Tatizo la ajira Tanzania linavyotumiwa kutapeli vijana

Abdul Nondo

JF-Expert Member
Oct 28, 2016
515
2,875
Tar.20/07/2023 siku ya Alhamis saa moja jioni nilipokea simu kutoka moja ya familia huko Kondoa -Dodoma ,wakisema wamepewa namba yangu na mtu kwamba naweza saidia juu ya changamoto yao. Na mimi nilitulia kuwasikia.

Familia hii inasema, mtoto wao mmoja wa kike umri miaka 22 alipata fursa ya ajira kupitia rafiki yake aliyesoma nae chuo, kazi kwenye kampuni moja iliyopo Dar es salaam inayojihusisha na utalii pia na kulea Watoto yatima katika vituo mbalimbali ndani na nje ya nchi na kwamba kampuni hiyo inahitaji wafanyakazi . Nilipouliza kampuni hiyo inaitwaje hata wao Wazazi wa Binti huyo walikuwa hawaijui kampuni hiyo.

Wakaendelea kusema kwamba kampuni hiyo ilihitaji wazazi wa Binti wamlipie Binti nauli kutoka Kondoa hadi Dar es salaam wao watampokea , pia wampe Binti yao fedha taslim Tsh.150,000 , pia wampe debe la mahindi (Unga) na Maharage vyote aende navyo Dar es salaam ili kujianda kabla ya kuanza kazi rasmi .

Wazazi walifanya kama walivyoambiwa , Binti akasafiri hadi Dar es salaam. Huku wazazi wakijua kwamba mtoto wao ameenda kupata ajira, kumbuka Binti huyu ana Elimu ya ngazi ya cheti alisomea mambo ya utalii . Wazazi waliniambia hofu wanayoipata ni kampuni kudai fedha Milion 4, baada ya Binti kufika Dar es salaam,watu wa kampuni inawapigia simu wazazi walipe Milion 4 kwa ajili ya Pasport ,Dollar Account , Malazi na mafunzo ili Binti yao aanze kazi rasmi . Wazazi wakasema wao wana hofu na hiyo kazi na Mtoto wao ni Mgeni Dar es salaam.Hawajui hata anapoishi ni wapi,wanaomba niwasaidie kujua mtoto wao alipo na ukweli wa hiyo ajira/kazi.

Niliomba namba za mtoto wao huyo ,nikaongea nae Jana jioni.Kumuuliza huko alipopokelewa ni wapi na anaishi wapi , ila Binti huyo alisema yeye hapajui na anasema hayupo peke yake kuna vijana zaidi ya 60 wakike na wakiume wamepangishiwa vyumba na kampuni.

Binti alisema yeye amepangishiwa chumba na wenzake wa nne chumba kimoja ila hapajui ni sehemu gani.Ilibidi atafute mtu muenyeji ndiye akanielekeza alipo,lengo ni kuanza kufuatilia kujua ukweli wa hiyo ajira na hiyo kampuni.

Eneo nililoelekezwa ni Mbezi ,eneo la Msakuzi kwa "Paul" kunaitwa Makalimawe . Huko nilikwenda kupata taarifa nyingi zaidi kutoka kwa Binti huyu na vijana wengine kwamba maeneo ya Msakuzi -Makalimawe ndiyo hiyo kampuni inatumia hizo fedha zao TSH 150,000 kuwapangishia vyumba ambapo chumba kimoja ni watu zaidi ya 4 wanaishi na vyakula walivyokuja navyo kutoka kwao Mahindi (Unga)/Mchele na Maharage ndiyo wanatumia kama chakula.

