Kabwe Vs. Wangwe - kisa cha mafahali wawili?

Zitto+air Lowassa=uchumi Unapaa-(mwanakijiji+abiria Wameachwa)-(chacha Wangwe+wananchi Wa Kawaida)=uchumi Wa Tanzania Unawayawaya
 
Sasa ndipo tuulize ile makala ya mwanakijiji ambayo ilisifiwa sana hapa akiponda hotuba ya Lowasa, ndio kusema uchumi umegeuka in 3 month time?
 
Pumba tu
na ZITTO wenu huyo ,
yani ninyi nani kawaloga ???
Hivi inawezekana ktk kongamano la kupata maelezo na takwimu sahihi za hali ya hewa ya dunia aende kuzielezea Enginear wa civil?? kulaleki walai Watu wa taifa lile!!!!!

Kazi ya serikali inaenda kuongelewa na wapinzani Uchumi wenyewe huo wa kubumba duuu hivi DR Watson hapa atapingika kweli kwa mawazo yake??
Hivi nani katuloga tukiitwa tusipate kuitika, tukitazama tusipate kuona?????
Hapo angeenda JK au Lowassa na kuhutubia kuwa uchumi ktk madini umepaa watu humu ungesikia vijembe
Lakini kwa vile JK na Lowasa wanapiga mabao ya visigino wakaamua kuwasukumia kipenzi wenu Kipofu ZITTO ili awapufushe vizuri.

watu wamekubali uchumi ktk madini unapaa sasa mwaka mpya akija Lowasa hapa akasema uchumi unapaa mtu hata bisha maana wameshakwisha pofushwa.
ZITO endelea kupotosha wapofu wanzako maana hata ktk vijimisemo vimo vinavyosema acha wafu wakazikane
 
Killtime et al.,
Nimerudia kusoma post yangu sijaona hata sehemu moja ambapo nimesema Zitto adanganye. Nitachosema mimi sioni kama ni kazi ya kiongozi wa upinzani kusifia ukuaji wa uchumi. There are plenty of people employed just to do that including the Ministers Finance and Economic Planning. Kuna mambo mengi ya kuongea kuhusu ile nchi ambayo wapinzani wanapaswa kuyabebea bango ambayo CCM hawawezi kuyasema. Sasa kama na sisi tutaongea kama CCM what will be the difference? So, msijibu hoja zangu kwa kuniwekea maneno, I will be the last person kusema kiongozi wa upinzani adanganye. Mimi nimfuatiliaji kidogo wa mambo ya siasa, sijapata kuona kiongozi makini wa upinzani anasifia mafanikio ya serikali. Sanasana huwa wanatakiana kila la heri baada ya kuchaguliwa, baada ya hapo ni vigongo kwa vigongo. As a politician you must be careful in choosing your words. The last thing you can do as an opposition leader is to shower praise on your opponent, especially in a country where the government is failing in almost every aspect, that will be irony at best and foolhardy at worst!

Kwa mtu mpinzani makini ukiona umeongea jambo halafu gazeti la Uhuru linaiweka positively as a leading news in its front page lazima ushtuke; ujue ulichoongea kilikuwa na maslahi zaidi kwa CCM kuliko opposition, sasa nauliza tena hivyo ndivyo tunataka kiongozi upinzani awe? Yaani awe kipaza sauti cha CCM?

Zitto-usidanganyike ndugu yangu, viongozi wa CCM wamechafuka vya kutosha kiasi kwamba hakuna anayeongea na wananchi wakamchukulia seriously tofauti na watu kama wewe, Slaa, n.k. Sasa be careful CCM watakutumia mwenyewe kueneza propaganda zao bila wewe kujua. Sasa subiri 2010, watanyanyua hiyo copy ya Uhuru na kusema tazameni hata Zitto mwenyewe anasema uchumi unakua, mambo safi, huyu ndiye shujaa wa Taifa anasema hivi. nyie mnataka nini? Bwana tafadhali usituongezee kazi sisi kwenye kampeni za 2010, washikaji kibao hapa JF hawatakuwepo, sisi ndio tutahangaika na wewe kwenye majukwaa!

Tumia majukwaa unayopewa na hizo taasisi ku-expound CHADEMA's economic vision which is so far not known by the majority of people in our country. Itapendeza kama next time tutajadili hapa a controversial economic policy ya chadema badala ya stats za kukua kwa uchumi, ambazo kimsingi ni hewa!

