Milima ya Uluguru
New Member
- Nov 3, 2019
- 2
- 3
BOMU LA AJIRA KWA VIJANA ALILOLIONA EDWARD LOWASSA.
Leo 15:15pm,03/11/2019.
•Ajira isiyotoa kipato cha kuridhisha.
•Ajira isiyokidhi matarajio.
•Ukosefu wa ajira jumla.
Sera zetu za kielimu,kiuchumi,kibenki na kijamii na pengine mifuko mingi kwa ajili ya kuongeza ajira inawaandaa vijana wengi kuwa wachuuzi badala ya kuwaandaa kuwa wazalishaji.Nachukizwa sana nikimuona kijana mwenye nguvu akizungusha karanga na jioni faida anapata 1,000 ikiwa ametembea Dar es Salaam yote.
Leo Wazambia,Wamalawi hawauzi karanga kuzunguka Lusaka au Lilongwe bali wanavuka mpaka wa Nakonde na Tunduma kuja kununua bidhaa hapa Tanzania na kwenda kuuza kwao na wanashangaa wakifika hapa na kutukuta tunauza karanga barabarani wakati tuna Bandari,Uwanja wa Ndege,barabara nzuri na Ardhi yenye rutuba,hatuna akili.
Naamini kama tungekuwa na watu Milioni kumi wenye akili ya kibiashara kama za Wakongwe awa wa biashara mfano wa Lowassa,Balabuu,Mo Dewji,Bhakhresa,Mengi,Asas basi Tanzania ingekuwa kama Israel, China ama Marekani awa ni "Business Oriented" na pia ni "Profit Oriented" kama walivyo Wakinga kutoka Njombe na Wachaga kutoka Kilimanjaro.
Nitoe mfano tu,kuna sekta kama ya ngozi, vijana wakiandaliwa vizuri uzalishaji wa kutengeneza viatu ni shughuli isiyohitaji mtaji mkubwa,Vijana wangepata ujuzi na na kutazama soko liko wapi na linahitaji nini? Kumbuka kuna Wazambia zaidi ya 500 kila mwezi wanafika Kariakoo kutafuta bidhaa yoyote ya kwenda kuuza kwao.Kariakoo kwao ni kama Dubai.
Toka Tunduma wanapita Mbeya,Iringa hadi Morogoro,Safari ndefu wanashangaa bure Nchi yetu,Wanapita Mikumi,wanamuona Simba na Twiga bure,
Kariakoo ndogo iliyopaswa kuwepo Morogoro haipo,Viongozi wa Mkoa wa Morogoro bado wamelala hawajaiona changamoto hiyo na kuifanya kuwa fursa ambayo ingetoa ajira kwa Vijana wengi.
Wamalawi,Wazambia zaidi ya 100 wanapita Morogoro kila mwezi kuja Kariakoo,Jijini Dar es Salaam ambapo naamini Soko la Kimataifa linalojengwa Morogoro lingeweza kuwa na Bandari kavu ili liweze kuhudumia na kupunguza kila kitu kuwepo Kariakoo tu.
Wamalawi zaidi ya 400,Wakongo zaidi ya 300,Wazimbabwe zaidi ya 200,Msumbiji zaidi ya 100,Warwanda na Waburundi zaidi ya 100,Wakenya na Waganda zaidi ya 50.Awa wote ni soko zuri la bidhaa yoyote bora itakayotengenezwa hapa Tanzania.
Kama Wafanyavyo Magereza,Serikali kupitia Veta ingetenga eneo moja ingenunua machine zote mfano za kutengeneza samani kuanzia kuranda, kuchana, moulding n.k. na wangeruhusu vijana wenye ujuzi kufanyia kazi zao kwenye hiyo karakana kwa makubaliano kila kazi inaandikishwa na ikikamilika kabla ya kutoka inalipiwa "machine charge".