Nilitaka kujua Ofisi ya hiyo kampuni ipo wapi ,wakaniambia Ofisi ipo Mbezi kwa wanaopajua walisema ipo Mbezi kwa Jimmy nikifika kwa Jimmy niulize kwa "Visuti" ndiyo jina maarufu la Ofisi hiyo inaitwa "VISUTI".Vijana hawa wakike na wakiume waliniambia wao huwa wanaenda kila siku saa 4 Asubuhi hadi saa 2 usiku wakipatiwa mafunzo alafu wanarudi walipopangishiwa vyumba vyao huko Msakuzi (Mbezi) kwa mguu , umbali wa kilometa 5.

Nilipouliza jina la Kampuni hiyo walisema kampuni hiyo inaitwa QI-Group Company au Q-NET GROUP na kwamba kujua hasa inajishughulisha na nini hadi mtu alipe hiyo fedha Milion 4 ,ndipo atajua hasa inajishughulisha na nini na ndipo atapata kazi rasmi ,ila mafunzo wanayopewa wao ni kuhusu fursa za biashara,na kuna fursa za kusafiri kwenda nje ya nchi na kufanya kazi nje ya nchi ndiyo maana hela hiyo mil.4 inahitajika ili kulipia Pasport na mambo mengine,ila yote haya na mengine kuhusu kazi watayajua hadi wakilipa fedha hiyo Mil.4.

Binafsi nilishtuka baada ya kuambiwa jina la kampuni hii ni Q-NET ,sababu kampuni hii naijua ni kampuni ya Upatu (Pyramid Scheme) na kitapeli ya Network Marketing ,na kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya watu kutapeliwa na kampuni hii nchini wakiambiwa walipe Milion 4 ili kujiunga kwa kununua bidhaa (Products) ili wapate faida zaidi.Na serikali kupitia Ofisi ya DCI iliwahisema inafanya uchunguzi juu ya utapeli wa kampuni hii tangu 2020 hadi sasa haijulikani kipi kilijiri.

Niliwaambia vijana kadhaa kwamba kama kampuni hiyo ni Q-NET basi waondoke na wasitoe fedha hizo bora fedha hizo wafungue biashara yeyote wafanye kuliko kuwapa sababu wanatapeliwa, mbaya zaidi kuna vijana tayari wameanza kulipa fedha hiyo Milion 4 na kampuni hiyo inapigia simu hadi wazazi wa Vijana hawa Mkoani wakiwasisitiza wajitahidi walipe fedha hiyo Mil.4 hata taratibu taratibu ili kijana apate fursa ya ajira na kazi.

Kinachoniumiza zaidi vijana wengi wakike na wakiume ni wenye Elimu ya Degree,Diploma wengine ngazi ya cheti na wengine kidato cha nne ila wametokea kuamini kampuni hii kiasi ambacho sielewi ,kipi wanachoaminishwa na wengi wao wanatokea mikoani na vijana hawa ni wazito kutoa ushirikiano kama unawauliza kupata taarifa.

Safari yangu iliendelea kutokea Mbezi -Msakuzi , Makalimawe eneo ambalo vijana hawa wamepangishiwa vyumba kwenye nyumba mbalimbali na kuanza kuitafuta hiyo Ofisi ya Q-NET kwa kutumia Bodaboda ,nikimwambia Bodaboda anipeleke kwa Jimmy ,ambapo ni Barabara ya Mpiji-Magoe na ukifika hapo kwa Jimmy ukiuliza kwa "VISUTI" tuu unaelekezwa ,sababu kuna vijana ambao muda wote wamevaa suti ndiyo wanaowapokea vijana hawa kutoka mkoani .

Nyumba ambayo wanasema ndiyo Ofisi ina Ghorofa moja na Geti ,ila hawaruhusu watu wageni kuingia hata kwenda kuonana na uongozi wa Ofisi hiyo,binafsi nilizuiliwa nisiingie hata niliposema nataka kujiunga bado walikataa ,hii ina ashiria ya kwamba wana mtandao wao unaowapa vijana hasa kutoka Mikoani .Nikiwa bado maeneo hayo kuangalia kama nitapata taarifa zaidi ilikuja bodaboda ikiwa na kijana amebeba Maharage na unga hadi Getini ,ili kupata taarifa haraka nilimuuliza kijana huyo anatokea wapi akasema anatokea Sumbawanga amekuja kwenye kampuni hiyo aliambiwa kuna fursa ya ajira, bodaboda aliyembeba kijana yule alisema vijana hao kila siku huwa wanawasili na yeye ndiye wanayemtumia mara nyingi kuwabeba vijana hao kutoka Mikoani ingawa hajui wanakuja kufanya nini na kwa kazi gani.

