini hebu niulize kumbe Said Kubenea ni darasa la saba? Najua yeyote mwenye mawazo na urais atapata shida sana kama akina Professor Mwandosya, Zitto mwenyewe kwa sababu nyie wote mwajua kubenea na Kaka kule monduli sasa wako vizuri. Ila frankly speaking Zitto ana mambo mengi sana na huwa hajui anataka nini na sio mpambanaji wa kweli.
 
watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana. Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >tanzania daima>mwanahalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana. Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa katibu mkuu wa chama ili wamiliki wa tanzania daima (mhe. Mbowe) na wa mwanahalisi (ndugu komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.

pole sana wachu
 
siku zote nimekuwa nasimamia yale ninayoamini. Sifanyi kazi zangu ili kufurahisha watu bali kuzingatia maadili yangu na itikadi yangu na maslahi ya nchi yangu. Sifanyi siasa za drama maana naamini katika siasa za hoja. Ya kamati yangu bunge ndio inaongoza kwa kusimamia vema fedha za umma. hutaki kuona kwa kuwa umelishwa sumu ya propaganda za kumchukia zitto bila sababu yeyote ya msingi. Mimi sijali nafanya kazi zangu.
kwa hili nakupa hongera 100%
naikubali sana kamati yako.
Unafaa kuwa waziri mkuu ila sio rais
 
well umeandika sana
1.Zitto kuwa na nia ya kuivuruga CHADEMA eti kwa mipango yake ya kuhamia ama kugombea Urais
Matendo ya Zitto yanaondoa nia safi aliyona nayo ya kuwa Rais-(ni vigumu kuamini Zitto ana nia ya kuisogeza mbele nchi kama akiwa rais kwa CDM/NCCR/CCM

2.kuvuruga chama chenu
zitto anautaka urais at any cost K

3.kujisafisha kwa udini ukabila ufisadi
udini (RAIS MUISLAM,MAKAMU MUISLAM,WAZIRI WA PESA,MAMBO YA NDANI,KIRANJA WA ZANZIBAR,MAKAMU KIRANJA ZENJI,ULINZI MUISLAM)+ufisadi (muulize mwanao wa chekechea)=hao ni CCM
Ukabila nenda TLP na CCM (ALL SINGIDA)

4.mizizi ya itikadi za KIJAMAA
Hata CCM wana sera za Kijamaa
hamna chama chenye sera nzuri kama CUF tuwe wakweli
Note:Sera za kwenye makabati na mezani hazisaidii kama hamna commitment (CDM wapo commited including Zitto)
NCCR inakosa watu wa aina ya CDM na sio inamkosa Zitto K.

5.nguvu na akili za Zitto
nakubali Zitto ana akili nyingi ila anaponzwa na tamaa.
Zitto hana nguvu kisiasa kama mwanzoni (Baada ya Mafisadi papa kukalia kuti kavu CCM Zitto hana tena jeuri kwani ni wazi alitegemea saaaanaa msaada kutoka kwa Rostam ili aendeshe siasa ndani ya CDM kwa manufaa ya CCM na sio kwa manufaa ya nchi.

My take:Kwa sasa Zitto hawezi kuhama CDM as Mapacha wamebanwa ndani ya CCM,
Kama Zitto ni jiwe kuliko CDM tunataka aondoke hata leo tena ahamie CCM asituletee undumilakuwili hapa.
Ndani ya CDM hamna mtu wa kulinganishwa na Dr. Slaa.Ni mamluki wa CCM ndani ya CDM wanaoleta ujinga na sasa wajue Zitto hatakuwa rais akiwa CDM kwa hiyo wawahi KWINGINE
Umenena vyema mkuu.
 