Ni kundi kubwa sana lingefaidika na uwekezaji huo na pia vipaji vingeonekana na kulifaidisha Taifa pengine tungegundua bidhaa nyingi za kuuza nje ya nchi kuingiza pesa za kigeni na kuongeza ajira kwa vijana pindi demand ama hitaji linapokuwa kubwa na kuhitaji Supply kuwa kubwa.
-Mkokotenge wa Muktadha wangu kuhusu Bomu la Ajira.
Kimkokotenge namaanisha kuwa kwa Tanzania na Afrika kuna changamoto nyingi sana ambazo ndio zilitakiwa zilete ajira kwa Vijana wetu.
Yaani nchi kama Marekani,Uingereza, Norway au Canada huko ambako ndio wasio na ajira wanazamia, huko ndiko kulitakiwa kuwe na tatizo la ajira, sababu changamoto zote almost zipo covered.
Huko hakuna tatizo la madaktari, madarasa, umeme, hospitali wala barabara, sasa wasomi watapata vipi ajira?
Ila Tanzania kuna tatizo la madaktari, walimu, maji, umeme, usafiri, zahanati n.k lakini madaktari, mainjinia, walimu, madereva n.k hawana ajira.
Sasa kwa lugha ya kimkokotenge ni kuwa Tanzania hatuna ukosefu wa ajira, bali ukosefu wa akili.
-Niilaumu Awamu ya tatu na ya nne kwa kulitengeneza Bomu hili.
Tuanze na awamu ya tatu, baada ya kubinafsisha mashirika mengi ya Umma, waliopewa dhamana wakaua Viwanda kabisa, Majengo ya makampuni mengi yakawa Magofu, Wizi wa vipuri ukatamalaki,Vipuri vikageuzwa chuma chakavu,Majengo na Viwanja vikakopewa kwenye mabenki na walipochukua mikopo walipeleka pesa sehemu nyingine badala ya kuendeleza Viwanda.
Hivyo hivyo kwenye mashamba mbali mbali, mengi hayakuendelezwa yalitumika kama mortgage ya kukopea benki.
Awamu ya nne, vijana wengi walihusudu wizi sana kuliko kujibiidisha na kazi, utapeli kila kona ulitamalaki, waliotapeli kupitia madini ndio walikuwa kifua mbele kuwa wafadhili wa chama, waliojihusisha na madawa ya kulevya ndio walikuwa wanachagua viongozi wa ngazi fulani fulani.
Wizi wa bandari ulikuwa na baraka zote, vijana wa bandarini ndio walikuwa watesi wa vijana wanaojitegenea kiasi kwamba kila mmoja aliitaka clearing and forwarding ili naye aibe.
Hawa vijana waliwakatisha wengine tamaa.Hela walioiba na kuja nayo Mtaani ikaua vipaji vya vijana wengi na kuwakatisha tamaa,Watu wakaona aibu kujiajiri na hata kuwa Wakulima, Kazi ya kuajiliwa ikaonekana ndio bora zaidi kuliko ya kujitegemea.
Ardhi yenye rutuba imejaa tele nchi nzima vijana hawa hawataki kwenda kuitumia ili kujitengenezea kipato.Vijana wanang'ang'ania kukaa mijini ili waendelee kujamiiana. Mikoa ya Tabora, Katavi, Tanga na Songea ardhi hutolewa bure kabisa.
Siku nikiwa Rais wa nchi hii, itakuwa ni kosa la jinai mtu kutamka ama kuandika kwamba Tanzania kuna tatizo la ajira ilihali tuna tatizo la changamoto kuigeuza fursa.Tukumbuke tuna bandari,barabara,Uwanja wa ndege na ardhi nzuri yenye rutuba.
Tanzania ina soko huru la ajira. Serikali na sekta binafsi zinaendeshwa zikitegemea kiasi fulani tu cha rasilimali watu. Ndio maana kuongeza nafasi ajira inapaswa kuongeza biashara (mzunguko wa pesa).
Makontena ya graduates ni makubwa mno kuliko nafasi zilizopo. Serikali haiwezi kwa namna yoyote ile kuongeza ajira yenyewe.
