OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 49,244
- 103,937
Hii video ni jamaa wa Kenya,anayolalamika ni mambo yanayotokea Tz kwa kiwango kikubwa sana.
Mtakubaliana na mimi kuwa Kundi kubwa la vijana hawaaminiki na kuwapa kazi katika shughuli zetu za ajira binafsi, ujitoe akili.
Nazungumzia ajira ndogo ndogo kama Salon, Mpesa, Duka, shamba, gari, carwash, guest house nk. Unampata kijana wa kumwachia ofisi, anafanya siku 2,3 anakuwa mwizi,hajali wateja.
Kule shamba kijana mwizi anaiba mbolea na mazao. Sijui tunakimbilia wapi!
Kabla ya kijana kulalamikia serikali na matajiri hawatoi ajira, unaaminika?