Mwita hii ni propaganda maalumu inafanywa kwa malengo maalumu. Sijawahi kutumika na CCM maisha yangu yote na CCM wanajua hivyo. Lakini ukitaka kuua nyota ya mwanasiasa yeyote wa upinzani ni kusema anatumika. Hata marehemu Chacha Wangwe walisema anatumika na CCM ili kumvunjia heshima wala hapakuwa na ushahidi wowote wa hivyo. Mpaka anakufa alikufa na kinyongo hiki. CCM hawawezi hata siku moja kunitumia. Nimekuwa ninafanya kazi zangu Bungeni kwa umahiri mkubwa sana and yet maadui zangu wa kisiasa wanasema haya mambo ya kipuuzi kabisa.

Ni juu yako unaamini hizi propaganda au unazipuuza. Lengo ni kunivunjia heshima mbele ya jamii. Kwa muda mrefu Mwanahalisi wamekosa cha kuandika juu yangu na wameamua kutumia mgogoro wa NCCR kunihusisha ili tu kuendeleza propaganza zao chafu dhidi yangu.

Zito mdogo wangu, baadhi yetu si wepesi wa kuchukuliwa na upepo ILA tuseme wazi kuwa kuna mambo ambayo tunapoyasikia, yakitolewa na vielelezo na bila hata ya kujibiwa na wewe binafsi kwa vielelezo, tunashindwa kuwa na uhakika wa dhamira yako. Tunashindwa kuelewa kuwa Zito unavyoonekana nje ndivyo ulivyo katika dhamira na akilini mwako. Tunashindwa kuelewa unachotamka mdomoni kama ndicho kilichopo moyoni. Mambo yafuatayo yalitamkwa juu yako, na hatujasikia ukiyabia:
  • Kuwa kabla ya uchaguzi mkuu ulikutana na Rostam kule SeaClif usiku kwa karibu masaa 4 - ni kweli au ni uwongo? Ulikuwa ni mkutano binafsi au wa kikazi?
  • Kulikuwa na mawasiliano ya mara kwa mara kati yako na Naibu mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wakati wa uchaguzi - ni kweli au siyo kweli? Mlikuwa mnaongelea mambo binafsi au ya kikazi?
  • Kuwa wakati wa kampeni, chama chenu kikiwa tayari na mgombea wa Urais, badala ya kumpigia kampeni, wewe ulisikika ukisema kuwa utakuja tena mwaka 2015 kama mgombea wa Urais na siyo wa ubunge. Je, uliyasema hayo? Kama ulikuwa unajua kuwa wakati huo utakuwa hujafikia umri unaotakiwa kikatiba kugombea nafasi hiyo, kwa nini ulitamka hivyo? Ulikuwa ukiongea uwongo wa uwazi kwa wapiga kura wako?
  • Hulka yako ya kila mara kutaka madaraka makubwa inawatia wasiwasi watu wengi. Licha ya kwamba katiba ya chama na nchi inakupa haki hiyo lakini kuna haki, hekima na busara - Je, si busara kwa mtu mwenye hekima kusubiri wenzako wakupendekeze kuliko kila mara wewe tu, hata kabla ya taratibu za ndani ya chama kutolewa, wewe umeshatamka, 'mimi nataka nafasi hiyo'. Umwenyekiti wa chama unataka, uongozi wa kambi ya upinzani bungeni unataka, urais unataka, n.k. Kumbuka maneno ya Mwalimu Nyerere alipochangia kongamano la Uongozi wa bara la Afrika - alipoulizwa ni mtu wa namna gani anafaa kuwa kiongozi wa nchi? Katika kujibu, alinukuu (sikumbuki kutoka kwa nani) akisema, 'Viongozi wazuri na wanafalsafa, lakini kwa bahati mbaya wanafalsafa wengi hawapendi madaraka. Wengi wa wanaoutafuta sana uongozi huwa ni wale wasiofaa, na wakipata hawataki kutoka madarakani'. Wananchi wengi tunawaogopa watu wanaopenda sana madaraka maana mara nyingi licha ya kushindwa kuongoza vizuri huwa ni ving'ang'anizi wa madaraka.
Zito kama unataka kulisaidia Taifa hili, tushirikiane kuwapata viongozi wazuri katika ngazi mbalimbali, hata kama wewe usipokuwa mmojawapo wa hao viongozi tunaowataka. Faraja yetu iwe kuwa na uhakika kuwa Taifa lina uongozi bora, hapo tutaweza kuiona dhamira yako murua ya kulipenda Taifa.
 