Aminia Kitila, wewe ni kada wa kweli wa CHADEMA. Nimependa kauli yako ya kumlinda Zitto. Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA hawezi kuwa kipaza sauti cha CCM mpaka wakamtoa ukarasa wa mbele kauli yake dhidi ya serikali kwa mapambio yote. Kuliko kusifia mpinzani wako ni afadhali ukae kimya. Lakini hapa ni zaidi ya hapo, kuna cha kusifia? Mbaya zaidi UHURU wakaandika ukurasa wa mbele kwamba awataka wananchi waiamini serikali. Hii serikali ya mafisadi ambayo upinzani umetangaza mgogoro nayo wa kitaifa mpaka hao mafisadi waliotajwa wachukuliwe hatua kwanza? Ni hii serikali iliyoeleta Richmonduli na hatimaye ikaathiri kasi ya ukuaji wa uchumi. Nashauri Zitto asiendeleze majibizano hapa. Yeye na Chacha wote wanalakujirekebisha kutokana na mjadala huu. Zitto na Chacha wote wajifunze kukanusha ama kuwaelekeza idara ya uenezi na propaganda kukanusha ama kutoa ufafanuzi badala ya kuingia mitego ya CCM na wahandisi wa habari walioko kwenye payroll ya Rostam Aziz.

Asha
 
Hili jambo la uchumi kukua ni jambo ambalo inategemea unaangalia nini?

a. Ukiangalia takwimu ni wazi kuna vitu vimeongezeka. Yawezekana kabisa kuongezeka kwa vitu hivyo kumetokana na kuongezeka kwa mchango wa vitu hivyo katika uchumi. Vitu hivyo yaani sekta mbalimbali za uchumi zawezekana kabisa kuwa zimeongeza mapato ya kitaifa na kuchangia katika Pato la Taifa.

b. Suala zima la kuangalia GDP kama kigezo cha kutangaza kuwa uchumi umekua bila kuelezea vizuri ni GDP ipi tunaiangalia na tumepimaje na zaidi ya yote ugumu wa kupima uzalishaji na uuzaji wa bidhaa mbalimbali zinaweza kutupa picha isiyo sahihi. Katika kupima uchumi unakuaje hatuna budi kuangalia elements zote muhimu GDP (Real na nominal), GNP, GDP per Capita, PPP n.k

c. Kwenye majibu ya Waziri Mkuu kwenye ile mada ya "kupaa kwa ndege ya Tanzania" nilikataa kitu kimoja ambacho kwangu bado ni mazingaombwe. Endapo mji una shule moja ya sekondari, mahitaji ya shule za sekondari ni sekondari saba, sasa mtu anapojenga sekondari mbili nyingine mtu anaweza akasema "sekondari zimeongezeka" kitu ambacho ni kweli lakini kuongezeka huko ni kwa lazima kukidhi majitaji.

d. Hatuwezi kuona maendeleo ya kweli na ongezeko la kweli hadi tutakapoweza kuzalisha na ziada. Sasa Zitto na bila ya shaka watu wa uchumi wanasema kweli kabisa kuwa kwa kuangalia vigezo vya kiuchumi ambavyo tunaweza kuvitumia kupima ni wazi kuwa sekta mbalimbali za uchumi mchango wake kwenye uchumi umeongezeka na hivyo kuchangia katika pato la Taifa. Tatizo linakuja tunapoangalia GDP per Capita ambayo inahusiana na hali ya maisha.

e. Uchumi unaonekana umekua kwa mtu wa kawaida (siyo kwenye makaratasi) pale ambapo maisha yao yanapokuwa yameboreshwa na wanafurahia pato kubwa lenye nguvu ya ununuzi. Sasa ukiweka na mfumo wa bei (adjusted to inflation) kukua kwa uchumi kuna maana gani kwa mtu wa kawaida?

Hapa ndipo tunakutana na tatizo zima la kupima ukuaji wetu wa uchumi. Binafsi naamini kabisa kuwa tatizo kubwa la kupima uchumi wetu ni kuwa tunatumia kanuni ambayo kwetu ni ngumu mno kufanya kazi under constant conditions.

Katika formula yao ya kupima uchumi (computing GDP)kuna elements ambazo sisi hatuziingizi na hivyo tunakosa kuelewa kweli kwa kiasi gani uchumi unakua.

Binafsi naamini changamoto kubwa ya wachumi wetu ni kuamua kutoka kwenye box la nadharia za uchumi za zamani na kujaribu kutafuta njia bora zaidi ya kupima uchumi wetu hasa katika mazingira yetu. Bado najaribu kuangalia kanuni nzima ya kupima uchumi na kuona jinsi ilivyongumu kuweza kupima uchumi wa nchi kama za kwetu.

