Juma Zubeir, kijana anayetengeneza maji ya betri. Vijana mnaohangaika na ajira mnalo la kujifunza hapa

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,277
9,912
Biashara ni vile unavyofikiri na kuwa mbunifu kwa kufanya kile kilichopo kichwani mwako, kwa kukiweka katika vitendo ili kiwe na tija na manufaa.

Hilo pia litaonekana kupitia juhudi zako binafsi, huku maarifa yakikufanya kufanikisha hilo, kisha baadaye watu kuona malengo yako.

Inasikitisha leo kuona kijana kamiza elimu ya Chuo kikuu anaranda mtaani zaidi ya miaaka 2 akiwa na baasha yake kutafuta kazi, Akili yaje yote ipo kwenye baasha na vyeti vyake.

Hebu tuone mfano wa kijana Zuber ambaye amejisjiri kwa kazi ya mutengeneza betri za maji pasi kuwa na taalima yoyote.

Juma Zubeir ambaye licha ya kutokuwa na elimu kubwa, lakini aliiona fursa na kuamua kujitosa na kumfanya awe mfanyabiashara mkubwa wa kutengeneza maji ya betri yanayotumika kwenye magari, paneli za umeme jua na pikipiki.

Kwa kutumia kipaji na ubunifu aliobarikiwa Zubeir mwenye elimu ya darasa la saba, amekuwa lulu na kivutio kikubwa kwa wakazi wa kijiji cha Lukozi wilayani Lushoto mkoani Tanga anakoishi.

Licha ya kuwa kivutio lakini amekuwa tegemezi kwa madereva wa bodaboda , magari na wanaotumia bidhaa hiyo.

Kupitia maji ya betri yanayotumika kwenye vyombo vya moto ambayo anayatengeza kwa kutumia kemikali na maji ya kawaida, Zubeir alisema biashara hiyo imemsaidia kupata fedha na kumudu gharama za maisha huku akiajiri watu sita.

“Huwa ninanunua kemikali kisha kuchanganya kiutaalam na maji ya kawaida. Bidhaa zangu ni tofauti na bidhaa nyingine kwa kuwa zangu ni bora ndio maana wateja ni wengi na maji haya ninayotengeneza hufanya betri kudumu,” alisema.

Alivyoanza kutengeneza maji ya betri

Zubeir alisema kabla ya shughuli hizo alianza kutengeneza betri za magari na kuzichaji ndipo alipopatia ujuzi wa kutengeneza bidhaa hiyo inayomnufaisha kimaisha.

“Nilikuwa natengeneza betri na kuzichaji, lakini kila wateja wakija wanalalamika kuwa betri hazina moto wakifika nyumbani. Ilibidi niumize kichwa na kutafuta suluhisho la kujua tatizo ni nini? Kupitia utundu wangu nilibaini kuwa maji waliokuwa wakiyatumia siyo mazuri ndipo ujuzi wa kutengeza maji haya uliponijia.”

“Sijawahi kusomea popote ujuzi huu; ni utundu wangu tu mwenyewe niliobarikiwa na Mungu. Nilianza kama masihara kutengeneza maji haya lakini mwishowe yalikuja kubadilisha maisha yangu kwa namna wateja wanavyoyahitaji,” alisema Zubeir.

Kwa mujibu wa Zubeir, utengenezaji wa maji hayo unaanza asubuhi hadi jioni ambapo kemikali zilizochanganywa na ‘sulphulic acid’ zinakuwa zimeshapoa kisha kuchujwa na kupimwa katika kipimo maalumu na baadaye kujazwa kwenye chupa kwa ajili ya kuuzwa katika maeneo mbalimbali ya Tanga.

Alisema kwa siku anazalisha chupa za lita moja 300 na kuziuza kati ya 2,000 kwa jumla na Sh3,000.

Zubeir alisema siku ya kwanza baada ya kutengeneza maji hayo aliyafanyia majaribio kwenye betri za wateja wake ndipo alipobaini yanafaa kwa matumizi ya vyombo vya moto.

“Nilianza na chupa za kawaida, tulizokuwa tukiziokota sasa hivi tunatumia chupa maalum ninazonunua Kariakoo (Dar es Salaam).Namshukuru Mungu kwa ubunifu huu, gharama ninayoitumia ni Sh200,000 lakini faida ninayoipata ni Sh600,000,” alisema Zubeir.

Alisema katika shughuli ya utengenezaji wa maji hayo ya betri, amewaajiri watu sita kati ya hao watatu ni vibarua ambao wanafanya kazi ya kusambaza bidhaa hiyo katika maeneo mbalimbali ya Lushoto, Bumbuli na Korogwe.

Malengo yake

Zubeir alisema malengo yake ni kufungua kiwanda kikubwa kwa ajili ya shughuli hiyo, ili kutoa ajira zaidi kwa wananchi wa Lushoto, akiomba Serikali kumsaidia ili kufanikisha ndoto hiyo.

