Tatizo la ajira na tiba yake

Tatizo la ajira na tiba yake

MISULI

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2014
Posts
7,856
Reaction score
5,561
SWALA LA UKOSEFU WA AJIRA NA NINI KIFANYIKE.

Na Sir Taylor

Habari ziwafikie;Waziri wa Elimu,Waziri Ajira na Vijana pamoja na Rais.

Kwanza ningependa kuwapa pole kwa majukumu ya kila siku katika kuwatumikia wananchi na Taifa letu kwa Ujumla.Najua mnapambana kweli katika kuhakikisha tatizo la ajira linatatuliwa miongoni mwa jamii yetu.Hili ni tatizo SUGU na sio kwamba limeanza awamu hii,lilikuwepo mda na kadri siku zinavyoenda linazidi kuwa kubwa sana.Naamini serikali haiwezi ikatoa ajira kwa wote na haitatokea na kwa hizi products za vyuo kadri zinavyozidi kuongezeka na ukiangalia Serikali imesitisha ajira hata serikali iseme inatoa ajira kiasi gani bado haitaweza kumaliza.

Ni kweli ajira sio lazima uajiriwe na serikali au taasisi binafsi.Nini hasa kinamfanya kijana ashindwe kujiajiri?

MFUMO WA ELIMU.

Elimu yetu inatosha kumfanya mhitimu wa chuo kikuu kujiajiri?Hapa sijazungumzia diploma na certificate. Mitaala yetu ya Elimu inakitu chochote cha kumfanya mhitimu akajiajiri?Kwa mfano mtu kamaliza Bachelor of education with Psychology au bachelor of Art in Education. Hawa ni waalimu kitaaluma,Je wana elimu yoyote ya ujasiliamali kusema ikawasaidie nje ya mfumo wa Ajira za serikali au sekta binafsi?

Asilimia 99 huyu mhitimu elimu yake imejikita katika kufundisha na kukabiliana na matatizo yanayoizunguka jamii kama jinsi ya kutatua migogolo nk.Hapa hamna elimu yoyote kuhusu kutambua fursa zinazomzunguka,jinsi gani azitumie yaani elimu nzima ya ujasiliamali hamna. Leo unamwambia ajiajiri,anaanza vipi?Hana elimu yoyote ya biashara, kilimo hata kutengeneza kiti tu hawezi.Miaka mitatu yote chuo Anafundishwa kusoma psychology ya mwanafunzi,mara kuandaa lesson plan nk.Anafika mtaani unamwambia jiajiri.

Nimeongelea kwa upande wa waalimu sababu hawa ndo wahanga wakubwa wa hili tatizo ingawa kuna profession nyingi tu ni tatizo.Kiujumla yapo matatizo mengi sana katika mfumo wetu wa elimu. Najua serikali mnajua hamuwezi kuajiri watu wote watakaokuwa wanahitimu masomo yao,hivyo basi ni muhimu kupitia upya mfumo mzima wa elimu ili uendane na kauli ya JIAJIRI.Mfano tunaambiwa serikali inawaalimu 7000+ wa Art wa ziada tu na inampango wa kuwapeleka shule za msingi.Kuna umuhimu gani tena wa kuendelea kuzalisha kitu kile kile ambacho huna matumizi nacho?HII NI WASTAGE IN EDUCATION.Kwanini mtaala usibadilishwe kuendana na hali iliyopo?

Kwa hali hii naona serikali ipunguze baadhi ya course ktk program husika au hata ikiacha hivihivo lkn course za biashara,ujasiliamali na nyingine zinazoweza kumfanya mhitimu ajiajiri ziingizwe katika mfumo.Hii itasaidia sana,mfano nje ya ualimu mtu anaweza anzisha hata genge lake na kwakua elimu ya biashara ipo ni rahisi kufanikiwa.Na hata kumsaidia kujua jinsi gani atumie fursa zilizopo.

SWALA LA MTAJI.

Ni ukweli usiopingika licha ya wengine kujua fursa zinazowazunguka na jinsi gani wazitumie,bado swala la mtaji huwa ni tatizo sana.Ni ukweli uliowazi serikali haiwezi kumpa kila mtu mtaji ajiajiri. Lkn bado serikali inaweza buni njia kuhakikisha mhitimu akimaliza chuo anapata mtaji endapo hata ajiriwa aweze kujiajiri.Kwa upande wangu ningeshauri Katika Hela ya kujikimu anayopewa Mwanafunzi chuoni,asilimia flani iwe inakatwa na kuingizwa ktk mfuko maalumu ambapo huyu mwanafunzi akihitimu anapewa kama mafao yake ambayo yanaweza msaidia kujiajiri na kuanza maisha mapya.Mfano Katika mwaka wa masomo mwanafunzi anapokea fedha ya kujikimu mara nne yaani sio chini ya 2Millions. Ambapo kila baada ya miezi miwili hupokea laki 5 na mwaka wa masomo ni miezi 8.Akawa anakatwa tufanye 50000 kila akiingiziwa hela,kwa mwaka wa kwanza ni laki 2 miaka mitatu laki 6.Laki 6 kwa mtu aliyeelimika na anaelimu ya ujasiliamali anaweza Fanya kitu na hata kama sio peke yake bado anaweza unda kikundi na wenzie wakafanya vitu vya maana sababu kila kitu wanacho.

SERIKALI KUWAWEZESHA VIJANA.

Kama tayari kijana anaelimu na angalau mtaji anao,serikali ni rahisi sana kumwezesha kufikia malengo yake nje ya mfumo wa ajira za serikali. Ipo mifano na njia nyingi za kumwezesha kijana.Mfano Vijana wanaweza kuunda kikundi cha kilimo,Hapa serikali inaweza kukisaidia kusajiri kikundi hiki kwa gharama ndogo na vilevile kupunguza gharama za pembejeo kwa vikundi kama hivi,kupunguza kodi mbalimbali za mazao kwa hivi vikundi na kuwajengea mazingira ya soko la uhakika la mazao yao.Pia kutoa shamba darasa kwa vikundi hivi kwani tayari wataalam wapo wengi sana.Hii itawahamasisha sana Vijana kujituma katika kazi na kuacha kusubiri serikali iwaajiri.

Naamini kwa kiasi kikubwa tatizo la ajira hasa wahitimu vyuo vikuu litapungua na serikali itakua na uhalali wa kusema vijana wajiajiri.Na hii itasaidia Vijana kuipenda serikali yao,maana chuki na hasira zilizopo kwa Vijana sasa ni kwamba hawaoni jitihada zozote za serikali katika kuhakikisha tatizo la ajira linapungua.Mfano ajira zilizotoka jana kuna course COED UDOM kati ya wahitimu 118 kachaguliwa mmoja tu,Hapo Kuna course kama BAD,BAED hata mmoja toka mwaka Jana hajaajiliwa.Kwa DUCE-UDSM, BAED 864 hawajui nini hatima yao.Mfano mwingine ni Usahili wa TRA ambapo zaid ya watu 30000 walijitokeza kuwania nafasi 400.Na kila mwaka jobless wanaongezeka sana mtaani.

Yapo makundi mbalimbali yasiyo na ajira na njia mbadala wa kutatua au kupunguza tatizo lakini kwa hili la wahitimu wa vyuo vikuu hizi njia mbili zikitumika nafikiri kwa kiasi flani tatizo linaweza pungua.

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Tiba ya ajira toa huyo rais maana kashindwa kazi ya kuwapa watanzania njia ya kupata ajiral leo hii kageuka kuwa mtoa rushwa mkubwa


Swissme
 
Back
Top Bottom