Steve Dii
JF-Expert Member
- Jun 25, 2007
- 6,402
- 1,305
Habari, habari, habari na habari zaidi kuhusu mifarakano yenu Mh. Zitto! Nimeamua kuibandika hapa ilihali bado upo hapa unaweka msimamo wako sawa kwa WanaJF...
SteveD.
Today, 11:19 AM: Currently Active Users Viewing This Thread: 15 (9 members and 6 guests)
SteveD, jamco_za, mfwatiliaji, kilitime, Zitto, MADELA WA- MADILU, Mama Lao, ibambasi, Adolf
Source link: Mwananchi.Wangwe, Zitto watishia uhai wa Chadema
Posted Date::12/27/2007
*Ndesemburo aonya chama kinaweza kusambaratika
Na Joyce Mmasi
SIKU chache baada ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoa tamko kuwa hakuna mgogoro ndani ya chama hicho na badala yake kinachofanyika ni mjadala hai, sasa imedhihirika zipo dalili za wazi kuwa huenda chama hicho kigawanyika.
Hali hiyo inadhihirishwa na kauli za viongozi wa juu wa chama hicho, makamu Mwenyekiti wa Chama hicho, Chacha Wangwe na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe kulumbana hadharani kupitia kwenye vyombo vya habari.
Wachunguzi wa masuala ya kisiasa nchini wanazitafsiri kauli za kushambuliana na kupingana hadharani zinazowahusisha viongozi wawili wa juu ndani ya chama hicho zisipodhibitiwa haraka huenda zikakifikisha chama pabaya na kubakia historia kama vilivyo vyama vya NCCR-Mageuzi na Tanzania Labour Party (TLP).
Mapema wiki hii, Wangwe ambaye pia ni Mbunge wa Chama hicho Jimbo la Tarime alikaririwa na vyombo vya habari akimshutumu Zitto kwa kauli yake ya kueleza kwamba kuwa uchumi wa nchi una kua.
Chacha Wangwe alisema kauli ya Zitto inaonekana kushabihiana na kukubaliana na CCM na akamfananisha na mtu anayedandia gari kwa nyuma kitu alichosema sio msimamo wa kambi ya upinzani wala wa Chadema.
Wangwe anasema katika kauli yake hiyo, Zitto amekuwa na tabia ya kuisifia CCM hali inayotia shaka na kuona pengine mwenzao anataka kupanda gari moja na CCM, ndio maana yeye kwa maoni yake anapinga hadharani na akawataka watanzania pia kujitokeza kusema kama wanaona jambo la kusema.
Hata hivyo, hali hii imeaanza kuwatia wasiwasi baadhi ya wanachama na viongozi wa juu wa chama hicho kwamba ikiachiwa huenda ndio itakuwa tamati ya chama hicho katika ulingo wa kisiasa.
Mmoja wanachama ambao wanatiwa wasiwasi na hali hiyo ndani ya chama hicho, ni mmoja wa waasisi wa chama hicho, Philemon Ndesamburo ambaye alimweleza mwandihishi wa Mwananchi jana kwa njia ya simu kuwa malumbano ya viongozi hao ni dalili mbaya ndani ya chama.
Alisema kiongozi mkubwa ndani ya chama akitoa kauli kwa umma sio sahihi kwa kiongozi mwingine ndani ya chama hicho kuanzisha malumbano hadharani, badala yake tofauti zao zinapaswa kujadiliana ndani ya vikao vya chama.
Ndesamburo ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Mjini kwa tiketi ya chama hicho, alisema hali hii ya viongozi wa chama kushambuliana hadharani isipokomeshwa inaweza kuleta mpasuko katika chama hicho.
Alisema hata kama kiongozi mmoja wapo amekosea au kasema kitu ambacho sio halali au ni kinyume na taratibu za chama, ni vyema hoja hizo zikapelekwa kwenye vikao vya chama na sio kuzungumzwa kwenye vyombo vya habari.
�Ni kweli chama chetu ni cha kidemokrasia, lakini tafsiri ya demokrasia sio kushambuliana au kukaribisha malumbano hadharani, bali ni kuzungumza na kukosoana ndani ya vikao vya chama,� alisema Ndesamburo.
Aliwataka viongozi wanaokimbilia kwenye vyombo vya habari kuzingatia kanuni na taratibu za chama za kujadiliana ndani ya vikao halali vya chama kwa kuwa kufanya hivyo ni makosa.
Mwanchama mwingine ambaye hakupenda kutajwa jina lake alisema kuwa malumbano yanoyoendelea kati ya Zitto na Wangwe sio ya kukijenga chama bali ni ya kuwania umaarufu.
Alisema inavyoonekana Wangwe hoja yake nikutaka kummaliza Zitto kutokana na umaarufu ambao amejipatia na kwamba hali hiy ni mbaya na kwa kuwa inaweza kusababisha viogozi hao kupigana ngumi.
Hata hivyo, Mkurugenzi wa vijana wa Chama hicho, John Mnyika alimweleza mwandishi wa Mwananchi jana kwamba hakuna ubaya viongozi kutofautiana hadharani na kwamba hiyo ndio tofauti iliyopo kati ya Chadema na vyama vingine.
Mnyika alisema Chadema ni chama cha kidemokrasia kama jina lake linavyojiainisha na kwamba wanachofanya wanachama au viongozi ni kutumia demokrasia waliyo nayo kukosoa na kuelimisha bila kuzifanya kauli zao kuwa ni msimamo wa chama.
�Chadema ni timu moja yenye nia na malengo yanayofanana, hakuna ugomvi wowote na tofauti za misimamo haziwezi kuvunja chama na badala yake zinakiimarisha chama chetu,� alisema Mnyika.
Mnyika alitoa mfano wa kutokukubaliana kulikozuka wakati Zitto alipochaguliwa kwenye Kamati ya Madini ambapo baadhi ya watu waliamini ndio mwisho wa chama hicho, lakini baada ya vikao vya chama yale mambo yaliisha na hali ikawa shwari kama kwanza.
�Ndio maana nasema, Chadema ni tofauti na vyama vingine, tunafanya siasa ambazo watanzania hawajazizoea, tunapotofautiana kimawazo haimaanishi kuwa kuna ugomvi baina ya mtu na mtu, yale ni mawazo ya watu na kamwe hayawezi kukivunja wala kuleta mpasuko wowote ndani ya chama.
Naye Chacha Wangwe aliiambia mwananchi kuwa anasema anachokiamini na kamwe haaoni kama kuna uhusiano wowote wa kauli zake kuhusishwa na uwezekano wa kuvunjika au kuleta mpasuko ndani ya chama.
�Kutofautiana sio kubomoka kwa chama na mtu mmoja kamwe hawezi kuvunja chama, hivyo nataka ieleweke kuwa hoja ya kuvunjika kwa chama hapa haipo,� alisema na kuongeza: �Chama chetu kina uhai kiko tofauti kabisa na CCM, sisi tunazungumza hadharani na sio kuficha ficha mambo, ndani ya Chadema tuna uhuru wa kusema na kutoa maoni bila kuingiliwa".
Alitoa wito kwa watanzania wote wawe kama yeye, waseme pale wanapokuwa na hoja, wasifichefiche mambo na akasisitiza kuwa msimamo wake ni kuwa CCM haijafanya lolote na haipaswi kusifiwa na kiongozi kutoka kambi ya upinzani kuwa imeleta maendeleo.
Alisema Zitto amekuwa na tabia ya kuisifia CCM na serikali yake jambo ambalo alisema linawapa mashaka wao kama kambi ya upinzani.
SteveD.