Zitto,nakuomba uwe mtulivu.Nimelisoma gazeti lote la Tanzania Daima lakini hakuna mahali popote umetajwa kwa jina.Ingawa Machali amezungumzia matatizo ya Kafulila na kusema tu anataka uenyekiti kwa kutumiwa na kigogo mmoja.Tanzania daima halijakutaja jina.Hata hivyo Machali amesema vituko vyote vya Kafulila amerekodi.Kumtaja tena Mbowe hapa kutazusha migogoro isiyo na maana.

Mnafiki ni chakula ya mamba, wewe sindio umeleta hii thread tena kwa juu umeandika habari nzito tena ya kusutushwa..

Heading yako umeandika Kafulila na Zitto waivuruga NCCR..

Kama ulisoma ukaona hakuna sehemu yoyote Zitto kaandikwa kwa nini uweke utumbo wako humu JF...

Zitto umewaona wanafiki wako kama alikuwa na nia nzuri kwa nini asiku-PM..

Ujue ulivyojitokeza limewashuka vibaya hawana pakutokea
 
Mimi nashangaa kitu kimoja japo huwa sipendi kushangaa katika maisha yangu ila kama binadamu sasa inabidi nishangae tena sana.Nimesoma comments za watu wengi naelewa kinachoendelea hapa ni nini sasa jamani.Kwanza kabisa tukubali kabisa kwamba Zitto anajisahau sana jamani mwaka jana wakati nasikiliza kampeni zake za mwisho kabla ya kupiga kura alisema kabisa kwamba kama atarudi tena kwa wananchi wake Kigoma basi si kuomba kura za ubunge 2015 ila atarudi tena kwa kuomba urais badala ya Ubunge.

Sasa ninachojiuliza ni kwamba kama katika report yake aliytoa sasa kwamba yeye hawezi kugombea tena urais kwamba katiba haimruhusu tena kwanini alitumia nafasi hiyo kuwadanganya wanananchi wa Kigoma?Alikua hajui kama katiba haimruhusu tena? Huu ni unafiki mkubwa sana wana JF wenzagu.wataalam wa mambo "wanasema unaposema uongo kumbuka na unachosema bwana"
 
Watu hawana hata uungwana wa kusema huyu mtu ni mgonjwa, hajatoka hospitali. Huruma ya kibinaadamu hawana.

Kuna uchawi gani zaidi ya huu? Mwelekeo ule ule >Tanzania Daima>MwanaHalisi yote yanamilikiwa na viongozi waandamizi wa chama changu. Nimechukia sana.

Nitawasilisha malalamiko rasmi kwa Katibu Mkuu wa chama ili Wamiliki wa Tanzania Daima (Mhe. Mbowe) na wa MwanaHalisi (Ndugu Komu) waeleze mwenendo wa magazeti wanayomiliki kuhusu mimi. Nimechoka kuzushiwa uwongo na magazeti haya kila kukicha.

Mdogo wangu Zitto pole sana na kuugua. Hakuna mchawi mkubwa dunia hii kama msengenyaji. Ukweli wa haya mambo unaujua wewe mwenyewe moyoni, muda ukifika mkuu prove them wrong. Na imani wewe ni mtu makini sana sitegemei mtu wa calibre yako uta panic. Its just a matter of time and time will tell.

Thanks and get well soon.
 
Mnafiki ni chakula ya mamba, wewe sindio umeleta hii thread tena kwa juu umeandika habari nzito tena ya kusutushwa..