Siwezi kushangaa kuwa yawezekana kuwa uchumi wetu unakua zaidi kuliko inavyoripotiwa na njia za benki ya dunia ambazo zinatumika nchi zote duniani (zilizoendelea na zinazoendelea).

Swali kubwa kwangu kwa ninyi mlio wachumi ni kuwa ni jinsi gani GDP inahusishwa na hali ya maisha ya wananchi na wananchi wanaweza kuelezea vipi maisha yao pale ambapo hayaendani na kiwango cha ukuaji wa GDP jinsi unavyoelezewa?

Swali jingine ni jinsi gani secta moja inavyoweza kuonesha kuwa uchumi umekuwa kwa vile tu uzalishaji na mauzo katika sekta ile umeongezeka sana bila kuathiri ukuaji wa sekta nyingine na kuinua pato la mtu binafsi? Kama Madini na Utalii vinachangia sana kwenye GDP je ni kwa kiasi gani sekta hizo zinabadilisha maisha ya watu maana haitoshi kuonesha kuwa sekta hizi zinachangia kwa kiasi kikubwa bila kuonesha ni jinsi gani maisha ya watu yanainuliwa.

Hapa nadhani suala la linkages linakuwa muhimu sana na kwa kweli la kimakusudi. Ninaishi mahali ambapo mfano huu ni dhahiri . Jirani yangu ni kampuni za magari (wanakotengeneza vipuri na vyombo mbalimbali vya magari). Upande mmoja kuna makampuni makubwa Matatu (GM, Chrysler, na Ford). Haya ndiyo yanaendesha uchumi wa jimbo la Michigan na pembeni yao ni makampuni yanayofanya kazi kama suppliers. Kwa kadiri makampuni hayo makubwa yanafanya vizuri ndivyo na suppliers nao wanafanya na ndivyo maisha ya watu wao yananufaika.

Katika Tanzania hatuna hizi linkages nzuri na hii ni point muhimu sana. Kwanini supplies wa Samani atoke Dubai? Kwanini nyanya zitoke Afrika ya Kusini; n.k Ni jinsi gani suppliers wetu wanaweza kuingia na kumeza biashara na hivyo kushiriki katika kuinua uchumi na kuinua maisha ya watu wetu? Nadhani lipo tatizo la kufanya hivyo na labda baadaye tutalijadili.
 
Zitto+Mwanakijiji=Human Development Index(HDI)

Zitto-Mwanakijiji=Mr ZERO

Zitto Kabwe+Chacha Wangwe=CHADEMA+ Ukuaji wa kweli wa uchumi

Zitto-Chacha= Air Lowasa+CCM

Ukuaji wa uchumi=Maisha Bora

Chacha-Zitto=Porojo za Vijiwe vya Bangi

Kabwe+WangweX (Mwanakijiji+Augostine Moshi+Kitila)= Hoja mbadala
 
Katika mambo ya uchumi bwana huwezi kusema uchumi umekua na watu wakakuelewa wakati hali zao za maisha hazijabadilika na kuwa bora zaidi ya zilivyokuwa awali. Utanukuu minamba kibao, wafadhili watakusifia weeee, lakini mwisho wa siku hali za watu wa kawaida ndio zina-matter na sana sana utaonekana unaongea pumba tu.
 
mwana kijiji siasa za nini si sema upo pamoja na ZITTO.

Mbona rocketi la Lowasa ulilipinga harafu leo una kuja na linkages za akina Zitto
PUMBA TUPU
warning
mtu ukiamua kuwa mwogo lazima ukumbuke uongo wote uliosema ili baadae usiukane uongo wako wa nyuma
 
Kwani wewe unataka Mwanakijiji aseme kile unachotaka wewe? Kwani tumekuwa russia hapa au north korea? Kama wewe unaona kuwa zitto amesema uongo si useme hivyo na usimamie hoja zako mbona unaanza vilio kuwa watu hawaoni unachoona wewe!

Jamani mpeni maziwa labda ana njaa huyu!
 
Ukiwa na ki-island nation cha watu 1000, kukawa na bilionea mmoja alyeingiza $1,000,000,001 kwa mwaka na wengine 999 walioingiza $1 kwa mwaka, katika mahesabu ya kufunga mwaka unaweza kabisa kusema watu katika hicho ki island nation wameingiza $ 1,000,000,001 + 999 = $1,000,000,1000, hivyo kwa wastani kila mtu ameingiza $1,000,000,1000 / 1000 which is about 1,000,0001 which is a very far cry from the paltry $1 which 99.9% earned.

The moral of the story is, financial indicators can be manipulated to say anything, all you have to do is choose the right ratio for the x/y axis and some clever delivery tricks.