Kijana huyo alipokelewa na vijana waliovalia "SUTI na TAI"na baadaye kuchukuliwa kupelekwa kwenye Mgahawa ili kunywa chai mtaa wa pili.

Ili bidi niwafuate kwa lengo la kupata taarifa zaidi , Kijana huyo anasema yeye anatokea Sumbawanga akiwa hajui anakuja kufanya kazi gani bali aliambiwa ni fursa ya kazi.Ila kijana mvaa suti kutoka kampuni hiyo ya Q-NET alionesha kuingilia mazungumzo akisema hiyo Milion 4 ni ya kununua Products ili kupata faida zaidi ,huku akiendelea kumuaminisha kijana yule kwamba kampuni hiyo sio ya kitapeli kwani inafahamika kimataifa .

Nimebahatika kushawishi vijana wakiume watatu na wasichana wawili kuondoka kurejea nyumbani,kati ya wasichana hao wawili ,mmoja ni yule niliyepigiwa simu na familia yake kutoka Kondoa , naye ameamua kuondoka.

Rai yangu kwa vijana wenzangu Mjini na vijijini, tuwe makini na aina ya fursa za kazi ambazo tunaaminishwa kupewa , hakuna kazi inayohitaji mtu atoe Milion 4 ili aipate kazi hiyo, vijana wenzangu tuwe makini. Hata kama nchi yetu ina tatizo la ajira ,hili halipaswi kutoandolea umakini katika utambuzi wa fursa za ajira ,hiyo Milion 4 ni bora hata kujiajiri mwenyewe kuliko kumpa mtu kwa tamaa ya kudhani utapata zaidi .

Pia rai yangu kwa serikali, jukumu kuu la serikali ni kulinda ustawi wa Wananchi wake , haiwezekani michezo ya kitapeli namna hii inafanywa bila hatua yeyote kuchukuliwa dhidi ya kampuni za namna hii na watu wake , tayari nimewasiliana na Wizara ya kazi , vijana na Ajira na wamelipokea suala hili kwa hatua zaidi nipo tayari kutoa ushirikiano wowote.Sababu suala hili ni kinyume na sheria zetu za nchi na sheria za kimataifa na inaweza kutafsiriwa kama "Human Trafficking ".

Ahsante.

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo,Taifa.
21/07/2023.

913182154.jpg
922541094.jpg
724028761.jpg
2121117840.jpg
 
Hao vijana elimu yao haijawasaidia hata kidogo, tena bora hao wa certificate nikimkuta mwenye degree ntampiga makofi na mitama
Nchi ya mazuzu hii. Wananchi hawataki kuwawajibisha viongozi wao na badala yake wanatafuta shortcut za kufikia mafanikio.

Anyways siku Tanzania ikija kugeuka kichwa chini miguu juu haitakalika. CCM imeshafikia ukomo wake na viongozi hawajali tena wananchi wanafanya nini.
 
Sijui wanapewaga nini huko hata ukitaka wanasua hawana ushirikiano. Mimi kuna shangazi yangu aliuza shamba kwa siri, akamtumia binti yake mil 3, baada ya mjomba kugoma kumpa hela binti akidai hakuna mantiki anachodai binti.

Mke anadai mjomba hataki binti yake afanikiwe anajali watoto wa mke mdogo.

baadae tena wakadai Mil 2, shangazi ikabidi amuambie mjomba kuna upungufu kwenye biashara yake, akampa. Kuja jua, kumbe alitumiwa binti. Ikapita miezi karibu 6 hakuna cha maana, ndoa mgogoro.