Heading yako umeandika Kafulila na Zitto waivuruga NCCR..

Kama ulisoma ukaona hakuna sehemu yoyote Zitto kaandikwa kwa nini uweke utumbo wako humu JF...

Zitto umewaona wanafiki wako kama alikuwa na nia nzuri kwa nini asiku-PM..

Ujue ulivyojitokeza limewashuka vibaya hawana pakutokea
Nakuombea kwa mungu akupe macho uone. Hayo uliyonayo yanakudanganya.
Gazeti la mwanahalisi lina habari nzito tena za kushtusha.

Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machali amemshutumu vikali David Kafulila kwamba anatumiwa na Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe kukivuruga chama hicho.

Mbunge huyo wa Kasulu anadai lengo kubwa la Kafulila ni kumwondoa mwenyekiti wa chama hicho James Mbatia ili yeye awe mwenyekiti.

Pili Machali amedai kwamba baada ya Kafulila kuwa mwenyekiti atamkaribisha Naibu Katibu mkuu wa Chadema Zitto Kabwe ili awe mgombea Urais kupitia NCCR.

Moses machali ameendelea kudai kuwa baada ya mpango huo kukamilika watatumia mbinu mbalimbali kuivuruga Chadema kwa kuhama na kundi kubwa la wanachama wake.

Mbunge huyo ameendelea kudai kuwa kamwe hatakubali mbinu hiyo kwani Zitto na Kafulila wanatumika kuua upinzani.

Alipoulizwa kwanini watake kumuondoa Mbatia kwanza amesema hiyo ni kutokana na sababu kwamba kamwe Mbatia hatamkubalia Zitto kugombea urais kupitia NCCR.

Source: MwanaHalisi
Tanzania Daima imetajwa hapa?
 
Zitto ni mtu ambaye anajua kucheza na akili za watu sana...

Wengi wetu tumeshindwa kumuelewa Zitto ni mwanasiasa wa aina gani.....

Ukweli ni kwamba Zitto ana ndoto nyingi sana kwenye kichwa chake...

Ndoto zake zina mletea matatizo sana kutokana na njia anazo jaribu kuzitumia kufikia utekelezaji wa ndoto zake....

Zitto unatakiwa kuweka sawa nyendo zako usije ukaji kwaa.
 
Moja, sina mpango wowote wa kuhama CHADEMA. Kila siku nasema nimekuwa mwanachama wa chama kimoja tu cha siasa maisha yangu yote, nimekuwa mwanachama wa CHADEMA toka nikiwa na umri wa miaka 16 na namwomba Mungu kila siku nife nikiwa ndani ya chama hiki. Najua kuna watu wanapenda sana nitoke CHADEMA kwa maslahi yao ya kisiasa wakiniona mimi ni tishio kwao. Napenda kuwaambia nimetumia nguvu nyingi sana kujenga chama hiki na sitahama. Waache kabisa kunizushia na kunijengea chuki mbele ya umma.

Pili, sihusikikwa lolote lile na yanayoendelea ndani ya NCCR na wala sina interest ya kuyajua. Mbunge wa Kasulu mjini ambaye alikuwa mwanachadema na kushinda Ubunge kwa sababu ya kutumia jina langu huko kwao Kasulu anaropoka (kama kweli kasema maneno hayo) na nitakapotoka Hospitali nitamtaka anithbitishie anayoyasema. Vijana wanapojiingiza kwenye siasa za uwongo kama wazee wao ni hatari sana kwa nchi. Sihitaji kwenda NCCR ili kugombea Urais kwani chama changu ni kikubwa zaidi na kitanipa Urais kwa urahisi kuliko NCCR ambacho ni chama kisicho na rekodi yeyote ya kupigania maslahi ya nchi hata wakati kilipokuwa chama kikuu cha upinzani nchini. Katiba hainiruhusu kugombea Urais mwaka 2015 na hata kama ikibadilishwa na kuniruhusu kugombea kwangu kutategemea sana mwafaka ndani ya chama changu. Anayedhani kwamba nia yangu ya kuwa Rais wa Tanzania ni ya kufa na kupona hamjui Zitto. Sifanyi siasa za kufa na kupona. Ninao uwezo wa kuwa Rais bora maana nina ajenda na ninatoka chama bora. Lakini pia nipo tayari kufanya kazi yeyote ile ambayo chama changu kitanipa.