Inachoweza ni kutengeneza mazingira mazuri ya kuongezeka shughuli za kiuchumi (ila sio zisizo rasmi).
Kwa akili zetu za sasa hata tulie usiku na mchana tatizo la ajira haliwezi kuisha kwa sababu watu wengi wana-invest muda wao kujitayarisha kuwa waajiriwa, huku nafasi za ajira ni Mathematically impossible kukua kwa rate hiyo hiyo.
Soko la ajira ni kama soko jingine tu.Utakuta mtu anafurahia pesa yetu ya shilingi kukosa thamani dhidi ya dola ya Marekani ilihali atakuwa anafurahia kuongezeka kwa tatizo la ajira hapa Tanzania,
Ni suala la demand and supply. Hata Serikali ifanye vipi, halitatuliki kama watu hawaelewi kuwa hawakuzaliwa kuajiriwa (kupewa), bali kutafuta.
Serikali inao wajibu kwani wao ndio watunga Sera watunga sheria na watengeneza kanuni lakini Ajira ni tatizo la ulimwengu mzima na haliwezi kupatiwa ufumbuzi na Serikali tu bila kuhusisha sekta binafsi na pengine kuhusisha akili za kibiashara za mtu mmoja mmoja kuzaa mawazo yatayotengeneza ajira kwa Vijana wengi zaidi.
-Muarobaini wa tatizo la Ajira Tanzania.
Ajira ni tatizo Sugu na sio kwamba limeanza awamu hii ya tano,lilikuwepo mda na kadri siku zinavyoenda linazidi kuwa kubwa sana.
Naamini serikali haiwezi ikatoa ajira kwa wote na haitatokea na kwa hizi products za vyuo kadri zinavyozidi kuongezeka na ukiangalia Serikali imesitisha ajira hata serikali iseme inatoa ajira kiasi gani bado haitaweza kumaliza.
Ni kweli ajira sio lazima uajiriwe na serikali au taasisi binafsi.Nini hasa kinamfanya kijana ashindwe kujiajiri?
•Mfumo wa Elimu.
Elimu yetu inatosha kumfanya mhitimu wa chuo kikuu kujiajiri?Hapa sijazungumzia diploma na certificate. Mitaala yetu ya Elimu inakitu chochote cha kumfanya mhitimu akajiajiri?.
Kwa mfano mtu kamaliza Bachelor of education with Psychology au bachelor of Art in Education. Hawa ni waalimu kitaaluma,Je wana elimu yoyote ya ujasiliamali kusema ikawasaidie nje ya mfumo wa Ajira za serikali au sekta binafsi?
Asilimia 99 huyu mhitimu elimu yake imejikita katika kufundisha na kukabiliana na matatizo yanayoizunguka jamii kama jinsi ya kutatua migogoro nk.
Hapa hamna elimu yoyote kuhusu kutambua fursa zinazomzunguka,jinsi gani azitumie yaani elimu nzima ya ujasiliamali hamna.
Leo unamwambia ajiajiri,anaanza vipi?Hana elimu yoyote ya biashara, kilimo hata kutengeneza kiti tu hawezi.Miaka mitatu yote chuo Anafundishwa kusoma psychology ya mwanafunzi,mara kuandaa lesson plan nk.Anafika mtaani unamwambia jiajiri,Wapi na wapi!?
-Mtaji umekuwa Wimbo wa Vijana.
Ni ukweli usiopingika licha ya wengine kujua fursa zinazowazunguka na jinsi gani wazitumie,bado suaa la mtaji huwa ni tatizo sana.
Ni ukweli uliowazi Serikali haiwezi kumpa kila mtu mtaji ajiajiri. Lakini bado Serikali inaweza buni njia kuhakikisha mhitimu akimaliza Chuo anapata mtaji endapo hata ajiriwa aweze kujiajiri.
Kwa upande wangu ningeshauri Katika Hela ya kujikimu anayopewa Mwanafunzi chuoni,asilimia flani iwe inakatwa na kuingizwa katika mfuko maalumu ambapo huyu mwanafunzi akihitimu anapewa kama mafao yake ambayo yanaweza msaidia kujiajiri na kuanza maisha mapya.