Tunachotaka ni kuona jinsi gani kama kuna ukuaji wa uchumi unatusaidia wananchi.Tanzania is not a stock market crazy country,I would not mind reports of negative growth if the actual conditions on the ground are showing improvement, the opposite is also true.

Enough with the spinning already!
 
mwafrika
kweli nina njaa maana hata hilo rocketi limeniacha sasa maziwa tayapata wapi? ndio maana nasema Pumbaaaaaaa pole sana mwaafrika baada ya pumba kumwagika ktk macho yako nawe huyoooooooo wapufuka

If A=B and B=C ni obviuos A=C by transistion property
statement ya Lowasa na ya Zitto kwa property hiyo ya transistion zipo sawa kabisa.
Ni jambo la ajabu sana ukipinga A ukaikubali C ndio maana NALIA kama ulivyobainisha, yani nini kimewasibu na PUMBA ZENU yani baada ya kuwapa mifugo wajipatie mlo ninyi mmeamua kuzitia ktk macho yanu haya MAMA WA KIAFRIKA
 
Duuh...., Pundit,mfano wako kiboko... hata watu kama mimi tusiopenda manamba namba nimeuelewa!! Shukrani.

SteveD.
 
mwafrika
kweli nina njaa maana hata hilo rocketi limeniacha sasa maziwa tayapata wapi? ndio maana nasema Pumbaaaaaaa pole sana mwaafrika baada ya pumba kumwagika ktk macho yako nawe huyoooooooo wapufuka

If A=B and B=C ni obviuos A=C by transistion property
statement ya Lowasa na ya Zitto kwa property hiyo ya transistion zipo sawa kabisa.
Ni jambo la ajabu sana ukipinga A ukaikubali C ndio maana NALIA kama ulivyobainisha, yani nini kimewasibu na PUMBA ZENU yani baada ya kuwapa mifugo wajipatie mlo ninyi mmeamua kuzitia ktk macho yanu haya MAMA WA KIAFRIKA

Haya yote hayabadili ukweli kuwa kama wewe unaona kuwa Zitto amedanganya au ametoa pumba, ni juu yako kuonyesha hizo pumba au huo uongo na kisha ukatetea hoja zako kwa hoja bila kulialia kuwa Mkjj na wengine hapa nao waseme hicho ulichoona wewe.

Kulialia sana kama kitoto kichanga ni signs za kutokuwa na hakika na unachosema na kwa hili nakupeleka

walewanaolialiabilasababuhatasikuyakirisimasi.co.uwiii
 
Mkumbo, Mpaka Kieleweke etc,

Nadhani kuna masuala ambayo hamtaki tu kuelewa au/na mnajaribu kuwa "laymen". Katika maelezo yangu ambayo nimeyaweka kama mada yangu huko Arusha (ambapo gazeti la uhuru limeandika wanavyotaka wao kuandika)sijaisifia serikali ya CCM hata kidogo. Nimeeleza ukweli, tena ukweli wa suala ambalo mimi nina authority nalo kama mtu ambae nimesomea uchumi na pia kama waziri kivuli wa uchumi. Siwezi kuchagua maneno ya kusema for political expediency. Ni lazima tuondokane na tabia ya kufinyanga ukweli. Tunapowaeleza ukweli wananchi ni rahisi sana kujenga hoja zetu bila kuwa embarrassed huko baadae na kutakiwa kukanusha. CCM imetufikisha mahala ambapo ni rahisi sana Mtanzania kukataa ukweli hata kama hana 'data' za kuthibitisha kukataa kwake. Hii ni matokeo ya Spins and propaganda
Ni ukweli uliowazi kabisa kabisa kuwa uchumi unakua toka 1996. Ukuaji umeshuka kidogo mwaka jana 2006. Nimeeleza kuwa kukua kwa uchumi kuna sababishwa na sekta ambazo hazina forward and backward linkages. Na ndio changamoto. Na hapa ndio sisi wanasiasa wa upinzani twapasa kuja na sera mbadala. Mfano CHADEMA tuliposema kuwa tunapitia mikataba ya madini katika ilani yetu ya uchaguzi mwaka 2005, tulikuwa tunajaribu kurekebisha hali hii. Mfano tungetaka all supplies za katika migodi zitoke Tanzania etc.
Mimi sijasema uchumi unapaa. Ni upuuzi kusema hivi. Suala la uchumi kupaa ni somo maalumu la mwaka wa pili Development Economics EC 213. Hapa MwanaKijiji alielezea vizuri sana dhana ya Rostow ya take-off stage. Hatuwezi kufikia hapa mpaka Ukuaji wa sekta ya kilimo ufikie 8-10 asilimia katika kipindi cha miaka 3 mfululizo. Hii ina maana yatupaswa kudouble uzalishaji katika kilimo na uzalishaji huu upelekee usindikaji etc na ndio maana wachumi tunaita rural growth na si tena agri growth maana tunataka rural infrastructure, rural manufacturing, rural micro-finane etc.