Ikabidi mjomba aanze utaratibu wa kumtoa huko, binti alivyo msnge anawapa taarifa za uongo, mara vijamaa vya hapo ofisini vinapewa simu vinaongea utumbo tu. Yule binti amerudi home mwezi jana, kapauka kama alikuwa machimboni. Hizi vitu ni pure cult.
 
Tar.20/07/2023 siku ya Alhamis saa moja jioni nilipokea simu kutoka moja ya familia huko Kondoa -Dodoma ,wakisema wamepewa namba yangu na mtu kwamba naweza saidia juu ya changamoto yao. Na mimi nilitulia kuwasikia.

Familia hii inasema ,mtoto wao mmoja wa kike umri miaka 22 alipata fursa ya ajira kupitia rafiki yake aliyesoma nae chuo, kazi kwenye kampuni moja iliyopo Dar es salaam inayojihusisha na utalii pia na kulea Watoto yatima katika vituo mbalimbali ndani na nje ya nchi na kwamba kampuni hiyo inahitaji wafanyakazi . Nilipouliza kampuni hiyo inaitwaje hata wao Wazazi wa Binti huyo walikuwa hawaijui kampuni hiyo.

Wakaendelea kusema kwamba kampuni hiyo ilihitaji wazazi wa Binti wamlipie Binti nauli kutoka Kondoa hadi Dar es salaam wao watampokea , pia wampe Binti yao fedha taslim Tsh.150,000 , pia wampe debe la mahindi (Unga) na Maharage vyote aende navyo Dar es salaam ili kujianda kabla ya kuanza kazi rasmi .

Wazazi walifanya kama walivyoambiwa , Binti akasafiri hadi Dar es salaam. Huku wazazi wakijua kwamba mtoto wao ameenda kupata ajira, kumbuka Binti huyu ana Elimu ya ngazi ya cheti alisomea mambo ya utalii . Wazazi waliniambia hofu wanayoipata ni kampuni kudai fedha Milion 4, baada ya Binti kufika Dar es salaam,watu wa kampuni inawapigia simu wazazi walipe Milion 4 kwa ajili ya Pasport ,Dollar Account , Malazi na mafunzo ili Binti yao aanze kazi rasmi . Wazazi wakasema wao wana hofu na hiyo kazi na Mtoto wao ni Mgeni Dar es salaam.Hawajui hata anapoishi ni wapi,wanaomba niwasaidie kujua mtoto wao alipo na ukweli wa hiyo ajira/kazi.

Niliomba namba za mtoto wao huyo ,nikaongea nae Jana jioni.Kumuuliza huko alipopokelewa ni wapi na anaishi wapi , ila Binti huyo alisema yeye hapajui na anasema hayupo peke yake kuna vijana zaidi ya 60 wakike na wakiume wamepangishiwa vyumba na kampuni.

Binti alisema yeye amepangishiwa chumba na wenzake wa nne chumba kimoja ila hapajui ni sehemu gani.Ilibidi atafute mtu muenyeji ndiye akanielekeza alipo,lengo ni kuanza kufuatilia kujua ukweli wa hiyo ajira na hiyo kampuni.

Eneo nililoelekezwa ni Mbezi ,eneo la Msakuzi kwa "Paul" kunaitwa Makalimawe . Huko nilikwenda kupata taarifa nyingi zaidi kutoka kwa Binti huyu na vijana wengine kwamba maeneo ya Msakuzi -Makalimawe ndiyo hiyo kampuni inatumia hizo fedha zao TSH 150,000 kuwapangishia vyumba ambapo chumba kimoja ni watu zaidi ya 4 wanaishi na vyakula walivyokuja navyo kutoka kwao Mahindi (Unga)/Mchele na Maharage ndiyo wanatumia kama chakula.

