Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,896
Zitto
Angalia usije ukawa HAAMBILIKI baba yangu. Kitila hajasema upindishe ukweli, hakuna mahali amesema hivyo. Alichosema ni kuwa mada yako lazima iwe na jicho la kisiasa lakini pia ibebe itikadi yako unayoiamini wewe binafsi kuhusu uchumi. Ni vyema ukatulia ukasoma vizuri kabla ya kujibu. Uliyoyasema mengi ni sahihi kabisa lakini inaelekea unaanza kujibu kwa jazba na kuibua mambo mengine ambayo hata hayapo. Sasa hilo la mwenyekiti wako Mbowe na Aishi limetoka wapi? Walau ungetoa mfano kwamba Mbowe ametoa kauli hadharani kuwa utalii watanzania kwa mfumo uliopo ni safi kabisa hapo ungeweza kuwa na cha kulinganisha. Huwezi kusema maharage ni sawa na nyama kwa kuwa tu zote zinatoa protini. Wewe Zitto ulipaswa useme kabisa kwamba katika kipindi cha miaka kumi 'uchumi wetu unakuwa kwa kiwango ambacho hakiridhishi. Huu ndio ujumbe mkuu wa mada yako. Ujumbe wako mkuu si "uchumi wetu unakua'. Siku nyingine ukiulizwa swali, uchumi wetu unakua au haukui? Jibu: Unakuwa kwa kiwango ambacho hakiridhishi. Hili ndio jibu pekee ambalo litakufanya wewe Waziri Kivuli na mtaalamu wa uchumi uwe tofauti na Msomi mwenzio Dr Ngasongwa waziri wa uchumi. Ama sivyo wote tutawaweka kundi moja la wasomi mchumia tumbo walio tayari kusema chochote kuwaridhisha Benki ya Dunia na IMF. Waliotayari kusema kile ambacho Mkapa na Kikwete wanapenda kusikia. Wewe hupaswi kuwa kundi hilo la kuimba mapambio. Wewe si msomi wa namna hiyo, wala si mwanasiasa wa nanmna hiyo. Kumbuka pia wewe ni Mbunge unalipwa mshahara kwa fedha za wananchi hivyo hizo kazi zako zingine binafsi hazipaswi kuingilia misimamo yako kama mwakilishi wa wananchi wa Kigoma Kaskazini. Hivyo, UHURU walipoyaweka maneno yako katika sura ambayo waliyaweka ulipaswa kuwa wakwanza kukanusha na kufafanua kama ambavyo walau umeeleza hapa kwa maneno ya moja kwa moja zaidi. Hii si mara ya kwanza wewe kuacha kukanusha kauli zenye utata. Hatukuona ukikanusha habari ya Mtanzania kwamba Rais Kikwete ni kiongozi mzuri anayefaa kuongoza taifa la Tanzania. Kusema hivi ilikuwa ni kama wale wananchi wa Kigoma Kaskazini uliowaaambia wamchague Mbowe kwa kuwa ni bora kuliko Kikwete, ama ushabiki wako kwa Salim Ahmed Salim kama ulivyosema mwenyewe katika moja ya michango ya kwenye forum basi ulikuwa ni utapeli wa kisiasa. Achana na hao wanaokupaka mafuta kwa mgongo wa chupa baba yangu. Wasikilize wenzio wakina Kitila wanaujumbe mzuri kwako na kwa chacha. Chukua jumbe zote hizi. Jifungie usome kwa utulivu. Avoid academic and political arrogance, it is the people who have raised you up, it is the people who will take you down.
Nimesema-kwa mwanasiasa kauli hata ukiitoa maliwatoni ukijisaidia ni kama vile umeitoa bungeni. Huwezi kusema kwamba hii niliisema wakati napiga soga jamani. Mwenzako EL kauli yake ya kwamba anakula mwanakijiji ni aliirusha hewani?
Usiingie mtego wa UHURU; walijua tu wewe ni mbishi kuliko, ndio maana wakakusifia ukurasa wa mbele. Walijua Chacha ni mropokoji, ndio maana Nipashe wakamkimbilia. Na walijua baada ya hapo wote nyinyi viburi, viburi, viburi tu! Nyamazeni kwa sasa, kaeni chini, mkubaliane, mseme kwa pamoja. Msiendelee kumwaga radhi hadharani. Ifikirieni CHADEMA zaidi ya kujifurahisha akili zetu.
Wala hakuna sababu ya kupashana na kupishana hovyo hovyo kama wakina Asha
Asha Abdala nimekupata. Ushauri wako nimeuchukua hata kama umenielewa vibaya. Wala sikuwa na sababu ya kubishana na kaka yangu Mkumbo. Tunajadiliana hapa mjadala wa wazi kabisa na hata mfano wa Aishi Hotel ni mfano tu wa kukoleza mjadala na wala sio kwa nia mbaya kwani Freeman anamiliki Hoteli hii kihalali, hakuiba na ni moja ya Hotel bora sana za kitalii hapa nchini.
Sikufurahishwa na headline ya Uhuru na nimesema. Lakini walichosema ndani ni sahihi. Mimi si mtu wa kukanusha kanusha tu. Unakanusha kuchwa cha habari, wakati habari yenyewe ina mambo sahihi?
Kama maelezo yangu yamekuundhi nisamehe tu, lakini nimesimamia nilichosema. Unajua ni rahisi sana sisi wanasiasa kubadili maneno unapoona watu na hasa marafiki wakifikiri vinginevyo. Mimi nimesimamia maneno yangu na nihukumiwe kwa maneno hayo. Pia ninaamini kuwa ni jukumu langu kufafanua maelezo yangu ili nieleweke. Sasa kama katika ufafanuzi wangu kuna jazba au academic arrogance inaonekana nisamehe kwa kweli maana si vizuri kwa kiongozi kuonekana arrogant. Lakini ufafanuzi wa hoja na facts usionekane ni arrogance, hata kidogo!
Ninamheshimu sana Kitila, ndio maana ninamweleza moja kwa moja kwani naye ananiamini sana. Hasiti kusema ninapokosea na mara kadhaa ameonesha tofauti zake humu katika forum. Msingi wa urafiki wetu ni debate na sio blind loyalty. Na huu ndio msingi wa mimi na yeye kuwa chama kimoja tunachokipenda na kukijenga kwa nguvu zetu wote.
Suala la Salim, sina cha kusema. Nilimuunga mkono nikiamini ni kiongozi mzuri. Kwa vyovyote vile kama CCM ingempitisha kuwa mgombea, mgombea wa chama changu angekuwa ni mzuri zaidi na ndio maana nipo CHADEMA na Salim yupo CCM. Nadhani turudi katika mjadala wa ukuaji wa uchumi na kama mjadala umekwisha basi tufunge mada na twende katika mada nyingine.
Ushauri nimepokea Asha Abdala..........