EL anaposema tunapaa katika hali ya sasa ni dhahiri anaonesha udhaifu katika dhana nzima ya kupaa. Kwa mwelekeo wa sasa na mwenendo wa mambo tunaweza kudash take-off stage na madhara yake ni kuwa na resource based economy (yaani kutegemea madini, utalii na gesi tu) na hivyo kupanua wigo kati ya masikini na tajiri. Hii ndio hatari tunayoisema kila siku ndani na nje ya Bunge.

Mimi, kama mchumi na kama mwanasiasa nasema Uchumi wetu umekuwa unakua kwa miaka kumi iliyopita. Ukuaji huu wa uchumi hauwezi kupunguza umasikini kwa sababu ni ukuaji unaoletwa na sekta mbili ambazo hazina manufaa kwa wananchi. Hatujafikia take-off stage, na hivyo uchumi haupai. Ili tufikie stage hiyo, ni lazima kilimo kama sekta inayogusa watu wengi ikue kwa asilimi kati ya 8 na 10 kwa miaka 3 mfululizo. Kwa mwelekeo wa sasa ambapo ukuaji wa sekta ya kilimo umeshuka (-1 point) matumaini ya kufikia ukuaji wa 8-10 ni mdogo.

Juhudi ziongezwe ili kuongeza uzalishaji vijijini/mashambani, kupanua miundombinu ya vijijini na kuweka sera mwafaka za kufanya sekta ya madini na ya utalii kuwa na mahusiano mazuri na sekta nyingine za uchumi.

Kama kuna mtu anasema yapaswa kupeleka kwenye chama kazi zangu za kitaaluma, lazima anakosea. Mimi sijakurupuka. Nimeweka hapa mada yangu. Itafikia wakati sasa sisi watu wa CHADEMA tutasema Mwenyekiti wetu awe analeta katika orodha ya watu waliolala Katika Hotel ya Aishi kule Machame, ambapo yeye mwenyekiti anaimiliki. Nimeripoti kile ninachoona ni academically correct na Mkumbo anakosea anaponiambia nipindishe ukweli. Maana Mkumbo is ethical, he inspired me at my early university days and we have a pact on ethical issues. Napenda kumkumbusha mwalimu Kitila kuwa siwezi kupindisha professional ethics for political expediency. That will be the last thing for me to do.

Undisputable fact is, the economy grows. The growth is narrow. It is not broadbased. Hence not sustainable growth. But, i insist, there is growth!
 
Ukiwa na ki-island nation cha watu 1000, kukawa na bilionea mmoja alyeingiza $1,000,000,001 kwa mwaka na wengine 999 walioingiza $1 kwa mwaka, katika mahesabu ya kufunga mwaka unaweza kabisa kusema watu katika hicho ki island nation wameingiza $ 1,000,000,001 + 999 = $1,000,000,1000, hivyo kwa wastani kila mtu ameingiza $1,000,000,1000 / 1000 which is about 1,000,0001 which is a very far cry from the paltry $1 which 99.9% earned.

The moral of the story is, financial indicators can be manipulated to say anything, all you have to do is choose the right ratio for the x/y axis and some clever delivery tricks.

Tunachotaka ni kuona jinsi gani kama kuna ukuaji wa uchumi unatusaidia wananchi.Tanzania is not a stock market crazy country,I would not mind reports of negative growth if the actual conditions on the ground are showing improvement, the opposite is also true.

Enough with the spinning already!

Pundit, safi!
Thats the meaning of GDP. Na ndio maana siku hizi katika vipimo vya standard of living wachumi wanatumia purchasing power Parity (PPP) ili kuweza kulinganisha nchi kutokana na gharama za maisha. UNDP nao wakaja na Human Dev Index ili kuweka in context social development. Hivyo, tunatofautisha kati ya Economic Growth na Economic Development. GDP is simply growth. Ukiwa na sekta moja imeboom, haleluya uchumi unapaa. Mfano ni Angola na Chad na pia Equatorial Guinea ambapo Uchumi ulikua ukikua kwa 20% kwa sababu ya mafuta tu ilihali wananchi ni masikini wa kutupwa. Ili ukuaji wa uchumi ulete maendeleo ya kiuchumi ni lazima uhusishe wananchi wengi zaidi katika shuguli za kiuchumi. Vinginevyo utarekodi ukuaji mkubwa bila maendeleo kuonekana.
Tanzania kuna ukuaji wa uchumi ambao haujaleta maendeleo ya kiuchumi katika kipindi cha miaka 10 iliyopita. Sijui mnanipata hapo!
Ukisoma mada yangu utakuta kwa mfano level of stuntedness miongoni mwa Watanzania ni kubwa mno ie 38%. Bado watoto wengi wanakufa mara baada ya kuzaliwa etc. Hizi ni changamoto Pundit!
 