Mfano Katika mwaka wa masomo mwanafunzi anapokea fedha ya kujikimu mara nne yaani sio chini ya 2Millions. Ambapo kila baada ya miezi miwili hupokea laki 5 na mwaka wa masomo ni miezi 8.Akawa anakatwa tufanye 50000 kila akiingiziwa hela,kwa mwaka wa kwanza ni laki 2 miaka mitatu laki 6.Laki 6 kwa mtu aliyeelimika na anaelimu ya ujasiliamali anaweza Fanya kitu na hata kama sio peke yake bado anaweza kuunda kikundi na wenzie wakafanya vitu vya maana sababu kila kitu wanacho.
-Sera za Ajira zilizopata kuwepo na zikashindwa.
Uchumi wetu umeshindwa kutengeneza ajira zenye tija inawezekana tatizo ni sera zetu na mikakati yetu kama mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini.
Pamoja na serikali kuwa na program na mikakati mbalimbali iliyolenga kuwawezesha wananchi wenye vipato vya chini kupitia Baraza la Taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi lililoundwa kwa sheria Na 16 ya mwaka 2004.likiwa na dhamana ya kusimamia,kuratibu shughuli zote za uwezeshaji wananchi.
•Tulipata kuwa na Mfuko wa wajasiriamali.
•Mfuko wa Maendeleo ya vijana.
•Mabilioni ya Jk,
•Mfuko wa uwezeshaji wananchi kiuchumi.
•Mfuko wa uwezeshaji wa wajasiriamali.
•Mfuko wa maendeleo ya vijana.
•Mfuko wa pembejeo za kilimo.
•Mfuko wa wanawake
•Mfuko wa uwezeshaji wa wajasiriamari wadogo wadogo
•Mfuko wa maendeleo ya jamii.
Sera ya Mkakati wa kukuza uchumi na kupunguza umaskini (MKUKUTA
Mpango wa kurasimisha mali na biashara (mkurabita),
Mpango wa kuboresha mazingira ya biashara (mkumbita)
Lakini bado kuna changamoto ya walengwa (targeting group ) ili kuwasaidia wanaohusika pesa hizi zinapelekwa kwenye makundi/watu machache pia kukosekana kwa chombo maalum cha kusimamia mikakati hii (target gruop)
Pia pamoja na kuwepo kwa utitiri wa mabenki hapa nchini karibu zaidi ya 45 bado wananchi maskini wa vijijini na mijini sio marafiki wa mabenki haya kwani hawajanufaika na huduma za mabenki kutokana kuwa na viwango vikubwa vya riba na masharti magumu pia kutokana na kutokuwepo kwa sheria ya saccos (saccoss act)
Zimeanzishwa saccoss nyingi sana ambazo zimewatia matatizoni wananchi wengi kwa kuuziwa mali zao kutokana na hizi saccoss kuwa na riba kubwa na masharti magumu.
Nchini Kenya mwaka 2014 katika bajeti yake ya Ksh trilioni 8.1 2014/2015 ilitenga ksh bilioni 1.8 sawa na sh. bilioni 32.4 za kitanzani kwa ajili ya mikopo kwa vijana kupitia mfuko wa vijana.
Mfuko huo ulisimamiwa na baraza la vijana Taifa la kenya (the national youth council of kenya) na wizara husika.
Je Tanzania kwenye bajeti yetu tunatenga shilingi ngapi kwa ajili ya Vijana na zinaweza kusimamiwa na naniii????
Ajira ni shughulk yoyote ya halali inayompatia mtu kipato.
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB) na Shirika la kazi Duniani (ILO) Tatizo la ukosefu wa ajira tunaweza kulitazama katika namna tatu (3) ambazo
1.Ajira isiyotoa kipato cha kuridhisha.
2.Ajira isiyokidhi matarajio.
3.ukosefu wa ajira jumla (jobless).
•Ajira isiyotoa kipato cha kuridhisha.