Zittophobics wanaishi kwa siasa za kumwaza Zitto na wamo kwenye vyama vyote vya siasa hapa nchini. Ninafanya kazi zangu za Ubunge kwa ufanisi na mafanikio makubwa sana, ninafanya kazi zangu za Uenyekiti wa Kamati ya Mashirika ya Umma kwa umakini mkubwa na ninafanya kazi zangu za Uwaziri Kivuli wa fedha katika hali ya kuridhisha sana. Maadui zangu wa kisiasa wanatamani nianguke. Kwa uwezo wa Mungu sitaanguka.

Tatu, Gazeti la Mwanahalisi limekuwa ni gazeti linalonisakama sana kila kukicha lina ajenda yake. Gazeti ambalo limepoteza mvuto wake kwa jamii halinishughulishi. Hata juzi Mzee Samweli Sitta amelishutumu kwa kununuliwa na mafisadi na kutumiwa. Niseme nini zaidi kuhusu gazeti hili linaloongozwa na mtu ambaye hata hajamaliza darasa la saba. Mwanahalisi wanajua kwamba wakiandika habari yenye jina langu mauzo yao yanakua makubwa. Hili ni gazeti mufilisi ambalo kazi yake ni kutumiwa tu.


Nne, WanaJF mnasema hili ni jukwaa ni Great Thinkers. Great thinkers huwa hawadaki habari na kuziamini na kuanza kutoa maoni bila kwanza kupata uhakika wa habari hizo.

Nasikitika kwamba watu wenye ugonjwa wa Zittophobiasis ni wengi sana humu. Ninawashauri kwamba jitahidini muwe objective na muone upande wa pili wa shilingi.

Habari hii ya Mwanahalisi ni habari ya kijinga sana kujaribu tu kunihusisha na vurugu za chama ambacho mimi si mwanachama wake. Kafulila na mimi ni marafiki na ni wabunge wa Kigoma. Lakini Kafulila na mimi hatuongei mambo ya vyama vyetu hata kidogo na yeye anajua kwamba sina interest na NCCR Mageuzi.

WanaJF msicheze ngoma isiyo yenu.

ugua pole mh.zitto,

Tunakuheshimu sana kama mwanasiasa bora na unayejenga hoja nzuri na mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na kiuongozi. lakini daima katika ngazi uliyofika epuka kuwa na jazba unapojibu hoja zako, natarajia siku moja uwe rais wetu na mtu unayeshika majukumu mazito sana, hekima na busara ndio uwe mwongozo wako wa kujenga hoja na si kushambulia kundi fulani,

Hapo umefanya kosa badala ya kuonyesha makosa ya mtu, umejega hoja ambayo inatedhalilisha jamii tusiokwenda shule, si mtu huyo tu bali mathalani mimi sijakanyaga ata shule ya chekechea lakini nina haki ya kudhaniwa kama nikitenda makosa basi si sababu ya mimi kutokwenda shule bali ni upeo wangu.

siku njema ila sitarajii utarudia tena kosa la kutushambulia sisi wananchi tuliokosa kwenda shule kwani wengine si kwasababu atukupenda shule ,pengie ni uwezo wa wazazi wetu, hivyo hukumu yako inaweza kutuumiza bila makosa

anyway siku njema , ila tumia muda mwingi kutulia kutokana na afya yako
 
Anadai awali Kafulila alimshirikisha mpango huo akakataa
mimi siwezi kubisha kuhusu habari hii; hebu na tujiulize swali moja, ni kwa nini Kafulila alifukuzwa CHADEMA? pili mwenendo wa Zitto CHADEMA hauna tofauti na ule wa Shibuda a.k.a mzee wa ujira wa mwiha, ambaye wanachadema wote tunamjua kuwa ni msaliti.
 