Tumekuelewa Mkuu Zitto,

Unanikumbusha siku zangu za A-Level tulikuwa na debate watu wa EGM na ECA (I forgot the specifics za debate) basi katika kuanza debate nikawa natumia opening kuwa courteous in an attempt at "eminent criticism" ambapo humpondei mpinzani katika his/her weakest point, bali katika strongest point.

Nikaanza debate kwa kusifia strongest point za mpinzani wangu ili kuendelea kuonyesha mapungufu hata ya hizo strongest points.Basi nilivyoanza wenzangu hawakunielewa wakaniona kama namsifia mpinzani, kumbe nilikuwa namjenga ili kusudi nionyeshe weakness yake, kwamba even at his best point, mpinzani wangu bado yuko flawed.

Nafikiri mheshimiwa Zitto hiki ndicho alichokifanya, amepiga bonge la eminent criticism.Kwamba hebu tukubali kwamba aspects fulani za uchumi zinakua, lakini hata kama zinakua ukuaji hauko sustainable na hauna manufaa kwa wananchi.

Tatizo la wengi, kama wale wenzangu katika ile timu ya debate ya A-Level, tumezoea kubishana mwanzo hadi mwisho, kwa sababu tuko opposing sides basi kubishana tu kila kitu hata pale indicators zinapoonyesha vinginevyo.

Disadvantage moja ya aina hii ya sophistication katika siasa za Tanzania ni kwamba kuna urahisi sana ya vyombo vya habari ku quote sentensi moja na kutangaza headline "Zitto asifia kukua uchumi" bila kuweka vitu kwenye context.

Kuna utani mmoja kwamba Papa John Paul alipofika New York 1979 aliulizwa na waandishi wa habari "Papa unajua kuna hookers New York City?" basi pengine kwa kushangazwa na hilo swali Papa ali-echo "Hivi kuna hookers New York City?".Basi kesho yake New york Post likazua headline "Papa aulizia kama kuna hookers New York City!" implication ikiwa kwamba alitaka kupona.

Beware of the paper touting profit marauding yellow journalism promoting ethics lacking mercenary like penmen.
 
Nimeripoti kile ninachoona ni academically correct na Mkumbo anakosea anaponiambia nipindishe ukweli. Maana Mkumbo is ethical, he inspired me at my early university days and we have a pact on ethical issues. Napenda kumkumbusha mwalimu Kitila kuwa siwezi kupindisha professional ethics for political expediency. That will be the last thing for me to do.

Undisputable fact is, the economy grows. The growth is narrow. It is not broadbased. Hence not sustainable growth. But, i insist, there is growth!
By the way Zitto ukweli ndio umekufikisha hapo! Na kama hukuzoe uongo utotoni/ujanani usijifunze sasa utaumbuka! Kitila Theory za uongo zinafundishwa hapo UDSM? Walahi munaabisha hicho chuo kama scholar kama wewe unaliweka hili wazi kiasi hicho! Sasa nina kila sababu ya kusoma btn the line maneno ya kina Dr. Senkondo, Prof. Baregu etc.
 