“Natamani niajiri vijana wengi zaidi ya hawa, shughuli hii inalipa sasa hivi silali njaa, nasomesha watoto. Changamoto ninayokumbana nayo ni mtaji mdogo, utakuta wateja ni wengi lakini bidhaa haitoshelezi,’’alisema.

Aaliongeza: “Pia nahitaji msaada kutoka kwa wadau mbalimbali wa viwanda, lengo langu jingine bidhaa hii ifike iuzwe nje ya Tanga ikiwa katika ubora zaidi. Hata hivyo maofisa wa Serikali wameshakuja kuniona hivi karibuni,” alisema Zubeir

Sido, halmashauri wajitosa kumsaidia

Wiki iliyopita alitembelewa na uongozi wa Shirika la Viwanda vidogo (Sido) mkoani Tanga na halmashauri ya Lushoto waliobaini kasoro kadhaa katika uwekezaji huo na kumuelekeza baadhi ya hatua za kufuata.

Kaimu meneja wa Sido Mkoa wa Tanga, Liberati Macha alisema taasisi hiyo kwa kushirikiana na halmashauri ya Lushoto walienda kumtembelea Zubeir kuangalia namna anavyotekeleza majukumu yake na changamoto zinazomkabili.

“ Tulivyofika tumeona upungufu wa kisheria na usio wa kisheria. Kwa mfano, eneo analofanyia kazi ni dogo na lipo katika ya makazi ya watu jambo ambalo ni hatari kwa afya kutokana na kemikali anazozitumia.Tulimshauri atafute eneo jingine kwa ajili ya shughuli hii.

“ Uzuri wenyewe Zubeir alishajiongeza kwa kutafuta eneo jingine ambalo alituonyesha na kuridhia kuwa lipo sawa.Pia tumeshawasiliana na ofisi ya mkemia mkuu kwa ajili ya kumwezesha ili asajiliwe na kutambulika rasmi na ofisi hiyo,” alisema Macha.

Alisema baada ya eneo hilo kupatikana Sido kwa kushirikiana na halmashauri, wataangalia namna ya kumsaidia ikiwa ni pamoja na kumpa huduma stahiki ili aweze kufanya kazi zake kwa ufanisi. Joel Makange anayefanya kazi na Zubeir, aliomba Serikali kuangalia namna ya kuwasaidia ili biashara yao ikue zaidi.

Naye, Mohamed Hamidu mtumiaji wa bidhaa hiyo aliusifu ubunifu wa Zubeir wa kutengeneza bidhaa hiyo ambayo imekuwa maarufu kwa wakazi wa Lukozi.

“Maji yake yapo vizuri tofauti na mengine yanayozalishwa kampuni asisi mbalimbali. Tunamuomba aendelee na uzalishaji huu asikate tamaa kwa sababu tunaitegemea bidhaa yake kwenye vyombo vyetu vya usafiri,” alisema.

Wakala wa maji hayo, Simon Abdallah alisema wateja anaowapelekea bidhaa hiyo hawajahi kumpelekea malalamiko dhidi ya bidhaa hiyo, badala yake wanaisifia kwa kusema betri zao zinakaa muda mrefu na moto.
 
Mleta Uzi kapungukiwa na Nutts Kichwani... Bora ubadilishe tu hiyo heading... Betri za Maji ? au Maji ya Betri?
 
Wewe hayo mambo yaujuzi yaache tu wewe ukikosa kazi unaweza kufanya kazi hiyo? Eti kijana mwenyewe nilasaba tu sio rahisi namna hiyo nikweli wahitim wengi wanategemea sana vyeti hiyo kweli sio sawa mm naamini swala laujuzi halitegemei elim pekee kunajamaa lasaba anajenga ila mara nyingi mainjinia wanajikuta wanaelekezwa na la saba.
 
“Nilianza na chupa za kawaida, tulizokuwa tukiziokota sasa hivi tunatumia chupa maalum ninazonunua Kariakoo (Dar es Salaam).Namshukuru Mungu kwa ubunifu huu, gharama ninayoitumia ni Sh200,000 lakini faida ninayoipata ni Sh600,000,” alisema Zubeir.
Anataja figures kubwakubwa asidhani sifa, akina Zakayo wanamtazama subiri wakienda ataanza kujikanyaga
 
kiwanda kingine hicho....
faida yake ni % 300...
tra wanacheka tu wakienda hapo atatia huruma!
 
Anataja figures kubwakubwa asidhani sifa, akina Zakayo wanamtazama subiri wakienda ataanza kujikanyaga
Yes amekosea kusema faida. Yaani hapa sio mfanyabiashara by nature sema ni innovator.yaani biashara hata Kama naingiza m kwa padei nalia kinyama kuwa biashara ni mbaya ,watakuja kuwambiwa fulani saivi Ana mijengo kama Mia hapa mjini
 
Back
Top Bottom