Katika Sekta binafsi hivi sasa hakuna namna,Mwajiri anakupangia tu Mshahara anaotaka yeye kama hutaki basi njia nyeupe uondoke.
Hivi sasa Mwajiri anasema biashara hailipi anavunja mkataba wako wa Permanent anakupa mkataba wa Mwaka au miezi sita ili akikufukuza asikulipe.
Mjasiriamali hana bidhaa yenye uhakika wa soko,Asubuhi ataiza mihogo ya kutafuta barabarani akisema inaongeza nguvu za kiume,na wengine wakiuza karanga akianzia Kinondoni,Ubungo,Ilala na kurudi Kinondoni bila faida.
•Ajira isiyokidhi matarajio.
kundi hili linajumuishwa kwenye kundi la ukosefu wa ajira japo linataka kufanana na kundi la kwanza ila tofauti yake ni hili kundi la wafanyakazi wanaofanya kazi halali za kutumia Taaluma,ujuzi,kipaji, nguvu na maarifa waliyonayo katika kufanya kazi lakini malipo wanayopata hayakidhi matarajio yao.
Mfano wa wafanyakazi katika kundi hili ni kama: wafanyakazi wa Majumbani,bar,hoteli,migahawa,walinzi binafsi,wafanyakazi wa migodini,viwandani,makampuni binafsi, Madereva wa vyombo vya moto mfano Malori,Mabasi,Magari binafsi,n.k
wafanyakazi awa asilimia 80 (80%) wanafanya kazi bila mikataba ya kazi.
Athari yake hulipwa mshahara kidogo pili huwa hatarini kupoteza maslahi yao pindi ajira yao inapositishwa ghafla au kufariki pengine kukosa fursa ya kujiunga kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii (social security) kwa maslahi yao ya baadae.
Hapa pia kuna kundi la wafanyakazi wa vipaji kama: Wasanii wa Muziki,Filamu,Ngumi,Mpira,vichekesho,Sarakasi,Mitindo n.k hawa wanafanya kazi kubwa lakini ujira wa kazi zao haukidhi matarajio yao kutokana na urasimu,
Wizi wa kazi zao au kunyonywa na wadhamini wao.
katika kundi hili pia hata wafanyakazi wa Serikali huangukia kundi hili kama: Walimu, wauguzi, wafanyakazi kwenye mashirika ya Umma,n.k.
Wafanyakazi hawa hufanya kazi kwa kujituma ili wapate ujira utakaokidhi matarajio yao lakini hali huwa tofauti kwani ufanya kazi hadi uzeeni bila kuwa na maisha yenye maendeleo kama matarajio yao kutokana na mishahara kidogo kulinganisha na hali halisi ya uchumi wa wakati husika pengine hali iliyochangiwa na mfumuko wa bei,thamani ya shilingi, n.k
•Ukosefu wa Ajira jumla(Jobless).
Kwa Taarifa ya shirika la kazi duniani ya mwelekeo wa ajira kwa vijana ulimwenguni [GrobaL EmpLoyment Trend for youth] inaonesha kuwa Tatizo la ajira kwa vijana Tanzania wenye elimu kuanzia sekondari na kuendelea ni kubwa kuliko wale wenye elimu ya kiwango cha chini.
Aidha watanzania wenye elimu za chini wamepata ajira lakini ajira zao ni duni ama kipato cha chini na za mazingira hatarishi kama sehemu mojawapo ya kuwatumikisha kwa kuwa uelewa wao juu ya masuala sheria na taratibu za kazi ni mdogo.
Hii ni ishara kuwa pamoja na Taifa kuzalisha wasomi wa ngazi za juu kwa idadi kubwa lakini bado soko la ajira halijawapokea wasomi hao wengi wao wapo mitaani wanataabika.
Serikali unaweza kugeuza jicho lake na kuangalia Sekta ya kilimo,ufugaji,uvuvi, huduma(hoteli,migahawa,bodaboda,n.k), biashara(machinga,mamantilie,wafanya biashara wadogo na wakubwa) na kuzifanya kuwa Sekta rasmi za Ajira.