Mkumbo, Mpaka Kieleweke etc,

Nadhani kuna masuala ambayo hamtaki tu kuelewa au/na mnajaribu kuwa "laymen". Katika maelezo yangu ambayo nimeyaweka kama mada yangu huko Arusha (ambapo gazeti la uhuru limeandika wanavyotaka wao kuandika)sijaisifia serikali ya CCM hata kidogo. Nimeeleza ukweli, tena ukweli wa suala ambalo mimi nina authority nalo kama mtu ambae nimesomea uchumi na pia kama waziri kivuli wa uchumi. Siwezi kuchagua maneno ya kusema for political expediency. Ni lazima tuondokane na tabia ya kufinyanga ukweli. Tunapowaeleza ukweli wananchi ni rahisi sana kujenga hoja zetu bila kuwa embarrassed huko baadae na kutakiwa kukanusha. CCM imetufikisha mahala ambapo ni rahisi sana Mtanzania kukataa ukweli hata kama hana 'data' za kuthibitisha kukataa kwake. Hii ni matokeo ya Spins and propaganda
Ni ukweli uliowazi kabisa kabisa kuwa uchumi unakua toka 1996. Ukuaji umeshuka kidogo mwaka jana 2006. Nimeeleza kuwa kukua kwa uchumi kuna sababishwa na sekta ambazo hazina forward and backward linkages. Na ndio changamoto. Na hapa ndio sisi wanasiasa wa upinzani twapasa kuja na sera mbadala. Mfano CHADEMA tuliposema kuwa tunapitia mikataba ya madini katika ilani yetu ya uchaguzi mwaka 2005, tulikuwa tunajaribu kurekebisha hali hii. Mfano tungetaka all supplies za katika migodi zitoke Tanzania etc.
Mimi sijasema uchumi unapaa. Ni upuuzi kusema hivi. Suala la uchumi kupaa ni somo maalumu la mwaka wa pili Development Economics EC 213. Hapa MwanaKijiji alielezea vizuri sana dhana ya Rostow ya take-off stage. Hatuwezi kufikia hapa mpaka Ukuaji wa sekta ya kilimo ufikie 8-10 asilimia katika kipindi cha miaka 3 mfululizo. Hii ina maana yatupaswa kudouble uzalishaji katika kilimo na uzalishaji huu upelekee usindikaji etc na ndio maana wachumi tunaita rural growth na si tena agri growth maana tunataka rural infrastructure, rural manufacturing, rural micro-finane etc.

EL anaposema tunapaa katika hali ya sasa ni dhahiri anaonesha udhaifu katika dhana nzima ya kupaa. Kwa mwelekeo wa sasa na mwenendo wa mambo tunaweza kudash take-off stage na madhara yake ni kuwa na resource based economy (yaani kutegemea madini, utalii na gesi tu) na hivyo kupanua wigo kati ya masikini na tajiri. Hii ndio hatari tunayoisema kila siku ndani na nje ya Bunge.

Mimi, kama mchumi na kama mwanasiasa nasema Uchumi wetu umekuwa unakua kwa miaka kumi iliyopita. Ukuaji huu wa uchumi hauwezi kupunguza umasikini kwa sababu ni ukuaji unaoletwa na sekta mbili ambazo hazina manufaa kwa wananchi. Hatujafikia take-off stage, na hivyo uchumi haupai. Ili tufikie stage hiyo, ni lazima kilimo kama sekta inayogusa watu wengi ikue kwa asilimi kati ya 8 na 10 kwa miaka 3 mfululizo. Kwa mwelekeo wa sasa ambapo ukuaji wa sekta ya kilimo umeshuka (-1 point) matumaini ya kufikia ukuaji wa 8-10 ni mdogo.

Juhudi ziongezwe ili kuongeza uzalishaji vijijini/mashambani, kupanua miundombinu ya vijijini na kuweka sera mwafaka za kufanya sekta ya madini na ya utalii kuwa na mahusiano mazuri na sekta nyingine za uchumi.

Kama kuna mtu anasema yapaswa kupeleka kwenye chama kazi zangu za kitaaluma, lazima anakosea. Mimi sijakurupuka. Nimeweka hapa mada yangu. Itafikia wakati sasa sisi watu wa CHADEMA tutasema Mwenyekiti wetu awe analeta katika orodha ya watu waliolala Katika Hotel ya Aishi kule Machame, ambapo yeye mwenyekiti anaimiliki. Nimeripoti kile ninachoona ni academically correct na Mkumbo anakosea anaponiambia nipindishe ukweli. Maana Mkumbo is ethical, he inspired me at my early university days and we have a pact on ethical issues. Napenda kumkumbusha mwalimu Kitila kuwa siwezi kupindisha professional ethics for political expediency. That will be the last thing for me to do.

Undisputable fact is, the economy grows. The growth is narrow. It is not broadbased. Hence not sustainable growth. But, i insist, there is growth!