Nimekuwa nikimtetea sana Zitto katika hizi propaganda kwa points tofauti. Leo naomba nitumie point nyingine... Ukiacha Zitto, Ben, Mkumbo, na wengine wachache waliochangia hii thread, wengine wote (including me Tuko), are ghosts. Nina uhakika kati ya wachangiaji humu wapo masupastaa wa kisiasa (wabunge, viongozi wa vyama na wa serikali). Hapa katajwa Machali, katajwa Kafulila, katajwa Zitto, katajwa Kubenea, katajwa Komu, kama wahusika wakuu (masupastaa) wa hii habari. Ni Zitto peke yake kajitokeza kwa jina lake. Hawa wengine wote (ambao naamini wengi wamechangia katika hii thread), wametumia majina na uhusika bandia. Nani wa kuaminiwa..., probably ni Zitto.

Hivi mnajua mimi ninaeandika hapa ni nani? Pengine mimi ni Kikwete, au Bilali, au Mbowe, au Komu, au Kubenea, au Kafulila... Lakini kwa sababu ninazozijua mimi nimejiita 'Tuko'... halafu naweza leta habari hapa leo nikajiita mwanaCCM, kesho mwanaCDM, keshokutwa mwanaNCCR, siku nyingine nikasema sina uanachama, ili mradi personality yangu ya siku hiyo ifitishe hoja au habari yangu.

Kama haya madai yana ukweli, naomba akina Kubenea, au Machali waje kwa majina yao hapa na watetee hoja zao, na sio kutumia majina ya uongo hapa kumchafua mtu. Huwa mara nyingi ukiangalia threads zinazomponda Zitto, utaona majina yaleyale yanajirudia. Imesemwa hapa kuna waajiriwa wa Nape (Ritz, Rejao, FaizaF, Mwita25 and the like) na inawezekana hawa pengine ni watu wawili wana IDs kibao. Sasa hapa ukweli ni kwamba kuna waajiriwa wa Zittophobiasis, na ni wachache sana ila wana IDs kibao, wanajipanga vizuri sana kuziandika na kuzipamba habari za kumchafua Zitto kuanzia Magazetini hadi humu JF na kwenye mitandao mingine. Na mtashindwa... Marasmus..
 
Naanza kuamini hii habari ina ukweli ndani yake.Zito kama sio kweli haya yaliyoandikwa humu angepinga kwa hoja.Nilikua mfuasi mzuri wa zito,lakini niliingiwa na mashaka alipoingia kwenye mgogoro na uongozi wake, lakini pili alipotangaza kwamba 2015 atarudi kwao akigombea nafasi tofauti na aliyooigombea wakati huo.Akimaanisha uraisi.Hili nilijiuliza sana kwa nini afanye hivyo wakati chama bado hakijapendekeza mgombea.Huu niliuona kama mgogoro unaoandaliwa ,maana asipoteuliwa kugombea itakuaje?kwa watu waliosoma na Zito UDSM wanasema ni "opportunist".Bado najaribu kutafakari pia uswahiba wake na JK.Huyu anaweza kuwa ni "KIGEUGEU" napia kuwa Nape wa CDM.

amegundua chama kinaendeshwa kikabila kama hautokei kilimanjaro au arusha ni vigumu kugombea urais ndani ya cdm.wakitaka wafanikiwe wamuache 2015 agombee ndani ya chama na sio kumshauri asigombee kwani inamuondelea ari ya mapambano ya kutetea wanyonge
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom