Kinachobainishwa hapo ni kuingiza mfumo wa mahakama ya kadhi ndani ya mfumo wenu wa Mahakama ili kusilete mgongano wa maamuzi yake na mahakama za kawaidia kama walivyoweka hata wenzenu Kenya.
Nitakupa mfano mdogo sana wa mabaraza ya ardhi ya kata na mahakama za mwanzo. haya hayaingiliani katika mamuzi sababu yamewekwa pale kisharia. Sasa kwanini unakwepa mahakama ya kadhi.
Mimi naamini wazi watakao pata hudima kwenye mahakama hizi ni raia wa Tanzania kama walivyo raia wengine wa Tz na hivyo kupunguza msongamano wa kesi nyyingi sana za madai kama talaka na miradhi katika mahakama zenu.
Suala langu hapa. Je Serikali ya JMTz ipo tayari kuwalipia wa TZ kama raia wake watakaoamua kutumia mahakama hizi kutafuta haki zao?
Fungukeni kiakili na mjitoe katika mental slavery.
walisema huyo muislamu mwenzetu atatusaidia sasa kawachinjia baharini...............................[/QUOTE
Sio Maaskofu waliosema kuwa ni chaguo la Mungu???
Poor thinking.....hivi ardhi ni ya dini gani.Ingawa waswahili husema ASIYEJUA MAANA USIMFUNZE MAANA lakini mimi nitavunja mwiko huo kwa kukujuza.
Mahakama ya Ardhi inashughulikia masuala yanayohusiana na mambo ya ardhi tu na si vinginevyo.
Mahakama ya kadhi itashughulikia masuala ya waislam hususan mirathi, talaka n.k na si vinginevyo.
Mahakama ya Biashara halikadhalika inashughulikia masuala yanayokhusu biashara tu.
Sasa kama una hoja , karibu.
Kuanzishwa mahakama y kadhi ndani ya dola n i muhimu ili ruling zake ziwe binding! Hata mabaraza ya usuluhishi ya kata yameanzishwa ndani ya dola!
bahati nzzuri sisi waislam linapokuja swala la kudai haki zetu za msingi hatuogopi kupigwa , wala kufa ikibidi... kitaeleweka tu,
Mkuu hawa jamaa wangekuwa na uelewa angalau kidogo tu wangeelewa ulichoandika hapo juu.Ushasema mahakama ya kadhi ni ibada. Sasa unataka nini iwe ndani ya dola ili iwe binding. Yaani ibada inapewa uhalali wake na dola/katiba ama imani ya kiroho ya muislam mwenyewe? Kama kweli mahakama ya kadhi ni ibada kama unavyodai basi maamuzi yake mtayaheshimu wenyewe bila kushurutishwa na serikali. Na by the way authority pekee inayoshangaza wataalam ni ya kidini haihitaji sanctions ili ifuatwe bali ni imani ya wahusika wa dini husika. Lakini mamlaka za kiserikali huhitaji sanctions ili watu waziheshimu. Halafu wewe unakuja na hoja dhaifu eti iwe ndani ya katiba ili iwe binding. Kwa hiyo unasema indirectly waislam hamtaiheshimu ibada ya kadhi hadi mshurutishwe na serikali?
Mbona imeanzishwa mahakama ya Ardhi na mahakama ya Biashara. Sasa kwanini isiwe hii ya kadhi?
Tatizo linalowasumbua waislamu ni elimu ndogo za maimamu wao hawa-judge mambo critically wanachukulia kirahisi tu na mara nyingi kwa jaziba.
Hao vijana wa kiislam wakiandamana usiku na mchana watasoma saa ngapi? Haya wasubirie sup.na disco huku vyuoni. Km si kuendelea kuukumbatia ujinga badala ya kupigania elimu ambayo ndo msingi wa maendeleo ya Taifa lolote.
Kweli wee unawaza kibarubaru. Haya ngoja nikuongezee na nyingine
1. Mahakama ya kazi (labour court)
2. Mahakama ya katiba
Nakushauri soma kisomo cha manufaa (ngumbaru) uongeze ufahamu wako.
Ttatizo nililolibaini huko Tanganyika kwa wakristo ni CHOYO na CHUKI dhidi ya haki za waislam. Ikiwa pamoja na kujiona wao ni first citizen na waislam ni second citizen.
Sioni sababu yoyote ya msingi na khasa ukiangalia hata wenzenu Kenya wameanzisha hivyo na ukitazama Kenya ina zaidi ya 75% ukristo ukilinganisha na tanganyhika ambao mnakaribiana kiidadi.
Kama JMT ina nia ya kweli kuanzishwa kwa mahakama hizo basi ni wajibu wao kuzifanya Ruling zake ziwe binding katika sheria za nchi ili zisilete mgongano na mahakama za kawaida.
na lazima muelewe mahakama hizo zitakuwa huru kwa kila mwenye kutaka kutuzitumia katika kutafuta haki yake na zitakuwa kwa raia wote wa TZ wanaotaka.
Poleni sana
Labda nikuulize kwani mkristo akienda kudai haki yake kwa kutumia mahakama ya kadhi atakataliwa? Mbona Islamic banking huko Tz nasikia kuna wakristo wengi sana wanajiunga.
Mbona aulalamiki ruzuku kubwa sana kutoka Serikalini zinazopewa shule na hata vyuo na mahospitali ya taasisi za kidini kama KCMC na Bugando?
Nafikiri soma mzizi wa khoja yangu.Mpwa kwani tatizo liko wapi endapo mtaanzisha wenyewe? ni lazima sana ianzishwe na serikali? Je kama itaanzishwa na serkali si mtakuja na hoja kuwa serikali inainglia uhuru wenu kama mnavyofanya kwa Bakwata sasa? Kuwa Bakwata haina maamuzi kwasababu ilianzishwa na serikali? tuamini lipi sasa toka kwenu? mara mnaitaka Serikali ianzishe wakati huo huo Bakwata haina maamuzi kwasababu ilianzishwa na Serkali? iweje serikali kuanzisha Bakwata iwe kosa kwenu lakini iwe safi ikianzisha Mahakama ya Kadhi ya watu wale wale wanaoipinga? Au kuna lingine zaidi ya Hilo? Na sula kwamba wakristo hawataki haki zenu na lenyewe halieleweki maana Rais Muislamu, Makamu zake ni waislamu, IGP muislamu, Mnadhimu wa Jeshi Muislam, Judge Mkuu Muislamu, Mkuu wa usalama Muislamu; so you have everything in your hand, mkristo kakaaatje hapo au anaingiaje hapo? Tumia busara kujenga hoja Mpwa