Zitto

Angalia usije ukawa HAAMBILIKI baba yangu. Kitila hajasema upindishe ukweli, hakuna mahali amesema hivyo. Alichosema ni kuwa mada yako lazima iwe na jicho la kisiasa lakini pia ibebe itikadi yako unayoiamini wewe binafsi kuhusu uchumi. Ni vyema ukatulia ukasoma vizuri kabla ya kujibu. Uliyoyasema mengi ni sahihi kabisa lakini inaelekea unaanza kujibu kwa jazba na kuibua mambo mengine ambayo hata hayapo. Sasa hilo la mwenyekiti wako Mbowe na Aishi limetoka wapi? Walau ungetoa mfano kwamba Mbowe ametoa kauli hadharani kuwa utalii watanzania kwa mfumo uliopo ni safi kabisa hapo ungeweza kuwa na cha kulinganisha. Huwezi kusema maharage ni sawa na nyama kwa kuwa tu zote zinatoa protini. Wewe Zitto ulipaswa useme kabisa kwamba katika kipindi cha miaka kumi 'uchumi wetu unakuwa kwa kiwango ambacho hakiridhishi. Huu ndio ujumbe mkuu wa mada yako. Ujumbe wako mkuu si "uchumi wetu unakua'. Siku nyingine ukiulizwa swali, uchumi wetu unakua au haukui? Jibu: Unakuwa kwa kiwango ambacho hakiridhishi. Hili ndio jibu pekee ambalo litakufanya wewe Waziri Kivuli na mtaalamu wa uchumi uwe tofauti na Msomi mwenzio Dr Ngasongwa waziri wa uchumi. Ama sivyo wote tutawaweka kundi moja la wasomi mchumia tumbo walio tayari kusema chochote kuwaridhisha Benki ya Dunia na IMF. Waliotayari kusema kile ambacho Mkapa na Kikwete wanapenda kusikia. Wewe hupaswi kuwa kundi hilo la kuimba mapambio. Wewe si msomi wa namna hiyo, wala si mwanasiasa wa nanmna hiyo. Kumbuka pia wewe ni Mbunge unalipwa mshahara kwa fedha za wananchi hivyo hizo kazi zako zingine binafsi hazipaswi kuingilia misimamo yako kama mwakilishi wa wananchi wa Kigoma Kaskazini. Hivyo, UHURU walipoyaweka maneno yako katika sura ambayo waliyaweka ulipaswa kuwa wakwanza kukanusha na kufafanua kama ambavyo walau umeeleza hapa kwa maneno ya moja kwa moja zaidi. Hii si mara ya kwanza wewe kuacha kukanusha kauli zenye utata. Hatukuona ukikanusha habari ya Mtanzania kwamba Rais Kikwete ni kiongozi mzuri anayefaa kuongoza taifa la Tanzania. Kusema hivi ilikuwa ni kama wale wananchi wa Kigoma Kaskazini uliowaaambia wamchague Mbowe kwa kuwa ni bora kuliko Kikwete, ama ushabiki wako kwa Salim Ahmed Salim kama ulivyosema mwenyewe katika moja ya michango ya kwenye forum basi ulikuwa ni utapeli wa kisiasa. Achana na hao wanaokupaka mafuta kwa mgongo wa chupa baba yangu. Wasikilize wenzio wakina Kitila wanaujumbe mzuri kwako na kwa chacha. Chukua jumbe zote hizi. Jifungie usome kwa utulivu. Avoid academic and political arrogance, it is the people who have raised you up, it is the people who will take you down.

Nimesema-kwa mwanasiasa kauli hata ukiitoa maliwatoni ukijisaidia ni kama vile umeitoa bungeni. Huwezi kusema kwamba hii niliisema wakati napiga soga jamani. Mwenzako EL kauli yake ya kwamba anakula mwanakijiji ni aliirusha hewani?

Usiingie mtego wa UHURU; walijua tu wewe ni mbishi kuliko, ndio maana wakakusifia ukurasa wa mbele. Walijua Chacha ni mropokoji, ndio maana Nipashe wakamkimbilia. Na walijua baada ya hapo wote nyinyi viburi, viburi, viburi tu! Nyamazeni kwa sasa, kaeni chini, mkubaliane, mseme kwa pamoja. Msiendelee kumwaga radhi hadharani. Ifikirieni CHADEMA zaidi ya kujifurahisha akili zetu.

Wala hakuna sababu ya kupashana na kupishana hovyo hovyo kama wakina Asha
 
By the way Zitto ukweli ndio umekufikisha hapo! Na kama hukuzoe uongo utotoni/ujanani usijifunze sasa utaumbuka! Kitila Theory za uongo zinafundishwa hapo UDSM? Walahi munaabisha hicho chuo kama scholar kama wewe unaliweka hili wazi kiasi hicho! Sasa nina kila sababu ya kusoma btn the line maneno ya kina Dr. Senkondo, Prof. Baregu etc.

Wewe nawe sasa unatia aibu, kelele tu kuwa uongo wakati hauuonyeshi huo uongo na kisha kusema ukweli ni upi. Kama ni kutaka kupondea Prof Baregu na Senkondo ambao mara nyingi wanapondea mafisadi wako wa ccm inabidi uende hapa:

ninatakakupondeawateteziwahakilakinininachemsha.co.kuzimu
 
Back
Top Bottom