Nilitaka kujua Ofisi ya hiyo kampuni ipo wapi ,wakaniambia Ofisi ipo Mbezi kwa wanaopajua walisema ipo Mbezi kwa Jimmy nikifika kwa Jimmy niulize kwa "Visuti" ndiyo jina maarufu la Ofisi hiyo inaitwa "VISUTI".Vijana hawa wakike na wakiume waliniambia wao huwa wanaenda kila siku saa 4 Asubuhi hadi saa 2 usiku wakipatiwa mafunzo alafu wanarudi walipopangishiwa vyumba vyao huko Msakuzi (Mbezi) kwa mguu , umbali wa kilometa 5.

Nilipouliza jina la Kampuni hiyo walisema kampuni hiyo inaitwa QI-Group Company au Q-NET GROUP na kwamba kujua hasa inajishughulisha na nini hadi mtu alipe hiyo fedha Milion 4 ,ndipo atajua hasa inajishughulisha na nini na ndipo atapata kazi rasmi ,ila mafunzo wanayopewa wao ni kuhusu fursa za biashara,na kuna fursa za kusafiri kwenda nje ya nchi na kufanya kazi nje ya nchi ndiyo maana hela hiyo mil.4 inahitajika ili kulipia Pasport na mambo mengine,ila yote haya na mengine kuhusu kazi watayajua hadi wakilipa fedha hiyo Mil.4 .

Binafsi nilishtuka baada ya kuambiwa jina la kampuni hii ni Q-NET ,sababu kampuni hii naijua ni kampuni ya Upatu (Pyramid Scheme) na kitapeli ya Network Marketing ,na kumekuwa na malalamiko ya muda mrefu ya watu kutapeliwa na kampuni hii nchini wakiambiwa walipe Milion 4 ili kujiunga kwa kununua bidhaa (Products) ili wapate faida zaidi.Na serikali kupitia Ofisi ya DCI iliwahisema inafanya uchunguzi juu ya utapeli wa kampuni hii tangu 2020 hadi sasa haijulikani kipi kilijiri.

Niliwaambia vijana kadhaa kwamba kama kampuni hiyo ni Q-NET basi waondoke na wasitoe fedha hizo bora fedha hizo wafungue biashara yeyote wafanye kuliko kuwapa sababu wanatapeliwa, mbaya zaidi kuna vijana tayari wameanza kulipa fedha hiyo Milion 4 na kampuni hiyo inapigia simu hadi wazazi wa Vijana hawa Mkoani wakiwasisitiza wajitahidi walipe fedha hiyo Mil.4 hata taratibu taratibu ili kijana apate fursa ya ajira na kazi.

Kinachoniumiza zaidi vijana wengi wakike na wakiume ni wenye Elimu ya Degree,Diploma wengine ngazi ya cheti na wengine kidato cha nne ila wametokea kuamini kampuni hii kiasi ambacho sielewi ,kipi wanachoaminishwa na wengi wao wanatokea mikoani na vijana hawa ni wazito kutoa ushirikiano kama unawauliza kupata taarifa.

Safari yangu iliendelea kutokea Mbezi -Msakuzi , Makalimawe eneo ambalo vijana hawa wamepangishiwa vyumba kwenye nyumba mbalimbali na kuanza kuitafuta hiyo Ofisi ya Q-NET kwa kutumia Bodaboda ,nikimwambia Bodaboda anipeleke kwa Jimmy ,ambapo ni Barabara ya Mpiji-Magoe na ukifika hapo kwa Jimmy ukiuliza kwa "VISUTI" tuu unaelekezwa ,sababu kuna vijana ambao muda wote wamevaa suti ndiyo wanaowapokea vijana hawa kutoka mkoani .