Mfano Kilimo Tanzania imejaliwa kuwa na hekta millioni 44 za ardhi inayofaa kwa kilimo kwa Mvua ya Uhakika lakini ni asilimia 23 tu ndiyo inayotumika.
Lakini pia Tanzania ina hekta millioni 29 zinazofaa kwa kilimo cha umwagiliaji na maji ya kutosha yapo lakini ni asilimia 1 (1%) tu ndiyo iliyo chini ya umwagiliaji.
karibu asilimia 70 (70%) ya ardhi ya ukulima wa mazao inalimwa kwa kutumia jembe la mkono, asilimia 20 kwa kutumia maksai na asilimia 10 kwa kutumia trekta.
Wakati huo bado kilimo kinategemea kwa kiasi kikubwa mvua. pamoja na serikali mwaka 2010 kutangaza program yake ya "kilimo kwanza" bado sekta hii inakabiliwa na changamoto kubwa sana kana kwamba "Kilimo Kwanza" iliferi.
Program ya kilimo inayofaa ni ile ambayo inazingatia kutenga si chini ya asilimia 12 (12%) ya bajeti kwa ajili ya kilimo kuendana na maamuzi ya viongozi wa nchi za umoja wa jumuiya ya maendeleo ya nchi za Afrika kusini (SADC) yaliyotolewa nchini Msumbiji Mwaka 2014 al maarufu makubaliano ya maputo (maputo protocal).
Ufugaji na uvuvi: Tanzania ni nchi ya pili Afrika baada ya nchi ya Sudan (Sudan kusini ikijumuishwa) kuwa na wingi wa mifugo wakati tunapata uhuru tulikuwa na mifugo karibu milioni 8 na sekta ya ngozi ilikuwa ni ya 5 katika mazao muhimu iliyoliinglizia Taifa fedha za kigeni kutokana na mauzo nje ya nchi.
Hivi sasa nchi yetu ina ng'ombe zaidi ya milioni 23,Mbuzi zaidi ya Milioni 16, Kondoo zaidi ya Milioni 7 na kuku zaidi ya milioni 38.
Bahati mbaya thamani ya mifugo mingi kiasi hicho haijajitosheleza kibiashara na mchango wa sekta hii katika pato la Taifa kwa sasa ni mdogo sana ukilinganisha na miaka ya nyuma.
Uvuvi: Tanzania ina pwani yenye rasilimali nyingi ya uvuvi.ina mwambao wa bahari wenye kilomita za mraba 64,000 pamoja na kilomita nyingine za mraba 223,000 za eneo la uvuvi bahari ya Hindi nchi yetu ina maziwa, Bahari, mito na mabwawa kama chanzo cha uvuvi.
Lakini sehemu kubwa ya samaki wanaovuliwa hutumika ndani ya nchi kama kitoweo na kiasi kidogo husafirishwa nje ya nchi. Tanzania bado haijatumia ipasavyo hazina yake kubwa iliyojaliwa na Mungu katika sekta ya uvuvi.
-Ushauri wangu na Suluhisho la Ukosefu wa Ajira.
Mfumo wa elimu lazima ufumuliwe upya ili elimu inayotolewa kwa wanafunzi iendane na mahitaji ya nyakati za sasa za kijamii, kiuchumi na kisiasa hasa upande wa mitaala.
Elimu isimamiwe na chombo kimoja,Pia ni muhimu tuwe na mjadala wa kitaifa juu ya lugha ya kufundishia mimi nina mapendekezo mawili katika hili.
•1-tunaweza kubadilisha mitaala yetu ya shule za Awali na msingi lugha ya kufundishia ikawa ni english kama shule za Academic (private).
Kuanzia darasa la kwanza ili kuondoa tatizo la wanafunzi wanapoanza kidato cha kwanza kutumia muda mwingi kujifunza lugha mpya ya english kutafsiri maarifa suala ambalo limekuwa gumu kuwapelekea kukariri kile alichoandika mwalimu badala ya kuelewa [The students are not called upon to know but to memorize the contents narrated by teacher].
