Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,675
- 40,555
Mojawapo ya magazeti yanayotoka leo nyumbani lina kichwa cha habari "Wangwe ampinga Zitto" kuhusu kauli yake kuwa uchumi wa nchi unakua. Hii si mara ya kwanza kiongozi huyo wa Chadema kumlenga kiongozi mwenzie aidha kwa uharaka wa kuzungumza na waandishi au kutokana na sababu binafsi. Kwa wale wanaokumbuka sakata la madini kule Tarime Wangwe alikuwa ni mmoja wa watu waliopinga sana kuhamishwa wananchi na kuna wakati aliwekwa lupango. Hata hivyo wananchi wa Tanzania wengi hawakumbuki mchango wake huo na harakati zake pamoja na Lissu kuhusu madini.
Hata hivyo hapa anakuja kijana ambaye hajalipa gharama ya uanaharakati na anaanza kuvuna matunda ya kazi za kina Wangwe kwa kuonekana ndiyo "mtetezi wa wananchi". Kwa Zitto kuendelea kutajwa tajwa haimsaidii sana Wangwe.
Wote wawili bila ya shaka ni watu wanaojiamini sana, wako huru kimawazo, wasio tayari kushauriwa na kusikiliza mashauri hayo. Sitashangaa wote wawili ndani ya Chadema wameanza kuwa "maverick politicians".
Wanasiasa hawa wawili wasipoangalia watakuwa ndio chanzo cha mgogoro ndani ya CHADEMA hasa kama wataendelea kutunishiana misuli kwenye vyombo vya habari. Vinginevyo tunachoanza kushuhudia ni vita ya mafahali wawili kama ya Mrema Vs. Marando, Nyerere Vs. Kambona, n.k
Binafsi nina ushauri ufuatao kwa wote wawili:
a. Stop talking to the press each time they extend their mics to you!
b. Tafuteni wasemaji wenu rasmi siyo kila kitu mkitolee maoni "no comment" nalo ni jibu.
c. Inapobidi mzungumze mjue ninyi mnazungumzia chama chenu hakuna kitu kama "maoni binafsi" kwa kiongozi wa chama!
d. Mitazamo yenu inapogongana zungumzeni kabla hayajafika kwenye vyombo vya habari.
e. Pale mnapotofautiana kimsingi na waandishi wanataka kujua, zungumzeni pamoja na waandishi siyo huyu anasema hili akiwa madongo kuinama na mwingine anasema lile madongo kuinuka! Mnawachanganya watu!
f. Kuna vitu vingine msivitoleee maoni hadi msikilize washauri!
Vinginevyo, mtaendelea kugongana hadharani na kuthibitisha kile ambacho Watanzania wanakifahamu kwa muda mrefu, wapinzani wana migogoro ya ndani!