Nyumba ambayo wanasema ndiyo Ofisi ina Ghorofa moja na Geti ,ila hawaruhusu watu wageni kuingia hata kwenda kuonana na uongozi wa Ofisi hiyo,binafsi nilizuiliwa nisiingie hata niliposema nataka kujiunga bado walikataa ,hii ina ashiria ya kwamba wana mtandao wao unaowapa vijana hasa kutoka Mikoani .Nikiwa bado maeneo hayo kuangalia kama nitapata taarifa zaidi ilikuja bodaboda ikiwa na kijana amebeba Maharage na unga hadi Getini ,ili kupata taarifa haraka nilimuuliza kijana huyo anatokea wapi akasema anatokea Sumbawanga amekuja kwenye kampuni hiyo aliambiwa kuna fursa ya ajira, bodaboda aliyembeba kijana yule alisema vijana hao kila siku huwa wanawasili na yeye ndiye wanayemtumia mara nyingi kuwabeba vijana hao kutoka Mikoani ingawa hajui wanakuja kufanya nini na kwa kazi gani.

Kijana huyo alipokelewa na vijana waliovalia "SUTI na TAI"na baadaye kuchukuliwa kupelekwa kwenye Mgahawa ili kunywa chai mtaa wa pili.

Ili bidi niwafuate kwa lengo la kupata taarifa zaidi , Kijana huyo anasema yeye anatokea Sumbawanga akiwa hajui anakuja kufanya kazi gani bali aliambiwa ni fursa ya kazi.Ila kijana mvaa suti kutoka kampuni hiyo ya Q-NET alionesha kuingilia mazungumzo akisema hiyo Milion 4 ni ya kununua Products ili kupata faida zaidi ,huku akiendelea kumuaminisha kijana yule kwamba kampuni hiyo sio ya kitapeli kwani inafahamika kimataifa .

Nimebahatika kushawishi vijana wakiume watatu na wasichana wawili kuondoka kurejea nyumbani,kati ya wasichana hao wawili ,mmoja ni yule niliyepigiwa simu na familia yake kutoka Kondoa , naye ameamua kuondoka.

Rai yangu kwa vijana wenzangu Mjini na vijijini, tuwe makini na aina ya fursa za kazi ambazo tunaaminishwa kupewa , hakuna kazi inayohitaji mtu atoe Milion 4 ili aipate kazi hiyo, vijana wenzangu tuwe makini. Hata kama nchi yetu ina tatizo la ajira ,hili halipaswi kutoandolea umakini katika utambuzi wa fursa za ajira ,hiyo Milion 4 ni bora hata kujiajiri mwenyewe kuliko kumpa mtu kwa tamaa ya kudhani utapata zaidi .

Pia rai yangu kwa serikali, jukumu kuu la serikali ni kulinda ustawi wa Wananchi wake , haiwezekani michezo ya kitapeli namna hii inafanywa bila hatua yeyote kuchukuliwa dhidi ya kampuni za namna hii na watu wake , tayari nimewasiliana na Wizara ya kazi , vijana na Ajira na wamelipokea suala hili kwa hatua zaidi nipo tayari kutoa ushirikiano wowote.Sababu suala hili ni kinyume na sheria zetu za nchi na sheria za kimataifa na inaweza kutafsiriwa kama "Human Trafficking ".

Ahsante.

Abdul Nondo.

Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana ACT Wazalendo,Taifa.
21/07/2023.View attachment 2695356View attachment 2695357View attachment 2695358View attachment 2695359
Hawa ni muda mrefu sana wapo mitaa yetu ya msakuzi huku alafu wte wanaonekana washamba hizo degree zao uchwara kbs,

huwa siku za jmoc unawaona wanaongozana rundo barabarani wakiwa wamevalia suti zao nyeusi km majambazi mchana jua Kaliiiii

ukiwaangalia nyuso zao wanaonekana kuridhishwa kwa ahadi kibao na nono na wengi nimewaangalia na kuwafuatilia ni wenye asili za kutoka dodoma, babat,masai
 
Back
Top Bottom