•2- Tunaweza kufundisha masomo yote kwa lugha ya kiswahili na lugha ya english ikawa ni lugha ya lazima kunzia chini hadi chuo kama lugha ya mawasiliano duniani na tunaweza kujifunza kutoka China,kwa sababu China hawauzi kichina au Japan hawauzi kijapani wanauza ujuzi na maarifa.
Wanafunzi wetu wameshindwa kupata maarifa na ujuzi kwa sababu ya lugha lazima tuchukue maamuzi magumu na ya haraka ili kulinusuru Taifa letu.
•Elimu ya ujasiliamali mdogo mdogo
•Mikopo katika makundi madogo madogo isiyo na riba.
•Msaada wa kisheria kulinda kazi zao (baraza la Taifa la vijana).
•Sera ya ajira ipitiwe upya na zile kazi ambazo zinaweza kufanywa na wazawa zilindwe kwa nguvu ya kisheria na kisera na hapa kinahitajika chombo makini cha kusimamia hilo.
Wafanyakazi wa majumbani,bar,migahawa,madereva, hoteli, hawa lazima wafanye kazi kwa mikataba iliyosainishwa serikali za mitaa kwa kuwa wanatoka sehemu mbalimbali ili mishahara yao ijulikane ni kiasi gani wanalipwa,
Pindi wanaposimamishwa kazi au kufariki watakuwa na nguvu za kisheria kudai malipo yao tatu watakuwa na fursa ya kujiunga na kunufaika na mifuko ya hifadhi ya jamii (social security)
Mfano wafanyakazi wa ndani,bar,migahawa akifanya kazi yenye malipo ya mshahara angalau wenye kima cha chini kabisa sh laki moja (100,000) kwa mwezi baada ya miaka 3 atakuwa na kiasi cha milioni tatu na laki sita huyu mtu tayari atakuwa na mtaji anaweza kufungua bar,mgahawa wa kwake mwenyewe au biashara yoyote.
Nimalizie kwa kuitolea mfano nchi ya Nigeria,Sekta ambayo inafuatia katika kuchangia pato la Taifa GDP ukiondoa sekta ya Mafuta na ya Mawasiliano,
Sekta ya muziki na filamu za Nollywood ndiyo inafuata baada ya kuirasimisha sekta hiyo toka Sekta isiyo rasmi hadi kuwa Sekta rasmi.
Inahitajika mikakati ya kisera na kisheria mfano hapa kwetu wasanii kila siku wanalia njaa tuu na nchi haipati chochote.
Suala la kisera kwa mfano viwanda vya sukari vijishughulishe na uzalishaji wa sukari tu suala la kuzalisha miwa wapewe wawekezaji wadogo au Serikali iwe na mashamba yake yatayotoa ajira kwa Vijana.
Watu binafsi wawe na Mashamba ya uhakika na sio leo unazalisha tani kumi na kesho ukiombwa tena tani kumi unasema huna,Sasa nani ataamini Uzalishaji wako wa kusuasua.
Lakini pia Viwanda siyo maua vinategemea uzalishaji na soko.
Nimalizie kwa kusema kama nchi inaimport mchele wakati huko Mbeya,Shinyanga wanahangaika na soko la mchele,
Kama nchi inaimport mafuta ya kula wakati wakulima wa alzeti singida wanahangaika na soko la mafuta yao,Kama Nchi inaangaika inaimport nyanya wakati nyanya za Morogoro ni nzuri.bila shaka uzalishaji utashuka sana,
Kama nchi inaimport nyama ya kuku kwenye supermarket unategemea nini hawa watu wetu watahimili ushindani sokoni.
pia.Ni wakati Sasa Mtanzania kuchukua fursa,
Changamoto tulizonazo ni ishara bado kuna soko la ajira hadi pale changamoto zitakapoisha.
Nikiishia hapa,Mimi ni,
Msemakweli Chakubanga.
Dar es Salaam.
0755078854.