Hivi ibada ya kiislamu haikamiliki mpaka unapoamua maamuzi ya Ndoa? hasa hasa mirathi? au ndio janja ya wachache katika juhudi za kuwakweza akina mama? Kwa ninavyo jua Suala kama hili linaweza kuamuliwa kwenye mahakama za kawaida kwa kufuata sheria hizo hizo za kiislamu, maana sheria zinazo tambulika ni za kimila ikiwa umeamua ndoa yako iamuliwe hivyo, au hizi zinazopitishwa na bunge au za dini, inategemeana na ulivyo andikisha utashi wako au kama hukuandikisha , basi mahakama itaangalia ulikuwa unaishi kufuatana na misingi ipi? kwa mfano kuna waislamu wengine kutokana na experience or exposure ya maisha ya sasa kesi zao wasingependa kuamuliwa kwa misingi hiyo je hao watawekwa upande gani? Aidha Mwanaume au awe Mke.
Maana siku hizi ndugu wamekaa mkao wa kula na si kusimamia Mirathi wala nini?
Naomba rafiki yangu Mkandara na GT naomba mnieleweshe hapa na hata mwana zuoni yoyote mwenye ilimu na mambo hayo ya kadhi.
Maana siku hizi ndugu wamekaa mkao wa kula na si kusimamia Mirathi wala nini?
Naomba rafiki yangu Mkandara na GT naomba mnieleweshe hapa na hata mwana zuoni yoyote mwenye ilimu na mambo hayo ya kadhi.